Wednesday 4 October 2017

HITORIA YETU

Afrika

Afrika duniani.
Afrika ni bara la pili duniani kwa ukubwa, likiwa na eneo la kilometa mraba 30,244,050 na wakazi bilioni 1.1 ambao ni takriban 15% za wakazi wote wa dunia (mwaka 2013[1]). Asia ndiyo bara pekee kubwa kushinda Afrika.

Jina

Afrika kutoka sateliti.
Neno "Afrika" limetokana na lugha ya Kilatini ya Waroma wa Kale.[2][3] Waroma kwa jina hilo hawakumaanisha bara lote bali eneo fulani katika Tunisia ya leo tu.
Inasemekana asili yake ni kabila la "Afrig" lililoishi sehemu zile,[4]lakini kuna pia maelezo mengine tofautitofauti.
Wakati huo Wagiriki wa Kale walitumia zaidi jina la Libya kwa ajili ya nchi kusini kwa Bahari ya Mediteraneo. Maeneo ya ndani kuelekea kusini mara nyingi yaliitwa kwa jina la "Ethiopia" linalomaanisha nchi ya watu weusiweusi (kwa Kigiriki"aithiops": aliyechomwa na jua).
Katika ramani za kale kutoka Ulaya maneno yote matatu ya "Afrika", "Lybia" na "Ethiopia" yanapatikana yakitumika kama jina la bara zima. Jina la "Afrika" limekuwa la kawaida kuanzia karne ya 16 BK.

Jiografia

Afrika imezungukwa na bahari karibu pande zote. Kuna kiungo chembamba cha nchi kavu upande wa kaskazini masharikina bara la Asia kwenye rasi ya Sinai [5] .
Upande wa kaskazini iko Bahari ya Mediteranea, upande wa mashariki kuna Bahari Hindi pamoja na Bahari ya Shamu na upande wa magharibi iko Bahari Atlantiki.
Kuna kisiwa kikubwa cha Madagaska na funguvisiwa mbalimbali.
Barani kuna nchi huru 54 zinazotambuliwa na Umoja wa Mataifa, maeneo 9 yenye hali ya pekee na madola mawili ambayo yanajitawala bila kutambuliwa kimataifa.
Kuna umbali wa kilomita 8,000 kutoka Ras ben Sakka nchini Tunisia (37°21' N, sehemu ya kaskazini kabisa) hadi rasi ya Cape Agulhas nchini Afrika Kusini (34°51'15" S, sehemu ya kusini kabisa)[6] .
Umbali ni 7,400 km kutoka upande wa magharibi (rasi ya Cape Verde, 17°33'22" W) hadi mashariki (Ras Hafun nchini Somalia, 51°27'52" E)[7].
Pwani yote ya Afrika ina urefu wa kilomita 26,000.
Nchi kubwa ya Afrika ni Algeria na nchi ndogo ni funguvisiwa vya Shelisheli katika Bahari Hindi.[8] Nchi ndogo Afrika bara ni Gambia.
Kijiolojia Afrika iko kwenye bamba la Afrika. Lile bamba la gandunia la Afrika linaenea mbali zaidi kuliko maeneo tunayotazama kuwa Afrika kijiografia, ni pamoja na maeneo chini ya bahari linapopakana na mabamba ya Ulaya-AsiaUarabuniUhindi na AustraliaAntaktikaAmerika ya Kusini na Kaskazini. Upande wa mashariki wa bamba la Afrika kuna ufa unaozidi kupanuka ikielekea kujitenga kutoka Afrika kama bamba la Somalia.

Tabianchi

Uoto barani Afrika
Tabianchi ya Afrika ni pana, kuanzia kanda za tropiki hadi kufikia maeneo ya nusu-aktiki (baridi) kwenye ncha za milima mirefu.
Nusu ya kaskazini ya bara ni jangwa au angalau yabisi. Sehemu za kati na za kusini zina maeneo ya savanna na kanda za msitu wa mvua.
Afrika ni bara lenye joto kuliko mabara yote na asilimia 60 za uso wake ni maeneo yabisi au jangwa. [9]

Nchi za Afrika


Wakazi

Mwanamke wa Benin.
Wataalamu wengi wanakubaliana kutambua Afrika kama asili ya binadamu wote walioko duniani. [10]
Mwaka 2010 idadi ya wakazi wa nchi zote za Afrika ilipita bilioni 1. Ni kwamba idadi yao imeongezeka sana katika miaka 40 iliyopita,ikipiku zile za Ulaya na Amerika.
Ilhali mwaka 1950 walikuwepo Waafrika milioni 229 pekee, idadi iliongezeka kuwa milioni 630 mwaka 1990 na milioni 1200 mnamo 2014[11] [12]
Hivyo asilimia ya watoto na vijana ni kubwa. Kuna nchi kadhaa ambako zaidi ya nusu ya wananchi wako chini ya umri wa miaka 25.[13] Wakazi wa Afrika ni vijana kuliko wale wa mabara mengine yote;[14][15] mwaka 2012 umri wa wastani ulikuwa miaka 19.7, wakati kidunia ulikuwa 30.4.[16]

Lugha

Makala kuu: Lugha za Afrika
Ramani ya lugha za Afrika:     Lugha za Kiafrika-Kiasia     Lugha za Austronesia     Lugha za Kihindi-Kiulaya     Lugha za KhoisanLugha za Kikongo-Kiniger:     Lugha za Kibantu     Lugha za Kisudani za Kati na Mashariki     Central Bantoid     Eastern Bantoid     Guinean     Lugha za Kimande     Western BantoidLugha za Kinilo-Sahara:     Kanuri     Nilotic     Lugha za Kisonghai
Zaidi ya lugha elfu za Kiafrika zinazungumzwa barani leo, ingawa nyingi zinazidi kufifia.
Kusini mwa AfrikaAfrika Mashariki na ya Kati watu wengi ni wasemaji wa lugha za Kibantu (kwa mfano Kiswahili). Asili yao ilikuwa pande za kusini za kanda ya Sahel na kutoka kule walienea katika sehemu nyingi za Afrika upande wa kusini kwa Sahara.[17]
Kuna pia vikundi vya wasemaji wa lugha za Kinilo-Sahara waliofika hadi Afrika ya Mashariki.
Wakazi asilia siku hizi wako wachache, wakionekana kama wasemaji wa lugha za Khoisan au za Wabilikimo.[18]
Watu wa Afrika Magharibi husema zaidi Lugha za Kiniger-Kongo hasa zisizo za Kibantu, pamoja na wasemaji wa lugha za Kinilo-Sahara.
Watu wa Afrika ya Kaskazini kiasili walikuwa hasa wa makundi matatu:
  • Waberber upande wa magharibi
  • Wamisri upande wa mashariki
  • wasemaji wa lugha za Kinilo-Sahara
Waarabu waliovamia eneo hilo lote tangu karne ya 7 BK wameleta lugha yao pamoja na dini ya Uislamu. Lugha yao imekuwa lugha ya watu wengi siku hizi. Wasemaji wa Kiberber bado wako wengi kidogo Moroko na Algeria na wachache katika sehemu za Tunisia na Libya.[19]
Kutokana na ukolonilugha za Kihindi-Kiulaya zinazumgumzwa pia, hasa KiingerezaKifaransa na Kireno.
Kiafrikaans ni lugha ya pekee ya Afrika Kusini yenye asili ya Ulaya.
Katika kisiwa cha Madagaska kwenye Bahari ya Hindi, inatumika lugha ya Kimalagasy, ambayo ni kati ya lugha za Austronesia.

Dini

Makala kuu: Dini barani Afrika
Ramani ya dini barani Afrika.
Waafrika wana imani za dini nyingi tofauti, lakini takwimu zinazotolewa hazina hakika, pia kwa sababu suala hilo ni nyeti kisiasa kwa serikali zenye mchanganyiko mkubwa wa watu, kama vile NigeriaEthiopia na Tanzania.[20][21]
Kadiri ya World Book EncyclopediaIslam ndiyo inayoongoza, ikifuatwa na Ukristo. Kumbe kadiri ya Encyclopedia Britannica, 45% za wakazi ni Wakristo, 40% ni Waislamu na 10% wanafuata dini asilia za Kiafrika. Wachache tu ni WahinduWabuddhaWabaha'i au hawana dini yoyote.

KATIKA HITORIA YA AFRIKA
Historia ya Afrika
Hapo kale, bara la Afrika lilishuhudia matukio mengi ya harakati za mwanadamu kuliko mabara mengine ya ulimwengu.
Wataalamu wa athari wamegundua athari za zamadamu zinazorudi nyuma kufikia hadi miaka milioni minne, na athari za ustaarabu wa Wamisri wa Kale huko Misri na Wafoinike huko Tunis na sehemu nyinginezo za Afrika ya Kaskazini katika karne ya 9 KK.
Harakati za madola makubwa ya Warumi na Waarabu ziliweza kuonekana kabla ya karne ya 4 BK, na Waarabu walianza kuingia Afrika huko Habasha (Ethiopia) tangu karne ya 7 BK na kutangaza dini ya Uislamu na kuieneza katika maeneo mbalimbali ya Afrika pamoja na kuanzisha biashara na ustaarabu na kuimarisha mamlaka zao katika Sudan ya wakati huo tangu karne ya 8 baada ya Kikristo.
Himaya za GhanaMali, na Songhai zilikuwa zikijulikana kwa utajiri mkubwa na biashara stawi iliyokuwa ikifanyika wakati huo ya dhahabu na bidhaa nyinginezo. Mwisho wa karne ya 15 BK, himaya ya Songhai ilikuwa na nguvu kuweza kuitia chini ya utawala wake mamlaka ya Mali. Sehemu nyingine za kusini mwa Afrika zilikuwa wakati huu hazijulikani sana, na historia yake ilikuwa bado haijasajiliwa.
Baina ya karne ya 1 KK na karne ya 16 BK watu waliokuwa wakizungumza lugha ya Kibantu watokao sehemu za Nigeria na Cameroon ya leo, ndio waliokuwa wameenea kwenye sehemu mbalimbali kusini mwa bara la Afrika, wakiwa wameanzisha vijijimashamba na mamlaka katika sehemu za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ya leo, za Luba na Mwememutapa, lakini makundi ya wachungaji wa wanyama walianza kuhamia kusini katika karne za 15 na 16 na kukutana na Wabantu. Ndipo walipoanzisha mamlaka zao za BunyoroBugandaRwanda na Ankole.

Ukoloni

Wazungu walianza kugundua bara la Afrika katika karne ya 15, wakati Wareno walipokuja kwenye fukwe za bara la Afrika kutafuta njia nyepesi na ya amani ya kufikia India, na kuweza kupata nafasi ya kushikilia biashara ya dhahabu na pembe na watumwa ambayo ilikuwa ikiendelea wakati huo katika bara la Afrika. Katika mwaka 1488 Bartolomeo Dias alizunguka Rasi ya Tumaini Jema (kwa Kiingereza: Cape of Good Hope), na katika mwaka 1498 Vasco da Gama alifika ufukwe wa Afrika Mashariki na kuendelea mpaka India.
Baada ya hapo, Ureno ulianzisha vituo vya biashara Afrika, ukifuatiwa na WaholanziWaingerezaWafaransa na Wazungu wengineo, na biashara ya watumwailiyosimamiwa na Waarabu na baadhi ya Waafrika wenyewe ikashika kani na kuwa na kasi na nguvu.
Wakati huohuo Waturuki walishikilia sehemu za kaskazini ya Afrika na Waomani wakashikilia ufukwe wa Afrika Mashariki.
Kati ya miaka 1880 na 1912, Wazungu waligawana bara la Afrika, na nchi zote zikawa chini ya utawala wa Wazungu isipokuwa Liberia na Ethiopia.
Wafaransa wakachukuwa Afrika Magharibi na Kaskazini na kwa hivyo nchi za Afrika Magharibi: Dahomey (sasa Benin), GuineaMaliCote d'IvoireMauritaniaNigerSenegal na Volta ya Juu (sasa Burkina Faso) zilikuwa chini ya utawala wake. Hali kadhalika, AlgeriaTunisia na Morocco zilitawaliwa na wao. Aidha, Wafaransa walitawala TogolandSomalilandMadagascarComoro, na Reunion.
Waingereza nao wakatawala Afrika Mashariki na Kusini, na kuwa sehemu ya Sudan na SomaliaUgandaKenyaTanzania (chini ya jina la Tanganyika), ZanzibarNyasalandRhodesiaBechuanalandBasutoland na Swaziland chini ya utawala wao na baada ya kushinda katika vita huko Afrika ya Kusini walitawala TransvaalOrange Free StateCape Colony na Natal, na huko Afrika ya Magharibi walitawala GambiaSierra Leone, the Gold Coast na Nigeria.
Wareno wakachukuwa sehemu ya GuineaAngola na Msumbiji na sehemu na visiwa fulanifulani huko Afrika ya Magharibi.
Wabelgiji wakachukua Kongo na Rwanda-Urundi, na Wahispania wakachukua sehemu ya Guinea, Spanish Sahara (sasa Sahara ya Magharibi), Ifni na sehemu nyingine za Morocco.
Wajerumani nao wakachukua Togoland, Cameroon na baadhi ya nchi katika Afrika ya Magharibi na Afrika ya Mashariki, lakini baada ya vita vya kwanza vya duniawakanyang'anywa.
Waitalia wakachukua LibyaEritrea na sehemu kubwa ya Somalia.

Uhuru

Nchi ya kwanza kujitawala upya katika Afrika ni nchi za Afrika ya Kusini zilizojiunga na kujiendesha wao wenyewe katika mwaka 1910. Misri, katika mwaka wa 1922walikuwa wanajiendesha wenyewe, na Tangier katika mwaka wa 1925.
Madola mengi ya Afrika yalianza kupigania uhuru katika miaka ya baina ya 1950 na 1960, na Wazungu wakasalimu amri na kuanza kutoa uhuru. Libya wakajinyakulia uhuru katika mwaka wa 1951, Eritrea katika mwaka 1952 ikiwa imejiunga na Ethiopia, Morocco katika mwaka wa 1956, na wakarudishiwa Tangier.
Katika mwaka huu wa 1956, Sudan na Tunisia vile vile walipata uhuru wao, na Ghana katika mwaka wa 1957, Guinea katika mwaka wa 1958, na vile vile Morocco wakarudishiwa Spanish Morocco.
Katika mwaka wa 1960 Ufaransa ukatoa uhuru kwa Cameroon, Jamhuri ya Afrika ya KatiChad, Congo (Brazzaville), Cote d'Ivoire, Dahomey (Benin), Gabon, Madagascar, Mali, Mauritania, Niger, Senegal na Volta ya Juu (Burkina Faso).
Vile vile, katika mwaka huohuo wa 1960 Congo (Kinshasa), Nigeria, Somalia, na Togo zikapata uhuru, na katika mwaka wa 1961 Sierra Leone na Tanganyika zikapata uhuru, na Afrika ya Kusini ikawa Jamhuri.
Katika mwaka wa 1962 Algeria, BurundiRwanda, na Uganda zikawa huru, na 1963 zikafuatia Zanzibar, Gambia na Kenya, na katika mwaka wa 1964 Malawi (Nyasaland), na Zambia (Rhodesia ya Kaskazini) zikapata uhuru.
Baada ya miaka miwili, katika mwaka wa 1966 Botswana (Bechuanaland) na Lesotho (Basutoland) zikajinyakulia uhuru. Mauritius na Swaziland katika mwaka wa 1968 na vile vile Guinea ya Ikweta. Hispania ikairudisha Ifni katika mwaka wa 1969 katika mamlaka ya Morocco.
Aidha, katika mwaka wa 1974 Guinea ya Kireno (Guinea-Bissau) ikapata uhuru wake, na katika mwaka wa 1975 Angola, Cape Verde, Mozambique, Sao Tome na Principe zikapata uhuru. Hispania vilevile ikaitoa Sahara ya Magharibi kwa Morocco na Mauritania katika mwaka wa 1976, lakini wananchi wakakataa kuwa chini ya nchi mbili hizi, kukazuka vita. Mauritania ukaitoa sehemu yake na kuipa Morocco katika mwaka wa 1979, tatizo ambalo mpaka sasa linaendelea baina ya Morocco na Sahara ya Magharibi, na Umoja wa Mataifa unajaribu kutatua tatizo hili. Waingereza wakawapa uhuru Shelisheli katika mwaka wa 1976, na Ufaransa ukatoa uhuru kwa visiwa vya Ngazija (Comoro).
Katika mwaka wa 1977 Jibuti (Nchi ya Afars na Issas) iliyokuwa ikitawaliwa na Wafaransa ikarudi kwa wenyewe. Rhodesia (Zimbabwe) ikapata uhuru halisi mwaka wa 1980, na South West Africa, iliyokuwa ikitawaliwa na Afrika ya Kusini ikapata uhuru katika mwaka 1990 na kuitwa Namibia.
Uingereza umebaki na visiwa vya Saint Helena na Ascension, na Ufaransa unaendelea kutawala Mayotte na Reunion. Hispania vilevile unaendelea kutawala visiwa vya Canarias pamoja na Ceuta na Melilla na visiwa viwili vingine vilivyoko karibu na Morocco.
NCHI ZILIZO PATA UHURU  

Nchi ya kimabara

Nchi ya kimabara ni nchi yenye eneo kwenye bara mbili au zaidi.
Mifano yake ni:
Nchi kadhaa yana maeneo ya ng'ambo kama urithi wa uenezi wa kikoloni, hasa kama wakazi wa maeneo yasiyopewa uhuru wamezoea au kukubali kabisa kuendelea kama raia wa nchi iliyokuwa mkoloni zamani.
Mifano yake ni:

No comments: