Tuesday 15 May 2018

tnt ilitengenezwa mara ya kwanza mwaka 1863

Trinitrotoluene

Trinitrotoluene au kifupi TNT ni kampaundi ya kikemia inayotumiwa hasa kama kilipukaji cha kijeshi.
TNT si kilipukaji kikali zaidi kushinda vingine lakini inapendelewa kwa sababu matumizi yake ni salama kushinda dainamiti au nitrogliserini. Gramu 1 ya TNT inachisha nishati ya jouli 4.184 ilhali gramu 1 ya dainamiti inaachisha jouli 7.500. TNT inayeyuka (kuwa kiowevu) kwenye sentigredi 80 ambayo ni chini ya halijoto yenye hatari ya kulipuka; hivyo inaweza kumwagwa kwa umbo linalotakiwa bila hatari.
Vilevile inavumilia mishtuko na joto bila mlipuko; katika ramia inahitaji mshtuko mkali kwa kusababisha mlipuko. Haiyeyuki kirahisi katika maji kwa hiyo ni salama kwa matumizi katika mazingira nyevunyevu. Tabia hizi zote zilisababisha kuitazamiwa kama kilipukaji salama.

Historia[hariri | hariri chanzo]

TNT ilitengenezwa mara ya kwanza mwaka 1863 na mwanakemia Mjerumani Julius Wilbrand[1] aliyeitumia kama dawa ya rangi njano. Baadaye tabia ya kilipukaji ilitambuliwa lakini haikutumiwa kwa miaka kadhaa kwa sababu vilipukaji kali zaidi kama dainamiti na nitrogliserini zilipendelewa.[2]
Jeshi la Ujerumani lilitambua mnamo 1902 ya kwamba hii ilikuwa faida kwa matumizi ya kijeshi kwa sababu ramia tenye TNT yalikuwa salama zaidi kwa utengenezaji na usafirishaji. Hasa waliona faida ya kwamba ramia ya TNT iliyofyatuliwa na mzinga dhidi ya manowari yenye kinga cha feleji iliweza kutoboa kinga kwanza na kulipuka ndani ya manowari. Hivyo uharibifu wake ulikuwa kubwa zaidi. Waiingereza bado walitumia ramia yenye kilipukaji kali zaidi iliyosababisha mlipuko wakati wa kugonga kinga ya nje na hivyo kuacha nguvu yake nje ya mabnowari. Hivyo Uingereza ulifuata mfano wa Wajerumani tangu 1907 na kujaza ramia zake kwa TNT.
Hadi leo TNT hutumiwa na jeshi za nchi nyingi duniani kwa ajili ya ramia na mabomu. Inatumiwa pia na makampuni ya ujenzi kwa milipuko ya kulengwa wakati wa kubomoa majengo au kuunda nafasi kwenye ujenzi wa barabara.

Tani TNT kama kipimo[hariri | hariri chanzo]

Nguvu ya mlipuko hutajwa kwa kipimo cha "tani ya TNT"; yaani nguvu inayotokea katika mlipuko wa kilogramu 1,000 (= tani 1) za TNT ambayo ni sawa na gigajouli 4.184 [3].
Milipuko mikubwa hasa ya mabomu ya nyuklia hupimwa kwa "kilotani" au "megatani" za TNT. Bomu la nyuklia la kwanza lililotupwa na Marekani huko Hiroshima (Japani) mwaka 1945 lilikuwa na nguvu ya kilotani 15. Mabomu makubwa yaliyotengenezwa wakati wa vita baridi yalikuwa na nguvu zaidi; Marekani iliandaa mabomu hadi megatani 25; mwaka 1961 Umoja wa Kisovyeti (Urusi) ililipusha bomu la nyuklia la jaribio lenye nguvu ya megatani 50 huko kwenye kisiwa Novaya Zemlya.
Hata nishati inayoachishwa wakati wa tetemeko la ardhi inapimwa kwa tani za TNT; tetemeko la ardhi ya 2011 iliyosababisha tsunami nchini Japani imekadiriwa kuwa na nishati ya gigatani 9,320 za TNT , sawa na mara milioni 600 nguvu la bomu la Hiroshima.[4]

Monday 14 May 2018

Watu wafariki kwa ugonjwa wa Ebola DRC

Watu 17 wafariki kwa ugonjwa wa Ebola DRC

Wizara ya afya nchini Congo imethibitisha kuzuka upya kwa ugonjwa wa Ebola, jimboni Equateur kaskazini magharibi mwa nchi hiyo. Visa viwili vya ugonjwa huo, vimethibitshwa baada ya kufanyika kwa uchunguzi.
    
Kongo Ausbruch von Ebola (Getty Images/AFP/D. Minkoh)
Ujumbe wa wataalamu wa afya kutoka serikalini, shirika la afya ulimwenguni na shirika la madaktari wasiokuwa na mipaka unatarajiwa kuwasili baadae siku ya Jumatano kwenye kijiji kilicho athirika na ugonjwa huo.
Wizara ya afya imesema jibu la haraka linahitajika kwa ajili ya kukabiliana na ugonjwa huo ambao kwa sasa umeibuka kwenye kijiji cha Ikoko Impenge, mtaani Bikoro jimboni Equateur. Dr Jean Jacques Muyembe kiongozi wa maabara ya utafiti wa ugonjwa wa Ebola na magonjwa mengine ya kuambukiza amesema kwamba kuna uwezekano mdogo wa ugonjwa huo kusambaa kwenye maeneo mengine
ARCHIV Ebola-Ausbruch in Liberia 2014 (picture alliance/AP Photo/A. Dulleh)
Ebola iliwahi kuripuka nchini Liberia na hapo juu ni wafanyakazi wa afya katika kituo cha ugonjwa huo Monrovia.
"Hatari ya kusambaa kwa ugonjwa huo ni ndogo sana kutokana na kwamba vijiji hivyo vinapatikana kwenye maeneo yasiyofikika kwa urahisi, ni takriban kilomita 200 msituni na mji wa Mbadaka mji mkuu wa jimbo la Equateur. Kwa sababu ugonjwa huo unadhaniwa kuibuka mwezi desemba mwaka jana lakini ni wiki iliopita ndio tumetaarifiwa…Nafiriki ni ugonjwa ambao tunaweza kuutokomeza haraka," amesema Muyembe.
Kwa mujibu wa taarifa ya wizara ya afya ni kwamba kuna visa 21 vya maambukizi ambapo miongoni mwake watu 17 tayari wamefariki, ndio vilisababisha kuweko na tahadhari kuhusu ugonjwa huo. Ujumbe uliopelekwa kwa ajili ya kukadiria tukio ulikuta visa vitano vya watu wenye homa na miongoni mwake watu wawili walikutwa na virusi vya Ebola.
Daktari Muyembe amesema kwamba mtu wa kwanza alihofiwa kufariki kutokana na ugonjwa huo ni afisa wa polisi kwenye kijiji cha Bokatola, ambae alionekana na  dalili za ugonjwa huo . Amesema toka tarehe 3 Mei hakujaripotiwa kifo cha mtu kwenye maeneo hayo.
Ebola-Virus Guinea (picture alliance/AP Photo)
Mripuko wa ugonjwa wa Ebola nchini Guinea
Shirika la Afya ulimwenguni WHO limelezea kwamba liko tayari kuunga mkono juhudi za serikali kwa  ajili ya kuutokomeza ugonjwa huo wa Ebola. WHO imesema imetenga dola milioni moja kwa ajili ya kupambana na ugonjwa wa Ebola jimboni Equateur.
Ni mara ya tisa sasa toka mwaka wa 1976, Congo kutangaza mripuko wa ugonjwa wa Ebola, virusi hivyo vya aina ya zaire vinatokana hasa na ulaji wa nyama mwitu.
Mara ya mwisho ugonjwa huo kuripotiwa nchini humo ilikuwa ni Mei mwaka jana kwenye jimbo la Bas-Uele ambako watu 4 walifariki miongoni mwa visa vinane vilivyothibitishwa.
Hakujakueko na uhusiano wowote baina ya virusi vya Ebola Congo na vile vilivyozuka  mwaka 2014 kwenye nchi za Afrika magharibi vilivyosababisha vifo vya zaidi ya watu 11.

Msichana wa miaka 19 ahukumiwa kifo Sudan

Msichana wa miaka 19 ahukumiwa kifo Sudan

Msichana mmoja aliye na miaka 19 amehukumuhiwa kifo na Korti moja nchini Sudan baada ya kupatikana na hatia ya kumuua mumewe wa kulazimishwa, alipojaribu kumbaka.
    
Indien - Kinderheirat (picture-alliance/AP Photo/P. Hatvalne)
Msichana huyo Noura Hussein alilazimishwa kuolewa na binamu yake akiwa na miaka 16, aliikataa ndoa hiyo na kukimbilia kwa jamaa yake aliyoishi naye kwa miaka mitatu. Baadaye mwezi Aprili mwaka huu alirejea nyumbani nje kidogo ya mji wa Khartoum  baada ya babake kumwambia ndoa hiyo imefutiliwa mbali. Lakini alikuta kuwa mipango ya harusi yake ilikuwa bado inaendelea.
Baada ya kuolewa, Noura alikataa kufanya tendo la ndoa na mumewe na ilipofika siku ya sita, mumewe alimbaka huku jamaa zake wa kiume wakimshikilia Noura kwa nguvu  ili kurahisisha kitendo hicho. Siku ya pili mumewe alijaribu tena kumbaka. Noura alimchoma kisu na kumuua wakati alipojaribu kuzuwia tendo hilo.
Africa Child Marriage Mosambik (picture alliance/AP Photo/S.Mohamed)
Mikono ya msichana aliye na miaka 18 na mumewe wa miaka 20
Aidha Korti ya Sharia inayofuata sheria za kiislamu ilimkuta msichana huyo na kosa la mauaji mwezi uliyopita na siku ya Alhamisi wiki hii, ikamhukumu kifo kwa kunyongwa.
Hata hivyo mawakili wake kwa sasa wana siku 15 za kukata rufaa huku wanaharakati wa kutetea haki za binaadamu wamepaza sauti zao juu ya hili kwa kumtolea wito rais Omar al Bashir kumsamehe msichana huyo,wakisema ilikuwa hatua ya kujilinda. 
"Chini ya sheria ya kiislamu familia ya mume inaweza kudai fidia ya fedha au kifo, walichagua kifo na hicho ndicho kilichofuatwa," alisema  Badr Eldin Salah, mwanaharakati kutoka Vuguvugu la vijana wa Afrika waliokuwa Kortini wakati hukumu hiyo ilipotolewa. 
Badr Salah ameongeza kuwa mawakili wa Noura watakataa rufaa dhidi ya hukumu hiyo lakini pia kunahitajika uungwaji mkono kutoka jamii ya Kimataifa na kutoka katika jumuiya kama Umoja wa Afrika, Umoja wa Mataifa na Umoja wa Ulaya.
Sheria za Sudan zinaruhusu ndoa pindi msichana anapovunja ungo
Sudan imechukua nambari 165 kati ya nchi 188 katika orodha ya Umoja wa Mataifa inayoshughulikia masuala ya usawa wa kijinsia, inayolinganisha nafasi ya  wanawake na wanaume kuhusu upatikanaji wa huduma  za afya, elimu, ujumuishwaji kisiasa na fursa za ajira.
Sudans Präsident Omar Hassan el Bashir, Porträt (dpa)
Rais wa Sudan Omar el Bashir
Sudan ni mojawapo ya nchi barani Afrika zilizo na sera dhaifu kuwalinda wanawake na wasichana. Kwa mfano Ubakaji katika ndoa pamoja na ndoa za utotoni hazichukuliwi kama kosa. Sheria za taifa hilo zinaruhusu msichana kuolewa pindi anapovunja ungo, na zinakubali pia msichana wa miaka kumi kuolewa na mlezi wake kwa ruhusa ya jaji.
Wakati huo huo Yasmeen Hassan Mkurugenzi wa shirika la Equality Now amesema Noura ni mhanga na anapaswa kushughulikiwa kama muathirika, huku akisistiza kuwa katika mataifa mengi muathirika kama Noura hupata huduma mbali mbali ili kuhakikisha anaondokewa na kiwewe baada ya kukutwa na tukio kama hilo.
Yasmeen anasema kumhukumu tu kwa tukio la uhalifu kutokana na kujilinda na shambulio  ni udhalilishaji wa haki zake chini ya katiba ya Sudan na chini ya sheria za kimataifa.
Mwandishi:  rama dee
Mhariri: radick dee david

kundi Alshabaab la ashtakiwa Ujerumani

Mshukiwa wa kundi la Alshabaab ashtakiwa Ujerumani

Waendesha mashtaka wa Ujerumani wamemfungulia mashitaka mwanamume mmoja kutoka Somalia anayedaiwa kuwa mwanachama wa kundi la wanamgambo wa Al Shabab
    
Somalia Al-Shabaab Kämpfer (picture alliance/AP Photo/F. A. Warsameh)
Maafisa nchini Ujerumani wamemfungulia mashitaka mwanamume mmoja kutoka Somalia anayedaiwa kuwa mwanachama wa kundi la waasi la Al Shabab anayetuhumiwa kufanya jaribio la mauaji na kusaidia katika mauaji. Waendesha mashitaka wa Ujerumani wamesema mtuhumiwa huyo mwenye umri wa miaka 20 anayetambulika kwa jina Abduqaadir A alijiunga na kundi hilo la waasi mwaka 2012 mjini Mogadishu na alipewa mafunzo ya kutumia bastola na magureneti.
Wakati wa mafunzo hayo, inadaiwa mshukiwa huyo aliandamana na wanachama wengine wa Al Shabab kwenda msikiti ambako walimuua mtu mmoja kwa kumpiga risasi tatu kichwani. Baadaye aliagizwa kumuua afisa mmoja wa serikali ya Somalia katika mkahawa mmoja. Alifanikiwa kutoroka Somalia mwezi Okotoba mwaka 2012 na alikimbilia Ujerumani mwaka 2014 kabla ya kukamatwa mwezi Februari mwaka huu.