Monday 20 November 2017

MWANAANGA

Neil Armstrong

Neil Armstrong
Neil Armstrong (5 Agosti 1930 — 25 Agosti 2012) alikuwa rubani mwanaanga wa Marekani aliyeshuka mwezini mwaka 1969, wa kwanza kabisa kati ya wanadamu wote.

Mwanaanga

Alizaliwa katika familia ya wakulima kwenye jimbo la Ohio tarehe 5 Agosti 1930.
Baada ya kumaliza shule alijiunga na jeshi ambako alipata mafunzo ya uhandisi na kuwa rubani. Mwaka 1952 alishiriki katika vita vya Korea.

Rubani wa majaribio

Mnamo mwaka 1955 aliajiriwa na taasisi ya mambo (shughuli za) (utafiti wa mambo) ya anga (NASA) kama rubani wa majaribio kwa aina mpya za ndege.
Mnamo mwaka 1958 alikuwa mmojawapo katika kundi la marubani waliotayarishwa kupelekwa kwenye anga la nje.

Mwanaanga

Baada ya kuundwa kwa NASA aliingia katika kundi la wanaanga. Safari yake ya kwanza ilikuwa 16 Machi 1966 kama mwanaanga kiongozi wa Gemini 8. Kilele cha safari hii ilikuwa kukutana kwa Gemini 8 na satelaiti nyingine na kuunganisha vyombo vyote viwili kwa muda wa masaa kadhaa.
Armstrong akiangalia chombo cha angani mwezini

Safari ya kwenda mwezini

Baadaye aliteuliwa kuwa makamu wa kikundi cha wanaanga waliokwenda mwezini kwa kutumia chombo kilichoitwa Apollo 11Ajali ya Apollo 1 iliyosababisha kifo cha mwenzake hapo kabla, ndiyo iliyompelekea kujiunga kwake na kundi la Apollo 11.
Tarehe 20 Julai 1969 Neil Armstrong pamoja na Edwin Aldrin waliutataga uso wa mwezi wakiwa wanadamu wa kwanza mwezini. Walitoka katika chombo cha angani na kutembea mwezini kwa mara ya kwanza. Picha hizo zilionyeshwa kote duniani kwa wakati huohuo. Akiwa katika hali hii, Armstrong alitamka maneno yafuatayo: "Hii ni hatua ndogo kwa mtu lakini hatua kubwa kwa ubinadamu."
Baada ya kurudi salama, Armstrong aliacha kazi katika NASA na badala yake akawa profesa wa uanaanga kwenye chuo kikuu cha Cincinnati katika mwaka 1971 hadi alipostaafu na kujishugulisha na biashara zake.

Mwanaanga

Mwanaanga Piers Sellers nje ya chombo cha space shuttle tar. 12 Juni 2006
Mwanaanga ni mtu anayerushwa katika anga la nje lililo nje ya angahewa ya dunia. Majina mengine yaliyokuwa kawaida ni "kosmonavti" (Kirusi космонавт) kwa wanaanga Warusi na "astronauti" (Kiing. astronaut) wa wanaanga kutoka Marekani. Wachina wametumia neno "taikonauti".
Mwanaanga wa kwanza katika historia ya binadamu alikuwa Mrusi Yuri Gagarin kutoka Umoja wa Kisovyeti aliyerushwa tarehe 12 Aprili 1961 kwa chombo cha angani Vostok akizunguka dunia lote mara moja katika muda wa dakika 108.
Alifuatwa 5 Mei 1961 na Alan Shepard kutoka Marekani aliyetumia chombo cha angani cha Mercury .
Mwanamke wa kwanza angani alikuwa Mrusi Valentina Tereshkova mwaka 1963.
Wanaanga wa kwanza waliofika kwenye uso wa mwezi walikuwa Wamarekani Neil Armstrong na Buzz Aldrin tar. 20 Julai 1969.
Hadi machi 2008 jumla ya watu 477 kutoka nchi 39 walifika kwenye kimo cha kilomita 100 juu ya uso wa dunia ambacho ni kimo ambako anga la nje linaanza kulingana na maelezo ya Shirikisho la Kimataifa kwa Usafiri wa Angani (Fédération Aéronautique Internationale (FAI)).
Kati ya hawa ni 24 waliofika mbali zaidi kuliko kilomita 2,000 juu ya uso wa dunia hadi njia ya mwezi kwenye anga.
Mwanaanga aliyekaa muda mrefu angani alkuwa Mrusi Sergei Krikalyov aliyefika angani mara sita akakaa jumla ya siku 803, masaa 9 na dakika 39 kwenye anga la nje.

Yuri Gagarin

Yuri Gagarin
Yuri Alexeyevich Gagarin (Kirusi Юрий Алексеевич Гагарин), alizaliwa tarehe 9 Machi 1934 huko Klushino karibu na SmolenskUrusi; alifariki tarehe 27 Machi 1968. Alikuwa mwanaanga wa kwanza katika historia yaani mtu wa kwanza aliyefika kwenye anga la nje.
Alimwoa Valentina Goryachova akawa na mabinti wawili ambao ni Galina na Yelena. Akajiunga na Jeshi la Anga la Urusi mwaka 1955.
Mwaka 1960 aliteuliwa katika kikosi cha kwanza cha marubani walioandaliwa kurushwa kwa anga la nje akateuliwa kuwa mtu wa kwanza wa kutoka duniani.
Tarehe 12 Aprili 1961 alirushwa na chombo cha angani Vostok 1 akizunguka dunia lote mara moja katika muda wa dakika 108. Akashuka Siberia.
Alipandishwa cheo na kuwa mkuu wa kituo cha kuandaa wanaanga Warusi. Mwaka 1968 alikufa katika ajali ya ndege alipofanya mazoezi ya urubani akazikwa kwenye makaburi ya heshima huko Moscow.
Picha za wanaanga

No comments: