Monday 16 October 2017

Viongozi wa Afrika

Jamii:Viongozi wa Afrika

Makala katika jamii "Viongozi wa Afrika"

Jamii hii ina kurasa 14 zifuatazo, kati ya jumla ya 14.

A

Kofi Annan

Kofi Annan

Kofi Annan
Kofi Annan alikuwa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa 1996 - 2006. Alizaliwa 8 Aprili 1938 huko KumasiGhana. Alipewa jina Kofi kuonyesha kuwa alizaliwa siku ya Ijumaa kuendana na utamaduni wa Ashanti. Jina Annan linamaanisha kuwa alikuwa ni mtoto wa nne kuzaliwa.

Elimu

Annan alienda shule ya Mfantsipim katika mji wa Cape Coast, Ghana (1954-1957). Baadaye, alienda Kumasi shule ya sayansi na teknolojia (sasa ni Kwame Nkruma Shule ya sayansi na teknolojia) kwa mwaka mmoja, na alipata udhamini ya Ford kusoma katika Marekani. Alisoma uchumi katika chuo kikuu cha Macalester, Saint Paul, Minnesota. Alipomaliza shahada ya kwanza mwaka 1961, alisoma mahusiano ya kimataifa katika chuo kikuu cha kimataifa masomo katika Geneva, Switzerland (1961-62). Alisoma katika chuo kikuu cha MIT, shule ya Sloan, na alipata shahada ya M.S.

Mtumishi wa Umoja wa Mataifa

Baada ya masomo ya uchumi alijiunga na huduma ya Umoja wa Mataifa mwaka 1962 katika WHO. 1974-1976 alifanya kazi Ghana halafu akarudi tena huduma ya UM. Akapanda ngazi kuwa Makamu wa Katibu Mkuu mhusika wa usalama aliwajibika kusimamia shughuli za wanajeshi walio chini ya UM.
Alihusika na vita ya Rwanda pia ya Yugoslavia ambako wanajeshi chini ya bendera ya UM walishirikiana.

Katibu Mkuu

1996 alichaguliwa kuwa Katibu Mkuu wa UM, akarudishwa cheo mwaka 2001. Tangu 1 Januari alifuatwa ofisini na Ban Ki-moon.

Mpatanishi nchini Kenya

Mwaka 2008 Annan alirudi katika habari za kimataifa alipofika Kenya kwa shabaha ya kupatanisha viongozi wa kisiasa waliopigana juu ya matokeo ya uchaguzi wa rais wa Kenya 2007. Akisaidiana na Grace Machel na rais mstaafu wa Tanzania Benjamin Mkapa aliendesha majadiliano kati ya wawakilishi wa ODM na PNU kwa muda wa wiki 5. Akafaulu kuleta mapatano ya ushirikiano kati ya pande zote mbili.

Maisha ya binafsi

Kofi Annan ameoa mara ya pili. Mke wake Nane Maria Annan anatoka Uswidi. Ana watoto watatu.

  1. Mohamed Abdelaziz

    Mohamed Abdelaziz

    Mohamed Abdelaziz, picha ya mwaka 2000
    Mohammed Abdelaziz ni katibu mkuu wa Polisario na rais wa Jamhuri ya Sahara ya Kidemokrasia ya Kiarabu inayodai kuwa dola la Sahara ya Magharibi.
    Alikuwa kati ya viongozi wa kwanza wa Polisario iliyopigania uhuru wa Sahara ya Magharibi. Alichaguliwa kuwa Katibu Mkuu wa Polisario mwaka 1976 halafu pia rais wa serikali ya Jamhuri ya Sahara. Anaishi katika kambi la wakimbizi la Tindouf (Algeria).
    Mohammed Abdelaziz kama kiongozi alikubali njia ya mazungumzo na diplomasia. Alihakikisha ya kwamba vita ya Polisario ilikuwa "vita" safi bila kutumia mbinu za ugaidi. Ana wapinzani wake wanaopendelea kurudi vitani dhidi ya Moroko. Amehakikisha

G

  1. Muammar al-Gaddafi

    Djibril Diallo

    Dakta Djibril Diallo ni mzaliwa wa Senegal. Amewahi kuwa mkurugenzi wa mawasiliano wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo, mshauri maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusiani na mkutano wa kimataifa wa haki za binadamu. Tena alikuwa waziri nchini Mali. Hivi sasa anajihusisha na ofisi ya Umoja ya Mataifa inayojihusisha na miradi ya kuleta amani kwa kutumia michezo. Diallo pia ni msemaji wa Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.

H

  1. Haile Selassie

    Haile Selassie

    Haile Selassie wa Ethiopia
    Haile Selassie (23 Julai 1892 – 27 Agosti 1975) alikuwa Kaisari au Negus Negeste wa Ethiopia. Alizaliwa katika kijiji kiitwacho Ejersa. Kabla ya kuwa mfalme aliitwa Ras Tafari Makonnen. Jina lake la kifalme lina maana ya "Utukufu wa Utatu (Mtakatifu)". Pia anafahamika kwa jina la Simba wa Yuda, Mfalme wa wafalme (H.I.M).
    Baba yake alikuwa mkabaila Mwethiopia aliyeitwa Ras Makonnen akawa gavana wa Harar, familia yake ina watoto 11. Alikuwa Mkristo muumini wa madhehebu ya Orthodoksi ya Ethiopia.
    Gavana wa mikoa
    Ras Tafari Makonnen alikuwa bado kijana alipopewa cheo cha gavana wa Sidamo mwaka 1907. 1911 akarithi nafasi ya gavana wa Harar.
    Wakati wa ugomvi kuhusu Negus Mwislamu Lij Iyasu (1913-1916) alisimama awali upande wa mfalme lakini alifaidika zaidi na uasi uliompindua Negus. Makabaila waliomwondoa Iyasu mwaka 1916 walimteua shangazi yake aliyekuwa binti wa Negus Negesti marehemu Menelik II Zauditu kuwa malkia, wakaamua pia Ras Tafari awe mwangalizi wake.

    Mtawala na Negus Negeste

    Kwa njia hii Ras Tafari akawa kiongozi muhimu zaidi nchini. 1928 Zauditu akampa cheo cha negus chini yake mwenyewe. Baada ya kifo cha Zauditu 1930 Ras Tafari akapokea taji na cheo cha Negus Negeste (au mfalme wa wafalme) wa Ethiopia akajiita Haile Selassie.
    Baada ya kupokea taji akafanya ziara ya Ulaya.

    Mwokozi wa Rastafari

    Habari zake zikaenea kote duniani zikasababisha kutokea kwa dini mpya ya Rastafari iliyopokea jina kutoka kwake, ingawa mwenyewe alibaki mwamini wa Kanisa la Orthodoksi, akiwa na daraja ya shemasi. Watu weusi kisiwani Jamaika, waliokuwa wajukuu wa watumwa wa asili ya Afrika, walisikia kwa mara ya kwanza ya kwamba Mwafrika anaheshimiwa na wafalme wa Ulaya, wakaona yeye ni mwokozi wa Mungu aliyerudi duniani kwa ajili ya watu weusi.
    Haile Selassie alifukuzwa katika Ethiopia mwaka 1936 Italia ilipovamia Ethiopia, akarudi 1941 kwa msaada wa Uingereza iliyoondoa Waiitalia nchini katika Vita Kuu ya Pili ya Dunia.

    Sifa na kasoro za utawala wake

    Utawala wa Haile Selassie uliingizwa Ethiopia katika Chama cha Mataifa ikiwa nchi ya kwanza ya Afrika kujiunga nacho. Baadaye ulimpa nafasi kubwa katika harakati ya uhuru wa Afrika na makao makuu ya Umoja wa Afrika yalijengwa Addis Ababa, mji mkuu wa Ethiopia.
    Katika siasa yake ya ndani alishindwa kuendeleza nchi yake yake. Alikosa nguvu na nia ya kumaliza utawala wa kikabaila nchini uliosababisha umaskini mkali kati ya wakulima waliopaswa kuwaachia wakabaila sehemu ya mazao.
    Hivyo kimataifa Haile Selassie aliheshimiwa sana lakini ndani ya nchi maendeleo yalikwama wanafunzi na wasomi wakikasirikia na wakulima maskini walikufa njaa mara kwa mara.

    Mapinduzi ya 1974 na kifo

    Njaa kubwa ya 1972–73 katika majimbo ya Wollo na Tigray ikafuatwa na mapinduzi ya kijeshi ya 1974. Kamati ya kijeshi ya Derg ikamkamata tarehe 12 Septemba 1974.
    Kifo chake kikatangazwa tarehe 28 Agosti 1975 na haieleweki kama aliuawa au kama alikufa kutokana na ugonjwa.
    Baada ya kuondolewa kwa Derg mabaki ya maiti ya Kaisari yalipatikana mwaka 1992 chini ya sakafu ya choo cha jumba la kifalme alikokamatwa. Tarehe 5 Novemba 2000 mabaki hayo yalipewa mazishi ya kifalme katika kanisa kuu la Kiorthodoksi la Addis Ababa.

    Flag of Ethiopia (1897-1936; 1941-1974).svgMakala hii kuhusu Kaizari fulani wa Uhabeshi bado ni mbegu.
    Je, unajua kitu kuhusu Haile Selassie kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?

I

  • Idris I wa Libya

    Idris I wa Libya

    Idris I wa Libya
    Idris I (Kiarabu: إدريس الأول idris-al-auwwal) (*12 Machi 1890 - 25 Mei 1983) alikuwa mfalme kwanza wa Libya kati ya 1951 hadi 1969.
    Jina lake la kiraia lilikuwa Muhamad Idris bin as-Sayyid ibn Muhamad as-Senussi (kiar.: محمد إدريس بن السيد المهدي ابن محمد السنوسي ). Alikuwa mjukuu wa Muhamad ibn Ali as-Senussi aliyeanzisha jumuiya ya Wasufi wa Senussi. Muhamad alirithi cheo cha babu yake. Alikubaliwa kama Emir wa Cyrenaika na Uingereza na Italia baada ya Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia. Baada ya Italia kuvamia Libya aliongoza vita ya porini.
    Tangu 1951 aliongoza taifa jipya la Libya. 1969 alipinduliwa na wanajeshi chini ya uongozi wa Muammar al-Gaddafi. Alikufa Misri uhamishoni mwaka 1983.

L

  1. Patrice Lumumba

    Patrice Lumumba

    Patrice E. Lumumba
    Patrice Lumumba (2 Julai 1925 – 17 Januari 1961) alikuwa mwanasiasa mwanamapinduzi wa nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Mwaka wa 1958 alikuwa miongoni mwa waanzishaji wa Chama cha Taifa la Kongo (kwa KifaransaMouvement National Congolais). Mwaka wa 1960 alipata kuwa Waziri Mkuu wa kwanza wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo baada ya kuongoza harakati za kugombea uhuru toka kwa utawala wa kikoloni wa Wabelgiji. Baada ya miezi miwili tu ya kuwa Waziri Mkuu, Lumumba alipinduliwa na baadaye kutiwa ndani kabla ya kuuawa katika mazingira ya kutatanisha katika eneo la Katanga upande wa kusini wa Kongo.

    Hadi kufikia uwaziri Mkuu

    Early life and career

    Patrice Lumumba alizaliwa na François Tolenga Otetshima, na Julienne Wamato Lomendja, ambao walikuwa wafugaji katika kijiji cha Katakokombe katika mkoa wa Mkoa wa Kasai katka jimbo la Kanyalwaunga.[1] alikuwa mwanachama wa Kikundi cha nidhamu jina halisi la Patrice Lumumba lilikuwa Élias Okit'Asombo. Jina hili likiwa na maana "heir of the cursed"ambalo lilitokana na neno la Tetela ambayo ni miongoni mwa makabila ya congo okitá/okitɔ́ ('Mrithi')[2] na asombó ('cursed or bewitched people who will die quickly').[3] Alikuwa na kaka za watatu ambao ni (Charles Lokolonga, Émile Kalema, and Louis Onema Pene Lumumba) na ndugu yao wa karibu (Tolenga Jean).[1]Alilelewa katika makuzi ya familia ya Kikatoliki, alisoma katika shule ya msingi ya Shule ya kiprotestanti , Shule ambayo ilikuwa inamilikiwa na wamisionari wa Kanisa Katoliki, na baadaye alipata mafunzo katika chuo kimoja cha serikali , alijishindia kozi mbalimbali na kisha kuajiriwa, alipata kazi katika mji wa Léopoldville ambao kwa sasa unajulikana kwa jina la Kinshasa) na baadaye katika mji wa Stanleyville ambao nao kwa sasa unajulikana kwa jina la Kisangani ambapo alifanya kazi kama karani wa posta na pia alikuwa akifanya kazi ya uuzaji wa bia kwa wasafiri. Mnamo mwaka 1951 alimuoa Pauline Opangu . Mwaka 1955 Lumumba alipanda cheo na kuwa Cercles wa mji wa Stanleyvillena baadaye alijiunga na chama cha Liberal Party of Belgium, ambapo alifanya kazi ya uhariri na usambazaji wa kijarida cha chama cha Chama cha Kiliberali cha Ubeljiji. Na baadaye alifanya ziara ya mafunzo ya wiki tatu nchini Ubeljiji,mwaka 1956 alikamatwa na kushitakiwa kosa la ubadhilifu na kuhukumiwa kifungo cha mwaka mmoja jela kwa kifungo cha nje na kisha baadaye wakili wa kibelgiji kuthibitisha kwamba Lumumba amesharejesha zile fedha aliachiliwa huru mnamo mapema mwaka 1956. Na baada ya kuachiliwa kwake alisaidiwa na kuanzisha chama chama w:Mouvement national congolais (MNC) mnamo. Mwaka 1958, alichaguliwa kuwa Rais wa chama hicho. Mnamo mwaka 1958 mwezi wa Desemba Lumumba na wenzake walikiwakilisha chama chao katika mkutano wa w:All-African Peoples' ConferenceBaraza la watu wote wa Africa mjini AccraGhana, katika mkutano huo wa Desemba wa Pan-African uliokuwa chini ya Rais wa Ghana hayati Kwame Nkrumah , Ndg Lumumba ambaye alionekana kuongea lugha nyingi zikiwemo za Tetela, French, Lingala, kiswahili, na Tshiluba alijitambulisha ziai dhidi ya imani yake kwa bara la afrika .[1]

    Uongozi wa MNC

    Mnamo mwezi wa Octoba, mwaka 1959, Lumumba, kama kiongozi wa chama cha MNC, alikamatwa kwa kosa la kuchochea vurugu za kupinga serikali ya kikoloni katika mji wa Stanleyville ambapo watu takriban 30 waliuawa na yeye alihukumiwa kwenda jela kwa muda wa miezi sita. Mnamo tarehe 18 ya mwezi Januari 1960 ambayo ilikuwa siku ya majaribio na hapohapo katika siku ya kwanza ya mkutano wa wa kuzungumzia hatma ya nchi ya kidemokrasia ya Kongo itakumbukwa kwamba licha ya Lumumba kuwa jela katika kipindi hicho cha chake cha MNC kilifanikiwa kuwashawishi wananchi kwenye uchaguzi uliofanyika mwezi Decemba na kushinda katika jamhuri ya Congo. Kutokana na nguvu ya umma iliyokuwa ikifanywa na wananchi wa Congo dhidi ya kuachiliwa kwa Lumumba kutoka kila kona, aliachiliwa na kuruhusiwa kuhudhuria katika mkutano wa Brussels. Mkutano huo ulifikia kilele tarehe 27, June 1960 kwa azimio la uhuru wa nchi ya Kongo na kupanga uchaguzi tarehe 30 ya mwaka huo huo wa 1960 Uchaguzi Mkuu wa Congo 11–25 May 1960. Lumumba na chama chake cha MNC walipata ushindi uliowawezesha kuunda serikali kwa tangazo la tarehe 23 June 1960 na Patrice Lumumba anapata cheo cha uwaziri mkuu akiwa na umri wa miaka 34 na Joseph Kasa-Vubu akiwa ndie Rais wake wa kwanza. Kwa mujibu wa katiba ya Congo mnamo tarehe 24 June serikali ilipitisha kura ya kijasiri ambayo iliamuliwa na baraza la maseneta kwamba tarehe 24 iwe ni siku ya ya kuadhimisha uhuru wa Congo.
    Maadhimisho ya uhuru wa Congo kwa mara ya kwanza yalifanyika mnamo tarehe 30 June 1960 ambapo maadhimisho hayo yalihudhuriwa pia na Mfarme Baudouinwa Ubeljijipamoja na vyombo mbalimbali vya habari kutoka nchi za nje. Lumumba alitoa hotuba yake kama Waziri mkuu katika nchi huru japo yeye alikuwa ameenguliwa katika ratiba ya shughuli hiyo.[4] Hotuba ya Mfalme wa Ubeljiji Mfalme Baudouin alihutubia kwa kutukuza utawala wa kikoloni, huku akilingania fikra za mjombae ambae alikuwa mfalme wa Ubeljijiakiitwa Léopold wa Pili glossing over atrocities committed during the Taifa huru la congo.[5] Mfalme aliendelea kutoa masharti, "aliwataka kuto kufanya mabadiliko yoyote mpaka hapo wao watakapo ona kwamba wanaweza kufanya vyema, na kwamba hawakutakiwa kufanya mabadiliko yoyote yalika bidhiwa na kwamba tutaendelea kutoa ushauri. "[6]Lumumba aliufahamisha umma kwamba uhuru uliotolewa na wabeljiji sio haukuja hivihivi:[6]
    kwa uhuru huu wa Congo hata kama tunasherehekea leo na wabeljiji , nchi rafiki ambayo tupo sawa kwa sawa, hakuna mkongoman hata mmoja ambaye atasahau kwamba vita waliyipigana hatimae wakashinda wamaeshinda, kwa mapambano yaliyokuwayakiendelea, mapambano ambayo kwamba watu tulijitoa ambayo kwayo watu walikuwa tayari kwa lolote hata kumwaga damu, kwa namna kwa hakika yalikuwa mapambano maukufu na yalikuwa na mwelekeo wa kukomesha utumwa ambao ulikuwa ukiendeshwa dhidi yetu kwa nguvu.[6]

    Filamu

    • Lumumba : Un crime d'Etat
    • Lumumba
    • La Mort du Prophète

M

  1. Nelson Mandela

    Nelson Mandela

    Tuzo Nobel.png
    Nelson Mandela
    Nelson Rolihlahla Mandela (18 Julai 1918 - 5 Desemba 2013) alikuwa mwanasiasa nchini Afrika Kusini, kiongozi wa mapambano dhidi ya siasa ya ubaguzi wa rangi (Apartheid), mfungwa jela kwa miaka 27 halafu rais wa kwanza aliyechaguliwa kidemokrasia katika nchi yake.
    Alikuwa mwanasheria na mwanachama, baadaye kiongozi wa chama cha ANC kilichopigania haki za binadamu wote nchini Afrika Kusini.

    Maisha

    Utoto na ukoo

    Mandela alizaliwa tarehe 18 Julai 1918 katika familia ya kabila la Waxhosa kwenye kijiji cha Mvezo karibu na Umtata iliyokuwa kwenye Jimbo la Rasi.[1]
    Alipewa jina la Rolihlahla linalomaanisha "anayevuta tawi la mti" kwa maana ya "mwenye kuleta matata" katika lugha ya Kixhosa[2]. Baadaye alijulikana kwa jina la ukoo wake "Madiba". Jina la Nelson alilipokea kutoka kwa mwalimu wake siku alipoanza kwenda shule.
    Alitoka katika familia ya kifalmeBaba wa babu yake Ngubengcuka alikuwa mfalme wa Wathembu katika maeneo ya Transkei wa jimbo la kisasa la Rasi Mashariki la Afrika Kusini.
    Baba yake Gadla Henry Mphakanyiswa alikuwa chifu na mshauri wa mfalme tangu mwaka 1915 hadi 1926Mama yake Nelson, Nosekeni Fanny, alikuwa mke wa tatu[3]
    Miaka ya kwanza aliishi kijijini alipojifunza mila na desturi za Waxhosa na kutunza mifugo pamoja na wavulana wengine.
    Baba aliaga dunia Nelson alipokuwa na umri wa miaka tisaAlibatizwa katika Kanisa la Kimethodisti akawa Mkristo wa kanisa hilo hadi kifo chake.
    Baada ya kifo cha baba, mama alimpeleka kwa chifu mkuu wa Wathembu aliyemlea kama mtoto wake. Pamoja na wazazi wake wapya alihudhuria ibada za kanisani kila Jumapili zilizoimarisha imani yake ya Kikristo.
    Akaendelea kusoma katika shule ya Kimethodisti aliposoma KiingerezaKixhosahistoria na jiografia. Katika ikulu ya chifu alisikia masimulizi mengi kuhusu historia ya Waafrika kutoka wageni waliokuja kumwaona baba wa kambo.

    Elimu

    Mwaka 1925 babake alimtuma kusoma shule ndogo ya Kimethodisti alipofanyikiwa vema. Baada ya kifo cha baba aliishi kwa chifu wa Watembo na hapo kwene umri wa miaka 16 alishiriki katika sherehe ya jando alipotahiriwa na kupokea jina Dalibunga.[4]
    Baadaye aliendelea kusoma kwenye shule ya sekondari ya „Clarkebury Boarding Institute“ huko Engcobo iliyokuwa shule ya bweni kubwa kwa ajili ya vijana kutoka Wathembo.[5]
    Photograph of Mandela, taken in Umtata in 1937
    Hapa alianza mazoezi ya michezo na kupenda kazi ya bustani aliyoendelea kwa maisha yote. [6] Baada ya miaka miwili alipokea cheti kidogo cha elimu ya sekondari.[7]
    Mwaka 1937 kwenye umri wa miaka 19 aliendelea kwenye chuo cha Wamethodisti huko [[Fort Beaufort[8]. Hapo alikuwa mara ya kwanza rafiki na kijana nje ya kabila lake aliyekuwa Msotho akaathiriwa na mwalimu mpendwa Mxhosa aliyevunja mwiko kwa kumwoa mke kutoka kwa Wasotho [9]Mandela alitumia muda mwingi huko Healdtown kwa kufuata michezo ya kukimbia na bondia.[10]
    Tangu 1939 alianza masomo kwa shahada ya kwanza kwenye Chuo Kikuu cha Fort Hare, chuo kwa ajili ya wanafunzi Waafrika katika jimbo la Rasi Mashariki. Masomo yake yalikuwa Kiingereza, anthropolojia, siasa na sheria. Wakati ule alitaka kuendelea kuwa mfasiri au afisa katika Idara ya Shughuli za Wazalendo (kitengo cha serikali ya Kizungu kwa maeneo ya Waafrika katika Afrika Kusini). [11] Katika bweni lake alikuwa rafiki wa Kaiser Matanzima na Oliver Tambo aliyeendelea kuwa rafiki yake kwa miaka mingi ijayo.[12] Pamoja na kupenda michezo Mandela alijifunza dansi ya Kizungu [13], alishiriki tamthiliya kuhusu about Abraham Lincoln,[14] akatoa darasa la Biblia katika kanisa.[15]
    Mandela alihukumiwa kifungo cha maisha kwa miaka 27 kutokana na harakati zake za kuupinga ubaguzi wa rangi. Alifungwa katika kisiwa cha Robben.
    Baada ya kuachiliwa huru mwaka 1990 alianzisha sera ya maridhiano au sera ya amani baina yake na watu weupe nchini Afrika Kusini, jambo ambalo watu wengi hawakulitegemea.
    Mwaka wa 1993, pamoja na Frederik Willem de Klerk alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Amani ambayo ni tuzo ya nadra sana kutolewa duniani.
    Baada ya kutengana na mke wake, Winnie Madikizela, alimuoa aliyewahi kuwa mke wa rais wa MsumbijiSamora Machel, [Graca Machel]
  2. Robert Mugabe

    Robert Mugabe

    Robert Mugabe (2009)
    Robert Gabriel Mugabe (* 21 Februari 1924) amekuwa kiongozi wa Zimbabwe tangu 1980. Yeye ni mwenyekiti wa chama tawala cha ZANU. 1980 alikuwa waziri mkuu na 1987 Rais wa Zimbabwe. Kabla ya wakati ule aliongoza upinzani wa ZANU dhidi ya serikali ya walowezi Waingereza nchini waliofuata siasa ya ubaguzi wa rangi.
    Mugabe alirudiwa katika uchaguzi mbalimbali. Tangu mwaka 2000 uchaguzi hizi zimekuwa mashakani kutokana na matishio na matumizi ya mabavu dhidi ya wapinzani. Utawala wa Mugabe umeitwa wa kidikteta tangu mwaka 2002. Kutokana na mashataka dhidi ya serikali ya Mugabe ya kudharau haki za binadamu nchi Zimbabwe ilisimamishwa ndani ya Jumuiya ya Madola. Mugabe pamoja na mawaziri wake na viongozi wa chama chake hawaruhusiwi kusafiri kwenda nchi za Umoja wa Ulaya na Marekani.
    Mwanzoni wa utawala wake Mugabe alisifiwa kujenga uchumi na sera ya elimu nchini. Zimbabwe ilikuwa nchi iliyouza vyakula vingi nje. Tangu mwanzo wa milenia mpya pamoja na mashtaki ya udikteta hali ya uchumi ulirudi nyuma. Takriban milioni mbili za raia wa Zimbabwe wameondoka nchini wakikaa kama wakimbizi Afrika Kusini.

    Tuhuma za mauaji na ukandamizaji

    Baada tu ya kushika madaraka, Mugabe aliamua kuimarisha jeshi lake la kumlinda (liitwalo Gukurahundi) ambalo lilijengwa na watu kutoka kabila lake la wa-Shona. Nchi hiyo ilikuwa tayari imegawanyika kikabila hata katika uchaguzi wa kwanza wa 1980, washona wote walimchagua Mugabe na Wa-Ndebele na wabunge kutoka chama cha ZANU. Wakati wandebele walichagua viongozi kutoka chama cha ZAPU kilichoongozwa na Joshua Nkomo.
    Mara baada ya uchaguzi tu mwezi Novemba 1980 Mugabe alianza kampeni ya kuua kwa wingi watu wa kabila la wa-Ndebele ambao mjia wao mkubwa unaitwa Bulawayo. Ingawa mauaji hayo hayakufikia kiwango cha yale ya Rwanda na Burundi, waliuawa wanawake, wanaume, watoto na hata vichanga vilivyokuwa matumboni. Mwaka 1981 pia Mugabe aliendelea kuua wandebele tukio ambalo halikutangazwa sana na vyombo vya habari. Kuanzia enzi hizo hadi leo raisi Mugabe amejaribu kushinda kila uchaguzi unaokuja nchini huko kwa kutumia nguvu za kikabila na mabavu.
    Mugabe ametangazwa upya na chama cha ZANU kama mgombea wa urais katika uchaguzi wa 2008.
    Administradors.pngMakala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu.
    Je, unajua kitu kuhusu Robert Mugabe kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?

N

  1. Kwame Nkrumah

    Kwame Nkrumah

    Kwame Nkrumah pamoja na Martin Luther King.
    Kwame Nkrumah (21 Septemba 1909 - 27 Aprili 1972) alikuwa Rais wa kwanza wa Ghana na mmoja wa viongozi wenye nia ya kujenga Muungano wa Afrika, tena mchochezi wa falsafa ya Umajinuni.

    Maisha

    Miaka ya kwanza katika Ghana

    Kwame Nkrumah alizaliwa mnamo mwaka 1909 katika kijiji cha Nkroful kwenye koloni la Gold Coast (leo Ghana). Nkrumah mwenyewe aliandika ya kwamba tarehe ilikuwa 18 Septemba 1909 iliyokuwa siku ya Jumamosi. Hii inalingana na jina "Kwame" ambalo katika utamaduni wa Waakan ni jina la mwanamume aliyezaliwa siku hiyo. Ila tu aliposoma Marekani alijulikana kwa jina la Francis Nwia Kofi Nkrumah na "Kofi" ni jina la mwanamume aliyezaliwa siku ya Ijumaa.
    Baba yake, ambaye jina lake halikuhifadhiwa, alikuwa na kazi ya fundi dhahabuMama yake aliitwa Nyanibah akaishi hadi kifo chake na kwa muda alitunza kaburi la mwanawe[1][2].
    Mtoto alilelewa kijijini pamoja na watoto wengine wa babake na ukoo. Mama alimsomesha katika shule ya msingi ya misioni ya Kanisa Katoliki[3]. Alipita madarasa kumi katika muda wa miaka minane.
    Mnamo 1925 alikuwa Mkristo aliyebatizwa akafundisha katika shule yake kama mwalimu msaidizi. Kutoka hapo alikaribishwa na mchungaji Alec Garden Fraser, mkuu wa chuo cha ualimu cha serikali mjini Accra kujiunga na masomo huko.[4] [5] Huko makamu wa mkuu Kwegyir Aggrey aliyewahi kusoma Marekani alimweleza mafundisho ya Marcus Garvey na W. E. B. Du Bois. Aggrey, Fraser na walimu wengine wa chuo walifundisha ya kwamba ushirikiano wa watu wa rangi zote ni shabaha kwa maendeleo ya Gold Coast. Lakini Nkrumah alifuata mwelekeo wa Marcus Garvey akiamini ya kwamba ni lazima nchi yake itawaliwe na Waafrika wenyewe.[6] [7]
    Baada ya kumaliza masomo yake mwaka 1930 Nkrumah aliajiriwa kama mwalimu wa shule ya msingi ya Kikatoliki huko Elmina na baada ya mwaka 1 alikuwa mwalimu mkuu wa shule ya Axim. Huko alianza kushiriki katika majadiliano ya kisiasa akaanzisha "Nzima Literary Society". Mwaka 1933 aliendelea na kuwa mwalimu kwenye seminari ya Kikatoliki mjini Amissa.

    Marekani

    Alipokuwa mwanafunzi wa chuo Nkrumah alisikia hotuba ya mwandishi Nnamdi Azikiwe (baadaye alikuwa rais wa Nigeria). Alikutana naye, na Azikiwe alimpa ushauri kuendelea na masomo yake huko Marekani kwenye chuo cha Lincoln College alikowahi kusoma mwenyewe an kilichokuwa chuo kwa Waamerika Weusi. Nkrumah angependelea kusoma London(Uingereza) lakini alishindwa mitihani ya kuingia. Hivyo kwa msaada wa mjomba tajiri alisafiri Pennsylvania na kuanza masomo huko Lincoln kwenye Oktoba 1935.[8].
    Hakuwa na pesa nyingi, hivyo alifanya kazi ndogo kama kusafisha vyombo hotelini. Siku za Jumapili alisali katika makanisa ya Weusi mjini Philadelphia na New York[9] Mwaka 1939 alimaliza masomo akapokea digrii ya bachelor katika fani ya uchumi.
    Chuo kikampa nafasi ya mhadhiri msaidizi kwa masomo ya falsafa akaendelea kusoma teolojia akachukua BA mwaka 1942. Alisoma pia Chuo Kikuu cha Pennsylvania alipomaliza digrii za master katika falsafa na ualimu.[10]. Wakati huohuo alishirikiana na mwanaisimu William Everett Welmers kutunga kitabu cha sarufi ya Fante iliyokuwa lugha yake ya kwanza.[11]
    Wakati wa likizo Nkrumah alipenda kwenda Harlem (New York) iliyokuwa kitovu cha kiutamaduni kwa Waamerika Weusi. Hapa alienda kuzunguka mitaani na kusikiliza wahubiri wa barabarani.
    These evenings were a vital part of Kwame Nkrumah's American education. He was going to a university—the university of the Harlem Streets. This was no ordinary time and these street speakers were no ordinary men .... The streets of Harlem were open forums, presided over [by] master speakers like Arthur Reed and his protege Ira Kemp. The young Carlos Cook, founder of the Garvey oriented African Pioneer Movement was on the scene, also bringing a nightly message to his street followers. Occasionally Suji Abdul Hamid, a champion of Harlem labor, held a night rally and demanded more jobs for blacks in their own community .... This is part of the drama on the Harlem streets as the student, Kwame Nkrumah walked and watched.[12]
    Chuoni Nkrumah alikusanya wanafunzi kutoka nchi za Afrika na kuanzisha "African Students Association of America and Canada" akichaguliwa kuwa mwenyekiti wake. Katika majadiliano ya kundi hili alisisitiza haja ya nchi zote za Afrika kushikamana baada ya uhuru, si kufuata shabaha za pekee kwa kila koloni. [13] Nkrumah alishiriki pia katika Mkutano wa Umoja wa Afrika mjini New York wa mwaka 1944 uliosisitiza Marekani kusaidia nchi za Afrika kufikia uhuru baada ya Vita Kuu ya Pili ya Dunia[14]
    Katika kipindi chake nchini Marekani Nkrumah alikutana pia na wafuasi wa Umarx, hasa wa mwelekeo wa Trotzki. Hasa C.L.R. James kutoka Trinidad alikuwa na athira juu yake. Nkrumah aliandika baadaye ni Johnson aliyemfundisha namna gani kufanya kazi ya kisasa kwa siri kama ni lazima.[15].
    Wakati Nkrumah alitaka kurudi Afrika baada ya vita kwenye mwaka 1945, James alitunga barua ya kumtambulisha kwa marafiki huko London akiandika: "Huyu kijana anakuja sasa kwenu. Si mtu mwelekevu mno, lakini fanyeni mnachoweza kumsaidia; anataka kuwafukuza Wazungu kutoka Afrika". [16]

    London

    60 Burghley Road, Kentish Town, London, where Nkrumah lived when in London between 1945-1947
    Nkrumah alfika London mwezi wa Mei 1945 akajiandikisha kwenye chuo cha London School of Economics kama mwanafunzi wa PhD katika anthropolojia. Aliacha baada ya mhula mmoja, akajiandikisha kwenye chuo kikuu kwa shabaha ya kufuata PhD ya falsafa lakini hakuendelea. Mwishoni alijaribu masomo ya sheria. Profesa wa falsafa Alfred Ayer hakumwona Nkrumah kuwa mwanafalsafa bora. Alisema juu yake: "Nilimpenda nikafurahi kujadili naye. Lakini kwangu hakuonekana kuwa na akili ya mchambuzi. Alitafuta majibu ya harakaharaka. Labda sehemu ya matatizo yake ilikuwa ya kwamba hajajikazia kuendeleza thesis yake. Kwake ilikuwa njia tu ya kupita muda hadi aliweza kurudi Ghana" [17]
    Nkrumah alitumia nguvu nyingi kupanga mikutano ya siasa. Alikuwa kati ya waratibu walioandaa mkutano wa Pan-African Congress mjini Manchester (15-19 Oktoba 1945).[18] Wajumbe wa mkutano huu walipatana kuelekea kwa Shirikisho la Maungano ya Madola ya Afrika na kujenga utamaduni mpya kwa Afrika bila ukabila na siasa itakayounganisha usoshalisti au ukomunisti na demokrasia[19] Kati ya wajumbe waliohudhuria walikuwa mzee W.E.B. Dubois pamoja na Waafrika walioendelea kuwa viongozi wa nchi zao baada ya uhuru kama vile Hastings Banda wa Nyasaland (Malawi), Jomo Kenyatta wa KenyaObafemi Awolowo wa Nigeria na C.L. R. James.[20]

    Kurudi Ghana

    Baada ya kurusi Gold Coast, Nkrumah kwenye mwaka 1947 alikuwa katibu mkuu wa chama cha United Gold Coast Convention (UGCC). Mwaka 1948 kulitokea ghasia ya "Accra Riots"; askari Waafrika wa jeshi la Kiingereza walioachishwa baada ya vita kuu walidai malipo waliyoahidiwa. Nkrumah alihutubia mkutano wao; baada ya maandamano yao kuvunjwa na polisi na watu kufa katika ghasia iliyofuata, polisi ilikamata viongozi wa chama cha UGCC.
    Mwaka 1949 Nrumah alitoka katika UGCC akaunda Convention People’s Party (CPP) iliyokuwa na madai makali zaidi. Mwaka 1951 CPP ilipata kura nyingi katika uchaguzi baada ya kudai uhuru mara moja. Nkrumah aliyekuwa tena mbaroni aliruhusiwa kugombea, alipata asilimia 98,5 za kura mjini Accra akaachwa huru. Mwaka 1952 alichaguliwa na Halmashauri ya Kisheria kuwa waziri mkuu wa koloni.
    Aliendelea kuongoza serikali na mwaka 1957 wakati wa uhuru alibadilisha jina la nchi kuwa Ghana. Hii ilikuwa koloni la kwanza kupata uhuru katika Afrika ya Magharibi, baada ya Liberia. Mwaka huohuo alifunga ndoa na Fathia Helen Ritzk, Mkristo wa Kikopti kutoka nchi ya Misri.

    Baada ya uhuru

    Nkrumah alianzisha mipango mingi ya kuendeleza Ghana kiutamaduni, kielimu na kiuchumi. Pamoja na Haile Selassie wa Ethiopia aliunda Umoja wa Muungano wa Afrika (kwa Kiingereza: Organisation of African Union - OAU). Alikaribia nchi za kikomunisti na kuajiri washauri na wahandisi kutoka Urusi na China.
    Alijipatia maadui kati ya machifu waliokuwa na mamlaka kubwa wakati wa ukoloni lakini sasa wengi waliachishwa au kupinduliwa na serikali kama hawakufuata maagizo yote kutoka juu. Alipata pia maadui kati ya wakulima tajiri wa kakao kwa sababu aliongeza sana kodi wakati bei ya zao hili kwenye soko la dunia ilipanda juu. Mnamo mwaka 1960 bei za kakao zilishuka sana na hapo alikosa pesa kwa miradi mingi aliyoanzisha wakati mapato ya kakao yalikuwa juu.
    Gharama za miradi kubwa zililipiwa kwa kukopa pesa nje ya nchi. Deni la taifa lilikua haraka. Baada ya bidhaa kadhaa kuwa haba, serikali ilijaribu kuongoza uchumi kwa mfano wa nchi za kikomunisti. Upinzani kati ya wananchi ulitazamwa kama uasi na watu wengi walikamatwa. Kodi zilipandishwa.
    Inasemekana ya kwamba pia huduma za siri za CIA (Marekani) na MI5 (Uingereza) zilichochea wapinzani wa Nkrumah waliopanga kumpindua. Mwaka 1966 alipokwenda safari ya kutembelea China na Korea ya Kaskazini kamati ya siri ya upinzani pamoja na jeshi la ulinzi na polisi ya kitaifa ilipindua serikali.
    Nkrumah alishindwa kurudi. Kwa miaka kadhaa alikaa Guinea. Baada ya kugonjeka alihamia kwa tiba huko Romania alipoaga dunia mwaka 1972.

    Vitabu vilivyoandikwa na Kwame Nkrumah

    A postage stamp from the Soviet Union marking the 80th anniversary of his birth
    • "Negro History: European Government in Africa", The Lincolnian, 12 April 1938, p. 2 (Lincoln University, Pennsylvania) - see Special Collections and Archives, Lincoln University
    • Ghana: The Autobiography of Kwame Nkrumah (1957). ISBN 0-901787-60-4
    • Africa Must Unite (1963). ISBN 0-901787-13-2
    • African Personality (1963)
    • Neo-Colonialism: the Last Stage of Imperialism (1965). ISBN 0-901787-23-X
    "The essence of neo-colonialism is that the State which is subject to it is, in theory, independent and has all the outward trappings of international sovereignty. In reality its economic system and thus its political policy is directed from outside." (Introduction)

O

  1. Olusegun Obasanjo

    Olusegun Obasanjo

    Obasanjo
    Matthew Olusegun Aremu Obasanjo (* 5 Machi 1937) ni jenerali mstaafu wa Jeshi la Nigeria aliyekuwa rais wa Nigeria mara mbili. Awamu lake la kwanza lilikuwa kama rais wa kijeshi kati ya 1976 hadi 1979 halafu awamu la pili kama rais aliyechaguliwa na wananchi kati ya 1999 hadi 2007.
    Obasanjo alizaliwa katika kabila la Wayoruba akalelewa kama Mkristo wa kibaptisti. 1958 akajiunga na jeshi akapanda ngazi haraka. 1967-1970 alishiriki katika vita dhidi ya Biafra. Baada ya uasi wa jeshi chini ya Murtala Mohammed mwaka 1975 alipewa cheo cha makamu wa rais. 1976 Mohammed aliuawa na wapinzani ndani ya jeshi waliokosa kumwua Obasanjo pia. Obansajo aliweza kukandamiza uasi akateuliwa na halmashauri ya kijeshi kuwa raisi mpya. Alitumia nafasi yake kuandaa uchaguzi wa 1979 akakabidhi madaraka kwa rais aliyechaguliwa Shehu Shagari.
    Kati ya 1980 hadi 1995 alikuwa na vyeo mbalimbali vya kimataifa akagombea nafasi ya Katibu Mkuu wa UM halafu alikuwa mwenyekiti wa halmashari ya Transparency International (TI). Dikteta wa kijeshi Sani Abacha alimfunga gerezani kati ya 1995 hadi 1998.
    Wakati wa uchaguzi baada ya kifo cha Abacha aligombea uraisi kama mgombea wa chama cha People's Democratic Party akashinda akawa rais tena tangu 1999. Mwaka 2003 alirudishwa madarakani.
    Obasanjo alijaribu kubadilisha katiba ili aweze kuwa na nafasi ya tatu lakini hakufaulu kupata wabunge wa kutosha kwa kubadilisha katiba.
    Katika kura ya 2007 alisimama upande wa mgombea Umaru Yar'Adua aliyechaguliwa. Kukabidhi kwa madaraka kutoka Obasanjo kwenda Yar'Adua kulikuwa mara ya kwanza katika historia ya Nigeria ya kwamba marais wawili waliochaguliwa na wananchi waliweza kufuatana.

R

  1. Rais wa Nigeria

    Rais wa Nigeria

    Goodluck Jonathan
    Rais wa Nigeria ni mkuu wa dola wa The President of Shirikisho la Jamhuri ya Nigeria na kiongozi wa serikali. Vyeo vyake ni "Rais wa Shirikisho la Jamhuri ya Nigeria" na Amiri Jeshi Mkuu wa jeshi la Nigeria. Rais wa sasa ni Goodluck Jonathan.

    Masharti

    Kila mtu anaweza kuchaguliwa kuwa rais wa Nigeria kama
    • yeye ni raia wa Nigeria
    • umri wake ni miaka 40 au zaidi
    • ni mwanachama wa chama cha kisiasa nchini na kukubaliwa na chama hiki
    Kufuatana na katiba anaweza kuhudumia awamu mbili za miaka minne akichaguliwa tena baada ya awamu ya kwanza.

    Madaraka ya rais wa Nigeria

    Kufuatana na katiba rais huwa na madaraka yafuatayo:
    • kukubali na kutia sahihi sheria zilizopitishwa bungeni
    • kurudisha sheria bungeni akiwa na mashaka kama sheria inalingana na katiba
    • kupeleka sheria mbele ya mahakama kuu itakayoamua kama inalingana na katiba
    • kuitisha bunge kwa makao maalumu kwa shughuli za pekee
    • kusimamika maafisa kufuatana na katiba au sheria
    • kusimamika kamati za utafiti
    • kuitisha kura ya wananchi kulingana na sheria
    • kupokea na kutambua mabalozi wa nchi za nje
    • kusimamika mabalozi
    • kusamehe wakosaji waliohukumiwa na mahakama

    Orodha ya wakuu wa dola na maraisi wa Nigeria

    Katika orodha ifuatayo kuna majina ya watu waliokuwa wakuu wa dola nchini Nigeria tangu uhuru katika mwaka 1960:
    JinaTarehe za uraisiAlikotoka
    MwanzoMwishoNamna ya kumaliza kipindi
    Abubakar Tafawa Balewa (Waziri Mkuu)1 Oktoba 196015 Januarii 1966Alipinduliwa na jeshiNorthern People’s Congress
    Nnamdi Azikiwe1 Oktoba 196316 Januari 1966National Council of Nigeria and the Cameroons
    Johnson Aguiyi-Ironsi16 Januari 196629 Julai 1966Alipinduliwa na jeshijeshini
    Yakubu Gowon1 Agosti 196626 Julai 1975Alipinduliwa na jeshiJeshini
    Murtala Mohammed29 Julai 197513 Februari 1976Kifo baada ya kujeruhiwa na waasi wa kijeshiJeshini
    Olusegun Obasanjo13 Februari 19761 Oktoba 1979Alishindwa katika uchaguziJeshini
    Shehu Shagari1 Oktoba 197931 Desemba 1983Alipinduliwa na jeshiNational Party of Nigeria
    Muhammadu Buhari31 Desemba 198327 Agosti 1985Alipinduliwa na jeshiJeshini
    Ibrahim Babangida27 Agosti 198526 Agosti 1993alijiuzuluJeshini
    Ernest Shonekan26 Agosti 199317 Novemba 1993alijiuzulu(bila chama)
    Sani Abacha17 Novemba 19938 Juni 1998KifoJeshini
    Abdulsalami Abubakar8 Juni 199829 Mei 1999Alishindwa katika uchaguziJeshini
    Olusegun Obasanjo29 Mei 199929 Mei 2007Alishindwa katika uchaguziPeople's Democratic Party
    Umaru Yar’Adua29 Mei 20075 Mei 2010KifoPeople's Democratic Party
    Goodluck Jonathan5 Mei 2010People's Democratic Party

S

  1. Shaka Zulu

    Shaka Zulu

    Picha ya Shaka Zulu mnamo mwaka 1824
    Shaka (pia: Tshaka, Tchaka au Chaka; halafu: Shaka Zulu, Shaka ka Senzangakhona) (* takriban 1781 - 1828 BK) alikuwa kiongozi wa Wazulu aliyebadilisha ukoo mdogo wa Kinguni kuwa kabila au taifa kubwa lililotawala maeneo mapana ya Afrika Kusini hasa Natal ya leo.
    Sifa zake zimetokana na uwezo wa kupanusha utawala wake kutoka eneo ndogo la 260 km² kuwa 28.500 km², kuvunja nguvu ya makabila mengine na kuyaunganisha na taifa lake. Katika historia ya kijeshi ya Afrika alianzisha mbinu mpya zilizopanusha uwezo na enzi yake. Sifa hizi, jinsi ilivyo mara nyingi na viongozi wanaotegemea nguvu ya kijeshi, zimeenda pamoja na vita na uharibufu mwingi. Miaka ya Shaka ilianzisha kipindi cha mfecane yaani "uharibifu" kinachokumbukwa na mataifa mengi ya Afrika Kusini.

    Maisha yake

    Kijana

    Shaka alikuwa mtoto wa chifu Senzangakhona ka Jama na Nandi binti wa chifu wa Langeni. Jina lake ni kutokana na neno la kizulu "iShaka" linalomtaja mdudu ambaye katika imani ya utamaduni wa Kizulu anasemekana kuvuruga hedhi ya wakinamama. Jina hili ni dalili la kuzaliwa nje ya utaratibu. Hivyo miaka ya kwanza ya Shaka ilikuwa miaka migumu bila baba anayejulikana rasmi akisikia kudharauliwa na watu wengine. Utoto huu ulisababisha hasira ndani yake akalipiza kisasi baadaye.
    Kama kijana Shaka alikaa kwa kabila kubwa zaidi ya Mthethwa alikoingia pamoja na hirima yake katika jeshi. Wakati ule ukoo wa Wazulu walikubali Wamthehtwa kuwa mabwana wao. Chifu wa Mthethwa alikuwa Dingiswayo aliyeanzisha utaratibu mpya wa impi yaani kupanga watu wake vitani katika vikundi na kuwa na ngazi mbalimbali za mamlaka. Shaka alihudumia miaka sita katika vita za Dingiswayo akawa hodari sana na kujifunza uongozi alioboresha baadaye.

    Kurudi kwa Wazulu

    Baada ya kifo cha babake Shaka alirudi kwa Wazulu kwa msaada wa Dingiswayo akachukua uongozi mnamo mwaka 1812. Baada ya kuwa kiongozi akalipiza kisasi maadui wa utoto wake akiwaua kwa njia mbalimbali.
    Shaka aliendelea kukubali ubwana wa Mthethwa na Dingiswayo hadi huyu aliuawa vitani na kabila la Ndwandwe mwaka 1817. Lakini pamoja na hayo alipigana vita na koo au makabila madogo jirani. Mbinu yake ilikuwa kuwashambulia waliompinga au kuwa hatari kwake; wanawake na watoto waliingizwa katika ukoo wake, pamoja na wanajeshi wa kiadui wasiouawa lakini waliokubali kumfuata baada ya kushindwa. Kwa njia hiyo ukoo mdogo wa Wazulu uliendelea kukua.
    Eneo la milki ya Shaka

    Kupanusha utawala na mfecane

    Baada ya kifo cha Dingiswayo mw. 1817 Shaka alishambulia kabila kubwa la Ndwandwe akawashinda kwenye mapigano ya kilima cha Gqokli kwa sababu ya mbinu zake za kijeshi ingawa idadi ya watu wake ilikuwa nusu tu ya adui.
    Katika miaka iliyofuata Shaka aliendelea kushambulia vikundi vya jirani na kuwaingiza katika utawala wake. Makabila mengine walimfuata bila vita wakikubali uongozi wake na kuingiza vijana wao katika impi au vikosi vya kijeshi vya Shaka. Alituma viongozi au majenerali zake pamoja na impi pande mbalimbali hadi Msumbiji au pia Zimbabwe. Vikundi kama Ndebele huko Zimbabwe au hata Wangoni katika Tanzania ni matokeo ya matembezi ya impi za kizulu zilizoenda mbali na kupoteza mawasiliano na nyumbani.
    Vita hizi zilisababisha makabila mengine kukimbia na kuhamahama wakishambulia majirani zao hivyo kupanusha eneo la vita katika nchi mbali na Wazulu wenyewe. Kipindi hiki kinakumbukwa kwa majina kama "mfecane" (Kizulu) au "difaqane" (Kisotho) kuwa miaka 30 ya vita na kifo.
    Katika mawazo ya wataalamu Shaka aliandaa upanuzi wa Makaburu kwa uharibifu wa vita zake. Makaburu walipoanza kuenea ndani ya Afrika Kusini walikuta maeneo mazuri bila watu lakini maghofu ya kuonyesha watu waliwahi kuishi hapa. Pamoja na hayo makabila mengine kama WasothoWaswaziWandebele au Wagazawalioshambuliwa walijifunza mbinu za kijeshi wakifaulu kujitetea na kuanzisha mataifa makubwa yakiunganisha wenyewe koo na makabila madogo zaidi.

    Kifo

    Utawala wa Shaka ulikuwa na tabia za kinyama zilizosababisha chuki nyingi dhidi yake. Baada ya kifo cha mamake Nandi alikuwa na hasira kiasi cha kuua watu 7000 kati ya wanajeshi wake kwa kosa la kutoonyesha huzuni ya kutosha na kuamuru kipindi cha kufunga miezi mitatu. Aliamuru mashamba yasilimwe kwa mwaka mmoja na kila mwanamke aliyeonekana kuwa na mimba katika kipindi hiki aliuawa pamoja na mumewe. Wataalamu wengine huona ya kwamba wakati ule Shaka alionekana kuwa na kichaa. Maadui walifanya mipango dhidi yake mwishowe aliuawa na ndugu zake. Mwaka 1828 impi nyingi zilikuwa mbali vitani ikuli ikawa bila ulinzi wa kutosha. Kaka zake Dingane na Mhlangana walimwua na kutupa maiti shimoni.
    Dingane alimfuata Shaka akaua vingozi wengi waliokuwa waaminifu kwa Shaka.

    Mafanikio ya kijeshi ya Shaka

    Shaka aliboresha utaratibu alioukuta katika utumishi wa Dingiswayo. Wataalamu hutofautiana ni kiasi gani ya kwamba Shaka alianzisha mbinu kadhaa au kiasi gani ndiye Shaka aliyeunganisha mbinu mbalimbali zilizowahi kujulikana lakini yeye alifuata utaratibu kuzitumia kushinda viongozi wote wengine. Kati ya mbinu alizotumia ni zifuatazo:

    Silaha mpya

    Utamaduni wa Wanguni ulikuwa mikuki ya assegai na kila mtu alibeba tatu. Shaka aliona silaha za kutupwa ni hasara. Aliongea mwenyewe na wahunzi akawapa wanajeshi silaha katikati ya mkuki na upanga - "Iklwa". Haikufaa kutupwa bali kushikwa hivyo kuwalazimisha watu wake kushambulia na kuwa karibu na adui. Aliwapatia pia vigao vizito vya ngozi ya ngòmbe.

    Kutembea bila viatu

    Alilazimisha watu wake kuacha vyandalua na viatu na kutembea pekupeku. Hii iliongeza kasi ya impi zake na uwezo wao wa kushambulia haraka. Inasemekana ya kwamba Shaka aliua wote waliolalamika walipoamriwa kuacha viatu vyao.

    Kujenga nidhamu

    Shaka alijenga nidhamu ya watu wake kwa kuwa na utaratibu wa mamlaka kati yake mwenyewe na vikosi vidogo zaidi. Sehemu nyingine ilikuwa adhabu kali: askari asiyeweza kuonyesha damu kwenye silaha yake aliweza kuuawa baada ya kurudi vitani. Impi ambazo zilipata sifa machoni pa Shaka ziliruhusiwa kuoa baada ya ushindi.

    Kuwa na vikosi vya kusaidia mizigo

    Shaka alitumia wavulana wadogo kuanzia umri wa miaka sita waliongozana na impi wakibeba mizigo au kuwafuata wanajeshi kwa ngombe kama chakula. Hata hii iliharakisha mwendo wa impi zake.

    Impi za hirima

    Hirima au vikundi vya kujumuisha watu wa umri moja ni tabia ya utamaduni kwa Wabantu wengi. Shaka alipoanzisha impi zake -badala ya kushambulia na watu wake wote mara moja jinsi ilivyokuwa kawaida awali- alitumia vikundi vilivyokuwepo tayari kiutamaduni kama msingi wa impi zake.

    Muundo wa Kichwa cha Mbogo

    Shaka alitumia mpangilio wa impi zake vitani kwa umbo la "Kichwa cha Mbogo": 1. vikosi viwili upande wa kushoto na kulia vilikuwa kama "pembe za mbogo" 2. kikosi kikubwa cha katikati kilikuwa kama "uso" au "kifua" 3. vikosi vya ziada au vya wazee vilikuwa "viuno" vilivyotumika ama kuongeza uzito wa mashambulio panapohitajika au kuimarisha utetezi pale ambako adui alisogea mbele.

T

  1. Desmond Tutu

    Desmond Tutu

    Tuzo Nobel.png
    Desmond Tutu, Askofu mkuuEmeritus wa Cape Town
    Desmond Mpilo Tutu (alizaliwa tarehe 7 Oktoba, mwaka 1931) ni Askofu mkuu wa Kanisa Anglikana nchini Afrika Kusini. Ilivyofika mwaka wa 1984 alipokea Tuzo ya Nobel ya Amani.

    Maandiko

    • Crying in the Wilderness, 1982
    • Hope and Suffering: Sermons and Speeches, 1983
    • The Words of Desmond Tutu, 1989
    • The Rainbow People of God: The Making of a Peaceful Revolution, 1994
    • Worshipping Church in Africa, 1995
    • The Essential Desmond Tutu, 1997
    • No Future without Forgiveness, 1999
    • An African Prayerbook, 2000
    • God Has a Dream: A Vision of Hope for Our Time, 2004

    Tuzo ya Nobel ya Amani

    Tuzo ya Nobel

    Alfred Nobel (1833 - 1896)
    Medali ya Tuzo ya Nobeli
    Ramani inayoonyesha idadi ya washindi wa Tuzo ya Nobel nchi kwa nchi
    Commons-logo.svg
    Wikimedia Commons ina media kuhusu:
    Tuzo ya Nobel ni tuzo ya fedha kwa ajili ya mafanikio ya pekee katika fani mbalimbali. Ilianzishwa na Alfred Nobel.
    Tangu mwaka wa 1901 imetolewa kwa watu waliofaulu katika fani zifuatazo: FizikiaKemiaTiba (au Fiziolojia), Fasihi na Amani. Tangu mwaka wa 1969, tuzo ya sita imeongezewa kwa Uchumi. Siku hizi Tuzo ya Nobel ni tuzo ya kimataifa mashuhuri kabisa duniani. Wanaotuzwa hupokea hati, medali ya dhahabu na kiasi cha pesa cha takriban € milioni 1,2 (kinategemea mapato ya riba kutokana na mfuko wa fedha iliyotengwa kwa kusudi hii na Alfred Nobel). Maazimio kuhusu tuzo za kila mwaka hutolewa kufuatana na wasia wa Alfred Nobel na kamati zifuatazo:
    1. Tuzo ya Nobel ya Fizikia inateuliwa na Taasisi ya Taaluma ya Sayansi ya Sweden
    2. Tuzo ya Nobel ya Kemia inateuliwa na Taasisi ya Taaluma ya Sayansi ya Sweden
    3. Tuzo ya Nobel ya Tiba inateuliwa na Karolinska Institutet Stockholm
    4. Tuzo ya Nobel ya Fasihi inateuliwa na Taasisi ya Taaluma ya Sweden kwa lugha na fasihi
    5. Tuzo ya Nobel ya Amani inateuliwa na kamati ya Nobel ya Norway iliyochaguliwa na Bunge la Norway
    6. Tuzo ya Nobel ya Elimu ya Uchumi inateuliwa na Taasisi ya Taaluma ya Sayansi ya Sweden

    Orodha ya Washindi wa Tuzo ya Nobel[hariri | hariri chanzo]

    Watu walioshinda Tuzo ya Nobel ni wafuatao:
    1901 – Wilhelm Conrad Röntgen (Fizikia), Jacobus Henricus van’t Hoff (Kemia), Emil von Behring (Tiba), Sully Prudhomme(Fasihi), Henri Dunant na Frederic Passy (Amani);
    1902 – Hendrik Antoon Lorentz na Pieter Zeeman (Fizikia), Hermann Emil Fischer (Kemia), Ronald Ross (Tiba), Theodor Mommsen (Fasihi), Elie Ducommun na Charles-Albert Gobat (Amani);
    1903 – Antoine Henri Becquerel pamoja na Pierre Curie na Marie Curie (Fizikia), Svante Arrhenius (Kemia), Niels Ryberg Finsen (Tiba), Bjornstjerne Bjornson (Fasihi), Randal Cremer(Amani);
    1904 – Lord Rayleigh (Fizikia), William Ramsay(Kemia), Ivan Pavlov (Tiba), Frederic Mistral na Jose Echegaray y Eizaguirre (Fasihi), Taasisi ya Haki ya Kimataifa (Amani);
    1905 – Philipp Lenard (Fizikia), Adolf von Baeyer (Kemia), Robert Koch (Tiba), Henryk Sienkiewicz (Fasihi), Bertha von Suttner(Amani);
    1906 – Joseph John Thomson (Fizikia), Henri Moissan (Kemia), Camillo Golgi na Santiago Ramon y Cajal (Tiba), Giosue Carducci(Fasihi), Theodore Roosevelt (Amani);
    1907 – Albert Abraham Michelson (Fizikia), Eduard Buchner (Kemia), Alphonse Laveran (Tiba), Rudyard Kipling (Fasihi), Ernesto Teodoro Moneta na Louis Renault (Amani);
    1908 – Gabriel Lippmann (Fizikia), Ernest Rutherford (Kemia), Paul Ehrlich na Ilya Mechnikov (Tiba), Rudolf Eucken (Fasihi), Klas Pontus Arnoldson na Fredrik Bajer (Amani);
    1909 – Guglielmo Marconi na Ferdinand Braun (Fizikia), Wilhelm Ostwald (Kemia), Emil Theodor Kocher (Tiba), Selma Lagerlöf (Fasihi), Auguste Beernaert (Amani);
    1910 – Johannes Diederik van der Waals (Fizikia), Otto Wallach (Kemia), Albrecht Kossel (Tiba), Paul von Heyse (Fasihi), Ofisi ya Kimataifa ya Amani (Amani);
    1911 – Wilhelm Wien (Fizikia), Marie Curie (Kemia), Allvar Gullstrand (Tiba), Maurice Maeterlinck (Fasihi), Tobias Asser na Alfred Fried (Amani);
    1912 – Nils Dalen (Fizikia), Victor Grignard na Paul Sabatier (Kemia), Alexis Carrel (Tiba), Gerhard Hauptmann (Fasihi), Elihu Root (Amani);
    1913 – Heike Kamerlingh Onnes (Fizikia), Alfred Werner (Kemia), Charles Richet (Tiba), Rabindranath Tagore (Fasihi), H. La Fontaine (Amani);
    1914 – Max von Laue (Fizikia), Theodore William Richards (Kemia), Robert Barany (Tiba), (hakuna tuzo kwa Fasihi wala Amani);
    1915 – William Bragg na Lawrence Bragg (Fizikia), Richard Willstätter (Kemia), Romain Rolland (Fasihi), (hakuna tuzo kwa Tiba wala Amani);
    1916 – Verner von Heidenstam (Fasihi), (hakuna tuzo nyingine);
    1917 – Charles Glover Barkla (Fizikia), (hakuna tuzo kwa Kemia wala Tiba), Karl Adolph Gjellerup na Henrik Pontoppidan (Fasihi), Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu(Amani);
    1918 – Max Planck (Fizikia), Fritz Haber (Kemia), (hakuna tuzo nyingine);
    1919 – Johannes Stark (Fizikia), Jules Bordet (Kemia), (hakuna tuzo kwa Tiba), Carl Spitteler (Fasihi), WoodrowWilson (Amani);
    1920 – Charles Édouard Guillaume (Fizikia), Walther Nernst (Kemia), August Krogh (Tiba), Knut Hamsun (Fasihi), Leon Bourgeois (Amani);
    1921 – Albert Einstein (Fizikia), Frederick Soddy (Kemia), (hakuna tuzo kwa Tiba), Anatole France (Fasihi), Karl Hjalmar Branting na Christian Louis Lange (Amani);
    1922 – Niels Bohr (Fizikia), Francis William Aston (Kemia), Archibald Vivian Hill na Otto Meyerhoff (Tiba), Jacinto Benavente (Fasihi), Fridtjof Nansen (Amani);
    1923 – Robert Millikan (Fizikia), F. Pregel (Kemia), Frederick Banting na John Macleod (Tiba), William Butler Yeats (Fasihi), (hakuna tuzo kwa Amani);
    1924 – Karl Manne Georg Siegbahn (Fizikia), Willem Einthoven (Tiba), Wladyslaw Reymont (Fasihi), (hakuna tuza kwa Kemia wala Amani);
    1925 – James Franck na Gustav Hertz (Fizikia), Richard Zsigmondy (Kemia), (hakuna tuzo kwa Tiba), George Bernhard Shaw (Fasihi), Austen Chamberlain na Charles Dawes(Amani);
    1926 – Jean Perrin (Fizikia), Theodor Svedberg (Kemia), Johannes Fibiger (Tiba), Grazia Deledda (Fasihi), Aristide Briand na Gustav Stresemann (Amani);
    1928 – Owen Richardson (Fizikia), Adolf Windaus (Kemia), Charles Nicolle (Tiba), Sigrid Undset (Fasihi), (hakuna tuzo kwa Amani);
    1929 – Louis-Victor Broglie (Fizikia), Arthur Harden na Hans von Euler-Chelpin (Kemia), Christiaan Eijkman na Frederick Hopkins (Tiba), Thomas Mann (Fasihi), Frank Kellogg(Amani);
    1930 – Chandrasekhara Raman (Fizikia), Hans Fischer (Kemia), Karl Landsteiner (Tiba), Sinclair Lewis (Fasihi), Nathan Söderblom (Amani);
    1931 – (hakuna tuzo kwa Fizikia), Carl Bosch na Friedrich Bergius (Kemia), Otto Warburg (Tiba), Erik Axel Karlfeldt (Fasihi), Nicholas Butler na Jane Addams (Amani);
    1932 – Werner Heisenberg (Fizikia), Irving Langmuir (Kemia), Charles Sherrington na Edgar Douglas Adrian (Tiba), John Glasworthy (Fasihi), (hakuna tuzo kwa Amani);
    1933 – Erwin Schrödinger na Paul Dirac (Fizikia), (hakuna tuzo kwa Kemia), Thomas Hunt Morgan (Tiba), Ivan Bunin (Fasihi), Norman Angell (Amani);
    1934 – (hakuna tuzo kwa Fizikia), Harold Urey (Kemia), George MinotWilliam Murphy na George Whipple (Tiba), Luigi Pirandello (Fasihi), Arthur Henderson (Amani);
    1935 – James Chadwick (Fizikia), Frederic na Irene Joliot-Curie (Kemia), Hans Spemann (Tiba), (hakuna tuzo kwa Fasihi), Carl von Ossietzky (Amani);
    1936 – Carl David Anderson na Victor Francis Hess (Fizikia), P. Depye (Kemia), Henry Dale na Otto Loewi (Tiba), Eugene O’Neill (Fasihi), Carlos Saavedra Lamas (Amani);
    1937 – Clinton Davisson na George Thomson (Fizikia), Norman Haworth na Paul Karrer (Kemia), Albert Szent-Györgyi (Tiba), Roger Martin du Gard (Fasihi), Cecil of Clelwood(Amani);
    1938 – Enrico Fermi (Fizikia), Richard Kuhn (Kemia), Corneille Heymans (Tiba), Pearl S. Buck (Fasihi), Tume ya Nansen kwa Wakimbizi (Amani);
    1939 – Ernest Orlando Lawrence (Fizikia), Leopold Ruzicka na Adolf Butenandt (Kemia), Gerhard Domagk (Tiba), Frans Eemil Sillanpää (Fasihi), (hakuna tuzo kwa Amani);
    (1940-42 Tuzo ya Nobel haikutolewa kwa sababu ya Vita Kuu ya Pili ya Dunia.)
    1943 – Otto Stern (Fizikia), Georg von Hevesy (Kemia), Henrik Dam na Edward Doisy (Tiba), (hakuna tuzo kwa Fasihi wala Amani);
    1944 – Isidor Rabi (Fizikia), Otto Hahn (Kemia), Joseph Erlanger na Herbert Spencer Gasser (Tiba), Johannes Jensen (Fasihi), Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu (Amani);
    1945 – Wolfgang Pauli (Fizikia), Artturi Ilmari Virtanen (Kemia), Alexander FlemingErnst Boris Chain na Howard Walter Florey (Tiba), Gabriela Mistral (Fasihi), Cordell Hull (Amani);
    1946 – Percy Bridgman (Fizikia), James SumnerJohn Howard Northrop na Wendell Stanley (Kemia), Hermann Muller (Tiba), Hermann Hesse (Fasihi), Emily Balch na John Raleigh Mott (Amani);
    1947 – Edward Appleton (Fizikia), Robert Robinson (Kemia), Carl na Gerty Cori na Bernardo Houssay (Tiba), Andre Gide (Fasihi), Jumuiya ya Marafiki (‘’Society of Friends’’) (Amani);
    1948 – Patrick Blackett (Fizikia), Arne Tiselius (Kemia), Paul Hermann Müller (Tiba), T.S. Eliot (Fasihi), (hakuna tuzo kwa Amani);
    1949 – Hideki Yukawa (Fizikia), William Giauque (Kemia), Walter Hess na Antonio Egas Moniz (Tiba), William Faulkner (Fasihi), John Boyd-Orr (Amani);
    1950 – Cecil Frank Powell (Fizikia), Kurt Alder na Otto Diels (Kemia), Philip HenchEdward Kendall na Tadeus Reichstein (Tiba), Bertrand Russell (Fasihi), Ralph Bunche (Amani);
    1951 – John Douglas Cockcroft na Ernest Walton (Fizikia), Edwin McMillan na Glenn Seaborg (Kemia), Max Theiler (Tiba), Par Lagerkvist (Fasihi), Leon Jouhaux (Amani);
    1952 – Felix Bloch na Edward Purcell (Fizikia), A.J.P. Martin na R.L.M. Synge (Kemia), Selman Waksman (Tiba), Francois Mauriac (Fasihi), Albert Schweitzer (Amani);
    1953 – Frits Zernike (Fizikia), Hermann Staudinger (Kemia), Hans Krebs na Fritz Lipmann (Tiba), Winston Churchill (Fasihi), George Marshall (Amani);
    1955 – Willis Lamb na Polykarp Kusch (Fizikia), Vincent du Vigneaud (Kemia), Hugo Theorell (Tiba), Halldor Laxness (Fasihi), (hakuna tuzo kwa Amani);
    1956 – William ShockleyJohn Bardeen na Walter Brattain (Fizikia), Nikolay Semyonov na Cyril Hinshelwood (Kemia), Werner ForssmannAndre Cournand na Dickinson Richards(Tiba), Juan Ramon Jimenez (Fasihi), (hakuna tuzo kwa Amani);
    1957 – Tsung-Dao Lee na Chen Ning Yang (Fizikia), Alexander Todd (Kemia), Daniel Bovet (Tiba), Albert Camus (Fasihi), Lester Pearson (Amani);
    1958 – Pavel CherenkovIlya Frank na Igor Tamm (Fizikia), Frederick Sanger (Kemia), George BeadleEdward Tatum na Joshua Lederberg (Tiba), Boris Pasternak (Fasihi), Padre Dominique Pire (Amani);
    1959 – Emilio Segre na Owen Chamberlain (Fizikia), Jaroslav Heyrovsky (Kemia), Arthur Kornberg na Severo Ochoa(Tiba), Salvatore Quasimodo (Fasihi), Philip Noel-Baker(Amani);

No comments: