Tuesday 28 November 2017

Adolf Hitler

Adolf Hitler

Hitler, 1937
.Adolf Hitler (BraunauAustria20 Aprili 1889BerlinUjerumani30 Aprili 1945) alikuwa dikteta wa Ujerumani kuanzia mwaka 1933 hadi kifochake.

Maisha

Utoto na familia

Adolf Hitler akiwa mtoto mchanga.
Alizaliwa nchini Austria mwaka 1889. Wazazi wake walikuwa mtumishi wa forodha ya Austria Alois Hitler na mamake Klara aliyekuwa mke wa tatu wa Alois. Adolf alikuwa na ndugu watano lakini kati ya hao ni dadake Paula pekee aliyeishi kufikia umri wa mtu mzima, wengine wote walikufa mapema. Alikuwa pia na ndugu wawili kutoka ndoa ya mke wa pili wa baba na hao waliitwa Alois mdogo na Angela waliokaa katika familia ya Alois mzee baada ya kifo cha mama.
Kutokana na kuhamishwa kwa baba mara kwa mara Adolf alisoma kwenye shule za msingi tofauti kati ya 1895 hadi 1899. Kuanzia mwaka 1900 alisoma kwenye shule ya sekondari mjini Linz lakini hakufauli alipaswa kurudia madarasa mawili. Hakupenda somo la dini lakini alivutwa na historia na jiografia. Baba alimpiga mara nyingi katika kipindi kile akikasirika juu ya kutofaulu shuleni. Baada ya kifo cha baba Alois mwaka 1903 mamake alimhamisha kwenda shule nyingine mjini lakini alishindwa hapa pia akarudi nyumbni kwa mama bila ya kumaliza masomo yake.
Alipokaa Linza Adolf alifahamika na mafundisho ya kiongozi wa chama cha "Alldeutsch" [1] na hasa chuki dhidi ya Wayahudi na dharau dhidi ya mataifa ya Waslavoni ya Ulaya.
Tangu 1906 Hitler alijisikia kuwa yeye ni msanii alipeleleza nafasi za kusoma uchoraji. Mwaka 1907 aliomba kupokelewa katika chuo cha sanaa mjini Vienna alishindwa. Akarudi nyumbani baada ya kusikia mamake alikuwa mgonjwa wa kansa. Aliangalia nyumba hadi kifo cha mama kwenye Disemba 1907. Mama alitibiwa na daktari Eduard Bloch aliyekuwa Myahudi; Adolfa alimshukuru sana kwa juhudi zake na baadaye alimlinda Bloch dhidi ya mateso yaliyoandaliwa kwa Wayahudi katika miaka ya 1930 baada ya Hitler kuwa mtawala wa Ujerumani na tangu 1938 pia juu ya Austria.

Msanii asiyefaulu Vienna na Munich

Tangu Januari 1908 alitumia urithi wa mama pamoja na pensheni ya mjane kwa kuhamia Vienna alipokaa hadi 1913. Alijaribu tena kupata nafasi kwenye chuo cha sanaa cha Vienna akashindwa tena. Mtu aliyeishi pamoja naye katika chumba kimoja alisema wakati ule Hitler alivutwa zaidi na opera za Richard Wagner kuliko siasa.
Tangu mwisho wa 1908 alibadilisha vyumba alipokaa mara kwa mara akitafuta kupanga vyumba kwa bei nafuu zaidi; inaonekana matatizo ya pesa yaliongezeka. 1910-1911 alipaswa kuishi katika bweni la wanaume wasio na nyumba[2].
Tangu 1910 Hitler alikuwa na mapato madogo kwa njia ya kunakili picha alizouza kupitia watu walioishi pamoja naye katika bweni. Wengine waliouza picha kwa niaba yake walikuwa Wayahudi lakini tofauti na daktari wa mamake hawakupata usaidizi wowote baadaye waliteswa kama Wayahudi wote baada ya kuvamiwa kwa Austria 1938.
Hitler alisoma mengi wakati ule na hasa maandiko yaliyotangaza ubora wa mbari wa Kigermanik na chuki dhidi ya Wayahudi.
Mwaka 1913 alihamia Munich katika jimbo la BavariaUjerumani. Alikuwa amepokea urithi wa babake pia alitaka kujiondoa katika wajibu wa kufanya huduma ya lazima ya kijeshi katika Austria-Hungaria. Aliendelea kunakili picha na kuziuza kwenye maduka ya sanaa. Februari 1914 alikamatwa na polisi ya Bavaria na kupelekwa Austria lakini huko iliamuliwa hafai kwa huduma ya kijeshi akarudi Munich. Wakati wa kukaa Munich alisoma maandiko ya Houston Stewart Chamberlain kuhusu ubaguzi wa kimbari.

Mwanajeshi 1914 - 1918

Mwaka 1913 alihamia Munich katika jimbo la Bavaria (Ujerumani). Mnamo Agosti 1914, wakati wa mwanzo wa Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia, alijitolea kwa jeshi la Bavaria ambapo kutokana na bidii na ukakamavu wake alipanda cheo na kuwa praiveti. Mwisho wa vita mwaka 1918 alikuwa na cheo cha koplo.

Kuingia siasa

Baada ya vita alikosa kazi lakini aligundua kipawa chake cha kuhutubia watu, akajiunga na siasa na kuingia katika chama kidogo cha Nazi (NSDAP) alikopanda ngazi haraka.

Jaribio la mapinduzi 1923

Adolf Hitler (kulia) pamoja na dikteta wa Italia Benito Mussolini.
Hitler alivutwa sana na mfano wa Benito Mussolini, kiongozi wa kifashisti wa Italia, aliyefaulu mwaka 1922 kupindua serikali ya Italia kwa maandamano makubwa ya wafuasi wake kuelekea Roma.
Mwaka 1923 Hitler alijaribu kumwiga Mussolini kwa kupindua serikali ya jimbo la Bavaria - kama utangulizi wa kupindua serikali ya kitaifa huko Berlin- lakini alikamatwa na kuhukumiwa kwa uasi huo kifungo cha miaka mitano, ingawa alitumikia miezi tisa tu. Chama chake kilipigwa marufuku.
Hitler akiwa kijana aliwahi kusoma vitabu vya Mwingereza Chamberlain aliyedai kwamba kuna mbari mbalimbali za watu zenye tabia na thamani tofauti sana.
Akiwa gerezani aliandika kitabu kilichoitwa "Mein Kampf" ("Mapambano Yangu") alikojaribu kueleza imani na siasa zake. Humo alieleza pia chuki dhidi ya Wayahudi na itikadi yake ya ubaguzi wa kimbari.
Katika itikadi hiyo mbari ya juu ni watu wa Ulaya ya Kaskazini aliowaita "Waaria", na wale ambao ni duni zaidi ni watu weusi. Vikundi vingine vimo katikati. Lakini watu wabaya kabisa katika itikadi hiyo ni Wayahudi ambao ni wajanja wakuu upande mmoja, lakini hawana uwezo wa kuunda kitu kwa upande mwingine. Hivyo wanajaribu kwa ujanja wao kutawala dunia kwa kuiba fikra na mafanikio ya Waaria.

Kujenga chama

Baada ya kutoka gerezani alirudia siasa. Alijitahidi kushika utawala wa chama cha NSDAP akakubaliwa kuwa kiongozi mkuu. Ndani ya chama alianzisha vikosi viwili vilivyovaa sare vikifanya mazoezi kama wanamgambo na kuwa tayari kupigana na maadui wa kisiasa wakati wa maandamano.
Kikundi cha SA ("Sturmabteilung" - "Kikosi cha kushambulia") kilikuwa na watu wengi sana kikavuta hasa wanaume wasio na kazi waliovaa sare ya kahawia. Kikosi cha pili kilikuwa na watu wachache kikaitwa "SS" ("Schutzstaffel" - "Kikosi cha ulinzi") waliovaa sare nyeusi.
Chama chake hakikufaulu hadi 1929, wakati uchumi wa dunia pamoja na wa Ujerumani ulipoporomoka vibaya katika mdodoro mkuu. Mamilioni waliachishwa kazi na kuona njaa. Katika hali hiyo watu walianza kupigia kura vyama vyenye itikadi kali.
Katika uchaguzi wa mwaka 1930 kura za NSDAP ziliongezeka kutoka 2.6% hadi 18.3%. Serikali za Ujerumani zilikuwa za vyama vingi na dhaifu.
Mwaka 1932 chama cha NSDAP kilipata 33% za kura na kuwa chama chenye kura nyingi zaidi nchini na chama kikubwa katika bunge la Reichstag. Katika hali hiyo viongozi wa Dola la Ujerumani waliamua kumwingiza Hitler katika serikali mwaka 1933.

Chansela na kiongozi wa Ujerumani

Tarehe 30 Januari 1933 Hitler akawa Chansela wa Ujerumani. Mara moja alichukua nafasi kuwakandamiza wapinzani wake na baada ya mwaka mmoja hata wale waliomwingiza madarakani.
Baada ya mwaka mmoja utawala wake ulisimama imara kabisa ilhali wapinzani wengi walikamatwa na kupelekwa katika makambi ya KZ.
Hitler alifuata siasa ya kujenga uchumi na kurudisha watu kazini akibahatika kwamba uchumi wa dunia ukapaa tena.
Hitler alifuta mapatano yote ya Ujerumani yaliyoweka mipaka kwa ukubwa wa jeshi lake kuwa watu 100,000 tu akajenga jeshi kubwa zaidi, akaanzisha utawala wa kidikteta wa "Dola la Tatu" akipiga marufuku vyama vya upinzani. Alitesa wapinzani wote na watu wa mbari alizochukia, hasa Wayahudi.

Siasa dhidi ya Wayahudi

Chuki dhidi ya Wajerumani waliokuwa Wayahudi aliionyesha kwa sheria mbalimbali zilizokuwa kali zaidi na zaidi. Idadi ya Wayahudi katika Ujerumani ilikuwa ndogo, takriban nusu milioni kati ya wakazi milioni 62. Kila Mjerumani akitaka kuajiriwa na serikali au kupata nafasi ya masomo alitakiwa kuorodhesha wazazi na mababu hadi kizazi cha pili. Kwa njia hiyo Hitler alipanga Wajerumani wote katika vikundi vya "Waaria" (ambao hawana Wayahudi katika familia), "Wayahudi" (watu wenye asili ya Kiyahudi, hata kama wameshakuwa Wakristo tangu vizazi kadhaa au hawakufuata dini), "Wayahudi nusu" kama mzazi mmoja alikuwa Myahudi, "Wayahudi robo" kama mmoja kati ya mababu na mabibi wanne alikuwa Myahudi. Wayahudi na Wayahudi nusu walifukuzwa katika ajira ya serikali na walikataliwa kufanya kazi mbalimbali.
Sheria kuhusu "Aibu wa mbari" ilikataza ndoa kati ya "Waaria" na "Wayahudi"; "Wayahudi" waliondolewa uraia kamili.
Tokeo moja la siasa hiyo lilikuwa kuondoka kwa Wayahudi wengi kidogo katika Ujerumani; baada ya mashambulizi makali na mauaji mwaka 1938 mwelekeo huo uliongezeka. Hasa wanasayansi na wasanii wengi walihamia nchi huru.
Siasa yake katika mwaka 1939 ilisababisha Vita Kuu ya Pili ya Dunia.

Vita Kuu ya Pili

Behewa lililojaa maiti nje ya tanuri ya kambi la Buchenwald (Aprili 1945).
Hitler alifuata mwanzoni siasa ya kukusanya Wajerumani wote wa Ulaya katika Dola la Ujerumani.
Mwaka 1938 alifaulu kuteka Austria na maeneo ya Wajerumani katika Ucheki bila upingamizi wa kimataifa.
Lakini aliposhambulia Poland tarehe 1 Septemba 1939 tendo hili lilikuwa mwanzo wa Vita Kuu ya Pili ya Dunia kwa sababu Uingereza na Ufaransa walisimama imara kwa mikataba ya kusaidiana na Poland.
Wakati wa vita Hitler alichukua mwenyewe uongozi mkuu wa jeshi. Mwanzoni alifaulu hata dhidi ya ushauri ya majenerali wake, hasa wakati wa vita dhidi ya Poland na Ufaransa. Lakini maazimio yake ya 1941 ya kushambulia Urusi na kutangaza hali ya vita dhidi ya Marekaniyalikuwa mwanzo wa mwisho wake. Nguvu ya kiuchumi wa Ujerumani haikutosha kushindana na dunia yote.
Wakati wa vita aliamuru uuaji wa Wayahudi wote wa Ulaya, na inakadiriwa alifaulu kuwaua takriban milioni sita (2/3 ya Wayahudi wote wa Ulaya) pamoja na watu vya mbari mbalimbali kama Wasinti (kati ya 200,000 na 1,500,000).
Hasa alipoona ya kwamba vita dhidi ya Urusi haikufaulu haraka jinsi alivyotegemea aliamua kumaliza jambo lililosababisha chuki yake hasa. Azimio la "usuluhisho wa mwisho wa suala la Kiyahudi" lilichukuliwa mwisho wa mwaka 1941 na kutangazwa mbele ya viongozi wachache mnamo Januari 1942 katika Mkutano wa Wannsee.
Baadaye siasa ya kuwatenda Wayahudi vibaya na kuwaua katika maeneo fulani ilibadilishwa kulenga Wayahudi wote katika nchi zote zilizokuwa chini ya athira ya Ujerumani au kutekwa na jeshi lake. Hadi mwisho wa vita Wayahudi walikusanywa kutoka kote Ulaya na kupelekwa kwa reli hadi makambi ya mauti.

Mwisho wa vita na kifo

Gazeti la Marekani "Stars and Stripes" la tarehe 2 Mei 1945 latangaza kifo cha Hitler.
Maafisa wachache wa jeshi ya Ujerumani walipanga mara kadhaa kumwua Hitler. Tarehe 20 Julai 1944 alijeruhiwa na bomu ya Stauffenberglakini hakufa.
Tangu Januari 1945 Hitler alikaa katika boma imara chini ya ardhi kwenye ikulu yake mjini Berlin. Hakutoka mjini tena.
Tarehe 20 Aprili alishehereka mara ya mwisho sikukuu yake na kupokea wageni wachache. Siku iliyofuata vikosi vya kwanza vya jeshi la Urusi vilivuka mipaka ya Jiji la Berlin.
Tarehe 25 Aprili 1945 Berlin yote ilizungukwa kama kisiwa na jeshi la Wasovyeti na tangu 28 Aprili waliingia katika kitovu cha Berlin. Habari zilifika Berlin ya kwamba makamu wake Hitler kama Himmler na Goering walijaribu kutafuta mapatano na Marekani au Uingereza. Hitler aliwatangaza ni wasaliti akaamuru kuwakamata lakini amri hizi hazikutekelezwa tena maana hawakuwa karibu naye.
Katika hali hii Hitler alielewa ya kwamba hakuna njia ya kushinda na wataalamu hukubaliana ya kwamba hapo aliamua kujiua. Usiku wa 27 Aprili alimwoa mpenzi wake wa miaka mingi Eva Braun. Aliendelea kutunga wosia wake ambamo alimtaja mkuu wa jeshi la maji Karl Doenitzkuchukua madaraka yake kama mkuu wa dola na wa jeshi. Kwenye 29 Aprili jioni alipokea habari ya kwamba Benito Mussolini ameuawa huko Italia.
Tarehe 30 Aprili aligawa sumu kwa wote waliokuwa pamoja naye katika boma chini ya ardhi akawaruhusu kuondoka; aliagiza sumu ijaribishwe kwa mbwa wake mpendwa "Blondi". Mnamo saa 15.30 Eva Brau alijiua kwa kumeza sumu na Hitler alipigia risasi kichwani. Wasaidizi wa mwisho walibeba maiti hadi bustani ya ikulu na kuziweka katika shimo kutokana na mlipuko wa bomu; hapa wakazichoma kwa petroli.
Warusi waliingia saa chache baada ya vifo hivi. Walikuta maiti tarehe 5 Mei bila kutambua ni Hitler na Eva Braun. Tarehe 10 Mei msaidizi wa daktari wa meno wa Hitler aliweza kutambua maiti kutokana na meno. Mabaki yalizikwa baadaye karibu na makao makuu ya jeshi la Kirusi katika Ujerumani ya Mashariki; yalihamishwa mara kadhaa kila wakati makao makuu yalipohamishwa. Mwishoni mabaki ya maiti yalichomwa na Warusi tarehe 5 Aprili 1970majivu yalisagwa na yote kutupwa katika mto mdogo karibu na mji wa Magdeburg.
Taarifa hizi zilitunzwa kama siri kwa miaka mingi hadi mwisho wa Ukomunisti katika Urusi na hivi kulikuwa na uvumi wa kwamba Hitler hajafa na labda alikimbia hadi Amerika Kusini, jinsi idadi ya wasaidizi wake waliofaulu kutoroka.

No comments: