Monday 20 November 2017

Chombo cha angani

Chombo cha angani

Feri ya anga Atlantis ikiondokakwenye kituo cha anga MIR tarehe 4 July 1995
Chombo cha angani ni chombo kwa ajili ya usafiri katika anga a nje ya dunia yetu. Vyombo vya anga viko kwa kazi nyingi pamoja na mawasiliano, kubeba vifaa vya kutazama na dunia au hali ya hewa, kufanyia utafiti sayari nyingine au kusafirisha watu na mizigo.
Vyombo vingine vinaingia kwa muda mfupi tu juu ya angahewa bila kumaliza mzingo wa dunia. Vingine vinazunguka kwenye mzingo kwa muda mrefu hata miaka.
Chombo cha angani cha kwanza kilikuwa Sputnik 1 kilichorushwa na Umoja wa Kisovyeti mwaka 1957 na kuzunguka dunia kwa miezi 3. Kilifuatwa na chombo cha kimarekani Explorer 1 katika mwaka ufuatao.
Mtu wa kwanza kwenye anga la nje alikuwa Mrusi Yuri Gagarin aliyerushwa na Umoja wa Kisovyeti kwa chombo cha Vostok 1 tarehe 12 Aprili 1961 na kumaliza mzingo mmoja wa dunia. Marekani ilifuata 5 Mei 1961 kwa kumpeleka mwanaanga Alan Shepard nje ya angahewa lakini bila kumaliza mzingo kamili. Februari 1963 Mmarekani John Glenn alifaulu kutimiza mizingo 3 ya dunia.
Marekani iliendelea kuandaa safari ya kufika mwezini na kuwafikisha wanaanga Neil Armstrong na Buzz Aldrin mwezini tarehe 20 Julai 1969 kwa kutumia chombo cha Apollo 11.
Ilhali maandalizi ya safari za kupeleka watu kwenye anga la nje ni ghali sana bila kuleta faida kubwa kiuchumi au kisayansi kuna mamia vya vyombo vya anga vinavyozunguka dunia na kutekeleza kazi muhimu. Hivi huitwa pia satelaiti zikifuata mwendo wa kudumu wa kuzunguka dunia au kukaa mahali pamoja angani juu ya uso wa dunia. Utabiri wa hali ya hewa hutegemea data na picha kutoka vyomboanga. Sehemu ya majadiliano kwa simu na sehemu kubwa ya picha za televisheni hupita satelaiti, vilevile data za teknolojia kama GPS.
Vyomboanga vingine vinapewa kazi ya upelelezi angani hasa kukaribia sayari, kukusanya data zao na kuzituma duniani. Habari nyingi juu ya sayari za mfumo wa jua letuzimepatikana kutokana na upimaji uliotekelezwa na vyomboanga hivi. 
Je wajua 
Apollo 11 ilikuwa chombo cha angani cha kwanza kufikisha watu kwenye Mwezi

Apollo 11

A
Nembo ya Apollo 11
Apollo 11 ilikuwa chombo cha angani cha kwanza kufikisha watu kwenye Mwezi. Hii yote ilifanywa na NASA (Mamlaka ya Marekani ya Usafiri wa Anga). Kilirushwa angani mnamo 16 Julai 1969 kikibeba wanaanga watatu Neil ArmstrongBuzz Aldrin na Michael Collins.

Muundo wa Apollo 11

Chombo chenyewe kilikuwa na sehemu au moduli
  • moduli ya dambra (command module) penye vifaa vya kuendesha injiniusukani na sehemu walipokaa wanaanga wakati wa safari
  • moduli ya huduma (service module) penye injini, matangi ya fueli na oksijeni, vifaa vya mawasiliano
  • moduli ya feri ya mwezi yaani chombo cha kufikisha wanaanga wawili kwenye uso wa mwezi na kuwarudisha baadaye kwenye moduli ya jukwaa
Apollo 11.
Sehemu ya jukwaa pekee ilikuwa na oksijeni na shinikizo la hewa kama duniani na hapa wananga waliweza kukaa bila kuvaa suti za anga.

Apollo 11 mwezini

Baada ya kufika kwenye obiti ya kuzunguka mwezi, Amstrong na Aldrin waliingia katika feri iliyotenganishwa sasa na jukwaa na kufika mwezini.
Mnamo 20 Julai 1969 Armstrong na Aldrin walikuwa wanadamu wa kwanza kutua kwenye Mwezi wakati Collins akibaki kwenye obiti karibu na mwezi.
Baada ya masaa 22 feri iliruka tena na kuwarudisha kwenye moduli ya jukwaa. Wanaanga walihamia jukwaa na sehemu ya feri ilibaki katika obiti ya mwezi hadi kuanguka chini baadaye.

Kurudi duniani

Moduli za jukwaa na huduma zilielekea tena duniani. Katika obiti ya dunia moduli zote mbili zilitenganishwa ni jukwaa pekee iliyorudi duniani ikibeba wanaanga na kutua kwa msaada wa parachuti kwenye bahari ya Pasifiki takriban kilomita 24 kutoka manowari iliyowasubiri na kutuma helikopta kuwatoa nje ya maji.

No comments: