Tuesday 28 November 2017

Kuba

Kuba

-Kwa "kuba" (pia: kubba) kama sehemu ya jengo tazama Kuba (jengo)-
República de Cuba
Jamhuri ya Kuba
Bendera ya KubaNembo ya Kuba
BenderaNembo
Kaulimbiu ya taifa: KihispaniaPatria o Muerte
(„Taifa au mauti“)[1]
Wimbo wa taifa: "La Bayamesa" ("Wimbo la Bayamo")
Lokeshen ya Kuba
Mji mkuuHavana
23°8′ N 82°23′ W
Mji mkubwa nchiniHavana
Lugha rasmiKihispania
Serikali Jamhuri ya kijamii
Raul Castro
Uhuru
Kutoka Hispania
tangazo la Jamhuri ya Kuba
tarehe inayokumbukwa nchini Kuba

10 Oktoba 1868
20 Mei 1902
1 Januari 1959
Eneo
 - Jumla
 - Maji (%)

110,861 km² (ya 105)
negligible
Idadi ya watu
 - [[]] kadirio
 - 2013 sensa
 - Msongamano wa watu

(ya 73)
11,210,064
102/km² (ya 106)
FedhaPeso (CUC)
Saa za eneo
 - Kiangazi (DST)
EST (UTC-5)
(Starts 1 Aprili, end date varies) (UTC-4)
Intaneti TLD.cu
Kodi ya simu+53
-

Ramani ya Kuba
Kuba (pia: Kyuba; kwa Kihispania: Cuba) ni nchi ya kisiwanikatika Bahari ya Karibi kusini kwa Marekani.
Nchi inajumuisha kisiwa kikuu cha Kuba ambacho ni kisiwa kikubwa cha Antili Kubwa) pamoja na kisiwa cha Isla de la Juventud na visiwa vidogo vingine vingi.
Kuba ni nchi kubwa kati ya nchi za Karibi yenye wakazi wengi.
Utamaduni wake unaonyesha athari za historia yake kama kolonila Hispania kwa miaka mingi, pia ya wakazi wenye asili katika watumwa kutoka Afrika na ya kuwa jirani na Marekani.

Jiografia[hariri | hariri chanzo]

Kuba iko katika eneo ambako Bahari KaribiGhuba ya Meksiko na Atlantiki zinakutana.
Kisiwa kikuu kina urefu wa kilomita 1,250 na eneo la km² 104,556. Sehemu kubwa ni tambarare isipokuwa milima ya Sierra Maestra katika kusini magharibi inayofikia kimo cha mita 1,974.
Kisiwa cha pili ni Isla de la Juventud (Kisiwa cha Vijana) kilichoitwa Isla de Pinos (Kisiwa cha Misunobari) hadi mwaka 1978. Kisiwa hiki kina eneo la km² 2,200.
Kuba yote ina eneo la kilomita za mraba 110,860 pamoja na sehemu za bahari, nchi kavu peke yake ni km² 109,884.
Tabianchi ni ya kitropiki. Kuba inaguswa na mkondo wa bahari ya Karibi unaobeba maji fufutende kutoka ikweta. Majira makavu kiasi hutokea kati ya Novemba hadi Aprilimajira ya mvua zaidi kuanzia Mei hadi Oktoba.
Halijoto ya hewa ya wastani ni sentigredi 21°C katika Januari na 27°C wakati wa Julai. Halijoto ya juu ya maji ya Bahari Karibi na kwenye Ghuba ya Meksiko husababisha kutokea kwa dhoruba kali aina za tufani mara kadhaa kila mwaka.

Historia

Koloni la Hispania

Kuba ilikuwa koloni la Hispania kuanzia kufika kwa Kristoforo Kolumbus mwaka 1492 hadi mwaka 1898. Wenyeji asilia walikuwa Waindio lakini wengi wao walikufa haraka kutokana na magonjwa kutoka Ulaya na ukali wa ukoloni wa Wahispania.
Baadaye uchumi wa mashamba makubwa ya sukari ulijengwa kwa nguvu ya watumwa kutoka Afrika.
Kuanzia miaka ya 1860 watu wa Kuba walianza kupinga utawala wa Hispania na pia kudai mwisho wa utumwa. Mnamo 1898 manowari ya Kimarekani SS Maine ililipuka katika bandari ya Havana na tukio hili lilikuwa msingi kwa Marekani kutangaza hali ya vita dhidi ya Hispania. Marekani ilishinda katika Vita ya Marekani dhidi Hispania na kutawala kisiwa katika miaka iliyofuata.

Uhuru chini ya usimamizi wa Marekani

Baada ya majadiliano marefu Kuba ilipata uhuru wake kuanzia mwaka 1902 lakini ilipaswa kukubali mkataba uliotunza haki ya Marekani kungilia kati mambo ya ndani na kuipa Marekani eneo kwa kituo cha kijeshi.
Hadi mwaka 1934 Marekani iliingilia mara mbili na kupindua marais wawili wa Kuba, ama kwa kutuma jeshi lake au kwa kutumia wanajeshi wa Kuba. Eneo la Guantanamo Baykusini mwa Kuba limebaki hadi leo kama kituo cha kijeshi cha Marekani.
Mkataba mpya kati ya Marekani na Kuba wa mwaka 1934 uliongeza haki za Kuba. Wakati huohuo uasi wa kijeshi ulimwingiza sajenti Fulgencio Batista kwenye uwanja wa siasa. Batista alijipandisha cheo hadi kanali akashika mamlaka yote ya kijeshi na kuteua marais waliotekeleza matakwa yake.
Mwaka 1940 alichaguliwa mwenyewe kuwa rais, akarudi 1952 kwa kugombea tena urais lakini, baada ya kuona angeshindwa, alipindua serikali kwa njia ya uasi wa kijeshi akasimamisha katiba na kuwa dikteta wa Kuba hadi mwaka 1959. Chini ya serikali ya Batista ulaji rushwa na athira ya kiuchumi ya makampuni ya Kimarekani viliongezwa. Ukali wa utawala na mauaji ya wapinzani wengi vilisababisha kutokea kwa vikundi vilivyokuwa tayari kupinga serikali ya dikteta kwa silaha.

Mapinduzi ya 1959

Fidel Castro, kiongozi wa mapinduzi na wa nchi kwa miaka 49.
Tangu mwaka 1953 mwanasheria Fidel Castro alijaribu kukusanya wafuasi kwa mapinduzi akishambulia kituo cha kijeshi cha Moncada akakamatwa na kutupwa jela.
Mwaka 1955 wafungwa walisamehewa na Batista. Castro alianza tena kukusanya wafuasi waliobaki katika "Harakati ya 26 Julai" (MR-26-7). Maandamano ya upinzani yalifuatwa na polisi kukamata wanaharakati. Fidel Castor pamoja na nduguye Raul walikimbia Meksiko. Hapo alikutana na tabibu Mwargentina Che Guevara.
Mwaka 1956 Castro pamoja na Guevara na wafuasi 80 walivuka bahari kwa jahazi "Granma" wakajificha katika milima ya Sierra Madre. Kutoka huko walianza kushambulia vikosi vya jeshi la Batista.
Polepole idadi ya wapiganaji waliojiunga nao iliongezeka na wanajeshi wa serikali mara nyingi walihamia upande wa Castro. Tarehe 1 Januari1959 dikteta Batista alikimbia na kuondoka Kuba, vikosi wa wanamapinduzi waliingia Havana.

Baada ya mapinduzi

Mwanzoni Castro alionekana kama msemaji mkuu wa mapinduzi akimtangaza mwanasheria Manuel Urrutia kama rais mpya. Fidel alichukua cheo cha waziri mkuu katika Februari 1959.
Hapo mwanzoni serikali mpya ilikuwa muungano wa wapinzani wa udikteta na wanamgambo kutoka milimani. Uchaguzi wa vyama vingi ulitangazwa kama shabaha mojawapo ya kurudisha demokrasia. Katika miezi iliyofuata wanasiasa wenye mwelekeo wa kati waliondolewa polepole na Castro aliongeza idadi ya Wamarxisti katika vyeo vya juu.
Kuanzia 1960 na baada ya jaribio la Marekani kumpindua Castro huyu aliongeza mwelekeo wake wa kisoshalisti. Baada ya kupingwa na Marekani, Castro alitafuta ushirikiano na usaidizi kutoka Urusi wa kikomunisti.
Castro alitangaza siasa ya kikomunisti akaendelea kutawala bila uchaguzi huru hadi alipojiuzulu mnamo Februari 2008 kwa sababu za afya.

Watu

Wakazi wengi ni machotara. Vipimo vya DNA vimeonyesha kwamba Wazungu wameichangia 72%, Waafrika 20% na Waindio 8%.
Lugha rasmi na ya kawaida ni Kihispania. Inafuata Krioli ya Haiti.
Upande wa dini, baada ya serikali kuipinga vikali kwa miaka mingi, bado 59% ni Wakristo, hasa wa Kanisa Katoliki.

No comments: