Jamii:Historia ya Israeli
Vijamii
Jamii hii ina vijamii 2 vifuatavyo, kati ya jumla ya 2.
W
- Jamii hii ina kurasa 8 zifuatazo, kati ya jumla ya 8 A
-
Ahabu
Ahabu (kwa Kiebrania: אַחְאָב, Aẖ'av, ʼAḥʼāḇ), mwana wa Omri, alikuwa mfalme wa saba katika ufalme wa Israeli. William F. Albright alikadiria utawala wake kuwa miaka 869–850 KK, E. R. Thiele miaka 874–853 KK[1] na Michael D. Coogan miaka 871–852 KK.[2].
D
- Daudi (Biblia)
Daudi (Biblia)
Daudi (kwa Kiebrania דוד, Daud, kwa Kiarabu داوُد, Dāwūd) alikuwa mfalme wa pili wa Israeli ya Kale mnamo 1010 KK-970 KK. Alimfuata mfalme Sauli akafuatwa na Suleimani.Kama kijana alipelekwa kwenye jumba la mfalme Sauli alipopanda ngazi na kuwa kiongozi wa kijeshi.Kati ya matendo yake yaliyokumbukwa zaidi ni ushindi juu ya Mfilisti Goliathi.
H
- Herode Mkuu
Herode Mkuu
Herode Mkuu (73 KK hivi - 4 KK) ni jina la heshima linalotumika kumtajia mtu maarufu zaidi wa ukoo wa kifalme wa Yudeakatika karne ya 1 KK, yaani Herode (kwa Kiebrania הוֹרְדוֹס, Hordos, kwa Kigiriki: Ἡρῴδης, Hērōdēs).[1][2][3][4][5]Akiwa kwa asili mtu wa kabila la Waedomu upande wa baba na Myahudi upande wa mama, alitawala Yudea yote chini ya himaya ya Dola la Roma.Mkatili hasa, aliua hata mke wake mmojawapo na watoto watatu.Ingawa alifuata dini ya Uyahudi na kuanza kazi kubwa ya kupanua na kupamba hekalu la Yerusalemu, alizingatia zaidi ustaarabu wa Kigiriki na kuendeleza miji kipagani.Ni maarufu zaidi kutokana na taarifa za Injili ya Mathayo kuhusu jinsi alivyopokea kutoka kwa Mamajusi habari ya kuzaliwa kwa Mfalme wa Wayahudi, Yesu. Kwa hofu yake aliposhindwa kumtambua mtoto huyo, aliagiza wauawe watoto wote wa kiume chini ya umri wa miaka 2.Yaliyomo
[ficha]Familia[hariri | hariri chanzo]
Familia ya Herode Mkuu Mke Watoto Doride - Antipatro, alifariki 4 KK
Mariamne I - Aleksanda, alifariki 7 KK
- Aristobulo, alifariki 7 KK
- Salampsio
- Cypro
Mariamne II - Herode II, alifariki 6
- Herode Filipo
Malthace - Arkelao, mfalme mdogo wa Yudea
- Herode Antipa, mfalme mdogo wa Galilaya
- Olimpia
Kleopatra wa Yerusalemu - Herode Filipo II, mfalme mdogo wa Perea
- Herode
Pallade - Fasaele
Fedra - Rossane
Elpide - Salome
M
- Mfalme Sauli
Mfalme Sauli
.Mfalme Sauli (1079 KK hivi hadi 1007 KK) anajulikana na Biblia na Kurani kama mfalme wa kwanza wa Israeli (labda kuanzia 1049 KK hadi kifo chake, yaani kwa muda wa miaka 42).Sauli (kwa Kiebrania שָׁאוּל, Šāʼûl, "aliyeombwa"; kwa Kigiriki Σαούλ, Saoul; kwa Kiarabu طالوت, Ṭālūt), alipakwa mafuta na Samweli awe mfalme, lakini akaja kukataliwa kwa kukosa utiifu kwa Mungu na kwa kutokubali kukosolewa na nabii wake.Habari zake katika Vitabu vya Samweli[hariri | hariri chanzo]
Vitabu viwili vya Biblia ya Kikristo vinaitwa kwa jina la mtu huyo, ambaye kwa njia yake taifa la Israeli lilianza kuwa na umoja zaidi na hatimaye kuwa ufalme. Badala ya kila kabila kujitegemea, yote 12 yalikubaliana yawe na kiongozi mmoja wa kudumu ambaye cheo chake kirithiwe na mwanae. Kwa umoja huo waliweza kushinda maadui wao wengi.Vitabu hivyo vimekusanya kumbukumbu zote kuhusu mwanzo wa ufalme (1070-972 hivi K.K.), yaani kuhusu Samwelimwenyewe na wanaume wawili aliowapaka mafuta watawale Israeli kwa niaba ya Mungu: kwanza Sauli, halafu Daudi. Kumbukumbu hizo zilizokusanywa zilikuwa nyingi na tofauti, hivyo tunakuta humo tata nyingi kuliko katika vitabu vingine vyote vya Biblia. Hasa mna hoja za kukubali mfumo wa ufalme na hoja za kuukataa.Samweli aliwaamua Waisraeli kwa kuwakomboa mikononi mwa Wafilisti (1Sam 7), lakini ni muhimu hasa kwa kuwaanzishia ufalme kwa kuwaweka wakfu kwanza Sauli halafu Daudi. Kadiri ya 1Sam 8, yeye na Mungu hawakupendezwa na jinsi Waisraeli wengi walivyotaka kuiga mtindo wa mataifa yote: Samweli aliwaangalisha kuhusu matatizo na unyonyaji wa wafalme, naye Mungu aliona katika ombi hilo uasi ambao Waisraeli wanamkataa asiwatawale tena, lakini akamuagiza Samweli awakubalie.Ukweli ni kwamba mfalme aliwekwa wakfu kwa Mungu kama mwakilishi wake akitakiwa kutimiza matakwa yake, hasa kwa kusikiliza anamuambia nini kwa kinywa cha manabii wake. Ndiyo sababu Samweli alizidi kumuelekeza Sauli, na hatimaye akamkataa kwa ukaidi wake. Mabishano kati ya Samweli na Sauli ni mwanzo wa mabishano yote kati ya manabii na wafalme ambao hawakutaka kumtii Mungu, na hatimaye wakadhulumu na kuua manabii wake.Mamlaka ya neno la Mungu lililoletwa na nabii ilitakiwa kuwa juu ya mamlaka ya serikali na nguvu ya kijeshi alivyokuwa navyo mfalme. Lakini mara nyingi wafalme, kwa kujivunia cheo chao, walishindwa kumnyenyekea nabii wa Mungu, wakaona afadhali kufuata manabii wengine wengi waliosema uongo ama kwa kudanganywa na matarajio yao ama kwa kujipendekeza kwa mfalme na kwa taifa lote.1Sam 9:11-10:16 inasimulia Sauli alivyoteuliwa kuwa mfalme wa kwanza. Akitawala karibu miaka ishirini, alifanya makosa na kulaumiwa na Samweli, hata akakataliwa kabisa na Mungu kwa kutomtii kikamilifu (1Sam 15). Ingawa akaendelea kutawala kwa muda fulani, polepole alijitokeza kijana Daudi ambaye akaja kuanzisha ukoo wa kifalme wa milele.1Sam 16-17 inaanza kutuletea mkusanyo wa hadithi juu ya Daudi ambazo zinampatia sifa aliyostahili, ingawa nyingine zinagongana: k.mf. kama aliingia katika utumishi wa Sauli kutokana na uhodari wake katika muziki au katika vita. Uhodari huo wote ukaendelea kusifiwa ila Daudi aliutumia kwa utukufu wa Mungu: ndiye aliyeingiza alambalimbali katika ibada na kutunga zaburi kadhaa, na ndiye aliyeeneza utawala wa Israeli kuliko yeyote.Kadiri alivyozidi kupendwa na Mungu na watu, Sauli alimchukia kwa kijicho na kutaka kumuua (1Sam 18:6-16). Daudi alipolazimika kukimbia na kuunda kikosi chake akapata nafasi rahisi ya kumuua Sauli lakini alijizuia kwa kuheshimu krisma aliyopakwa awe mfalme (1Sam 24 na 26): hivyo ni mfano bora wa kujali wito wa Kimungu.Hatimaye Sauli alijiua vitani kwenye mlima Gilboa, alipoona ameshindwa kama alivyotabiriwa kwa adhabu ya Mungu.
S
- Solomoni
Solomoni
Mfalme Solomoni kadiri ya Biblia alikuwa mfalme wa tatu na wa mwisho wa Israeli nzima, akitawala kuanzia 970 KK hadi 930 KK hivi.Maisha yake[hariri | hariri chanzo]
Daudi alimchagua kuwa mrithi wake kwa sababu alikuwa uthibitisho hai wa msamaha aliopewa na Mungu kwa kuzini na hatimaye kumuua Uria.Ufalme wake ulitazamwa na Wayahudi kuwa na ustawi usio na mfano, kutokana na hekima yake na amani iliyopatikana wakati wote wa utawala wake.Ufalme wake uliweza kustawi kuliko ule wa baba yake kutokana na msingi imara aliouweka Daudi. Lakini mwenyewe aliudhoofisha na kusababisha mara baada ya kifo chake utokee utengano kati ya makabila ya Kaskazini na yale ya Kusini.Kati ya kazi muhimu alizozifanya, mojawapo ni kujenga hekalu la Yerusalemu na kuliweka wakfu kwa sherehe kubwa ya siku saba, ambapo Mungu alionyesha kibali chake kwa kulijaza kwa sura ya wingu (1Fal 8). Polepole hekalu hilo likaja kuwa la pekee hata patakatifu pengine pote pakakatazwa chini ya mfalme Yosia.Ingawa Solomoni anasifiwa kwa hekima yake, alishindwa kukwepa majivuno na tamaa, akataka kuwapendeza wake zake waliokuwa 700 (mbali na masuria 300), wengi wao Wapagani, hata akawajengea mahali pa kuabudia miungu yao akamchukiza Mungu hata akamtabiria mtoto wake atanyang’anywa sehemu kubwa ya ufalme (1Fal 11:1-13) ikawa hivyo.Hata hivyo mwishoni aliweza kulaumiwa kwa kuzidisha fahari, hasa upande wa wanawake waliomvuta kwenda kinyume cha imani ya Mungu pekee.Sala zake[hariri | hariri chanzo]
"Nipe mimi mtumwa wako moyo wa adili niwahukumu watu wako, na kupambanua mema na mabaya; maana ni nani awezaye kuwahukumu hawa watu wako walio wengi"? (1Fal 3:9)"Ee Bwana, Mungu wa Israeli, hakuna Mungu kama wewe, mbinguni juu wala duniani chini! Ushikaye maagano na rehema kwa watumishi wako, waendao mbele zako kwa mioyo yao yote". (1Fal 8:23)Baada ya kifo chake[hariri | hariri chanzo]
Kwa sababu hiyo, ufalme ulivunjika pande mbili mara baada ya kifo chake.Hata hivyo, Wayahudi waliendelea kumuona kama kielelezo cha hekima, wakaandika vitabu kwa kutumia jina lake au kwa kujifananisha naye.Yesu alijitangaza kuwa mkuu na mwenye hekima kuliko Solomoni.
Y
- Yehu
Yehu
Yehu (kwa Kiebrania יֵהוּא, Yēhû, maana yake: "YHWY ni mwenyewe"[1] ) alikuwa mfalme wa kumi wa Israeli baada ya Yeroboamu I.Ni maarufu kwa kuangamiza ukoo wa Ahabu ili kuokoa imani ya Mungu pekee iliyokaribia kutoweka kwa juhudi za malkia Jezebeli. Hivyo alikamilisha kazi ya manabii Elia na Elisha.Hata hivyo Biblia inamlaumu kama waandamizi wote wa Yeroboamu I kwa kuvumilia mahekalu mbadala ya Betel na Dan.William F. Albright alikadiria ufalme wake kudumu miaka 842–815 KK, wakati E. R. Thiele alikadiria miaka 841–814 KK.[3] - Yeroboamu I
Yeroboamu I
Yeroboamu I (kwa Kiebrania ירבעם השני au יָרָבְעָם; kwa Kigiriki Ιεροβοάμ; kwa Kilatini Jeroboam) alikuwa mwana wa Nebatiakatawala kwa miaka 22 Ufalme wa Israeli baada ya makabila 10 ya kaskazini kuasi ukoo wa Daudi wakati wa mjukuuwake Rehoboamu.Biblia inamhukumu hasa kwa kuanzisha sera ya kidini iliyowataka Waisraeli wamuabudu YHWH kwa sura ya fahali ya dhahabu katika mahekalu ya Dani na Beteli ili wasiende Yerusalemu, mji mkuu wa ufalme wa ukoo wa DaudiYaliyomo
[ficha]Historia[hariri | hariri chanzo]
William F. Albright alikadiria ufalme wake kudumu tangu mwaka 922 KK – hadi 901 KK, wakati E. R. Thiele alisema kuwa alitawala tangu 931 KK hadi 910 KK.[1]Katika Biblia[hariri | hariri chanzo]
Agano la Kale linamtaja mara nyingi kama chanzo cha dhambi kuu ya Waisraeli ambayo hatimaye ilisababisha ufalme uangamizwe na Waashuru katika karne ya 8 KK. - Yeroboamu II
Yeroboamu II
Yeroboamu II (kwa Kiebrania ירבעם השני au יָרָבְעָם; kwa Kigiriki Ιεροβοάμ; kwa Kilatini Jeroboam) alikuwa mwana na mwandamiziwa Yehoashi wa Israeli kama mtawala wa 14 wa Ufalme wa Israeli, ambao aliuongoza kwa mafanikio makubwa miaka 41.Hata hivyo Biblia haisisitizi mafanikio hayo, bali inamhukumu kwa kufuata sera ya kidini ya Yeroboamu I iliyowataka Waisraeli wamuabudu YHWH kwa sura ya fahali ya dhahabu katika mahekalu ya Dani na Beteli ili wasiende Yerusalemu, mji mkuu wa ufalme wa ukoo wa DaudiYaliyomo
[ficha]Historia[hariri | hariri chanzo]
William F. Albright alikadiria ufalme wake kudumu tangu mwaka 786 KK – hadi 746 KK, wakati E. R. Thiele alisema kuwa alitawala pamoja na baba yake tangu 793 KKhadi 782 KK, halafu peke yake hadi mwaka 753 KK.[1]Alishinda Syria (2Fal 14:26, 27), aliteka Damasko (14:28), na kurudisha mipaka ya Israel ilivyokuwa wakati wa mfalme Daudi.[2]Katika Biblia[hariri | hariri chanzo]
Agano la Kale linamtaja tu katika Kitabu cha Pili cha Wafalme 13:13; 14:16, 23, 27, 28, 29; 15:1, 8; Kitabu cha Kwanza cha Mambo ya Nyakati 5:17; Hosea 1:1; na Amosi 1:1; 7:9, 10, 11.
-
- Makala katika jamii "Wafalme wa Israeli"
Makala katika jamii "Historia ya Israeli"
Jamii hii ina kurasa 21 zifuatazo, kati ya jumla ya 21.
A
- Agripa II
Agripa II
Agripa II (aliyezaliwa 27/28), jina lake kamili lilikuwa Marcus Julius Agrippa: ndiye mfalme wa 7 na wa mwisho kutoka ukoo wa Herode Mkuu. Alikuwa mtoto wa Herode Agripa.[1]Tanbihi[hariri | hariri chanzo]
- ↑ Mason, Charles Peter (1867), "Agrippa, Herodes II", in Smith, William, Dictionary of Greek and Roman Biography and Mythology 1, Boston: Little, Brown and Company, p. 78
Vyanzo vingine[hariri | hariri chanzo]
- Yohanan Aharoni & Michael Avi-Yonah, "The MacMillan Bible Atlas", Revised Edition, p. 156 (1968 & 1977 by Carta Ltd.).
E
- Edomu
Edomu
Edomu (kwa Kiebrania אֱדוֹם, Edom, ʼĔḏôm, yaani "nyekundu"[1]) au Idumea (kwa Kigiriki Ἰδουμαία, Idoumaía; kwa KilatiniIdūmaea) walikuwa taifa la Kisemiti lililoshi kusini kwa Bahari ya Chumvi katika eneo ambao leo limegawanyika kati ya Israeli na Yordan.Biblia inawataja mara nyingi kama washindani wa taifa la Waisraeli[2]ambao walikuwa na undugu kutokana na mababu wao kuwa watoto pacha wa Isaka, mwana wa Abrahamu.Mataifa hayo mawili yaliendelea kushindana mpaka Edomu ilipomezwa na Israeli wakati wa Wamakabayo (karne ya 2 KK).Baada ya hapo, Mwedomu Herode Mkuu alipata kuwa mfalme wa Israeli (37 KK - 4 KK) na kuacha ukoo ulioendelea kutawala kwa kwikwi chini ya himaya ya Dola la Roma kwa mwaka 100 hivi. - Efraimu (babu)
Efraimu (babu)
I
- Israeli ya Kale
Israeli ya Kale
Israeli ya Kale ni jina la watu au taifa walioitwa taifa teule katika Tanakh au Biblia ya Kiebrania (kwa hiyo pia katika Agano la Kale lililo sehemu ya kwanza ya Biblia ya Kikristo.Kihistoria waliishi katika nchi iliyoitwa Kanaani, halafu Israeli (baadaye pia Palestina) kuanzia mnamo 1200 KK hadi mnamo mwaka 70 BK Waroma wa Kale walipovamia na kuharibu Yerusalemu, ambao tena mwaka 135waliwafukuza wote kutoka nchi yao.Wenyeji walijiita mwanzoni Wanaisraeli na baadaye pia Wayahudi.Mwanzo na mwisho wa historia ya Israeli ya Kale[hariri | hariri chanzo]
Historia ya Israeli ya Kale inaanza tangu kupatikana kwa taifa hilo katika nchi yake inayoitwa Israeli. Kufuatana na masimulizi ya Agano la Kale taifa la Israeli lilianzishwa na Wanaisraeli waliotoka Misri chini ya uongozi wa Musa na kuvamia Kanaani mnamo mwaka 1200 KK chini ya Yoshua.Wataalamu wengine wa kisasa wanaona ya kwamba taifa lilitokea hasa ndani ya nchi kwa kuungana kwa vikundi mbalimbali.Muungano huo wa vikundi na makabila ukawa taifa na kuunda ufalme wa kwanza wa Israeli wakati wa mfalmeSauli aliyefuatwa na Daudi na mwanae Suleimani.Baada ya kifo cha Suleimani likatokea farakano na jina la "Israeli" likatumiwa na ufalme wa kaskazini, wakati mji mkuu wa kale Yerusalemu ukaendelea kama mji mkuu wa ufalme wa Yuda.Falme zote mbili zilishindwa katika vita na kuanzia mwaka 587 KK hapakuwa tena na dola la kujitegemea, bali eneo lilikuwa chini ya falme mbalimbali kama vile Babiloni, Uajemi na Ugiriki wa Kale.Lakini harakati za Wamakabayo za kurudisha uhuru uliweza kuwafukuza Wagiriki na kuanzisha ufalme wa Kiyahudi kati ya 140 KK hadi 4 KK.Hata hivyo kuanzia mwaka 63 KK ufalme huo uliwekwa chini ya ulinzi wa Dola la Roma na polepole kugawiwa na hatimaye kuwa jimbo la Kiroma (tangu 70 BK).Maangamizi ya Yerusalemu mwaka 70 BK huhesabiwa kama mwisho wa Israeli ya Kale. Wataalamu wengine wanaona tayari uvamizi wa mji wa 587 KK na Wababeli kama mwisho wa kipindi hiki na kuangalia kipindi kati ya 587 KK hadi 70 BK kama kipindi kipya.Israeli wakati wa Yesu[hariri | hariri chanzo]
Wakati wa Agano Jipya, mji wa Yerusalemu, pamoja na nchi ya Israeli/Palestina, vilikuwa chini ya Dola la Roma, ambalo lilitawala maeneo yote yanayozunguka bahariya Mediteranea. Mkuu wa Dola alikuwa na cheo cha "Kaisari" akikaa mjini Roma (Italia).Waroma walidai utiifu na kodi za mataifa na makabila yote yaliyokuwa chini yao. Lakini hawakuwa na neno juu ya utamaduni na dini za nchi hizo.Utawala wa Kiroma ulirahisisha biashara na uchumi pamoja na mawasiliano katika maeneo haya yote. Waroma hawakuwa na mitambo ya injini lakini walikuwa wataalamu wa uhandisi. Walikuwa hodari sana kujenga barabara na nyumba za ghorofa. Majengo kadhaa waliyoyajenga husimama mpaka leo. Magofu ya miji yao yanaonekana leo hii kuanzia Misri na Algeria hadi Ujerumani na Asia. Wasanii wao walichonga sanamu za mawe za kudumu.Israeli/Palestina ilikuwa na serikali yake ya Kiyahudi lakini pia na liwali au gavana wa Kiroma. Waroma walizima kwa ukali majaribio yote ya kupindua utawala wao. Wayahudi katika Israeli walijaribu mara mbili kuwafukuza Waroma nchini: miaka 66-73 na 135 BK. Kila safari Waroma walilipiza kisasi, wakichoma moto miji na vijiji na kuwafanya wananchi kuwa watumwa au kuwaua kabisa.
J
- Jasoni wa Kurene
Jasoni wa Kurene
Jasoni wa Kurene (kwa Kigiriki Ἰάσων κυρήναιος) alikuwa Myahudi wa Kurene, Libya, aliyeishi katika karne ya 2 KK na kuandika historia ya vita vya ukombozi vya Wamakabayo hadi ushindi wao dhidi ya jemadari Nikanori (175 KK-161 KK).Maandishi hayo yaliyopotea yalikuwa katika vitabu vitano lakini yalifupishwa na kurekebishwa na Myahudi mwingine asiyejulikana katika kitabu kilichopo hadi leo maarufu kama Kitabu cha pili cha Wamakabayo, kimojawapo cha vitabu vya Deuterokanoni katika Biblia ya Kikristo ya madhehebu kadhaa. Tazama 2 Mak 2ː24.
K
- Kanaani
Kanaani
Kanaani ni jina la zamani la eneo la Mashariki ya Kati ambalo siku hizi limegawanyika katika nchi za Israeli na Palestina, Lebanoni na sehemu za Magharibi za Jordan na Sirya.Katika Biblia jina hilo (kwa Kiebrania כנען, knaʿn) linatumika zaidi kumaanisha sehemu ile tu ambayo ilitekwa na Waisraelina kuitwa Israeli. Sehemu hiyohiyo baadaye tena ilikuja kuitwa pia Palestina, yaani nchi ya Wafilisti.Baada ya mataifa hayo mawili kuteka sehemu kubwa upande wa Kusini kuanzia karne ya 13 KK, ile ya Kaskazini zaidi iliyobaki chini ya wakazi asili ilikuja kuitwa pia Foinike.Katika eneo hilo kati ya Mesopotamia na Misri kuanzia milenia ya 4 KK ulistawi ustaarabu muhimu wa Kisemiti ambao, kati ya michango mingine, ni asili ya alfabeti.Habari nyingi kuhusu ustaarabu huu zimejulikana hasa kwa njia ya akiolojia. - Kuhani mkuu
Kuhani mkuu
Kuhani mkuu ni cheo kikuu cha kuhani katika dini zenye ngazi mbalimbali ya ukuhani. Kwenye mahekalu makubwa yenye makuhani wengi, mmoja aliweza kuwa na nafasi ya kiongozi na kuitwa kuhani mkuu.Katika dini za Sumeri, Babeli na Misri ya Kale walikuwepo pia makuhani wakuu waliokuwa viongozi wa dini kwa ufalme wote. Katika Babeli kulikuwa pia na makuhani wakuu wa kike.Katika Biblia[hariri | hariri chanzo]
Katika Israeli ya Kale Kuhani Mkuu (kwa Kiebrania כהן גדול kohen gadol) alikuwa kiongozi mkuu pekee wa ibada za dini ya Uyahuditangu mwanzo wa taifa la Israeli hadi mwaka 70 B.K., hekalu la Yerusalemu lilipobomolewa moja kwa moja.Wakati wa Yesu alikuwa mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Israeli lenye wajumbe 70 chini yake. Chini ya utawala wa Dola la Roma kuhani mkuu wa Yerusalemu alikuwa pia na wajibu wa kisiasa kama kiongozi wa Wayahudi nchini.Waraka kwa Waebrania katika Agano Jipya unamtambulisha Yesu Kristo mwenyewe kuwa kuhani mkuu wa milele kufuatana na utaratibu wa Melkisedeki, ukisisitiza ubora wake kulingana na makuhani wa Agano la Kale.
M
- Makabila ya Israeli
Makabila ya Israeli
Makabila 12 ya Israeli (kwa Kiebrania בני ישראל, Bnai Yisraʾel, yaani Wana wa Israeli) waliunda taifa la lugha ya Kisemiti katika Mashariki ya Kati, wakiishi katika sehemu kubwa ya nchi ya Kanaani kati ya karne ya 15 KK na karne ya 6 KK), halafu wakawa wanaitwa Wayahudi na Wasamaria.Biblia inaeleza kuwa makabila hayo yalitokana na wana wa kiume 12 wa babu Yakobo, bin Isaka na mjukuu wa Abrahamu. Ni Yakobo aliyepewa kwanza jina la Israeli.Majina ya watoto hao na ya makabila yaliyotokana nao ni: Reubeni (babu), Simeoni (babu), Lawi (babu), Yuda (babu), Dan (babu), Naftali (babu), Gad (babu), Asheri (babu), Isakari (babu), Zebuluni (babu), Yosefu (babu) (wazao waligawanyika katika makabila mawili, kutokana na watoto wake Manase (babu) na Efraim (babu)), Benyamini (babu).Habari katika Kitabu cha Mwanzo[hariri | hariri chanzo]
Kadiri ya Mwa 25:19-34, Rebeka alimzalia Isaka watoto pacha wenye sura na silika tofauti, Esau na Yakobo. Wa kwanza analaumiwa hasa kwa kupuuzia baraka ya Mungu iliyokuwa haki ya kifunguamimba: kwa sahani ya dengu alikubali kukosa neema zile zote alizojitwalia Yakobo kwa imani yake (Eb 12:16-17).Mwa 27 inasimulia jinsi Yakobo, akifundishwa na mama yake, alivyoweza kubarikiwa na baba. Ingawa uongo wake haukubaliki (Hos 12:3-5), Mungu alithibitisha baraka ya Isaka kadiri ya desturi yake ya kumpendelea mdogo: hivyo Yakobo, aliyekimbia nchi yake ana fimbo tu, alirudi miaka ishirini baadaye ana wake 4, watoto 11 na mifugo wengi ajabu (Mwa 32). Kabla hajaingia nchi yake Mungu alishindana naye usiku kucha akalazimika kumbariki na kumtajia jina jipya, Israeli.Kama kawaida ya mitara, kulikuwa na upendeleo na wivu. Hasa Yosefu alichukiwa na kaka zake wote, ingawa alikuwa mnyofu hata kuwasimulia ndoto zake za ajabu (Mwa 37:2-11). Kijicho na chuki vilifikia hatua ya kuwafanya watamani kumuua. Walipopata nafasi walifanya njama, ingawa si wote. Mwisho uamuzi ukawa kumuacha hai lakini kumuuza kama mtumwa kwa wafanyabiashara walioelekea Misri (Mwa 37:12-36). Lakini katika maovu ya binadamu Mungu akazidi kushughulikia taifa lake teule. Hivyo Yosefu akawa mfano wa Yesu ambaye alichukiwa bure tu akauawa msalabani kwa wokovu wa wadogo zake wakosefu.Mwa 39 inaonyesha jinsi Yosefu alivyozidi kumtiii Mungu na kukwepa dhambi. Hivyo baada ya majaribu mbalimbali akatukuzwa kuwa liwali wa Farao kwa nchi yote, hasa kwa usimamizi wa akiba ya chakula (Mwa 41:1-49) kwa ajili ya miaka saba ya njaa aliyotabiri. Kadiri ya mpango wa Mungu njaa hiyo ikawalazimisha kaka zake waje kumuinamia, naye hakulipa kisasi; halafu, kama vile alivyotafsiri ndoto mbalimbali, aliwafafanulia maana ya matukio ya maisha yao katika mpango wa Mungu: kwamba ndiye aliyemtuma Misri kusudi awaokoe (Mwa 45:1-15).Mwa 46:1-7 inasimulia Yakobo na wazawa wake wote, jumla wanaume 70, walivyohamia Misri (miaka ya 1700 KK). Lakini hawakusahau nchi waliyoahidiwa na Mungu: ndiyo sababu Yakobo na Yosefu walidai waapiwe kuwa watakuja kuzikwa kwao (Mwa 49:29-50:26). Kabla ya kufa Yakobo aliwabariki watoto wake 12 na kwa namna ya pekee Yuda ambaye atatawala moja kwa moja (Mwa 49:8-12).Wataalamu wanafikiri baraka hiyo inaeleza hali ya makabila hayo wakati ilipoandikwa.Tanbihi[hariri | hariri chanzo]
- Manase (babu)
- Mapambano kati ya Israeli na Palestina
- Mazingira ya Yesu
- Mfalme Yekonia
- Mwana wa Daudi
S
U
- Uhamisho wa Babeli
- Manase (babu)
Manase (babu)
- Mapambano kati ya Israeli na Palestina
Mapambano kati ya Israeli na Palestina
Mapambano kati ya Israeli na Palestina ni ugomvi baina ya nchi ya Israeli na wakazi wa Palestina unaoathiri pia uhusiano na nchi jirani. Ugomvi huu ulianza katika karne ya 20 baina ya wakazi Wayahudi na Waarabu wa maeneo ambayo leo hii yako chini ya Israeli na Mamlaka ya Kitaifa ya Palestina. Ulisababisha tayari vita sita kati ya nchi ya Israeli tangu kuundwa kwake mwaka 1948 na jirani zake za Kiarabu. Mapambano yanaendelea, hayajapata suluhisho hadi sasa.Mapambano yalianza wakati wa kuongezeka kwa uhamiaji wa Wayahudi katika maeneo ya Palestina yaliyokaliwa na Waarabu. Kuundwa kwa Dola la Israeli kulisababisha vita ya kwanza baina ya Israeli mypa na nchi zote za jirani.Msingi katika itikadi
Wayahudi wa Ulaya waliokuwa wahamiaji wa kwanza kuja Palestina waliona uhamiaji wao kama kurudi kwenye nchi ya mababu wao kwenye mahali ambako taifa lao litazaliwa upya. Sehemu ya Wayahudi waliona mwendo wao si kurudi tu kwenye ardhi ya mababu kama taifa lakini pia utimiaji wa sala ya Kiyahudi yenye ombi la "kuonana katika Yerusalemu mwaka ujao". Mpaka leo wengine wanaona jambo hilo kutokana na ahadi za Mungu kwa taifa lao kadiri ya Tanakh (yaani Biblia ya Kiebrania).Kumbe wakazi Waarabu wa Palestina waliona uhamiaji wa wageni kutoka Ulaya kama harakati ya kikoloni iliyolenga kutwaa ardhi yao. Tena Waislamu kadhaa wanaona ya kwamba, tangu itwaliwe na jeshi la Uislamu katika karne ya 7 ardhi ya Palestina - Israeli imekuwa nchi ya Kiislamu inayopaswa kutawaliwa na serikali ya Waislamu daima. Wakristo hawakuwa wengi, tena wamezidi kupungua kwa kuhama kutokana na ugumu wa hali yao wanaojisikia kubaguliwa kama kundi dogo hata kati ya Wapalestina.Historia[hariri | hariri chanzo]
Utangulizi: Pogromu, Uhamiaji na Uzayuni[hariri | hariri chanzo]
Katika karne ya 19 idadi kubwa ya Wayahudi waliishi katika maeneo kadhaa ya Milki ya Urusi [1] yaliyotwaliwa na milki hiyo mnamo 1800.Uadui dhidi ya Wayahudi ulitokea dhidi ya utawala wa Kirusi [2] Kuanzia mwaka 1880 kulitokea ghasia mbalimbali ambako Wayahudi walishambuliwa katika miji ya Urusi. Wimbi la pili la ghasia hizo zilizoitwa pogromu likatokea mwaka 1905, ambapo Wayahudi zaidi ya 2000 waliuawa mjini Odessa [3]. Wakati ule Wayahudi wa Urusi walianza kuhamia nje: wengi wao walikwenda Marekani, lakini wachache walielekea Palestina.Mapogromu yalikuwa pia chanzo cha harakati mpya ya Uzayuni (Zionism) kati ya Wayahudi wa Ulaya. Uzayuni ulilenga kuwapa Wayahudi eneo maalum ili wapate kujenga upya taifa katika dola lao wenyewe, ambako wangekuwa wenyeji, si kundi la pekee katikati ya watu waliowadharau.Mwaka 1896 Theodor Herzl (1860-1904) aliandika kitabu "Dola la Wayahudi" alimodai kuundwa dola la pekee kwa ajili ya Wayahudi. Mkutano wa kwanza wa wafuasi wake ulichagua jina la "Zayuni" ambalo lilikuwa jina asilia la mlima wa hekalu mjini Yerusalemu; wakachagua jina hilo kwa sababu linataja mahali patakatifu zaidi pa Uyahudi. Mkutano huo uliazimia kuwa "Uzayuni unalenga kuunda makazi salama yaliyokubaliwa rasmi kwa ajili ya taifa la Kiyahudi katika nchi ya Palestina".Wazayuni walikusanya pesa kote Ulaya wakanunua ardhi katika Palestina na kuanzisha vijiji kwa ajili ya Wayahudi waliohima huko.Tamko la Balfour na chanzo cha mapambano
Vita ya Kwanza ya Dunia ilikwamisha mipango yote kwa sababu Palestina ilikuwa sehemu ya Milki ya Osmani iliyoshiriki katika vita pamoja na Ujerumani na Austria dhidi ya Urusi, Ufaransa na Uingereza.Mwaka 1917 wakati ambapo jeshi la Uingereza lilifaulu kusogea mbele kutoka Misri na kuingia Palestina, waziri wa mambo ya njeArthur James Balfour alitoa tamko la Balfour yaani tamko rasmi kuwa Uingereza inataka kusaidia mipango ya kuanzisha makazi ya Kiyahudi katika Palestina. Wakati uleule Waingereza waliwaahidi Waarabu kuundwa kwa dola la Kiarabu kwenye maeneo yaliyokaliwa nao katika Milki ya Osmani. Lakini wakati huohuo walipatana na Ufaransa kuhusu ugawaji wa maeneo ya Kiarabu ya Milki ya Osmani.Kwenye mkutano wa amani wa Paris wa mwaka 1919, ulioandaa Mkataba wa Versailles, mwakilishi wa Waarabu, Faisal bin Hussein bin Ali al-Hashimi, alipatana na mwakilishi wa Wazayuni, Chaim Weizmann, kuwa anakubali uhamisho wa Wayahudi kuja Palestina, na Palestina kuwa eneo la pekee tofauti na Dola la Waarabu ambayo Faisal alilenga kujenga Uarabuni pamoja na Syria na Irak. Haki za wakazi Waarabu zilitakiwa kulindwa na maendeleo ya pamoja kati ya wakazi Waarabu na Wayahudi kujengwa. Lakini Uingereza na Ufaransa waliendelea kugawa Mashariki ya Kati, hivyo Waarabu wengi hawakusikia ya kwamba mapatano ya Faisal yalikuwa na umuhimu tena.Baada ya vita Uingereza ilichukua utawala wa Palestina kama eneo la kudhaminiwa kwa niaba ya Shirikisho la Mataifa. Idadi ya Wayahudi waliofika kutoka nchi za Ulaya iliongezeka, lakini bado Wayahudi wengi walihamia Marekani, si Palestina. Hata hivyo shirika za Uzayuni ziliendelea kununua ardhi, kuanzisha vijiji vya Ujamaavilivyoitwa Kibbutz hata Tel Aviv ilikua kama mji wa Kiyahudi kandokando ya Yafo ya Kiarabu. Mnamo 1931 asilimia 17 ya wakazi wa Palestina walikuwa Wayahudi.Katika Palestina mufti mkuu wa Yerusalemu, Mohammed Amin al-Husseini, alichukua uongozi wa Waarabu akapinga kufika kwa Wayahudi wapya. Serikali ya Kiingereza ilisitasita kuamua juu ya msimamo wake - haikuzuia kufika kwa Wayahudi, lakini haikuwasaidia kujiimarisha nchini.Kati ya 1936 na 1939 kulitokea ghasia kubwa ya Waarabu dhidi ya polisi na jeshi la Kiingereza na dhidi ya makazi ya Wayahudi. Uingereza ulifaulu kukandamiza ghasia hii kwa jeshi lake. Kati ya Wayahudi vikundi vyenye silaha vilianzishwa vilivyolenga kutetea vijiji vya Kiyahudi na kulipiza kisasi kwa mashambulio. Vikundi hivyo viliendelea baadaye kuwa chanzo cha jeshi la Israeli.Siasa ya chuki dhidi ya Wayahudi iliyoendeshwa na Chama cha Nazi chini ya dikteta Adolf Hitler katika Ujerumani na nchi nyingine za Ulaya iliongeza namba ya Wayahudi waliopaswa kuondoka kwao Ulaya. Miaka baada ya 1933 takriban wakimbizi Wayahudi 250,000 walifika Palestina - hii ilikuwa sababu moja ya ghasia ya Waarabu miaka 1936-1939. Hadi mwaka 1945 Wayahudi walikuwa asilimia 33 ya wakazi wote wa Palestina.Baada ya vita kuu ya pili kulikuwa na laki za Wayahudi waliowekwa huru kutoka makambi ya KZ na wengi wao walielekea Palestina. Hapo Serikali ya Uingereza, iliyosita kuamua kama ilitaka kutekeleza ahadi zake kwa Waarabu au kwa Wayahudi, iliomba Umoja wa Mataifa kuamua juu ya hatua zijazo kwa ajili ya Palestina, maana ilikuwa eneo la kudhaminiwa na asili ya mamlaka hii ilikuwa imepita kutoka Shirikisho la Mataifa kwenda Umoja wa Mataifa.[4].Kuundwa kwa Dola la Israeli
Mwaka 1947 Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa ulipigia kura mpango wa ugawaji wa Palestina. Mataifa 33 yalipiga kura ya ndiyo, 13 hapana, 10 hayakusimama upande wowote. Hivyo eneo la Palestina lilitakiwa kugawiwa kwa dola la Kiyahudi, dola la Kiarabu na mji wa Yerusalemu. Mamlaka ya Uingereza yalitakiwa kwisha tarehe 14 Mei 1948.Waarabu walipinga ugawaji kwa kudokeza ya kwamba mpango wa ugawaji haukuwa adili kwa sababu zifuatazo. Mwaka 1947 Palestina ilikuwa na wakazi 1,845,000. Watu 1,237,000 au theluthi mbili walikuwa Waarabu, wakati watu 608,000 tu au theluthi moja walikuwa Wayahudi. Kumbe Dola la Kiyahudi lilitakiwa kupokea asilimia 56 cha ardhi, pamoja na maeneo yaliyofaa zaidi kwa kilimo ingawa mali ya Kiyahudi wakati ule ilikuwa asilimia 7 tu ya ardhi yote ya Palestina. Katika eneo la Dola la Kiyahudi takriban 40% ya wakazi wangekuwa Waarabu. Sehemu kubwa ya ardhi katika sehemu ya Dola la Kiarabu ilikuwa mlimani na haikufaa vema kwa ajili ya kilimo.Wawakilishi wa Kiyahudi walisema idadi ya Wayahudi itaongezeka haraka kutokana na uhamiaji wa Wayahudi wengine - wakati ule walikuwa bado laki za Wayahudi katika makambi katika nchi za Ulaya, ni hao ambao hawakuuawa na Wajerumani katika Holocaust.Mara baada ya azimio la UM, mapigano yalianza katika Palestina na kuwa vita ya wenyewe kwa wenyewe nchini. Vikundi vya wanamgambo wa Kiarabu vilishambulia makazi ya Kiyahudi kote nchini. Wayahudi pia walikuwa na vikundi vya wanamgambo.Tarehe 14 Mei mkutano wa wawakilishi Wayahudi ulitangaza Dola la Israeli kama nchi mpya. Waingereza waliondoa jeshi lao.Tarehe 15 Mei 1948 majeshi ya Misri, Yordani, Lebanoni, Syria na Irak yaliingia Palestina yakatwaa maeneo ya Kiarabu na kushambulia makazi ya Kiyahudi. Katika vita ya miezi 10 jeshi la Israeli lilifaulu kusimamisha wapinzani na kuwarudisha nyuma. Jeshi la Kiarabu pekee lenye uwezo lilikuwa Kikosi Arabu cha Yordani. Wakati wa kusimamisha mapigano Israeli ilikuwa imeongezeka maeneo yake ikatawala asilimia 78 za eneo la kukabidhiwa la awali yaani maeneo yote yaliyowahi kukusudiwa na Umoja wa Mataifa kwa ajili ya Dola la Kiyahudi pamoja na nusu ya maeneo yaliyokusudiwa kwa ajili ya Dola la Kiarabu.Ukanda wa Gaza ulitawaliwa na Misri na Ukingo wa Magharibi wa Yordani (mto) pamoja na mji wa kale wa Yerusalemu ukawa chini ya milki ya Yordani.Zaidi ya wakazi Waarabu 700.000 walilazimika kuondoka au walimkimbia kutoka miji na vijiji vyao, wakikaa nje ya maeneo yaliyotawaliwa sasa na Israeli. Waarabu 150,000 hivi walibaki ndani ya maeneo haya sasa kama raia Waarabu wa Israeli. Baada ya vita Israeli ilikataa kurudi kwa waliokuwa nje. Ndiyo asili ya Wakimbizi Wapalestina wanaoishi Syria, Lebanoni, Yordani na Misri, pamoja na hao wanaoendelea kukaa katika makambi katika maeneo ya Gaza na Ukingo wa Magharibi.Madola yote ya Waarabu isipokuwa milki ya Yordani yalikataa kuwapa wakimbizi hao haki za uraia, na kwa hiyo hadi leo wajukuu wamebaki kama wakimbizi katika nchi za kigeni bila uraia; wakisafiri wanatumia vitambulisho vilivyotolewa na UM, wanakosa haki ya kutafuta kazi au kushiriki katika siasa kama raia wa kawaida, hata kama familia zimeshaishi katika nchi hizo hadi kizazi cha tatu au nne.Wapalestina baada ya 1948
Jumuiya ya Nchi za Kiarabu ilianzisha taasisi iliyoitwa "Serikali kwa Palestina yote" (ing. All-Palestine Government, ar. حكومة عموم فلسطين hukumat 'umum Filastin) wakati wa vita (1948) iliyotambuliwa na nchi za Kiarabu isipokuwa milki ya Yordani. Ilikuwa na mamlaka fulani katika Ukanda wa Gaza pekee, ikafanya kazi chini ya usimamiziwa Misri na mwisho wa 1948 ilipelekwa Kairo ikafutwa na serikali ya Misri mwaka 1959.Taasisi mpya ikaundwa mwaka 1964 kwa azimio la Jumuiya ya Nchi za Kiarabu ikaitwa PLO (Palestine Liberation Organization, ar.: منظمة التحرير الفلسطينية [[munaẓẓamat at-taḥrīr al-filasṭīniyyah) ambayo ni maungano ya vikundi mbalimbali ya Kipalestina. Shabaha yake ilikuwa "ukombozi wa Palestina". Serikali ya Misri ilikuwa na athirakubwa katika PLO. Harakati ya Fatah mwanzoni haikushiriki. PLO iliendesha vikundi vya wanamgambo ya Fedayin Wapalestina walioshambulia mipaka ya Israel mara kwa mara.Yordani na Israeli (kwa Wapalestina walioweza kubaki kwao) zilikuwa nchi pekee zilizowapa Wapalestina uraia, lakini katika nchi nyingine walibaki kama wakimbizi bila uraia. Makambi yao yaliangaliwa na shirika la Umoja wa Mataifa linaloitwa UNRWA.Israel na majirani hadi 1973
Bada ya vita ya 1948-1949 nchi jirani zilikataa kutambua dola la Israeli. Hali ya vita ikaendelea ingawa bila mapigano kati ya majeshi makubwa. Wanamgambo wa Wafedayin Wapalestina waliendelea kuvuka mpaka kutoka makambi ya wakimbizi na kushambulia vijiji vya Kiyahudi. Wanamgambo hao walipata mara nyingi silaha na mafunzo kutoka kwa majeshi ya Misri na Syria.Vita ya 1948-1949 ilisababisha ghasia na mashambulio dhidi ya Wayahudi walioishi katika nchi za Kiarabu. Nchi kadhaa za Kiarabu ziliweka sheria za ubaguzi dhidi ya Wayahudi. Hivyo katika miaka baada ya kuundwa kwa Israeli karibu Wayahudi wote waliondoka au walifukuzwa katika nchi za Kiarabu na kufika kama wakimbizi katika Israel, Marekani au Ulaya. Jumla ya wakimbizi hao Wayahudi karibu ililingana na idadi ya Waarabu waliofukuzwa kutoka Palestina. Hivyo idadi ya wananchi Wayahudi wa Israeli iliongezeka sana.Uhusiano mbaya kati ya Israeli na majirani Waarabu ulisababisha vita zaidi.Mwaka 1956 Israeli ilishambulia Misri katika vita ya Suez kufuatana na mpango wa pamoja na Ufaransa na Uingereza baada ya kuona ununuzi wa silaha nyingi na Misri.Mwaka 1967 jeshi la Misri lilikusanya vikosi vingi vya jeshi lake katika rasi ya Sinai ikafukuza walinzi wa amani wa UM na kufunga mlango wa Tiran hivyo kuzuia usafiri wa meli baina ya Israeli na Bahari Hindi. Israeli ikajibu kwa kushambulia Misri tarehe 5 Juni 1967 katika Sinai ikaharibu jeshi la Misri katika muda wa siku 6. Wakati huohuo milki za Yordani na Syria ziliamua kushikamana na Misri zikashambulia eneo la Israeli. Tokeo lake lilikuwa ya kwamba jeshi la Israeli likatwaa Ukingo wa Magharibi wa Yordani na pia milima ya Golan hadi maadui walisalimisha amri tarehe 10 Juni. Pia eneo lote la Sinai likatwaliwa na Israel na Mfereji wa Suez ulifungwa.Vita ya Yom Kippur iliyofuata ilikuwa mashambulio ya Misri na Syria dhidi ya Israeli katika mwezi wa Oktoba 1973. Mashambulio yalianza kwenye sikukuu ya Kiyahudi ya Yom Kippur. Jeshi la Misri lilifaulu kuingia kwenye rasi ya Sinai na Syria kwenye milima ya Golan. Lakini Syria ilirudishwa nyuma haraka na Waisraeli walifikia kilomita 40 tu kutoka Dameski. Jeshi la Misri lilifeli zaidi hadi Israeli iliweza kuvuka mfereji wa Suez na kufunga kikosi kikubwa cha Wamisri nyuma ya mstari wa mapigano na kuingia katika mji wa Suez na hata kukaribia Kairo. Mnamo 23 Oktoba pande zote zilikubali kusimamisha mapigano kwa ombi la UM. Baada ya majadiliano marefu, kila upande ulirudisha wanajeshi wake kilomita kadhaa kwa kusudi la kuwa na umbali kati ya majeshi.Misri na Israeli zikaendelea kuwa na majadiliano na kupatana kufanya amani mwaka 1973. Israeli iliondoka katika Sinai na nchi zote mbili zikafungua ubalozi katika nchi ya pili. Ukanda wa Gaza ulibaki chini ya Israeli.Uamsho wa Wapalestina na PLO
Vita ya siku 6 ya 1967 ilileta uamsho kati ya Wapalestina katika makambi ya wakimbizi. Kundi la Fatah lililoundwa mwaka 1959 nchini Kuwait liliongeza sifa zake kutokana na kupigana na jeshi la Israeli mwaka 1968 katika kambi la Karame (Yordani). Fatah lilijiunga na PLO na mwenyekiti wake Yasser Arafat akawa mwenyekiti wa PLO. Alileta mwelekeo mpya kuwa Wapalestina wanapaswa kujikomboa badala ya kutegema nchi za Waarabu wengine. Vikundi vya PLO viliendelea na mashambulio pamoja na kutumia mbinu za kigaidi dhidi ya wananchi raia wa Israeli.Tangu 1968 vikundi vya PLO viliteka nyara ndege au watu raia kwa shabaha ya kuwabadilisha na wafungwa Wapalestina katika Israeli. Hadi mwaka 1970 PLO ilikua kuwa na mamlaka kubwa nchini Yordani hadi jeshi la nchi hiyo iliwafukuza vikosi vya PLO kutoka milki ya Yordani.Hapo Arafat na sehemu ya askari wake walihamia Lebanoni. Wakati wa vita ya wenyewe kwa wenyewe ya Lebanoni PLO ilichukua upande na kushiriki lakini sehemu nyingine za vikundi vya Kipalestina vilishikamana na serikali za nchi za Waarabu zilizoshiriki pia katika vita hiyo ndani ya Lebanoni. Baada ya mashambulio ya Israeli PLO ilifukuzwa kutoka Lebanoni na kuhamia Tunisia mwaka 1982.Intifada ya kwanza
Katika miaka iliyofuata Wapalestina katika Ukanda wa Gaza na Ukingo wa Magharibi wa Yordani walisikia maisha kuwa vigumu zaidi. Wengi wao walikuwa vijanawaliozaliwa chini ya utawala wa Israeli. Vijana wengi walikosa kazi. Hawakuwa na matumaini katika jitihada za PLO iliyokuwa mbali nao.Basi, baada ya ajali ya barabarani ambako Wapalestina wanne waliuawa na gari la kijeshi la Israeli, mnamo Disemba 1987 ililipuka ghasia ya ghafla iliyoitwa intifada. Wapalestina waliandamana barabarani, watoto na vijana walitupa mawe dhidi ya askari wa Israeli. Kundi jipya la Hamas lilichokoza mwendo huu na kuongoza upinzani. Katika miezi iliyofuata Wapalestina 1,551 na Waisraeli 422 waliuawa.Kutangazwa kwa "Dola la Palestina" na majadiliano kati ya PLO na Israeli
Mwaka moja baada ya intifada ya kwanza PLO katika mji wa Tunis ilitoa tamko la kutangaza "Dola la Palestina". Katika tamko hili PLO ilitambua kwa mara ya kwanza kuwepo kwa Israeli. Tamko hili lilikuwa msingi kwa nchi kama Marekani kutambua pia PLO kama mwakilishi wa Wapalestina na baadaye kwa majadiliano ya kwanza kati ya PLO na Israeli.Wakati wa Vita ya Ghuba ya 1990/91 Arafat aliamua kuwa upande wa Saddam Hussein aliyeshambulia Kuwait. Hii ilisababisha kufukuzwa kwa Wapalestina wengi kutoka Kuwait baada ya vita na kushindwa kwa Iraq. Nchi za Kiarabu kama Misri na Saudia zilizowahi kusaidia PLO lakini zilichukua msimamo dhidi ya Saddam Hussein zilikata misaada yao kwa PLO. Kudhoofishwa kwa PLO kwa njia hii ilisaidia pia kuanzisha majadiliano ya moja kwa moja. Katika mkutano wa amani wa Madrid, Hispania, Wapalestina walishiriki kwa mara ya kwanza katika majadiliano na Israeli.Mapatano ya Oslo na kuanzishwa kwa mamlaka ya kitaifa ya Palestina
Tangu Januari 1993 wawakilishi wa PLO na Israeli walikutana kwa siri mjini Oslo, Norwei. Arafat alitamka kutambua Israeli na kuachana na mbinu za kigaidi katika barua kwa kiongozi wa Israeli Yitzhak Rabin. Rabin na Arafat walikutana Washington, D.C. na kutia sahihi mapatano ya kwanza yaliyokuwa mwanzo wa mfuatano wa majadiliano marefu yaliyolenga kuleta amani kati ya Wapalestina na Israeli katika muda wa miaka 5.Kwa jumla mapatano hayakuweza kufikia mwisho. Lakini katika hatua za kwanza Mamlaka ya Kitaifa ya Palestina yaliundwa kama mbegu ya serikali kamili. Jeshi la Israeli ilijiondoa katika Gaza na sehemu za Ukingo wa Magharibi wa Yordani zilizowekwa chini ya mamlaka mpya.Mwaka 1995 uongozi wa PLO ulihamia Palestina na kuanzisha ofisi kuu ya Mamlaka ya Palestina huko Ramallah.Kukwama kulisababishwa na shaka kama ifuatavyo:- katika jamii ya Israeli kama Arafat na upande wa Kipalestina walitaka kweli kujenga amani na kusimamisha ugaidi wakati mashambulio dhidi ya askari na wananchi raia wa Israeli yalipoendelea kutokea. Kilele cha upinzani ndani ya Israeli kilikuwa uuaji wa waziri mkuu Rabin mwaka 1995 uliofanywa na mpinzani Mwisraeli.
- Katika jamii ya Wapalestina kama Israeli ilitaka kweli amani kwa sababu kujengwa kwa makazi kwa walowezi Waisraeli nje ya mipaka ya Israeli ya 1967 kuliendelea.
- Sehemu ya vikundi vya kisiasa upande wa Palestina, hasa Hamas, ilikataa kukubali mapatano yaliyofikiwa.
- Swali la pekee lilihusu hali ya Yerusalemu ya Mashariki ambayo Wapalestina wanaidai kama mji mkuu wao ambayo iko nje ya mipaka ya Israeli ya 1967. Lakini Israeli iliwahi kutangaza kuunganishwa kwa mji huu wote na kuitawala sehemu ya magharibi na ya mashariki kama mji mmoja wa Israeli usioweza kutengwa tena.
- Tatizo ni pia suala la "haki ya kurudi" kwa ajili ya watoto na wajukuu wa wakimbizi Wapalestina wa mwaka 1948 wanaotaka kurudi kwenye makazi ya mababu yaliyo sasa ndani ya eneo la Israeli.
Katika uchaguzi wa mwaka 1996 chama cha Benyamin Netanyahu kilishinda kura ya bunge la Israeli. Netanyahu hakukubali majadiliano; alidai kuwa yaliimarisha tu wapinzani wakali wa Israeli upande wa Wapalestina na kusabisha mashambulio na ugaidi zaidi.Mwaka 2005 jeshi la Israeli lilitoka kabisa katika Ukanda wa Gaza na kubomoa vijiji vya walowezi Wayahudi kule.Mafarakano kati ya Wapalestina yaliendelea kuongezeka kati ya Fatah na Hamas. Mwaka 2007 Chama cha Hamas kilichukua mamlaka juu ya Gaza kikaendelea kushambulia Israeli kwa makombora. Israeli ilijibu kwa kufunga mipaka ya Gaza na kungilia ndani ya Ukanda wa Gaza kijeshi mara kadhaa.Kutokana na mashambulio dhidi ya wananchi wa Israeli yaliyoendelea Waisraeli walianza kujenga fensi na ukuta wa kutenganisha Ufuko wa Magharibi na Israeli yenyewe. Ukuta huu wenye urefu hadi mita nane umesaidia kupunguza sana mashambulio dhidi ya raia, lakini umejengwa zaidi kwenye ardhi ya Kipalestina na kuongeza matatizo kwa wananchi.Israeli inaendelea kujenga makazi na vijiji kwa walowezi wa Kiyahudi ndani ya eneo la Kipalestina. Jeshi lake linashika vituo vingi katika ufuko wa magharibi na kutawala mwendo wa watu huko na kuzuia usafiri mara kwa mara kwa kulinda usalama wake.Farakano kati ya Hamas upande wa Gaza na Mamlaka ya Kipalestina mkononi mwa PLO-Fatah upande wa Ramallah haijapata suluhisho. - Mazingira ya Yesu
Mazingira ya Yesu
Mfululizo wa kurasa juu ya Yesu
[ficha]Yesu Kristo na Ukristo [ficha]Mazingira ya Yesu [ficha]Mitazamo juu ya Yesu Mazingira ya Yesu ni jumla ya mambo ya kijiografia na ya kihistoria yaliotangulia au kuendana na maisha ya Yesu Kristo, akimuathiri kama binadamu katika namna yake ya kuwaza, kusema na kutenda.Jiografia na historia ya awali
Nchi ambayo Yesu alizaliwa akafundisha ni nchi ileile ambayo Mungu aliwaahidia Waisraeli tangu zamani za Abrahamu, ni nchi ileile waliyoiteka chini ya Yoshua, ni nchi ileile waliyoirudia kutoka utumwani Babeli. Awali ilikuwa sehemu ya Kanaani, baadaye ikaitwa Israeli na hatimaye Palestina kutokana na Wafilisti waliokuwa wameteka sehemu ya pwani kusini karibu wakati uleule wa Waisraeli kuteka sehemu kubwa ya nchi wakitokwa Misri (karne ya 13 KK).Historia ya jirani
Katika karne ya 2 KK Wayahudi, walipodhulumiwa na Antioko Epifane ili waasi dini yao, walianza kupigania uhuru wao wa kidini na wa kisiasa chini ya ukoo wa Wamakabayo, ambao kwa imani na ushujaa mkubwa wakafaulu kushinda majeshi ya kutisha (1Mak 3:18-22), kutakasa hekalu (1Mak 4:36-61) na kurudisha ufalme wa Israeli mpaka baada ya Warumi kuweka Uyahudi chini ya himaya yao (63 K.K.).Madhehebu na hali ya imani
Matukio hayo ndiyo asili ya kundi la Mafarisayo (yaani “waliojitenga”), walioshika kwa bidii Torati kadiri ya mapokeo ya walimu wa sheria, wengi wao wakiwa walei. Kwa jumla walileta uamsho wa kiroho kati ya Wayahudi, lakini walidharau wenzao wasiojua Biblia ya Kiebrania.Pia walishindana sana na Masadukayo kuhusu masuala ya dini na ya siasa hata kusababisha mauaji; kwa kuwa Masadukayo (waliokuwa na nguvu kati ya makuhani) walikataa mafundisho hayo mapya huku wakishika Torati tu.Baada ya Torati kuzidi kuzingatiwa na Wayahudi, wataalamu wake pia walizidi kuheshimiwa kama watu wa Neno la Mungu, wanaoleta mwanga wake katika maisha ya jamii.Hekima, iliyotafutwa hasa chini ya Wagiriki, ilipotambulika kuwa inapatikana katika Torati, wataalamu hao wakaja kushika nafasi ya watu wa hekima kama vile hao walivyoziba pengo lililoachwa na manabii.Wayahudi walizoea hali hiyo kiasi kwamba wakaona vigumu kumkubali Yesu ambaye hafafanui Torati kwa kufuata mapokeo ya wataalamu, bali kwa kujiamini kama manabii waliojiona wabebaji wa Neno la Mungu.Alijitangaza kuwa ndiye Hekima ya milele ambaye ndani yake tunamjua Mungu, hivyo mwenendo wake na mafundisho yake haviwezi kuishia mambo yaliyozoeleka, kwa sababu kila mara ya Mungu yanapindua ya binadamu. La kufanya ni kujitahidi kufuata, halafu kuelewa: ndiyo wongofu ambao Yesu aliudai pamoja na imani.Utawala wakati wa Yesu
Lakini wakati wote wa Agano Jipya, yaani tangu Yesu alipozaliwa hadi mwisho wa maisha ya mitume wake, nchi hiyo haikuwa huru, bali chini ya himaya ya Warumi, ingawa pengine hao waliwakabidhi vibaraka, yaani watawala wenyeji waliowekwa na wakoloni.Vibaraka hao ni Herode Mkuu (37-4 K.K.) na wazawa wake, ambao tena hawakuwa Waisraeli halisi bali Waedomu ingawa kabila lao lililazimishwa kuingia dini ya Uyahudi karne iliyotangulia. Ukoo huo unajulikana kwa ukatili, uchu wa madaraka na uzinifu wake.Vilevile maliwali wa Kirumi waliowekwa pengine kutawala nchi au sehemu fulani walionyesha mara nyingi ukatili na dharau kwa Waisraeli na dini yao, hata kusababisha chuki na mapigano kati ya jeshi lao na wananchi. Mfano mmojawapo ni Ponsyo Pilatoaliyesimamia Uyahudi kuanzia mwaka 26 hadi 36 B.K.Mbali na hayo, utawala wa Roma, ulioenea Ulaya Magharibi na Kusini, Afrika Kaskazini na nchi za Mashariki ya Kati kupakana na Iraqya leo, kwa jumla ulihakikisha hali ya amani kwa muda wote wa Agano Jipya na karne za kwanza za Kanisa.Manufaa ya hali iliyokuwepo
Hali hiyo, pamoja na umoja wa dola hilo lote, na urahisi wa mawasiliano kwa njia ya barabara zilizotengenezwa na Warumi, na uenezi wa lugha ya kimataifa (Kiyunani), ilichangia kasi ya uenezaji Injili. Lugha hiyo ndiyo iliyotumiwa na waandishi wote wa Agano Jipya ili vitabu vyao viwafaidishe watu wengi zaidi, ingawa baadhi yao hawakuijua vizuri.Lugha asili ya Yesu na ya Mitume ilikuwa Kiaramu ambacho ni jamii ya Kiyahudi na ambacho polepole kilishika nafasi yake kati ya Wayahudi kuanzia karne VI K.K.Mikoa ya Palestina wakati ule
Hao wote walitokea mkoa wa Galilaya, uliokuwa chini ya Herode Antipa kuanzia mwaka 4 KK. Huko kulikuwa na mchanganyiko wa watu (Waisraeli na mataifa), kiasi kwamba huko Wayahudi wenyewe walifuata kwa urahisi desturi za Kiyunani hata wakadharauliwa na wenzao wa Kusini (Yerusalemu na mkoa wa Yudea).Kati ya mikoa hiyo miwili ulienea mkoa wa Samaria ambao wakazi wake walijenga uadui mkubwa na Wayahudi baada ya uhamisho wa Babeli, walipokataliwa kuchangia ujenzi wa hekalu la pili la Yerusalemu. Samaria pamoja na Yudea ilikuwa chini ya liwali wa Roma kuanzia mwaka 6 BK. - Mfalme Yekonia
Mfalme Yekonia
Mfalme Yekonia (kwa Kiebrania יְכָנְיָה, Yekonia, au יְהֹויָכִין, Yehoiakin, pia kifupi Konia) alikuwa mtawala wa ufalme wa Yudakutoka ukoo wa Daudi.Alitawala miezi mitatu tu (9 Desemba 598 KK - 15 Machi 597 KK) baada ya baba yake mfalme Yehoyakimu huku mji wa Yerusalemu ukiwa umezingirwa na jeshi la mfalme Nebukadneza II kutoka Babuloni.Mji ulipotekwa, aliondolewa madarakani (2Fal 24:17) na kupelekwa uhamishoni alipokaa gerezani miaka 37.Hatimaye alitolewa na kuwa mgeni wa mfalme wa Babuloni hadi kifo chake (2Fal 25:27): habari hiyo imeandikwa mwishoni mwa kitabu cha pili cha Wafalme kama utangulizi wa ukombozi wa Wayahudi wote.Kama alivyotabiri nabii Yeremia (Yer 22:28-30), hakuna mzao wake aliyetawala tena. - Mwana wa Daudi
Mwana wa Daudi
Mfululizo wa kurasa juu ya Yesu
[ficha]Yesu Kristo na Ukristo [ficha]Mazingira ya Yesu [ficha]Mitazamo juu ya Yesu Mwana wa Daudi ni jina la heshima la wanaume waliotokana na vizazi vya mfalme Daudi na hivyo kuhusishwa na ahadialilopewa na nabii Nathani kwamba ukoo wake utatawala milele (2Sam 7:1-29).Kwa namna ya pekee jina hilo lilitumika kwa Yesu aliyetambuliwa na wengi kuwa ndiye Masiya aliyetazamiwa, ama wakati wa maisha yake au baada ya kifo chake.Injili ya Mathayo na Injili ya Luka zinasisitiza haki ya Yesu kuitwa hivyo kwa kuorodhesha vizazi kati ya Daudi na Yosefu, mume wa Bikira Maria, mama yake.
S
- Sedekia
Sedekia
Sedekia (kwa Kiebrania צִדְקִיָּהוּ, Tsidkiyyahu|Ṣiḏqiyyā́hû, "Haki yangu ni YHWH"; kwa Kigiriki Ζεδεκίας, Zedekías; kwa KilatiniSedecias), alikuwa mfalme wa mwisho wa Yuda.Kisha kuwekwa madarakani na Nebukadneza II, mfalme wa Babuloni, kwa kiapo cha kuwa mwaminifu kwake, aliasi na kusababisha Yerusalem izingirwe tena na jeshi na hatimaye itekwe na kuteketezwa mwaka 597 KK.Ilitokea hivyo kwa sababu Sedekia alishindwa kutekeleza maelekezo aliyopewa na nabii Yeremia, ambaye utabiri wake ulitimia daima, lakini mfalme aliogopa mawaziri wake waliomuendesha walivyotaka. Kwa kushindwa kutii Neno la Mungu na kwa kuvunja kiapo chake, Biblia inamhukumu kwamba "alitenda yaliyo mabaya mbele ya Bwana". (2Fal 24:19-20; Yer 52:2-3)Nebukadneza aliagiza watoto wote wa Sedekia wauawe mbele yake na hatimaye alimpofusha na kumpeleka uhamishoni Mesopotamia alipobaki hadi kufa.
U
- Uhamisho wa Babeli
Uhamisho wa Babeli
Uhamisho wa Babeli unamaanisha kipindi cha Wayahudi kulazimishwa na Wababuloni kuishi ugenini hasa baada ya Yerusalemu kutekwa na kuangamizwa na mfalme Nebukadreza II.Matukio
Uwezekano wa kurudi ulipatikana tena Babuloni yenyewe ilipotekwa na Koreshi Mkuu, mfalme wa Uajemi (539 KK). Huyo aliwaruhusu warudi kwao na kujenga upya hekalu la Yerusalemu.Hata hivyo waliokubali hawakuwa wengi, nao walirudi vilevile kwa awamu. Kati yao kulikuwa na asilimia ya makuhani na Walawikuliko kawaida, kutokana na uhusiano wao na ibada hekaluni.Wayahudi wengine waliona maisha huko Mesopotamia yamekuwa na maendeleo kuliko yale ya awali nchini kwao.Maana ya kidini[hariri | hariri chanzo]
Vitabu mbalimbali vya Biblia vinahusika na matukio hayo kama ifuatavyo.Utabiri wake unapatikana hasa katika kitabu cha Yeremia, lakini pia katika Kitabu cha Ezekieli, bila kusahau Kumbukumbu la Sheria ambamo Musa alihimiza Waisraelikushika masharti ya Agano la Mlima Sinai ili wapate baraka na kukwepa laana.Sababu zinafafanuliwa hasa na Vitabu vya Wafalme, Mambo ya Nyakati, Kitabu cha Ezra na Kitabu cha Nehemia.Vyote vinalaumu dhambi kama chanzo cha maangamizi hayo. Utume wa Yesu
Mfululizo wa kurasa juu ya Yesu
[ficha]Yesu Kristo na Ukristo [ficha]Mazingira ya Yesu [ficha]Mitazamo juu ya Yesu Utume wa Yesu katika Injili, unaanza na ubatizo wake kwa mkono wa Yohane Mbatizaji katika mto Yordanina unakamilika katika mji mtakatifu wa Yerusalemu kwa kifo chake msalabani.[1]Injili ya Luka (3:23) inasema Yesu Kristo alipoanza utume wake alikuwa "na umri wa miaka 30 hivi".[2]Kwa kawaida wataalamu wa Biblia wanakadiria kwamba mwaka wa kubatizwa ulikuwa kati ya 27 na 29 BKna ule wa kuuawa kati ya 30 na 33.[3]Awali Yesu, baada ya kubatizwa na kukaa siku 40 katika jangwa la Yudea, alifanya kazi ya kitume zaidi katika mkoa wa Galilaya, huko alikokulia,[4] akihubiri na kuponya, pamoja na kufukuza pepo wachafu.Mbali ya hiyo miujiza yake, ni muhimu mwenendo wake wa kukaribiana na watu wa kila aina, bila ubaguzi: tendo lake la kushiriki karamu pamoja na wakosefu lilichukiza wengi, hasa kati ya madhehebu ya Mafarisayo waliokwepa watu hao. Kumbe kwa Yesu lilikuwa dokezo la kwamba Mungu anawaalika wote kutubu na kuingia raha ya ufalme wake.Wakati huohuo aliita baadhi kumfuata kama wanafunzi katika safari zake. Kati yao aliteua mitume 12 kama mwanzo wa Kanisa lake.[1][5]Hao aliwaita mitume kwa sababu aliwapeleka kwanza kwa Waisraeli (Math 8) lakini baada ya kufufuka kwa mataifa yote pia (Math 28:16-20).[6][7]Baada ya kifodini cha Yohane Mbatizaji, Yesu alijiandaa kwenda Yerusalemu kwa mara ya mwisho ili kukamilisha utume wake kwa kujitoa kafara alivyotabiriwa na Yohane: "Huyu ndiye mwanakondoo wa Mungu aondoaye dhambi ya ulimwengu".[8][9]Utume wake wa mwisho mjini Yerusalemu ulianza na tukio la kuingia Yerusalemu kwa shangwe ya Wayahudi walioamini kwamba ndiye Masiya, hasa baada ya muujiza mkuu alioufanya, yaani kumfufua Lazaro wa Bethania kutoka kaburini siku ya nne baada ya kifo. Injili zinasimulia kirefu zaidi habari za hiyo wiki ya mwisho.[15]Picha
V
- Vita za Misalaba
Vita za Misalaba
Vita za Misalaba (pia: Vita vya msalaba) vilitokea kati ya mataifa ya Wakristo wa Ulaya na watawala Waislamu wa nchi za Mashariki ya Kati wakati wa karne za 11 hadi 13, hasa kuanzia 1095 hadi 1291 katika jina la dini na kwa baraka za Kanisa Katoliki. Kaisari wa Bizanti aliomba msaada wa Wakristo wa magharibi dhidi ya mashambulio ya Waturuki Waislamu. Hivyo Papa aliwaita mataifa ya Kikatoliki ya Ulaya kuikomboa nchi takatifu. Tangu mwaka 1096 hadi mwaka 1270 kampeni za kijeshi zilianzishwa Ulaya kuelekea Yerusalemu.Kwa maana nyingine na pana zaidi "vita vya msalaba" vilikuwa jitihada za watawala wa Ulaya kutetea haki za Wakristo wenzao wa nchi hizo, au kujitetea kwa silaha na vita na wakati huohuo kueneza himaya yao pamoja na Ukristo.Jina
Jina limetokana na desturi ya wanajeshi wa vita ya kwanza ya misalaba kushona alama ya msalaba juu ya nguo zao kama dalili ya kiapo walichotoa cha kuwafukuza Waislamu katika mji wa Yerusalemu. Walifundishwa kuwa vita hivyo ni vitakatifu: atakayekufa atafika mbinguni kwa hakika. Wataalamu wanahisi kama hapo athari za mafundisho ya Kiislamu juu ya "jihadi" zimeingia katika Ukristo.Hali ya Wakristo wa Yerusalemu na Mashariki ya Kati
Tangu mwaka 637 BK mji wa Yerusalemu pamoja na nchi nzima ya Palestina ilikuwa mikononi mwa Waarabu Waislamu waliofaulu kushinda jeshi la Bizanti. Wakazi wengi wa nchi hiyo waliendelea kufuata dini zao, hasa Ukristo na Uyahudi, lakini sehemu ya wananchi polepole waligeukia pia Uislamu.Yerusalemu iliendelea kuwa lengo la wahiji Wakristo waliotaka kutembelea mahali ambako Yesu Kristo aliishi, hasa Kanisa la Kaburi na Ufufuo wa Yesu.Watawala Waarabu waliwahi kuahidi kuheshimu Wakristo walioishi chini ya utawala wao na kutunza haki zao.Hali hiyo ilibadilika vibaya mara ya kwanza wakati ya khalifa Al Hakim wa Misri aliyewatesa Wakristo kuanzia mwaka 1001; Kanisa la Kaburi na Ufufuo lilibomolewa pamoja na makanisa mengi nchini Palestina. Dhuluma ya Al Hakim ililegezwa na waandamizi wake, na kanisa hilo la Yerusalemu likajengwa upya kwa msaada wa Kaisari wa Bizanti.Amani katika mashariki ya kati ilivurugika tena kutokana na uenezi wa Waseljuki waliokuwa kabila kubwa la Waturuki kutoka Asia ya kati waliokuwa wamehamia magharibi, kupokea Uislamu na kutawala Uajemi pamoja na maeneo ya jirani. Mwaka 1071 jeshi la Waseljuki lilishinda Wabizanti kwenye mapigano ya Manzikert na kutwaa sehemu kubwa ya Anatolia (leo Uturuki) pamoja na Siria na Palestina. Vikosi vya Seljuki walishambulia pia mara kwa mara wahiji Wakristo kutoka Ulaya walioelekea kaburi takatifu mjini Yerusalemu na hija ya Kikristo ya Yerusalemu ikaona kipindi kigumu. Wakristo waliohiji huko kutoka Ulaya walishambuliwa njiani mara kwa mara.Mwaka 1095 Kaisari Aleksios I wa Bizanti alipanga kuwaondoa tena Waseljuki katika Anatolia kutoka sehemu walizowahi kutwaa miaka michache ya nyuma. Hapa alituma mabalozi kwa Papa Urban II wa Roma kwa kusudi la kupata msaada wa askari wa kukodiwa kutoka Ulaya. Alifanya hivyo miaka 40 baada ya kutokea kwa farakano la mwaka 1054 kati ya makanisa ya Waorthodoksi na Roma, labda kwa tumaini la kuanzisha upya maelewano.Wito wa Papa Urban II mwaka 1095
Papa Urban II aliwapokea mabalozi wa Bizanti katika Italia akasikia ombi la Kaisari. Inaonekana aliona nafasi ya kuwaelekeza mashariki makabaila wadogo wa Ulaya ambao walizoea kuvuruga amani ya Ulaya kwa mapigano ya mfululizo na vita ndogondogo, wakiharibu mali ya watu wengi.Kwenye sinodi ya Clermont, mbele ya maaskofu na maabati wa Ufaransa alitangaza ombi la msaada kutoka Bizanti na kuhimiza makabaila kupokea wito huu wa kuwasaidia Wakristo wenzao wa mashariki badala ya kuharibu mali ya watu wa nyumbani. Hotuba ya Papa ikapokewa na sinodi na umati mkubwa wa wasikilizaji walioitikia kwa sauti moja "Mungu anaitaka" (Deus lo vult).Makabaila kadhaa walipiga magoti mbele ya Papa wakiomba baraka kwa mipango yao ya kuitikia wito wake. Wengine walisikia habari hizo baadaye, na makabaila wengi wa Ufaransa waliamua kujiunga na mradi wa kwenda mashariki kuwasaidia Wakristo wa huko na kuwaondoa Waislamu katika nchi zilizowahi kuwa za Kikristo.Wahubiri walizunguka Ulaya kutangaza mpango huo. Ni wahubiri hao waliosambaza ujumbe wa kwamba shabaha ya vita ni Yerusalemu, ingawa wala Kaisari Aleksios wala Papa Urban waliwahi kutumia jina hilo. Lakini wakati ambapo watu wengi hawakujua kusoma na kuandika wala hawakuwahi kuona ramani jina la Yerusalemu lilijulikana kote hata kama wasikilizaji wengine hawakuelewa tofauti kati ya mahali pa dunia hii na Yerusalemu wa mbinguni uliohubiriwa pia kanisani.Vita vya msalaba vilivyoanza na kuendelea
Mwaka 1096 vilikusanyika vikundi vya watu wa kawaida walioongozwa na wahubiri waliotaka kwenda mashariki kwa hiari yao, ingawa si wanajeshi. Umati huo waliomba na kutisha miji walipopita wapewe chakula na misaada kwa sababu wengi hawakuwa na kitu wenyewe. Katika miji ya Ujerumani ya magharibi na kusini walianza kushambulia Wayahudi walioishi huko na kuwaua wengi.Mwaka 1099 jeshi la Ulaya lilifika mbele ya kuta za Yerusalemu. Baada ya mapigano mafupi jeshi la msalaba liliwashinda wateteaji Waislamu. Katika hasira ya mapigano waliua ovyo wakazi wengi sana, wazee na watoto, wakiwemo Waislamu, Wakristo na Wayahudi. Kabaila Mfaransa alipokea cheo cha "Mfalme wa Yerusalemu".Lakini miaka 100 baadaye Sultani Salah-ed-Din wa Misri aliwafukuza tena wanamsalaba kutoka Yerusalemu. Miaka 40 baadaye alirudisha mji kwa hiari baada ya kupatana na Mfalme Mjerumani. Lakini muda wote huo Wazungu walitawala sehemu ya Palestina na Siria tu. Waislamu waliwaona kama maadui. Hata Wakristo wenyeji (Waorthodoksi) hawakuwakubali kuwa wakombozi kwani walijaribu kuwaunganisha Wakristo wote chini ya Kanisa Katoliki. Safari moja iliyoondoka Ulaya mwaka 1204 ili kuikomboa Yerusalemu, kumbe ilifika mpaka Bizanti tu ambako wanajeshi wa msalaba waliteka mji, kupora utajiri na kumfukuza Kaisari wa Bizanti. Miaka 100 baadaye Kaisari alirudi na kuunda upya Ufalme wa Roma ya Mashariki.Mwaka 1291 jeshi la Kiislamu liliwafukuza kabisa wanajeshi wa msalaba katika nchi takatifu wasirudi tena. Lakini walikuwa wamevunja nguvu ya Bizanti kiasi cha kutosha. Kumbe Ulaya Magharibi iliharibu ulinzi wa dola la mashariki dhidi ya Waturuki waliofaulu baadaye kuingia Ulaya. Badala ya kufukuzwa, jeshi la Waturuki lilianza kuishambulia Ulaya Kusini-Mashariki. Mwaka 1453 ulianguka mji wa Bizanti, na mwaka 1529 Waturuki walifika mpaka Vienna, mji mkuu wa Mfalme wa Ujerumani. Hapo walirudishwa nyuma. Lakini nchi nyingi za Ulaya Kusini-Mashariki pamoja na Wakristo wao walikaa chini ya Waturuki kwa karne tatu zijazo.Tathmini
Kwa ujumla majaribio ya vita vya msalaba ya kuikomboa nchi takatifu yalishindikana. Vita hivyo vilidhoofisha Wakristo wa Mashariki waliozoea kuishi chini ya Waarabu Waislamu. Kipindi cha vita vya kidini kilisababisha mateso mengi kwa Wakristo Waorthodoksi chini ya Waislamu. Walidaiwa kulipa madeni yaliyoachwa nyuma na nduguzao kutoka Ulaya Magharibi.Katika uhusiano mgumu kati ya dini hizo mbili kule Ulaya na Mashariki ya Kati, Waislamu walivunja ahadi nyingi walizozitoa, lakini mahali pengi Wakristo walipewa nafasi za kuendelea kuishi kati ya Waislamu. Maisha haya yalikuwa mara nyingi magumu, lakini mahali pengi waliruhusiwa kuendelea na ibada zao (ila waliweza kukataliwa kujenga makanisa au hata kutengeneza makanisa ya kale isipokuwa kwa kulipa tena kodi za nyongeza). Katika mambo ya ndoa au urithi wa mali walikuwa chini ya makanisa yao. Viongozi wa makanisa yao waliwajibika mbele ya serikali ya Kiislamu juu ya ushirikiano mwema.Kwa namna hiyo jumuiya za makanisa kama vile la Kigiriki, la Kikopti, la Kisiria, la Kiarmenia n.k. zilihifadhiwa mpaka leo katika nchi za Kiarabu, isipokuwa idadi ya waumini wao iliendelea kupungua. Sababu kuu ni kwamba kama Mkristo alikuwa amegeuka Mwislamu hakuweza kurudi tena. Sheria ya Kiislamu inamruhusu Mkristo kugeukia Uislamu, lakini mtu aliyekuwa Mwislamu anastahili adhabu ya kifo akigeukia Ukristo au dini nyingine. Pamoja na hayo, Wakristo wengi walianza kuhamia nchi ambako watakuwa raia huru bila kasoro.Wakati ule Wakristo wengi walikosa vilevile ustahimilivu kwa watu wenye imani tofauti. Hakuna Mwislamu aliyeweza kubaki katika nchi za Hispania na Ureno baada ya kuvunjwa wa utawala wa Kiarabu. Lakini ipo mifano mingine: Wakristo wote walifyekwa Uarabuni kwenyewe kumbe Waislamu waliweza kubaki chini ya Waaustria Wakristo waliotawala nchi za Ulaya Kusini-Mashariki. Kweli kati ya dini hizo mbili hakuna anayeweza kujisifu tu juu ya historia yake bila kukiri makosa na kasoro zake.
Wamakabayo
Wamakabayo (kwa Kiebrania מכבים au מקבים, Makabim au Maqabim; kwa Kigiriki Μακκαβαῖοι) walikuwa familia ya mashujaa wa Israeli walioongoza mapigano dhidi ya dola la Waseleuki ili kupata uhuru wa dini na hatimaye uhuru wa taifa upande wa siasa pia.Mashujaa hao walikuwa kuhani Matatia na wanae watano waliopokezana kushika uongozi kuanzia Yuda MakabayoHabari zao zinasimuliwa katika kitabu cha kwanza cha Wamakabayo na kitabu cha pili cha Wamakabayo vilivyoandikwa na watu tofauti katika karne II KK na ambavyo vyote viwili ni kati ya vile vya Deuterokanoni vinavyokubaliwa na Wakristo wengi kama sehemu ya Biblia. Ushujaa wao unasifiwa pia na waraka kwa Waebrania kama kielelezo cha imani.Pia kuna vitabu vingine viwili juu yao (Wamakabayo III na Wamakabayo IV) ambavyo havimo katika toleo la Septuaginta wala katika Biblia ya Kikristo.Ukoo wao (Wahasmonei) ulitawala Yudea tangu mwaka 164 KK hadi 63 KK, wakisisitiza dini ya Uyahudi na kupunguza athari ya ustaarabu wa Ugiriki wa kale kati ya Wayahudi.Mazingira yao: uenezi wa utamaduni wa Kiyunani (333-63 K.K.)
Kwa muda mfupi sana Aleksanda Mkuu wa Makedonia (Ulaya Kusini Mashariki) aliteka Asia (mpaka India) na Misri. Kuanzia hapo utamaduni na lugha ya Kiyunani vikaenea pote, hata kwa Wayahudi wengi, hasa walioishi nje ya nchi yao.Chini ya utawala wa Kiyunani unabii ukaja kwisha (1Mak 9:27): badala yake yalitolewa maandiko ya kiapokaliptiko (hasa kitabu cha Danieli ambacho ni kama Ufunuo wa Agano la Kale), hadithi (Yona, Tobiti, Esta, Yudithi) na vitabu vya hekima(Mhubiri, Yoshua bin Sira, Hekima).Humo tunaona maendeleo ya ufunuo, hasa kwa sababu Wayahudi wengi walianza kusadiki ufufuko wa wafu na mengineyo.Nguvu ya imani hiyo iliwasaidia kukabili dhuluma na kifo (2Mak 7:1-41) chini ya Antioko Epifane (175 KK - 164 KK) aliyetaka kuwalazimisha waache kufuata Torati ili wajilinganishe na watu wengine. Tena akijidai kuwa tokeo la Mungu Mkuu alijenga altare kwa mungu wake ndani ya hekalu la Yerusalemu.Hapo Wayahudi wakaanza kupigania uhuru wao wa kidini na wa kisiasa chini ya ukoo wa Wamakabayo, ambao kwa imani na ushujaa mkubwa wakafaulu kushinda majeshi ya kutisha (1Mak 3:18-22), kutakasa hekalu (1Mak 4:36-61) na kurudisha ufalme wa Israeli mpaka baada ya Warumi kuweka Uyahudi chini ya himaya yao (63 K.K.).Ndiyo asili ya kundi la Mafarisayo (yaani “waliojitenga”), walioshika kwa bidii Torati kadiri ya mapokeo ya walimu wa sheria, wengi wao wakiwa walei. Kwa jumla walileta uamsho wa kiroho kati ya Wayahudi, lakini walidharau wenzao wasiojua Maandiko Matakatifu. Pia walishindana sana na Masadukayo kuhusu masuala ya dini na ya siasa hata kusababisha mauaji; kwa kuwa Masadukayo (waliokuwa na nguvu kati ya makuhani) walikataa mafundisho hayo mapya huku wakishika Torati tu.
Y
- Yezebeli
Yezebeli
Yezebeli (kwa Kiebrania אִיזֶבֶל|אִיזָבֶל |Izével|Izável|ʾÎzéḇel|ʾÎzāḇel) alikuwa malkia wa Israeli kama mke wa Mfalme Ahabu katika karne ya 9 KK.Binti wa mfalme Ethbaal wa Tiro, Finisia, alimhimiza mumewe kuachana na imani ya taifa lake katika Mungu pekee, YHWHakaangamiza manabii wake (1Fal 16:21-31 ).Aliyeokoa imani hiyo ni nabii Elia ambaye katika mlima Karmeli alishinda manabii wa miungu Baal na Ashera waliotunzwa na Yezebeli (1Fal 18).Kazi yake ilikamilishwa na mwanafunzi wake, nabii Elisha aliyempaka mafuta Yehu awe mfalme na arudishe Israeli kwa Mungu wake. Katika mapinduzi yake, Yezebeli aliuawa kikatili (2Fal 9:1-36) kama alivyotabiri Elia.Kwa uovu wake, Yezebeli anatajwa na Kitabu cha Ufunuo pia (2:20-23). - Yuda (ufalme)
Yuda (ufalme)
Ufalme wa Yuda (kwa Kiebrania מַמְלֶכֶת יְהוּדָה, Mamlekhet Yehuda) ulikuwa nchi ya Mashariki ya Kati katika karne ya 10 KK hadi karne ya 6 KK.[1][2]Mara nyingi unaitwa ufalme wa Kusini kwa sababu ulitokana na mgawanyiko wa Ufalme wa Israeli ulioendelea upande wa kaskazini.Ufalme huo uliongozwa daima na ukoo wa Daudi, isipokuwa miaka 6 (842 KK - 837 KK) aliposhikwa utawala malkia Atalia, binti au dada wa mfalme wa Israeli Ahabu. Hata hivyo kwa muda mrefu watawala wa Yuda walikuwa vibaraka wa Ashuru au nchi nyingine za jirani.[3][4]).Hatimaye, chini ya mfalme Sedekia, mfalme Nebukadneza II wa Babuloni aliangamiza ufalme huo na mji mkuu wake, Yerusalemu, mwaka 587, akihamisha kwa awamu tatu wakazi wake hadi Mesopotamia.Mwaka 539 Koreshi Mkuu, mfalme wa Persia, aliteka Babuloni na kuruhusu Wayahudi warudi kwao, si tena kama ufalme, bali kama wilaya iliyoitwa Yehud, chini ya Zerubabeli, kitukuu wa Yekonia, wa pili kuanzia mwisho kati ya wafalme wa Yuda. - Yudea
Yudea
Yudea (kwa Kilatini IVDAEA, kwa Kiebrania יהודה, Yehûḏāh au Yehuda, kwa Kigiriki Ἰουδαία) ni jina la jimbo la Dola la Roma kuanzia mwaka 6 hadi 135 BK.Asili ya jina ni kabila la Yuda, ambalo kuanzia karne ya 8 KK lilibaki karibu peke yake kati ya makabila 12 ya Israeli.
- Manase (babu)
No comments:
Post a Comment