Koloseo
Koloseo mwaka 2007 wakati wa usiku
Koloseo (
Kiitalia:
Colosseo) ni kiwanja cha michezo cha kale mjini
Roma
kilichopo katika hali ya maghofu kutokana na umri wake wa miaka 2000.
Ni kati ya majengo mashuhuri mjini Roma na duniani kwa ujumla. Wakati wa
Dola la Roma ilikuwa jengo kubwa kabisa liliilojengwa na Waroma wa Kale.
Koloseo ilijengwa kuanzia mwaka 70 hadi 80 BK.
Kaisari Vespasiano alianzisha ujenzi kwa kutumia mapato ya uwindo wa vita ya Waroma dhidi ya
Uyahudi na hasa hazina ya
hekalu ya Yerusalemu. Ilikamilishwa na
Kaisari Titus.
Kiwanja kilikuwa na nafasi kwa watu 45,000 hadi 50,000. Watazamaji
waliangalia maonyesho ambako watu au wanyama waliuawa. Michezo hii
iligharamiwa na serikali kwa ajili ya wakazi wa mji kama burudani.
Falsafa ya kisiasa ya Roma ilisema ya kwamba watu watulia wakipewa
"panem et circenses" yaani "chakula na michezo".
Baada ya ushindi wa Ukristo mashindano ya kuua watu yalipingwa na
kanisa. Shindano la mwisho lilitokea mwaka 434/435. Mapigano dhidi ya
wanyama yaliendelea hadi mwaka 523. Lakini baada ya mwisho wa Dola la
Roma idadi ya wakazi wa Roma ilipungua na Koloseo haikutumiwa tena kwa
michezo.
Katika karne zilizofuata wakazi wa Roma walitumia Koloseo kama windo
la mawe kwa ajiliy a ujenzi. Hivyo sehemu kubwa ya jengo imepotea.
Sehemu za ndani za Koloseo
Uharibifu ulusimamishwa na
Papa Benedikto XIV aliyetangaza Koloseo kuwa kumbukumbu kwa mashahidi Wakristo waliouawa hapa na tangu 1744 imehifadhiwa.
Michezo katika Koloseo
Michezo katika Koloseo ilikuwa hasa ya aina mbili:
- mashindano ya wapiganaji walioshindana kwa silaha za kweli hadi kifo. Wapiganaji waliitwa na Waroma kwa jina la "gladiator"
yaani mwenye upanga. Wengi wao walikuwa watumwa lakini wengine walikuwa
watu huru. Walijifunza mapigano kwa silaha kwa ajili ya maonyesho na
kuitumia kwenye kiwanja mbele wa watazamaji. Walioshinda walipata tuzo
na zawadi nyingi. Wegine walikufa na kusahauliwa.
- mashindano kati ya watu na wanyama pori. Waroma wa Kale walikamata
wanyama pori kutoka Ulaya na Afrika ya KAskazini kwa ajili ya maonyesho
haya. Wanyama waliuawa kwenye kiwanja mbele ya watazamaji na magladiator
lakini ilitokea pia ya kwamba wavindaji waliuawa na wanyama.
Waroma wa Kale walipenda maonyesho haya.
Wakristo jinsi waliowekwa mbele ya simba
Palikuwa pia na michezo ya pekee:
- kiwanja kilijazwa maji na jahazi pia manowari ndogo ziliwekwa humo
ili zishindane. Michezo hii ilikuwa ghali sana na ni makaisari tu
walioweza kugharamia michezo ya aina hii.
- Tangi karne ya 3 Wakristo waliuawa kiwanjani kama sehemu ya
maonyesho. Ukristo ulikuwa dini marufuku katika Roma ya Kale hadi mwaka 313.
Wakati mwingine Wakristo walikamtawa kwa wingi na kupewa hukumu ya
mauti. Walionekana walifaa kwa maonyesho ambako walisimamishwa mbele ya
wanyama pori kama simba au dubu.