Friday 24 November 2017

Jamii:Historia ya kale

Makala katika jamii "Historia ya kale"

M

  • Michoro ya miambani

    Michoro ya miambani

    WikiLettreMini.svgMakala hiyo kuhusu "Michoro ya miambani" inatumia neno ambalo si kawaida na matumizi yake ni jaribio kwa jambo linalotajwa.
    Wasomaji wanaombwa kuchangia mawazo yao.
    Kamusi za Kiswahili ama zinatofautiana kuhusu matumizi ya neno hili au hazieleweki au hazina neno kwa jambo linalojadiliwa.
    Michoro ya miambani huko Kondoa, Tanzania
    Michoro ya miambani (ing. rock art) ni jina kwa michoro ya aina mbalimbali iliyofanywa na wanadamu kwenye uso wa miamba asilia. Ni aina ya sanaa inayoweza kuwa na umri mkubwa sana.
    Wataalamu wa akiolojia hutofautisha kati ya
    • Petroglifi (ing. petroglyph) – zinazotokana na kukata nyufa kwenye uso wa mwamba
    • Piktografi (ing. pictograph) – zinazotokana na kutumia rangi juu ya mwamba, hasa kwenye michoro ya mapango.
    Michoro ya aina hii hupatikana katika mabara yote na nchi nyingi. Mfano mashuhuri ni Michoro ya Kondoa nchini Tanzania.
    Inapatikana kwenye uso wa mwamba unaosimama kama ukuta ama kwenye mtelemko mkali wa mlima au ndani ya mapango.
    Picha

Z

  • Zama za Chuma

    Zama za Chuma

    Vifaa vya chuma
    Zama za Chuma katika historia kilikuwa kipindi kirefu baada ya watu kuanza kutumia vifaa vya chuma. Kabla yake, walikuwa wakitumia vifaa vya shaba na awali mawe yaliyochongwa tu.
    Sehemu nyingi za UlayaAfrika na Asia walifikia Zama hizi za Chuma kunako mwaka wa 500 KK. Kwa upande wa Ulaya, ni kipindi cha kabla ya historia, kwa sababu watu wa Zama za Chuma hawakuwa wakiandika kumbukumbuzao.

    Uhunzi

    Chuma ni rahisi kukipata, lakini ni vigumu sana kukitengenezea vifaa. Inabidi kukiyeyusha kwa halijoto ya juu kuliko shaba. Watu waliojifunza namna ya kutengeneza vifaa kwa kutumia chuma walikuwa na uwezo wa kufanya vitu vingi sana kwa vyuma hivyo.
    Hii inamaanisha kwamba tabia za watu hubadilika. Kwa mfano, watu wengi wana uwezo zaidi wa kumiliki jembe la chuma. Wameweza kulima mashamba yao vizuri na mazao kukua vyema kabisa.
    Baadhi ya watu walibuni sarafu ili kusaidia kununua na kuuza mazao yao na vifaa vyao vya chuma.
  • Zama za Mawe

    Zama za Mawe

    Mawe yaliyochongwa kuwa na kona kali kwa matumizi kama kisu.
    Mtu wa zama za mawe akikata mti.
    Zama za Mawe zilikuwa kipindi kirefu cha historia ya kale ya binadamu. Watu walitumia vifaa vya mawe kwa shughuli zao za kila siku.

    Utamaduni wa watu kwenye chanzo cha zama za mawe

    Mwanzoni watu walidumisha maisha yao kwa kukusanya matundamizizi na kuwinda wanyama.
    Kwa umbile na akili yake binadamu ana uwezo wa kuwinda wanyama wakubwa kama chakula na kutumia ngozi yao kama mavaziya kujikinga dhidi ya baridi.
    Lakini meno na makucha yake hayafai kupasua ngozi ya mnyama mkubwa au kukata nyama yake vipande-vipande akitaka kubeba windo hadi mahali penye familia yake. Vilevile makucha hayafai sana kuchimba mizizi kwa chakula.
    Hapo binadamu aliweza kutumia vitu vinavyopatikana kiasili katika mazingira: jiwe lenye kona kali, tawi la mti lenye ncha kali pamoja na vipande vya mifupa. Hivyo vyote vilisaidia shughuli za kuchimba, kupasua na kukata.[1]
    Kuna mabaki mengi ya mawe yaliyochongwa kwa matumizi kama vifaa na mabaki hayo yamekuwa msingi wa jina "zama za mawe". Vifaa hivyo na mabadiliko yake vinaonyesha maendeleo katika maisha ya binadamu na kuongezeka kwa uwezo wake wa kupambana na mazingira yake.
    Kwa hiyo ni kipindi cha matumizi ya mawe yaliyochongwa kuwa vifaa baada ya kipindi ambako watu walitumia fimbo tu au mawe katika hali asilia na kabla ya kipindi ambapo watu walielewa namna ya kutumia metali.
    Kifaa cha mawe sahili - zama za mawe ya kale
    Shoka la mkononi - bapa pande mbili (mwishoni mwa Zama za mawe ya kale) - inaonyeshwa kutoka mitazamo mbalimbali

    Vipindi vya zama za mawe

    Wataalamu wa akiolojia wametambua ya kwamba vifaa vya mawe vinaonyesha tabia tofautitofauti.
    • Kuna vifaa sahili sana kama jiwe lililogongwa mara moja ili kipande kivunjike na ncha kali ipatikane.
    • Kuna pia vifaa vya mawe vinavyoonyesha maendeleo zaidi; vilifanyiwa kazi kwa siku kadhaa kiangalifu ili kunyoshwa, kung'arishwa na kutobolewa kwa kuweka pini.
    Kutokana na tofauti kubwa katika hali ya vifaa vya mawe wataalamu wanaona ya kwamba wanaonyesha historia ndefu ya maendeleo ya teknolojia ya kushughulikia jiwe ambako watu walianza kwa vifaa sahili na kuendelea kujifunza zaidi na kuboresha matokeo ya juhudi zao.
    Kwa hiyo wataalamu wengi wanatofautisha:
    Si tofauti katika ubora wa vifaa pekee, lakini kuna pia dalili nyingine zinazoonyesha ya kwamba watu walibadilisha maisha yao, namna ya kujipatia chakula na makazi.
    Kila mtu aliweza kugonga jiwe dhidi ya jiwe hadi ncha kali ilipatikana. Lakini mashoka ya mawe yaliyohitaji siku za kazi makinifu yanaonyesha kuwepo kwa jamii iliyokuwa na mafundi wa pekee walioweza kunyosha ufundi wao wakilishwa na wengine ni pia dalili ya biashara iliyofanywa hasa tukikuta vifaa vya jiwe fulani katika maeneo ambako jiwe hili halipatikani kiasili.
    Pamoja na matokeo mengine ya utafiti wa akolojia, kama vile mabaki ya makaburi, vyombo vya ufinyanzinyumba na vifaa vingine, wataalamu waliweza kupata picha ya undani zaidi kuhusu maisha na jamii ya watu wa zamani zile.
    Teknolojia ya kupunguza jiwe hadi kupata kisu chembamba - zama za mawe ya kati (Levallois)
    Matumizi ya ncha ya jiwe kwenye mkuki

    Vifaa vya mawe

    Zama za mawe ya kale

    Vifaa vya kwanza vilikuwa mawe yaliyokatwa upande mmoja ili kuwa na kona kali moja. Hatuwezi kujua kwa uhakika tukiona jiwe la aina hii kama kama ilikuwa tokeo la mgongano wa mawe katika mkondo wa maji mtoni au kutokana na kuanguka kwa jiwe kutoka mlimani au kama jiwe limepigwa kwa kusudi kwa jiwe lingine kwa shabaha ya kupata kona kali. Lakini mawe haya yalifaa kutumiwa kwa kukata pia si vigumu kuvitengeneza.
    Mifano ya kale kabisa ya mawe yaliyogongwa kwa mawe mengine kwa kusudi la kupata kona kali zimepatikana katika eneo la ziwa Turkana (leo nchini Kenya) yalitegenezwa miaka milioni 3.3 iliyopita[2].
    Ngazi iliyofuata ni mawe yaliyofanyiwa kazi zaidi hadi kuwa "shoka la mkononi". Hapo jiwe la kufaa lilipigwa na kupunguzwa pande zote mbili hadi kuwa na bapa pande mbili. Sehemu ya juu ilibaki bila ukali kwa kuishikilia mkononi. Kuna mahali ambako mabaki mengi ya mashoka haya ya mkononi yamepatikana katika hali mbalimbali: mawe yaliyopigwa kiasi, mawe yaliyovunjika vibaya na kutupwa, vipande vidogo vilivyopasuliwa wakati wa kuipa shoka umbo lake na kadhalika. Mahali pale panatazamwa kama karakana au viwanda vya kutengeneza vifaa vya mawe. Mahali mashuhuri katika Afrika ya Mashariki ni bonde la Isimila(karibu na IringaTanzania ya leo).

    Zama za mawe ya kati

    Kipindi hiki kinatazamwa kilianza miaka 300,000 iliyopita na kudumu hadi miaka 25,000 - 50,000 [3] iliyopita.
    Mabamba makali ya mawe yamefungwa katika ubao wa mundu ya kukatia majani au mazao
    Kipindi hiki kinaonyesha maendeleo ya teknolojia. Watu walianza kutumia pia vipande vidogo vikali vilivyopatikana wakati wa kupunguza jiwe. Vibanzi vikali vya mawe vilifungwa sasa kwenye pini ya ubao kwa gundi la miti. Kwa njia hii vifaa kama kisuchusa au mundu vilipatikana. [4]

    Matatizo ya lugha ya "zama za mawe"

    Zama za mawe zilikuwa vipindi virefu sana cha miaka elfu nyingi. Wataalamu wamegawanya zama hizi kwa vipindi mbalimbali kama Zama za mawe za kale na Zama za mawe za kati. Tofauti hizi zinaonekana kutokana na lakini wataalamu wa siku hizi wanaona ya kwamba mgawanyo huu ulitazama zaidi historia ya Ulaya isiyolingana na historia ya sehemu nyingine za dunia.
    Tatizo kuu la mafundisho ni ya kwamba ni kipindi cha teknolojia bila kuangalia pande nyingine za maendeleo ya kibinadamu.
    Kwa mfano chuma haikutumiwa huko Amerika hadi karne ya 16 na huko Pasifiki hadi karne ya 17. Hata hivyo jamii za Amerika kama Azteki au Wainka walikuwa na teknolojia nyingine mbalimbali na waliweza kudumisha miji mikubwa kushinda miji ya Ulaya ya wakati ule.
    Hata hivyo lugha ya "zama za mawe" imekuwa kawaida duniani na wataalamu wanaendelea kuitumia wakijua kasoro zake kwa sababu hadi hasa hakuna mawazo ya kufaa zaidi.
  • Zama za Shaba

    Zama za Shaba

    Moja ya silaha za kawaida za shaba wakati wa Zama za Shaba.
    Zama za Shaba - Muséum de ToulouseUfaransa.
    Zama za Shaba (kwa Kiingereza bronze age) kilikuwa kipindi cha historia ambacho watu walitengeneza vifaa vyao kwa kutumia metali ya shaba na baadaye bronzi yenye mchanganyiko wa metali mbili: vipande tisa vya shaba kwa kipande kimoja cha stani.
    Malighafi nyingine, kama mbao na mawe, zilikuwa zikitumika pia kwa zana, lakini shaba ilikuwa nzuri zaidi kwa kukatia na kuchongea, na ilikuwa rahisi sana kuitengenezea umbo la kitu.
    Zama hizo za Shaba hazikutokea wakati mmoja kila mahali, kwa sababu makundi tofauti ya watu walianza kutumia shaba kwa vipindi tofauti kabisa. Kwa mfano, Ulaya Magharibi Zama za Shaba ziliisha kunako miaka ya 2000 KK hadi 800 KK. Kumbe upande wa Mashariki ya Kati zilianza takriban miaka elfu moja nyuma.

No comments: