Tuesday 3 October 2017

Utamaduni wa Afrika inajumuisha tamaduni zote ambazo ziliwahi kuweko katika bara la Afrika.
Dhana ya utamaduni wa Afrika nzima ilijadiliwa kwa makini katika miaka ya 1960 na 1970 katika muktadha wa harakati ya Négritude, lakini imepoteza mtindo katika masomo ya Afrika.
Mpasuko mkuu ni kati ya Afrika ya Kaskazini (pamoja na Pembe la Afrika), ambayo ni sehemu ya ulimwengu wa Kiislamu, na Afrika ya kusini kwa Sahara, ambayo imegawanywa katika idadikubwa ya tamaduni za kikabila.
Mikasama kuu ya kikabila ni Afro-Asiatic (Afrika ya kaskazini, Chad, Pembe la Afrika), Niger-Congo (sanasana Kibantu) katika sehemu kubwa ya Afrika kusini kwa SaharaNilo-Saharan katika maeneo ya Sahara na Sahel na sehemu za Afrika ya Mashariki na Khoisan (wazawa wachache wa Tanzania na Kusini mwa Afrika.
Usambazaji mpana wa Kibantu kusini mwa Afrika, kunakojumuisha maeneo ya Afrika ya MagharibiAfrika ya MasharikiAfrika ya Kati na vilevile Afrika ya Kusini, ni matokeo ya uenezi wa Kibantu katika milenia ya 1 BK. Utumizi mpana wa Kiswahili kama lingua franka unaonyesha zaidi Kibantu kama athari ya tamaduni ya "Afrika nzima".

Watu

Asili ya wakazi wengi wa Afrika ni kuwa wazawa.
Afrika ina makabila mengi ambayo hayawezi kuhesabika, na vikundi vya kikabila na vya kijamii. Baadhi ya vikundi hivi vinaashiria wakazi wengi ambao ni mamilioni ya watu. Vikundi vingine ni vikundi vidogo vya watu elfu kadhaa. Baadhi ya nchi zina zaidi ya makabila 20 tofauti, na ni tofauti sana katika imani.

Lugha

Ramani zinazoonyesha mgawanyo wa familia ya lugha za Afrika na baadhi ya kubwa lugha za Afrika. Ile ya Kiafrika-Kiasia inahusu Afrika Kaskazini kupitia Pembe la Afrika na Asia ya Magharibi. Ile ya Niger-Congo imegawanywa ili kuonyesha ukubwa wa familia ndogo ya Kibantu.
Bara la Afrika lina mamia ya lugha, na kama lahaja zinazozungumza na makabila tofauti zinajumuishwa, idadi ni kubwa zaidi. Kupitia makadirio mengi, Afrika ina zaidi ya lugha elfu. Lugha na lahaja hizo zote hazina umuhimu sawa: baadhi huzungumzwa na watu mia chache tu, nyingine huzungumzwa na mamilioni.
Kati ya lugha maarufu zaidi zinazozungumzwa ni KiarabuKiswahili na Kihausa. Nchi chache za Afrika hutumia lugha moja na kwa sababu hii, lugha rasmi kadhaa zinatumika, za Kiafrika na za kutoka nje. Baadhi ya Waafrika pia wanaweza kuzungumza lugha mbalimbali kama vile KimalagasiKiingerezaKifaransaKirenoKihispaniaKibambaraKisotho na nyinginezo.
Lugha za Afrika huonyesha umoja wa tabia na vilevile utofauti, kwani ni wazi katika vipimo vyote vya Afrika. Familia nne kuu na maarufu za lugha za kienyeji ni:
Senta ya mapema ya maandiko ilikuwa African Ink Road.
Pamoja na nchi chache mashuhuri katika Afrika ya Mashariki, karibu nchi zote za Afrika zilisiliki lugha rasmi zilizoasilika kutoka nje ya bara na kuenea kupitia ukoloni au uhamiaji wa binadamu. Kwa mfano, katika nchi mbalimbali, Kiingereza na Kifaransa hutumiwa kwa mawasiliano katika nyanja za umma, kama vile serikalibiasharaelimu na vyombo vya habariKiarabuKireno na Kiafrikaans ni mifano la lugha zisizo za asili ya Kiafrika ambazo hutumika na mamilioni ya Waafrika leo, katika nyanja za umma na za kibinafsi. Tofauti ni Kimalagasi kisiwani Madagaska, ambako Waafrika walihamia kutoka barani wakikuta wenyeji kutoka Indonesia.

Sanaa na Afrika

Afrika ina mila tajiri ya sanaa. Sanaa za Afrika hujieleza katika aina mbalimbali ya mchongo wa mbao, shaba na matendo ya sanaa ya ngozi. Sanaa ya Afrika pia inajumuisha uchongaji, uchorajiufinyanzi, mavazi ya mwili na ya kichwa katika sherehe na mikutano ya kidini.
Utamaduni wa Afrika daima umetilia mkazo vile mtu anavyojitokeza na majohari yamebaki vidude muhimu ya kibinafsi. Vipande vingi vya majohari vimetengenezwa na simbi vifaa kama vya simbi. Vilevile, miundo ya maskhara zinatengenezwa na umakini na ni sehemu muhimu ya utamaduni wa Afrika. Maskhara hutumika katika sherehe mbalimbali kuashiria mizimu na vizuka, wahusika katika hadithi na miungu.
Katika mila nyingi ya sanaa ya Afrika, baadhi ya mandhari adhimu kwa utamaduni wa Afrika hujirudia kama vile wapenzi wawili, mwanamke na mtoto, mume na silaha au mnyama, na mtu kutika nje au mgeni. Wapenzi wawili wanaweza kuwakilisha mizimu, mwanzilishi wa jamii, wapenzi wawili waliooana au mapacha. Mandhari ya wapenzi wawili adimu huonyesha undani wa wanaume na wanawake. Yule mama na watoto au watoto hufumbua hamu kubwa ya wanawake wa Afrika kupata watoto. Mandhari pia inaashiria mama mirihi na watu kama watoto wake. Mandhari ya mtu na silaha au mnyama mandhari inaashiria fahari na nguvu. Mgeni anaweza kuwa ametokea kutoka baadhi ya makabila au awe mtu kutoka nchi nyingine, na zaidi upotovu wa mgeni huonyesha pengo kubwa kutoka kwa mgeni.
Fathi Hassan anachukuliwa kama mwakilishi wa sanaa ya kisasa ya Afrika.

Folklore na dini ya kimila

Kama tamaduni zote za kibinadamu, "Folklore" ya kiafrika na masimulizi huashiria pande mbalimbali za utamaduni wa Afrika [1] Kama karibu staarabu na tamaduni zote, hadithi za mafuriko zimekuwa zikienea katika maeneo mbalimbali ya Afrika. Kwa mfano, kulingana na hadithi ya chuchu au Mtwa, kinyonga aliposIkia kelele ya ajabu akiwa mtini, shina ya mti huo ulifunguka na maji ilimwagika kama gharika kuu iliyoenea kote ardhini. Wapenzi wa kwanza wa binadamu waliibuka kutoka majini. Vilevile, hadithi moja kutoka Cote d'Ivoire inasema kwamba mhisani mmoja alipatiana kila kitu alichokuwa nacho. Mungu wake, Ouende , alimtuza kwa kumpa utajiri, alimshauri aondoke kutoka eneo hilo, na alituma miezi sita ya mvua kuharibu jirani wake wachoyo.

Upishi

Afrika ni bara kubwa na vyakula na vinywaji vyake hudhania mivuto ya kienyeji, na utumizi wa vyakula vya kikoloni vya kimila, vikijumuisha pilipili , njugu na mahindi, vilivyoanzishwa na wakoloni. Upishi wa Afrika ni mchanganyiko wa matunda na mboga ya kimila, maziwa na bidhaa za nyama. Mlo wa kijiji cha Afrika mara nyingi huwa ni maziwa na bidhaa za maziwa. Wanyama na samaki hukusanywa kutoka eneo kubwa la Afrika.
Upishi wa kimila ya kiafrika inatabia ya utumizi wa Wanga kama umakini, ikifuatwa na kitoweo yenye nyama au mboga, au yote mawili. Mihogo na viazi vikuu ndizo mboga kuu. Waafrika pia hutumia mboga zilizopashwa moto na ambazo zina pilipili. Vyakula vya mboga vilivyopashwa moto au kuchemshwa, mbaazi, maharagwe na nafaka, mihogo, viazi vikuu na viazi vitamu huliwa kwa wingi. Katika kila eneo la Afrika, kuna aina mbalimbali ya matunda ya pori na mboga ambazo hutumika kama chakula. Mtengomaji, ndizi na migomba ni baadhi ya matunda yanayojulikana.
Tofauti hujulikana katika tabia za kula na kunywa barani Afrika. Hivyo, Afrika Kaskazini, pamoja Mediterania kutoka Moroko hadi Misri zina tabia tofauti za chakula kuliko Waafrika wa Sahara ambao hula mlo wa kujikimu. Nigeria na sehemu za pwani za Afrika Magharibi hupenda vyakula vya pilipili. Idadi ya Waafrika ambao si waislamu pia hutumia vileo, ambayo huenda vyema na vyakula vingi vya kiafrika. Pombe inyojulikana sana ndani ya Afrika ni mvinyo kutoka Ethiopia inayoitwa Tej iliyotengenezwa kutumia asali.
Mbinu za kupika za Afrika Magharibi mara nyingi kuchanganya samaki na nyama, pamoja na samaki iliyokaushwa. Upishi wa Afrika Kusini na nchi jirani kwa kiasi kikubwa zinapika vyakula vya machanganyiko, kwa kupata mvuto kutoka wahamiaji kadhaa ambao ni pamoja na Wahindi ambao walileta supu ya adesi,(dals) na muchuzi, Malays waliokuja na michuzi yao ya viungo, na Wazungu na "mixed grills" ambao sasa injumuisha nyama ya wanyama wa Afrika. Kimila, vyakula vya Afrika Mashariki ni tofauti kwa maana kwamba bidhaa za nyama haviko kwa ujumla. Ng'ombe,kondoo na mbuzi walichukuliwa kama aina ya sarafu, na kwa ujumla wanyama hawa hawatumiwi kama vyakula. Mivuto ya Kiarabu yanajitokeza katika upishi wa vyakula vya Afrika Mashariki - mchele uliopikwa kwa viungo katika mtindo fulani, matumizi ya karafuu, mdalasini na viungo vingine vingi, na juisi.
Waethiopia wanadai kuwa wa kwanza kulima kahawa, na wana sherehe za aina nyingi za kahawa , kama sherehe ya chai ya kijapani. Kutoka Ethiopia, kahawa ilienea Yemen, kutoka huko ilienea Arabia, na kutoka huko ikaenea duniani kote.

No comments: