Friday 26 January 2018

ugunduzi

Karl Friedrich Benz


Karl Friedrich Benz alizaliwa tar. 25 Novemba 1844 akiitwa Karl Friedrich Michael Vaillant huko Mühlburg / Karlsruhe Ujerumani wa Kusini Magharibi. Baada ya kumzaa mamake Josephine Vaillant akaolewa na babake Johann Georg Benz. Hivyo akaitwa Karl Friedrich Michael Benz lakini baadaye akajiita Carl Friedrich Benz.
Alikuwa mhandisi Mjerumani mwenye sifa ya kuwa alitengeza motokaa ya kwanza au gari la kwanza lililotumia nguvu ya nishati ya petroli.
Mwaka 1864 alichukua digri ya uhandisi, mw. 1871 alianzisha kampuni yake ya kwanza. Hapo alitengeneza injini ya petroli ya mapigo mawili mwaka 1878/79 aliyoendeleza kuwa injini ya mapigo manne. Benz hakuwa mhandisi wa kwanza kutengeneza injini za aina hii, Mjerumani mwenzake Nikolaus Agosti Otto aliwahi kuchukua hataza ya injini ya mapigo manne mwa. 1876. Injini za aina hii zilifanya kazi viwandani vikiendesha mashine mbalimbali.
1886 Benz alikuwa mtu wa kwanza aliyeweka injini ya petroli kwa gari. Gari lake la kwanza lilikuwa na magurudumu matatu yenye nguvu-farasi 0.8. Mke wake Bertha Benz alifanya safari kubwa ya kwanza kwa gari hili kwa umbali wa km 89 kutoka Mannheim kwenda Pforzheim (yote Ujerumani wa Kusini Magharibi). Alipoishia petroli alipaswa kuinunua katika duka ya madawa kwani hapakuwapo na kituo cha petroli bado.
Benz aliendelea kutengeneza gari lenye magurudumu manne. Kwa jina la "Velo" lilikuwa motokaa ya kwanza iliyotengenezwa kwa wingi duniani.
Benz aliona kupanuka kwa biashara yake watoto wake wakiendelea kuendesha makampuni yake. Mwaka 1926 kampuni ya Benz iliunganishwa na kampuni ya Gottlieb Daimler kwa jina la "Daimler-Benz".
Karl Benz aliaga dunia tar. 4 Aprili 1929.

Monday 15 January 2018

majengo ya zamani

Koloseo

Koloseo mwaka 2007 wakati wa usiku
Koloseo (Kiitalia: Colosseo) ni kiwanja cha michezo cha kale mjini Roma kilichopo katika hali ya maghofu kutokana na umri wake wa miaka 2000. Ni kati ya majengo mashuhuri mjini Roma na duniani kwa ujumla. Wakati wa Dola la Roma ilikuwa jengo kubwa kabisa liliilojengwa na Waroma wa Kale.
Koloseo ilijengwa kuanzia mwaka 70 hadi 80 BK. Kaisari Vespasiano alianzisha ujenzi kwa kutumia mapato ya uwindo wa vita ya Waroma dhidi ya Uyahudi na hasa hazina ya hekalu ya Yerusalemu. Ilikamilishwa na Kaisari Titus.
Kiwanja kilikuwa na nafasi kwa watu 45,000 hadi 50,000. Watazamaji waliangalia maonyesho ambako watu au wanyama waliuawa. Michezo hii iligharamiwa na serikali kwa ajili ya wakazi wa mji kama burudani. Falsafa ya kisiasa ya Roma ilisema ya kwamba watu watulia wakipewa "panem et circenses" yaani "chakula na michezo".
Baada ya ushindi wa Ukristo mashindano ya kuua watu yalipingwa na kanisa. Shindano la mwisho lilitokea mwaka 434/435. Mapigano dhidi ya wanyama yaliendelea hadi mwaka 523. Lakini baada ya mwisho wa Dola la Roma idadi ya wakazi wa Roma ilipungua na Koloseo haikutumiwa tena kwa michezo.
Katika karne zilizofuata wakazi wa Roma walitumia Koloseo kama windo la mawe kwa ajiliy a ujenzi. Hivyo sehemu kubwa ya jengo imepotea.
Sehemu za ndani za Koloseo
Uharibifu ulusimamishwa na Papa Benedikto XIV aliyetangaza Koloseo kuwa kumbukumbu kwa mashahidi Wakristo waliouawa hapa na tangu 1744 imehifadhiwa.

Michezo katika Koloseo

Michezo katika Koloseo ilikuwa hasa ya aina mbili:
  • mashindano ya wapiganaji walioshindana kwa silaha za kweli hadi kifo. Wapiganaji waliitwa na Waroma kwa jina la "gladiator" yaani mwenye upanga. Wengi wao walikuwa watumwa lakini wengine walikuwa watu huru. Walijifunza mapigano kwa silaha kwa ajili ya maonyesho na kuitumia kwenye kiwanja mbele wa watazamaji. Walioshinda walipata tuzo na zawadi nyingi. Wegine walikufa na kusahauliwa.
  • mashindano kati ya watu na wanyama pori. Waroma wa Kale walikamata wanyama pori kutoka Ulaya na Afrika ya KAskazini kwa ajili ya maonyesho haya. Wanyama waliuawa kwenye kiwanja mbele ya watazamaji na magladiator lakini ilitokea pia ya kwamba wavindaji waliuawa na wanyama.
Waroma wa Kale walipenda maonyesho haya.
Wakristo jinsi waliowekwa mbele ya simba
Palikuwa pia na michezo ya pekee:
  • kiwanja kilijazwa maji na jahazi pia manowari ndogo ziliwekwa humo ili zishindane. Michezo hii ilikuwa ghali sana na ni makaisari tu walioweza kugharamia michezo ya aina hii.
  • Tangi karne ya 3 Wakristo waliuawa kiwanjani kama sehemu ya maonyesho. Ukristo ulikuwa dini marufuku katika Roma ya Kale hadi mwaka 313. Wakati mwingine Wakristo walikamtawa kwa wingi na kupewa hukumu ya mauti. Walionekana walifaa kwa maonyesho ambako walisimamishwa mbele ya wanyama pori kama simba au dubu.