Friday 9 March 2018

Miaka 6o tangu kuripuliwa bomu la kwanza la atomiki duniani

HABARI ZA ULIMWENGU

Miaka 6o tangu kuripuliwa bomu la kwanza la atomiki duniani

July 16, mwaka 1945 katika Jangwa la Mkoa wa New Mexico, huko Marekani, kulifanywa jaribio la mwanzo la kuliripuwa bomu la atomiki ambalo limeibadilisha dunia yetu hii. Bomu hilo lilikuwa na nguvu mara alfu mbili zaidi kuliko bomu lolote lililokuweko hapo kabla; na sio tu lilipodondoshwa huko Hiroshima na Nagasaki lilipelekea Japan kusalimu amri katika Vita Vikuu vya Pili vya Dunia, lakini, wakati huo huo, lilianzisha enzi mpya ambayo tunaishi nayo hivi sasa, enzi ya kutishwa kutumai silaha hiyo.
Rais Truman (miaka 60 iliopita) akitangaza kusalimu amri Ujerumani katika Vita Vikuu vya Pili vya Dunia
Rais Truman (miaka 60 iliopita) akitangaza kusalimu amri Ujerumani katika Vita Vikuu vya Pili vya Dunia
Bomu la mwanzo la atomiki lilitengenezwa huko Los Alamos, katika maabara yalio ya siri iliokuweko katika milima ya New Mexico. Mwanafizikia Robert Oppenheimer aliiongoza shughuli hiyo katika kipindi cha chini ya miaka miwili.
Dakika moja baada ya saa sita za usiku hapo July 13, siku tatu kabla ya kuripuliwa bomu hilo, gari iliondoka huko Los Alamos, ikiwa na madini ya Plutonium. Mahala pa kufanywa jaribio palikuwa katika Bonde liliokuwa jangwani. Muda mfupi kabla ya kutuwa juwa, bomu hilo liliripuliwa:
Insert: Atm: Countdown/Explosion…
Joe Lehman, mmoja kati ya watu wachache walioshuhudia tokeo hilo, anasema:
Insert: O-Ton Joe Lehman:
+Umeme, mara dhoruba kubwa ya upepo, mtikisiko mkubwa na sura ya uyoga wa atomiki, tena sura inakuja kama ya nguzo iliosimama angani ambayo inazidi kwenda juu na juu. Na baada ya dakika kuna mwangaza wa kama juwa linalotuwa ambao unangara kutokana na vichembe chembe vya mavumbi yalioko hewani- Rangi unazoziona ni za kuvutia sana.+
Umeme kama wa radi uliopanda juu kwa kasi ya mita 120 kwa sekundi ulionekana hadi Albuquerque, umbali wa kilomita 300. Huu ulikuwa sio mchezo wa kimaumbile, lakini ni nguvu za mwanadamu. Kilomita tatu kutoka hapo, katika mahandaki wanasyansi walikuwa wakishuhudia tokeo hilo, na mmoja wao alikuwa mwanasayansi na jenerali wa jeshi, Jack Aeby:
Insert: O-Ton:
+Wengi wetu mwanzo tulibakia na mawazo yetu wenyewe. Lakini tulipokusanyika, nilihisi tumenywea, tumeathrika na kile tulichokianzisha. Tukaanza kujiuliza kama kufanya hivyo ilikuwa ni fikra nzuri. Mimi mwenyewe nilijiuliza.+
Mwenyewe Robert Oppenheimer, muasisi wa bomu hilo, alijihisi atabakia kuwa mtu aliyeiharibu dunia hadi atakapokufa.
Wengi wa wanasayansi walioshiriki katika mradi huo wa kutengeneza bomu la atomiki, mradi uliopewa jina la Manhattan, walifikiri kwamba habari za kufaulu majaribio ya kuripuwa bomu la kinyukliya yataifanywa Japan ivikomeshe Vita Vikuu vya Pili vya Dunia. Lakini Rais Truman wa Marekani na wanajeshi wake waliamuwa vingine. Wiki tatu baadae mabomu ya atomiki yalidondoshwa huko Hiroshima na Nagasaki. Mwenyewe Rais Truman aliandika hivi katika kijitabu chake cha makumbusho ya kila siku:
+Nimemtaka waziri wa vita, Simpson, atumie silaha hiyo kuyashambulia malengo ya kijeshi, wanajeshi na manuwari za Wajapani na sio kuwashambulia wanawake na watoto. Melengo yawe tu ya kijeshi. Ni uzuri kwa dunia kwamba sio Hitler na gengi lake au sio Stalin waliovumbua Bomu la atomiki. Inatisha kwamba kuna mtu aliyelitengeneza bomu hilo, lakini sisi tunaweza kubadilisha kuwa la manufaa.+
Mashambulio ya mabomu huko Hiroshina na Nagasaki, Japan, hapo Agosti mwaka 1945 yalichukuwa siku hiyo maisha ya watu 130,000, wengi wao wakiwa ni raia. Nguvu kubwa ya uharibifu wa bomu hilo ilimshangaza pia mvumbuzi wake, Robert Oppenheimer, na kumweka katika hali ya wasiwasi.
Hivi sasa, mahala ambapo bomu la kwanza la atomiki liliripuliwa ni kimya, watu wameihama sehemu hiyo. Lile shimo kubwa lililoachwa kutokana na mripuko huo limefukiwa; na miaka sitini baadae mahala hapo pana miyale mingi ya kinyukliya.
Bila ya shaka, watu waliofanya kazi katika mradi huo wa Manhattan wamekuwa kila wakati wakichunguzwa, kiafya. Baadhi yao wamekufa kutokana na kansa ya mapafu, wakati huo kila mmoja wao alikuwa anavuta sigara. Mmoja au wawili kati yao walikufa kutokana an ajali ya magari, lakini kansa ya mapafu walioipata wengi wao ilitokana na miyale ya kinyukliya.
Wanasayansi hao walitambua kwamba mradi waliokuwa wanaofanyia kazi ulikuwa wa hatari pia kwa afya zao, lakini habari zilizoletwa Marekani kutoka Ulaya na wanasayansi wengi wa atomic, wengi wao wakiwa ni Wayahudi, zilikuwa za kutisha. Habari hizo zilisema kwamba Adolf Hitler na gengi lake walikuwa na Uranium walioipata kutoka Tschekoslovakia, hiyvo inahitaji Marekani iharakishe kutengemeza bomu hilo. Hapo tena yakaanza mashindano ya nani atafaulu kwanza kulifikia lengo hilo. Wamarekani walishughulika kujifariji na mshtuko waliopata kwa manuwari zao kushambuliwa na ndege za Wajapani huko Pearl Harabou, na jeshi la Ujerumani lilikabiliana na kushindwa huko Stalingrad. Hivyo, ililazimu kujengwa maabara ya utafiti wa atomiki kwa haraka kama iwezekanavyo, na ndipo Los Alamos pakachaguliwa kuwa ni mahala muwafaka pa kufanya jaribio hilo, na mradi huo ukapewa jina la Manhattan.
Wengi waliokuweko hapo walikuwa hawajui kwanini ni wako hapo. Polisi wa jeshi wa wakati huo, Lawrence Antos, anasema:
Insert: O-Ton:
+Tulipofika, tulifikiri hapo patakuwa kambi ya wafungwa wa kivita wa Kijapani. Tuliamini wafungwa wa kivita wa Kijapani watapelekwa Los Alamos.+
Kulikuwa na kanuni kali kwa wale wanaofanya kazi huko. Maabara yalikuwa mbali na majengo ya kuishi, eneo zima lilizungukwa na senyenge na kulindwa. Hamna mtu yeyote aliyeruhusiwa kwenda umbali wa zaidi ya kilomita 100, na wanasanyansi walikuwa hawawezi kuwasiliana na jamaa zao.
Maabara ya Los Alamos ilipanuka kutoka kuwa na wafanya kazi 400 hadi 4,000, mabingwa wa madini, wale wa Plutonium, wanakemia, wote hao wakishughulika na suala juu ya namna ya kuliripuwa bomu hilo la atomiki.
Insert: Atmo: Test
Jaribio hilo lilifaulu. Saa kumi na moja na dakika 29 sekundi 45 bomu la mwanzo la atomiki duniani liliripuliwa. Mwanadamu aliingia katika enzi ya atomiki. Vita Vikuu vya Pili vilimalizika kwa kudondoshwa mabomu hayo huko Hiroshima na Nagasaki, nchini Japan. Kama bomu la atomiki ni mafanikio au hasara, kwa mwanadamu aliyeliunda, ni suali gumu kulijibu.

    No comments: