Monday 9 October 2017

Jamii:Orphaned articles from Novemba 2010

Makala katika jamii "Orphaned articles from Novemba 2010"

Jamii hii ina kurasa 11 zifuatazo, kati ya jumla ya 11.

D

  • Ian Duncan
    Ian Duncan
    World Rally Championship record
    Active years1983–1999
    TeamsSubaruToyota
    Rallies15
    Championships0
    Rally wins1
    Podiums4
    Stage wins4
    Total points80
    First rally1983 Safari Rally
    First win1994 Safari Rally
    Last rally1999 Safari Rally
    Ian Duncan (alizaliwa mnamo 23 Juni 1961) ni mmoja ya madereva wa rally ambao wamefanikiwa sana nchini Kenya. Alikuwa bingwa wa Rally nchini Kenya mara tano (1987, 1988, 1989, 1991 na 2000), na alifanikiwa kupata ushindi wa "outright" katika michuano wa magari ya Rally wa Dunia aliposhinda shindano la 42 la Trustbank Safari Rally mwaka wa 1994. Hii ilikuwa moja kati ya tamati zake za nafasi kumi za kwanza mfululizo katika tukio hilo kuanzia mwaka wa 1990 hadi mwaka wa 1996, licha ya kiwango chake cha sifa mbaya.

    Wasifu

    Ian alilelewa katika shamba ya wazazi wake katika sehemu ya Limuru. Ladha yake ya kwanza ya kuendesha gari ilitokea wakati alikuwa na umri wa miaka karibu kumi, huku akimsaidia mama yake wakati alikwama katika barabara za shamba wakati wa mvua. Alihudhuria Shule ya Upili ya St Mary's, kwani nia yake zaidi ilikuwa katika kutengeneza magari na pikipiki. Pia alishiriki katika Motocross na kushinda taji la 125cc la kitaifa miaka ya 1979 na 1980. Alishiriki katika Safari Rally kwa mara ya kwanza mwaka wa 1983 huku akiliendeaha gari la Nissan Pick-Up huku naibu dereva wake akiwa Gavin Bennett, na alimaliza katika nafasi ya tisa na huku akipata ushindi wa darasa na kupata usikivu wa watu rally.[1]
    Ushindi wake wa kwanza wa kitaifa wa Rally ulikuwa katika mji wa Nakuru mwaka wa 1987 wakati alikuwa anaendesha gari ya aina ya Toyota Celica Cam Twin Turbo huku naibu dereva wake akiwa Ian Munro.[2] Duncan alishinda mchuano wake wa kwanza wa kitaifa mwaka huo huo kwani alishinda mashindano mengi. Alishinda tuzo la mwendesha motokaa wa mwaka wa kitaifa mwaka wa 1987.
    Alishiriki kwa kutumia Group A Subaru Legacy na Toyota Celica Turbo 4WD katika miaka ya 1990. Mbali na Safari Rally, alishiriki katika mikutano ya kampeni za WRC mara chache tu. Tokeo lake bora lilikuwa kumaliza katika nafasi ya 8 kwa jumla na kushinda darasala kundi N katika shindano la safari rally la Acropolis Rally mwaka wa 1990 nchini Ugiriki huku naibu dereva wake akiwa Yvonne Mehta (mke wa Shekhar Mehta).
    Baadaye alianza kuendesha gari la aina ya Toyota Hilux ambalo lilikuwa na injini ya lita 4.5 na alilitumia katika mchuano wa rally wa kitaifa wa Kenya (Kenya National Rally Championship (KNRC)). Mnamo Novemba mwaka wa 2006 Duncan alishinda Guru Nanak Rally na kuwa dereva wa kwanza kushinda taji la KNRC kwa mara ya kumi.[3] Alipewa adhabu ya asilimia nne ya muda kwa sababu hakuwa ameliandikisha gari lake. Aliendeleza rekodi yake mwaka wa 2007 na kwa mara nyingine tena akashinda Guru Nanak Rally.
    Duncan ameshinda tukio la Rhino Charge off-road katika miaka ya 1998, 2006 na 2007.[4] Ameshiriki katika mashindano ya pikipiki. Mnamo mwaka wa 2003, alichukua nafasi ya pili katika Kenya Enduro, Motocross na vilevile Michuano ya rally .[5]
    Alitumia gari lake mpya, Nissan Patrol Pick-up, mnamo Oktoba mwaka wa 2008. Mwaka wa 2008 pia alishinda mchuano wa kitaifa wa autocross. Mnamo mwaka wa 2009, miaka 15 baada ya kushinda Safari Rally halisi, Duncan alishinda Safari classic rally huku akiliendesha gari la mwaka wa 1967 la Ford Mustang huku naibu dereva wake akiwa naibu dereva wake wa sasa, Amaar Slatch. Bingwa mtetezi Bjørn Waldegård alimaliza katika nafasi ya pili.

    Ushindi wa WRC

     # TukioMsimuNaibu-derevaGari
    1Kenya 42 Trustbank Safari Rally1994David WilliamsonToyota Celica Turbo 4WD
  • Jason Dunford
    Personal information
    Full nameJason Edward Dunford
    NationalityBendera ya Kenya Kenya
    Height6 feet 0 inches (1.83 m)
    Weight165 lb (75 kg)
    Sport
    SportSwimming
    Stroke(s)Butterflyfreestyle
    College teamStanford University
    Edward Jason Dunford (alizaliwa tarehe 28 Novemba 1986 mjini Nairobi ni mwogeleaji kutoka Kenya. Yeye hushindana katika mashindano ya uogeleaji ya "butterfly" na "freestyle". Ameshinda dhahabu katika mashindano ya Universiade, michezo ya All-Africa na mashindano ya ubingwa wa Afrika, na kufika fainali katika mashindano ya Olimpiki, mashindano ya ubingwa wa Dunia na kozi fupi ya ubingwa wa Dunia. Ameshikilia pia rekodi za Afrika, Universiade na Olimpiki. Mengi ya mafanikio yake hayajawahi kuonekana kamwe katika historia ya uogeleaji ya Kenya .

    Maisha ya familia

    Jason ni mwana wa Martin na Geraldine Dunford. Martin Dunford ni Mwenyekiti wa kundi la Tamarind ambayo inamiliki hoteli maarufu ya Carnivore. [1] Geraldine, mjukuu Block Ibrahim, mwanzilishi wa hoteli za Block, ni mtendaji wa masoko. Martin pia ni makamu wa mwenyekiti wa Shirikisho ya Uogeleaji ya Kenya na mlezi wa Nairobi Amateur Swimming Association (NASA).[2]
    Dunford ana kaka wawili, Robert na David. Kifungua mimba, Robert, alihitimu katika shule ya kiuchumi ya London ambapo alikuwa nahodha wa klabu ya raga. Kitinda mimba, David, pia ni mwogeleaji na yeye huwakilisha Kenya. Familia hiyo ni ya wazungu wachache nchini Kenya.

    Wasifu

    Wasifu wa Mapema

    Jason Dunford alianza kuogelea akiwa na umri wa miaka mitano akiwa Kenton College, shule ya msingi mjini Nairobi, chini ya kocha Andrew Nderu, ambapo alijiimarisha katika makundi ya umri mjini Nairobi.[2] . Akiwa na umri wa miaka 13, mwogeleaji huyu mwenye kipaji cha uogeleaji alihama kwenda kusoma katika Chuo cha Marlborough (ambacho ni skuli ya upili) nchini Uingereza.[3]
    Dunford alishindana katika mashindano ya kozi fupi ya ubingwa wa Dunia mwaka wa 2004 huko Indianapolis, na mwaka wa 2005 mjini Montreal katika mashindano ya ubingwa wa Dunia, lakini aliambulia patupu katika raundi za kwanza.[4]
    Akiwa chuoni Marlborough alikutana na kocha Petro O'Sullivan, ambaye alikuwa mwogeleaji mkuu wa kimataifa wa Uingereza wa kitambo katika masafa ya mita 400 ya kibinafsi. O'Sullivan alikuwa ameogelea katika Chuo Kikuu cha Georgia, na ni yeye aliyempa moyo Jason kwenda kusomea katika chuo za Marekani ndiposa aweze kuendeleza wasifu wake wa uogeleaji. Mwaka wa 2005, baada ya kumaliza gredi zake za A (A-levels), Dunford alihamia katika Chuo Kikuu cha Stanford, Marekani ambako alipata udhamini wa uogeleaji. Wakati huu yeye anasomea Biolojia ya Binadamu.[5]

    2006-2007 - Kilele wa Bara

    Katika kozi fupi mashindano ya ubingwa wa Dunia ya 2006 huko Shanghai alifika nusu fainali katika matukio mawili: mita 100 "freestyle" na mita 100 "butterfly".[6]
    Mashindano ya kuogelwa ya mabingwa barani Afrika ya 2006 mjini DakarSenegal, ndio ulioanzisha mafanikio yake kwani alikuwa Mkenya wa kwanza milele kushinda medali ya bara ya kuogelea kwa kushinda dhahabu katika shindano la "butterfly" la mita 100 siku ya kwanza ya mashindano hayo. Alimaliza mashindano haya na medali mbili za dhahabu("butterfly" mita 100 na "backstroke" mita 50), tatu za fedha ("butterfly" mita 50 kipepeo,"freestyle" mita 100 na mita 200) na moja ya shaba ("freestyle" mita 50).[5] Isitoshe alivunja idadi ya rekodi kadha za kitaifa. Kakake mdogo David Dunford pia alifanya vyema kwa kushinda medali mbili za dhahabu na moja ya fedha ("backstroke" mita 100, "backstroke" mita 200 na "backstroke" mita 50) [7]
    Mafanikio yake yalimwezesha kupata nafasi ya pili katika kundi la tuzo la mwanaspoti wa mwaka wa Kenya mwaka wa 2006, nyuma Alex Kipchirchir, mmoja wa wakimbiaji wengi wa Kenya wenye uungwana duniani. Kakake Daudi Dunford alteuliwa kama mwanaspoti anayeahidi katika tuzo hizo.[8]
    Dunford alishiriki katika mashindano kadhaa katika mashindano ya ubingwa wa Dunia wa mwaka wa 2007 huko MelbourneAustralia. Tokeo lake bora lilikuwa kufika fainali ya "butterfly" katika mita 100, ambapo alimaliza wa nane. Akielekea fainali, aliweka muda wa sekunde 51.85 [9] rekodi mpya ya Afrika [10] na kumshinda mshindi wa michezo ya Commonwealth, Ryan Pini wa Papua Guinea Mpya ilikupata nafasi ya nane ya kuingia katika fainali. Yeye pia akawa mwogeleaji wa kwanza kutoka Kenya kufuzu kwa Olimpiki. Alifuzu kushiriki katika Olimpiki ya mwaka wa 2008 ambao ulikuwa wakati wa kiangazi huko Beijing, Uchina katika mashindano ya "butterfly" ya mita 100 na vilevile ya "freestyle" ya mita 100 . Katika hafla ya mapema, baadhi ya waogeleji kutoka Kenya wameshiriki katika Olimpiki, lakini tu baada ya kupewa "wildcard" ya IOC ya uogeleaji.Kadi hii inaiwezesha nchi ambayo kaikufuzu kwa njia ya kawaida kushiriki katika olimpiki.
    Wakati wa michezo ya All-Africa ya mwaka wa 2007 huko Algiers Jason Dunford alishinda medali tatu za dhahabu (zote za shindalo la "butterfly" katika mita 50,100 na 200), mbili za fedha ("freestyle" mita 50, "backstroke" mita 100 ) na tatu za shaba ("backstroke" mita 50 na "freestyle" mita 200 na 100).[11] Kutokana na juhudi zake katika michezo hizi na mashindano ya ubingwa wa dunia huko Melbourne, Dunford alituzwa tuzo la Safaricom la mwanaspoti mwanaume wa mwaka wa 2007.[12]

    2008-2009 - Olimpiki na Universiade

    Alishiriki katika mashindano ya ubingwa wa dunia ya FINA ya kozi fupi mwezi Aprili mwaka wa 2008 huko Manchester na akafika fainali ya shindano la "butterfly" la mita 100, ambapo alimaliza katika nafasi ya 8.|2008 huko Manchester na akafika fainali ya shindano la "butterfly" la mita 100, ambapo alimaliza katika nafasi ya 8.[13]
    Katika michezo ya Olimpiki, mwaka wa 2008, alishiriki katika tukio mbili. Katika mashindano ya "freestyle" ya mita 100, alimaliza katika nafasi ya 24 kwa ujumla, na kukosa nusu fainali. Hata hivyo, aliweka rekodi mpya ya kitaifa ya sekunde 49.06.[14] Katika tukio lake kuu, shindano la "butterfly" la mita 100, alifuzu kushiriki katika nusu fainali kwa kuweka rekodi mpya ya Olimpiki ya sekunde 51.14 na wakati huo huo kuboresha rekodi yake ya kibinafsi ya Afrika. Rekodi ya Olimpiki ya awali (sekunde 51.25) iliwekwa na Michael Phelpskatika michezo ya Olimpiki ya mwaka wa 2004.[15] Rekodi ya Dunford ya Olimpiki haikukaa muda mrefu; dakika chache baadaye Milorad Čavić wa Serbia aliweka rekodi ya sekunde 50.76, akifuatiwa na waogeleaji wengine wawili (pamoja na Phelps) ambao pia walivunja rekodi ya Dunford.[16] Alifika fainali na kumaliza katika nafasi ya 5 kwa muda wa sekunde 51.47.
    Desemba mwaka wa 2008 katika mashindano ya uogeleaji ya Afrika mjini Johannesburg, yeye alishinda medali tatu za dhahabu na mbili za fedha.[17]
    Shindano lake la kwanza kuu lilikuwa mwaka wa 2009 katika [[Universiade ya kiangazi jijini Belgrade, ambapo alishinda shindano la "butterfly" la mita 100 kwa muda wa sekunde 51.29.|Universiade ya kiangazi jijini Belgrade, ambapo alishinda shindano la "butterfly" la mita 100 kwa muda wa sekunde 51.29.[18]]] Katika nusu fainali aliweka rekodi mpya ya Universiade ya sekunde 50.85[19], ambayo pia ilivunja rekodi ya Afrika tena.[20] Katika shindano la "butterfly" la mita 50 alipata fedha nyuma ya Jernej Godec wa Slovenia, lakini yeye ndiye aliyekuwa na kasi zaidi katika nusu fainali, muda wake wa sekunde 23.09 ukiwa rekodi mpya ya Universiade[21], ambayo bado ipo hata baada ya fainali.[22] Dunford pia akawa mwanamedali wa shaba wa mita 100 katika shindano la "freestyle".[19]
    Wakati wa mashindano ya ubingwa wa Dunia wa 2009 alimaliza katika nafasi ya sita katika mashindano ya "butterfly" ya mita 50 [23] na ya mita 100 [24]. Katika nusu fainali ya 100 ya "fly" aliweka rekodi mpya ya Afrika (sekunde 50.78) [25]

E

  • Edger Luhende Ngelela

    Edger Luhende Ngelela


    Edger Luhende Ngelela
    Eddie gr (7).JPG
    Maelezo ya awali
    Amezaliwa15 Oktoba 1980 (umri 36)
    Kazi yakeMwimbaji, Mtunzi, Muigizaji, Muongozaji na mtengeneza Filamu
    Edgar Leonard Luhende Ngelela (amezaliwa 15 Oktoba 1980[1]) ni msanii katika masuala ya muziki, uchoraji, uigizaji, uongozaji na utengenezaji wa filamu kutoka nchini Tanzania. Yeye ni mtoto wa kwanza katika familia ya mama na marehemu mzee Luhende, wanaoishi katika mkoa wa Shinyanga nchini Tanzania. Baada ya kuzaliwa familia ya mzee Ngelela Ilihamia katika Mkoa wa Mwanza.

    Baadaye walihamia katika Mkoa wa Shinyanga hadi Edgar alipoanza darasa la kwanza baada ya kusoma shule ya awali (maarufu kama vidudu).

    Wasifu

    Maisha ya awali

    Edgar Leonard Luhende Ngelela alizaliwa mnamo tar. 15 Oktoba 1980 katika hospitali ya Mkoa wa MorogoroTanzania. Alianza kusoma elimu ya awali maarufu kama vidudu, kabla ya kuanza darasa la kwanza huko huko katika Mkoa wa Shinyanga.
    Mwaka 1987, baada ya kumaliza elimu yake ya awali, alianza elimu yake ya msingi katika shule ya msingi Mwenge, lakini mwaka huohuo alihamia katika shule ya kimataifa iliyoko mkoani Arusha inayoitwa Mtakatifu Constantine. St Constantine, ambako aliendelea na darasa la kwanza hadi darasa la tatu, na badaye kutokana na hali ya hewa mkoani humo, ilimshinda Edgar kiafya. Hivyo, familia yake iliamua kumwamishia katika shule ya msingi ya Nyakahoja iliyoko mkoani Mwanza, ambapo ndipo alipomalizia elimu yake ya msingi.
    Baada ya kumaliza darasa la Saba, aliendelea na masomo yake ya sekondari ya awali katika shule ya Lububu katika wilaya ya Nzega Mkoani Tabora, ambapo alisoma kwa muda wa miezi minne kutokana na sababu mbalimbali hakuweza kuendelea na masomo kwani alisoma miezi minne tu, kati ya miezi kumi na mbili aliyotakiwa kusoma.
    Mwaka uliofutia, yaani, mwaka 1996, alihamishiwa nchini Kenya ambapo kutokana na unataratibu wa elimu ya nchini Kenya alitakiwa kufanya maandalizi kabla ya kujiunga na kidato cha kwanza kwa muda wa mwaka mmoja na mwaka 1997, alianza kidato cha kwanza katika shule ya wavulana ya Isebania iliyoko kama kilometa mbili kutoka katika mpaka wa Sirari katika wilaya ya Kurya hadi mwaka 2000, ambapo alimaliza kidato cha nne katika shule hiyo.

    Chuo

    Huku akiwa anatuma maombi katika vyuo mbalimbali hatimaye alipata nafasi katika chuo cha sanaa Bagamoyo nchini Tanzania ambapo alikuwa akichukua stashahada ya sanaa kwa muda wa miaka mitatu, na baada ya kuhitimu masomo yake ya sanaa chuoni hapo alijiunga na chuo kikuu cha Dar Es SalaamChuo Kikuu cha Dar es Salaam ambapo alikuwa akichukua shahada ya Sanaa ya Maonesho na Sanaa ya Ufundi (Bachelor of Arts in Fine and Performing Arts) ambapo mwaka 2008, alitunukiwa shahada yake ya kwanza katika masula ya sanaa za maonesho na sanaa za ufundi.
    Baada ya kumaliza elimu yake katika chuo kuku cha Dar es Salaam na kupata shahada yake, alianza kuchua shahada ya uzamili katika masuala hayo hayo ya sanaa, masomo aliyohitimu mwaka 2010.

    Sanaa

    Edgar alianza kufanya sanaa tangu akiwa mdogo sana, kabla hata hajaanza kusoma shule yoyote, lakini baada ya kuanza shule ya msingi, Edgar aliendelea na shughuli za Uchoraji pamoja na muziki huku akiwa ansoma, jambo ammbalo familia yake haikulipenda kwa kuhisi kuwa alikuwa hatumii muda wake kusoma.
    Akiwa shuleni katika shule ya Msingi Nyakahoja akiwa darasa la nne alianza kuigiza na hapo ndipo walianza kumpenda na kumpa nafasi mbalimbali za kuingiza hasa uigizaji mkuu kutokana na kuonekana kuwa na kipaji cha sanaa. Alipomaliza elimu yake ya msingi, Edgar alizawadiwa cheti cha uchoraji, miziki na uigizaji, kutokana kuonesha kuwa na kipaji
    Baada ya kumaliza elimu ya msingi, Edgar hakuishia hapo kwani alipoanza kidato cha kwanza katika sekondari ya Isebabia nchini Kenya alichaguliwa kuwa kiongozi katika maswala ya Burudani mbalimbali, na pia alikuwa mwenyekiti wa Klabu za sanaa mbalimbali hapo shuleni. Wakati akiwa binafsi anaendelea kuimba na kuchora. Mara nyingi alikuwa akiimba nyimbo za wanamuziki wengine.
    Baada ya kufika kidato cha pili, Edgar aliamua kutunga wimbo wake mwenyewe wa kwanza ambao ulikuwa katika lugha ya kiingerwza ulioitwa so many reasons, ambao haukupata nafasi ya kurekodiwa na badala yake alikuwa akiimba katika matamasha mbalimbali ya kishule.

    Uchoraji

    Edgar kwa sasa anatengeneza kitabu cha katuni kinachoitwa Marcus, ambapo kinahusisha hadithi za katuni, pia ametafsiri kitabu cha Muheshimiwa mstahiki bwana Maneno ambapo hadi hivi sasa bado anashughulika na wataalamu mbalimbali wa michezo ya kuigiza kama vile Bwana Edwin Semzaba ili kuusahihisha kama mchezo wa kuigiza.

    Uigizaji

    Katika sanaa za waigizaji naye ni miongoni mwa watu wachacha katika Tanzania wenye uwezo wa kufanya maigizo bubu (mime), na amefundishwa na Bwana Nkwabi Nhangasamala aliyepata ujuzi huo nchini Ujerumani.

    Sanaa ya picha

    Akiwa kidato cha tatu Kaka yake Edgar alirudi kutoka Urusi akiwa na kifaa cha kupigia picha au kamera na kumpa Edgar ambapo ndipo Edgar alipovutiwa masuala ya kupiga picha na kuanza kujifunza kupiga picha huku akipiga picha katika sherehe mbalimbali.

    Bagamoyo

    Edgar alianza kusoma masomo yake ya sanaa katika chuo cha sanaa Bagamoyo mwaka 2001, akiwa na wimbo wake mmoja alioutunga tangu akiwa shule ya sekondari, lakini akiwa chuoni hapo, Edgar alipata wazo la kutunga wimbo wake mwingine katika lugha ya Kiswahili ambapo mwaka huo huo alitunga wimbo wake wa Kiswahili uliojulikana kama Mpweke kutokana na kuwa mpweke katika sanaa kutokana na familia yake kushindwa kumkubali kama msanii.

    Upigaji gitaa

    Mwezi wa kumi mwaka 2001, Edgar alianza rasmi mafunzo ya kupiga gitaa, na hadi kufikia mwezi wa kumi na mbili akiwa tayari ameshatunga wimbo wake wa mpweke alianza kutunga na kuimba kwa kutumia gitaa, ambapo alikuwa bado alikuwa akiimba kama msanii mdogo.
    Akiwa hapo chuoni, alipata nafasi ya kukutana na wasanii wakongwe kama vile, Vitalis Maembe, ambaye ni msanii aliye rekodi nyimbo nyingi za asili, John Sombi ambaye naye ni msanii katika nyimbo za asili na amesharekodi nyimbo mbalimbali.
    Chuo cha Bagamoyo kiliamua kutunga nyimbo mbalimbali katika album ambapo Edgar alishiriki kama mpiga gitaa katika nyimbo mbalimbali kama vile , Sumu ya teja, na masamva za wasanii wa Bagamoyo. Huku akiwa ndio anamalizia mwaka wake wa kwanza.

    Baada ya Bagamoyo

    Baada ya kumaliza chuo cha sanaa Bagamo, Edgar alirudi nyumbani na baadae kidogo alipata nafasi ya kwenda kufanya onesho nchini Uingereza katika sanaa ya maigizo na nyimbo, katika eneo la North Landon ukumbi Azure karibu na uwanja wa Wimbley. Baada ya kurudi kutoka Uingereza, Edgar alipata nafasi ya kurekodi wimbo wake wa kwanza katika studio ya Zamunda na ndio aliporekodi wimbio wa Sema Ndio, hii ikiwa ni mwaka 2005. wimbo ambao bado haukumaliziwa na kuachwa kama demo. Hii ilitokana na ushauri wa mtayarishaji wa nyimbo hiyo kuwa ibaki studio kwa muda kidogo ikisubiria wakati wake.
    Baadae alianza masomo ya chuo kikuu, na mwaka 2006, alikutana rafiki yake anayeitwa Edson Tibaijuka na kuanzisha kundi linaloitwa E2E ambapo lilidumu kwa muda wa mwaka mzima, ambapo Edson aliliimarisha Kundi lake la awali la Da'voice na kwa kushirikiana na Edgar na kufanya kundi la watu hilo kuwa na watu wanne. Huku Edgar akiwa na ujuzi wa kupiga gitaa, aliendelea kupiga gitaa katika nyimbo mbalimbali.
    Kabla ya kuamua kurekodi nyimbo zake, walirekodi wimbo akiwa na kundi la Da'voices, na kurekodi nyimbo kama 'Promise' na 'Inaniuma' ambazo katika nyimbo hizo Edgar alipiga gitaa.
    Mwaka 2009, mwezi wa kumi, ndipo walipoanza kutafuta kurekodi wimbo wao wenyewe kama kundi la Dar Voices, ambao wamaeshirikina na msanii mweingine anaitwa Chiss Mc, katika wimbo naona ambao Edgar aliimba na kupiga gitaa. Mpaka sasa kama Da'voice wamerekodi nyimbo mbalimbali.

    Kazi za kujitegemea

    Anatarajia Kutengeneza nyimbo za kutosha katika aina mbalimbali za tamaduni, zinazojulikana kama mix culture , na kutoa nyimbo mbalimbali, mazingira ya nyimbo ambazo zimechanganya tamaduni mbalimbali na kushirikiana na wasanii mbalimba.
  • Philip Emeagwali
    Philip Emeagwali
    WasifuPhilip Emeagwali (amezaliwa 23 Agosti 1954) ni mhandisi ,Igbo kutoka Nigeria na mwanasayansi wa kompyutaMwanajiolojia ambaye alikuwa mmoja wa washindi wawili wa Tuzo la mwaka wa 1989 la Gordon Bell, zawadi kutoka IEEE, kwa matumizi yake ya kompyuta yenye nguvu zaidi - mashine ilitokuwa na visindukaji 65000 - iliyosaidia katika uchambuzi maeneo ya petroli .
    Emeagwali alizaliwa katika Akure, Nigeria tarehe 23 Agosti 1954.[1] Aliacha shule mwaka wa 1967 kwa sababu ya vita vya Nigeria vya Biafran. Wakati alipofikisha miaka kumi na nne, alitumbukizwa ndani ya jeshi laBiafra . Baada ya vita alimaliza masomo sawa na ya shule ya upilikwa kujifunza na alienda Marekani kusoma katika chuo kikuu chini ya udhamini. Kwa kweli, Emeagwali alisomea Uingereza baada ya kutoka Afrika.[onesha uthibitisho] Aienda Marekani baadaye. Alipata shahada ya hisabati kutoka Chuo Kikuu cha Oregon mwaka wa 1977. Alipata Shahada ya bwana katika uhandisi wa mazingira kutoka Chuo Kikuu cha George Washington mwaka wa 1981, na shahada nyingine ya bwana ya Hisabati kutoka Chuo Kikuu cha Maryland, College Park mwaka wa 1986. Yeye pia alipewa shahada ya uhandisi wa bahari, pwani na marina kutoka Chuo Kikuu cha George Washingt mwaka huo. Alikuwa pia anafanya kazi kama mhandisi katika Ofisi ya Ardhi katika Wyoming reclamation katika kipindi hiki.

    Tuzo

    Emeagwali alipokea $ 1.000 [2] mwaka wa 1989 katika tuzo la Gordon Bell Nobel, kwa kuzingatia maombi ya CM-2 kompyuta ya kuhifadhi mafuta . Alishinda katika Kigezo cha "bei / utendaji" , kwa takwimu ya utendaji ya400 Mflops / $ 1m iliyokuwa sabamba na utendaji wa Gflops 3.1 . (kiingizi kilichoshinda katika kigezo cha "utendaji kilele " mwaka huo, pia kwa ajili ya usindikaji wa ujumbe ulio na uhusiano wa mafuta katika CM-2 - iliyofanikiwa na Gflops 6 , au 500 Mflops / $ 1m, lakini majaji waliamua kutopatiana tuzo zote mbili kwa timu moja .) [3] Huu mfumo ulikuwa programu ya kwanza kutumia mbinu ya pseudo-time katika mtindo wa kuhifadhi.[4]
    Mbali na zawadi yenyewe, hakuna ushahidi kuwa kazi ya Emeagwali iliwahi kubaliwa kuchapishwa katika maandiko ya kisayansi, wala kwamba alikuwa na madhara yoyote ya kudumu kwenye uwanja wa utendaji wa juu wa kompyuta au maendeleo ya Mdahalishi. [5] Wala hana utambulizi wowote kulingana na matokeo yake. (Hata hivyo ana alamaMarekani kwa jina la tovuti yake, "EMEAGWALI.COM".) [6] Hata hivyo, zaidi ya miaka ishirini , yeye amepokea tuzo nyingi zaidi na kutambulika kutokana na ushindi wake wa tuzo la Bell Nobel ,[7] kuanzia mmoja kutoka Benki ya Dunia - IMF Klabu ya Afrika na kuchaguliwa kama Mwafrika wa 35 mashuhuri ( Mwanasayansi Mwafrika Mashuhuri) wa wakati wote "katika utafiti uliofanywa na jarida la New African .[8] Mafanikio yake yalinukuliwa katika hotuba na Bill Clinton kama mfano wa vile Wanigeria wanaweza kufanya wakipewa nafasi.[9]Yeye pia ni hulka wa mara kwa mara katika makala ya mwezi ya Historia ya mtu mweusi katika vyombo vya habari. [10][11]

    Kesi mahakamani

    Emeagwali alisomea shahada ya Ph.D. katika Chuo Kikuu cha Michigan kutoka mwaka wa 1987 hadi 1991. Hoja zake hazikukubaliwa na kamati ya watahini wa ndani na nje na hivyo hakupata shahada. Emeagwali alianzisha kesi mahakamani, na kusema kuwa uamuzi huo ulikuwa ukiukaji wa haki za kiraia na kwamba chuo hiki kikuu kilikuwa na ubaguzi kwa sababu ya rangi yake. Kesi hiyo ilifutiliwa mbali, kama ilivyokuwa rufaa katika ya Mahakama ya Michigan ya Rufaa.[12]
  • Roland Emmerich

    Roland Emmerich


    Roland Emmerich
    Roland Emmerich.5132 (cut).jpg
    Roland Emmerich mjini Berlin (2007)
    Amezaliwa10 Novemba 1955 (umri 61)
    Stuttgart, Baden-Württemberg, West Germany
    Kazi yakeMwongozaji wa filamu, mtayarishaji na mwandishi-skrini
    Miaka ya kazi1984–mpaka sasa
    Roland Emmerich (amezaliwa tar. 10 Novemba 1955) ni mwongozaji wa filamu, mwandishi-skrini, na mtayarishaji kutoka nchini Ujerumani. Anafahamika sana kwa kutengeneza filamu nyingi za majanga na mapigano. Filamu zake zimepata jumla ya mauzo zaidi ya bilioni $3 kwa hesabu ya dunia nzima, na kuwa zaidi ya hao wazawa wengine-waongozaji filamu kutoka barani Ulaya. Filamu zake zimepata mapato zaidi ya bilioni $1 kwa nchini Marekani, na kumfanya kuwa mwongozaji filamu wa nchini humo wa 14 kwa mapato makubwa wa muda wote.[1][2][3] Ameanza shughuri zake katika soko la filamu kwa kuongoza filamu ya The Noah's Ark Principle ikiwa kama moja ya tasnifu yake akiwa Chuo Kikuu na kuwa mmoja kati walioanzisha kampuni ya utengenezaji wa filamu ya Centropolis Film Productions mnamo 1985 akiwa na dada'ke. Vilevile anafahimika kwa kuweka bayana kuwa yeye ni bwabwa.

    Maisha ya awali na kazi

    Emmerich alizaliwa mjini Stuttgart, Ujerumani na kukulia katika kitongoji cha Sindelfingen.[4] Akiwa kijana, amepata kusafiri mbali kabisa huko barani Ulaya na Amerika ya Kaskazini katika matembezi yaliyotolewa hela na baba'ke, Hans, tajiri mwanzilishi wa kampuni ya utengenezaji wa mashine za bustani.[5] Mnamo mwaka wa 1977, akaanza kusoma katika Chuo Kikuu cha Filamu na Televisheni cha Munich akiwa na nia ya kusomea msanifu matayarisho. Baada ya kutazama Star Wars Episode IV: A New Hope, akaamua kujiandikisha katika shule za vipindi vya uongozaji wa filamu.[6] Akatengeneza kipande kifupi cha filamu kikiwa kama hitimisho la tasnifu yake mnamo mwaka wa 1981, ametunga na kuongoza urefu mzima wa The Noah's Ark Principle, ambayo hatimaye ilichaguliwa kama filamu funguzi ya Tamasha la Filamu la Berlin la mwaka wa 1984.[7]

G

  • Edi Gathegi

    Edi Gathegi

    Edi Gathegi
    Edi Mue Gathegi (alizaliwa tarehe 10 Machi 1979) ni Ani muigizaji wa filamu na jukwaani kutoka Marekani. Bila shaka anatambulika kwa jina lake la kawaida la Dr. Jeffrey Cole (aka "Big Love") kwenye maigizo ya televisheni House, vilevile kama Cheese kwenye filamu ya mwaka 2007 Gone Baby Gone na kama Laurent kwenye filamu za Twilight na New Moon.

    Maisha Yake ya Utotoni

    Ingawa alizaliwa jijini Nairobi,Kenya , Gathegi alikulia AlbanyCalifornia.[1] Kabla ya kutunukiwa shahada ya kwanza katika Chuo Kikuu cha CaliforniaSanta Barbara ,alijishughulisha sana na kucheza mpira wa kikapu na aliucheza vizuri mpaka pale alipoumia goti lake;Hali hii ilimutamausha kwa hivyo alianza masomo ya uigizaji kama "kozi rahisi". Hapo ndipo aligundua penzi lake katika taaluma ya uigizaji.[1] Baada alijiunga na Tisch School of the Arts akiwa katika Chuo Kikuu cha New York akisomea kozi ya baad ya kufuzu ya uigizaji.[1] Kazi ya Gathegi katika taaluma ya uigizaji ilianzia kwenye maigizo[2] baadhi ya mafanikio yake kwenye uigizaji ni pamoja na Two Trains Running michezo iliyoigizwa huko Old Globe TheatreAs You Like ItTwelfth Night,OthelloA Midsummer Night's Dream, na Cyrano de Bergerac, miongoni mwa maigizo mengine.[3]

    Kazi

    Mara ya kwanza Gathegi kuwa na jukumu la nafasi ya kuigiza kama mtaalamu ni kwenye filamu ya Haitian Cabbie mwaka 2006 Crank .Ingawa awali alikuwa amejaribwa kuigza sehemu ya muhusika Kaylo, maprodiusa walimpatia Efren Ramirez nafasi hiyo na badala yake wakampa Gathegi nafasi ya kuigiza kam Haitian Cabbie.[2] Mwanzo alipinga wazo la yey kuigiza lafudhi ya Haiti lakini alifunzwa na rafiki yake kutoka Haitian.[2] Mwaka 2007 baada ya kuigiza kama muhusika mkuu katika Lincoln Heights na Veronica Mars, Gathegi alikuwa muigizaji maarufu alipoigiza kama Bodie katika Death Sentence , Darudi in The Fifth Patient na kama Cheese katika Gone Baby Gone .Baadaye aliigiza mara kwa mara kama Mormon Intern Dr Jeffrey Cole kwenye igizo la televisheni lililohusu magonjwa na tiba House , na muigizaji mgeni [10] [11] na Life on Mars mwaka 2008 kabla ya kuigiza kama Laurent katika Twilight . kwa mara ya kwanza Gatheji alipojaribiwa kwenye filamu ya mwaka 2008, iliyotokana na jina la kitabu cha kwanza kwenye msururu wa pragramu za televisheni za Stephenie Meyer Twilight Series, alikuwa bado hajasikia kkuhusu mfululizo wa maigizo hayo na wala hakujua kwamaba angeigiza kama mzimu wa kutisha.[4] kwa sasa amesoma mfululizo wote na yeye hujiita kama shabiki sugu.[4][5]
    Gathegi aliigiza kama naibu wa Martin kwenye filamu ya My Bloody Valentine 3D ya mwaka 2009.[1] Ananuia kuongoza kwenye toleo la [[chimbuko pana la filamu kwa jina Joe Turner's Njoo na Gone na pia alirejea nafasi yake kama Laurent katika filamu ya Twilight na New Moon.|chimbuko pana la filamu kwa jina Joe Turner's Come and Gone na pia alirejea nafasi yake kama Laurent katika filamu ya Twilight na New Moon.[6]]]

    Filamu

    mwakaAnwaniDhimaVidokezo
    2006CrankHaitian Cabbie
    2007HouseDr Jeffrey ColeTV series
    Gone Baby GoneCheese
    The Fifth PatientDarudi
    Death SentenceBodie
    Lincoln HeightsBoaTV series
    2008TwilightLaurent
    2009My Bloody Valentine 3DNaibu Martin
    The Twilight Saga: New MoonLaurent
  • Sebastian Giovinco

    Sebastian Giovinco


    {{{jinalamchezaji}}}
    Maelezo binafsi
    Tarehe ya kuzaliwa{{{tareheyakuzaliwa}}}
    Mahala pa kuzaliwa   {{{nchialiozaliwa}}}
    * Magoli alioshinda
    Sebastian Giovinco (alizaliwa mnamo 26 Januari 1987 mjini Turin) ni mwanakandanda mwenye uraia wa Kiitaliano anayeichezea klabu ya Serie A ya Juventus. Giovinco ni mchezaji wa kiungo kati anayeshambulia na mwenye ujuzi wa kuchenga na kutengeneza mchezo unaovutia.
    Kutokana na ufupi wake kimo na ujuzi wake, Giovinco alipewa jina formica atomica (mdudu atom, baada ya mhusika wa kipingi cha runinga cha Hanna-Barbera ) na ingawa alikuwa katika hatua za kwanza za wasifu wake wa kandanda, leo anafikiriwa kama mmoja wa wanakandanda wa Kiitaliano wenye ahadi.

    Wasifu

    Maisha Yake ya Awali

    Giovinco alizaliwa mjini Turin kwa wavyele wahamiaji wa Italia ya kusini; mama yake anatoka Catanzaro, Calabria na baba yake anatoka Palermo, Sicily. Alilelewa akiwa na hamu sana ya kucheza kandanda na mchezo wake wa kusisimua uliivutia klabu ya Juventus ambao ilimleta katika mfumo wao wa mwaka wa 2001, akiwa na umri wa miaka 14. Kisha akapanda safu za klabu za mfumo wao wa vijana, na alisisimua kwa kushinda Campionato Primavera na bianconeri katika kampeni yao msimu wa 2005-06.

    Mchezo wake wa kwanza katika timu ya kwanza ya Juventus

    Giovinco alifaulu kujumuishi katika timu ya Juventus ya kwanza na akacheza mechi yake ya kwanza mnamo 12 Mei 2007 katika ligi ya Serie B dhidi ya Bologna, kuingia kama mbadala wa Raffaele Palladino, na kuashiria mara moja ujuzi wake kwa kumwadalia David Trezeguet pasi safi ambayo aliifunga.

    Mkopo katika klabu ya Empoli

    Mnamo 4 Julai 2007 alikopwa nje kwa klabu ya Empoli timu ya Serie A ya Tuscan ambayo pia ilishiriki katika Kombe la UEFA la msimu wa 2007-08. Giovinco alifunga bao lake la kwanza la Serie A mnamo 30 Septemba 2007 wakati Empoli iliicharaza Palermo mabao 3 kwa 1. Bao lake ndilo lililosababisha ushindi.
    Giovinco alisababisha riba kutoka kwa vyombo vya habari wakati alifunga bao lake la pili wiki chache baadaye, mnamo 4 Novemba. Bao hilo lilikuwa la kusawazisha katika dakika ya mwisho dhidi ya AS Roma, lilikuwa kombora ndefu lililokunjwa la "free kick" kutoka upande wa kulia, bao ambalo lililinganishwa na baadhi ya wapenda kandanda kama la Ronaldinhodhidi ya Uingereza katika kombe la dunia la mwaka wa 2002.

    Kurejea Juventus

    Mnamo 26 Juni 2008 ilithibitisha kuwa Giovinco angerudi Juventus kwa kampeni ya 2008-2009 , kumpatia nafasi ya kucheza katika kiwango cha kombe la mabingwa barani Ulaya vilevile.
    Giovinco alicheza mechi yake ya kwanza ya Juventus dhidi ya Catania mnamo 24 Septemba 2008. Giovinco aliingia kama mbadala wa mchezaji mwenzake wa timu ya Juventus,Pavel Nedved, mwisho wa nusu ya pili, na kucheza mchezo wa kusisimua kwa kumwandalia Amauri pasi safi aliofunga katika ushindi wa Juventus wa 1-0. Alifunga bao lake la kwanza katika Jesi ya Juventus dhidi ya wapinzani Lecce tarehe 7 Desemba 2008 kutoka kwa "FreeKick". Giovinco pia amefunga mabao dhidi ya Catania katika Coppa Italiana nyingine dhidi ya Bologna katika maonyesho ya mchezaji bora wa mechi.

    Wasifu wa Kimataifa

    Giovinco ameiwakilishwa Italia katika kila kiwango ya vijana kuazia mika chini ya 16 ikiendelia juu. Alitajwa katika kikosi cha Italia ch vijana wasiozidi umri wa miaka 21 na kocha mkuu Pierluigi Casiraghi tarehe 1 Juni 2007 ilikucheza mechi yake ya kwanza katika kiwango hicho katika mechi ya kufuzu dhidi ya Albania. Yeye ndiye aliyemwandalia Acquafresca pasi safi ambaye alifunga. Timu hiyo ya Italia ya vijana wasiozidi umri wa miaka 21 ilishinda mechi hiyo 0-1.
    Pia alishiriki katika shindano la Toulon mwaka wa {2008 ambapo aliteuliwa kama mchezaji mwenye thamana zaidi au ukipenda mchezaji bora zaidi katika shindano hilo, kwa kufunga mabao mawili katika mechi ya ufunguzi dhidi ya Ivory Coast, na kufunga penalti ya ushindi katika mechi ya nusu fainali dhidi ya Japani. Italia hatimaye ilishinda shindano hilo, kwa kuicharaza Chile 1-0 katika fainali.
    Giovinco kisha alishiriki katika Michezo ya Olimpiki ya mwaka wa 2008 kwa ajili ya timu ya Kiitaliano. Alifunga bao la kwanza katika ushindi wa 3-0 dhidi ya Honduras katika mechi ya ufunguzi ya shindano hilo ambapo alifunga bao hilo kutoka nje ya boksi kwa mguu wake wa kushoto. Pia alionyesha mchezo wa kuvutia katika mechi ya pili dhidi ya Korea Kusini. Ndoto yake ya kushinda taji la Olimpiki lilitumbukia nyongo baada ya Italia kupoteza 3-2 dhidi ya Ubelgiji katika robo-fainali.

    Tuzo

    Klabu

    • 2005-06 Torneo di Viareggio
    • 2005-06 Campionato Primavera
    • 2006-07 Serie B

    Timu ya Kitaifa

    Vijana wasiozidi umri wa miaka 21 ya Italia
    • 2008 International Tournament of Toulon
  • Jem Godfrey

    Jem Godfrey

    Jeremy "Jem" Godfrey (alizaliwa 6 Oktoba 1971) ni Mtayarishi wa myimbo, mchezaji wa Keyboard na Mtunzi wa miziki kutoka United Kingdom.
    Godfrey alihusika na ufanisi wa nyingi za nyimbo nyingi kwa ushirikiano wa Bill Padley wa Wise Buddah, ikiwemo single ya Atomic Kitten "Whole Again", ambayo kibaki katika matuzo mawili ya Ivor Novello Award na Utayarishaji wa roleo la kimataifa "Kiss Kiss" ya Holly Valance.
    Alishinda katika tuzo za Ivor Novello on 25 Mei 2006 kwa single iliyo na mauzo bora zaidi, "That's My Goal", kwa The X-Factor Shayne Ward[1].
    "That's My Goal", ilitolewa nchini UK mnamo 21 Desemba 2005. Baada ya kuuza nakala 742,000 katika juma, ilikuwa ya Single bora zaidi ya Krismasi ya mwaka wa 2005. Ilishikilia nafasi ya juu kwa majuma manne na ikakaa kwa 75 bora hadi Juni 2006, ambazo ni wiki 21. Kwa wakati huo basi iliorodheshwa ya 4 ya mauzo ya kasi zaidi nchini UK ya wakati wote, ikishindwa na Candle In The Wind ya Elton John, "Anything Is Possible/Evergreen ya Will Young na "Unchained Melody" ya Gareth Gates ambazo zilikuwa na mauzo ya 685,000, 403,000 and 335,000 mtawalia katika siku zao za kwanza za mauzo. Kufikia leo, "That's My Goal" imeuza makala 1,080,000.
    Mnamo 2004, Gdfrey aliunda kundi la “progressive rock " la Frost* ambao kufikia leo wametoa albamu mbili za studio na albamu moja ya Live.
    Mnamo 2009, Godfrey alitangaza katika Frost* wakati wa majadiliano kuwa amechanga msaada wa keyboard Mbili kwa albamu ya Big Big Train, The The Underfall Yard.[2].

    Diskografia

    Mtunzi wa Single

    Utunzi Mwingine

    M0tayarish

    • Blue - All Rise (2002, Programming, Mcheza vyombo)
    • Ronan Keating - Destination (2002, Arranger, Mtayarishi, Mcheza Vyombo)
    • Disneymania (2002, Mtayarishi)
    • Atomic Kitten - Feels So Good (2002, Arranger, Programming, Mtayarishi, Mcheza vyombo)
    • Holly Valance - Footprints (2002, Arranger, Programming, mchezaji vyombo vingi, Mtayarishi, Kuchanganya)
    • Various Artists - Now Dance 2003 (2002, Mtayarishi)
    • Various Artists - Now, Vol. 53 (2002, Arranger, Mtayarishi)
    • Lulu - Together (2002, Arranger, Programming, Mtayarishi, Ucheza vyombo)
    • Atomic Kitten - Atomic Rooster (2003, Arranger, Keyboards, Programming, Mtayarishi, Mcheza vyombo)
    • Various Artists - Brit Awards 2003 (2003, Producer)
    • Atomic Kitten - Feels So Good (2003, Arranger, Programming, Mtayarishi, Uchezaji vyombo)
    • Gareth Gates - Go Your Own Way (2003, Mcheza vyombo)
    • Various Artists - Hit 56 (2003, Mtayarishi)
    • The Lizzie McGuire Movie Original Soundtrack (2003, Mtayarishi)
    • Various Artists - Now, Toleo la 54 (2003, Mtayarishi)
    • What a Girl Wants Original Soundtrack (2003, Mtayarishi, Kuchanganya)
    • Ronan Keating - 10 Years of Hits (2004, Arranger, Programming, Mtayarishi, Mcheza vyombo)
    • Blue - Best of Blue (2004, Mtayarishi, Mcheza vyombo)
    • Play - Don't Stop the Music (2004, Mtayarishi, Mcheza vyombo)
    • Gareth Gates - Go Your Own Way (2004, mtayarishi, Kuchanganya, Mcheza vyombo)
    • Atomic Kitten - Greatest Hits (2004, Arranger, Keyboards, Programming, Producer, Remixing, Instrumentation)
    • Lulu - Greatest Hits (2004, Arranger, Programming, Producer, Instrumentation)
    • Various Artists - Hip to Hip/Can You Feel It, Pt. 1 (2004, Arranger, Multi Instruments, Producer)
    • Various Artists - Hip to Hip/Can You Feel It, Pt. 2 (2004, Mtayarishi, Mcheza vyombo)
    • Various Artists - I Love 2 Party 2004 (2004, Mtayarishi)
    • Disney's Mega Movie Mix (2004, Mtayarishi)
    • Cherie - No. 1, Pt. 1 (2004, Mtayarishi, Mcheza vyombo)
    • Cherie - No. 1, Pt. 2 (2004, Mtayarishi, Mcheza vyombo)
    • Jennifer Ellison - Bye Bye Boy (2004, Mtayarishi, Kuchanganya, Mwanamuziki)
    • Blue - 4Ever Blue (2005, Mtayarishi, Mcheza vyombo)
    • Atomic Kitten - Access All Areas: Remixed and B-Sides (2005, Arranger, Keyboards, Programming, kuchanganya (Remix), Mtayarishi, Mcheza vyombo)
    • Various Artists - Handbag Handbag Handbag: The Soundtrack to the Perfect Girls' Night Out (2005, Mtayarishi)
    • Frost* - Milliontown (2005, Keyboards, Vocals, Mtayarishi)
    • Frost* - Experiments In Mass Appeal (2008, Keyboards, Vocals, Moose Whispering, Producer)
    • Frost* - Frost*Fest (2009, Keyboards, Vocals)
  • Don Gordon (Mwigizaji)

    Don Gordon (Mwigizaji)

    Wasifu fupi

    Jina la kuzaliwa: Donald Walter Guadagno
    Siku ya Kuzaliwa: 13 Novemba 1926 (1926-11-13) (umri wa miaka 83)
    Pahali pa Kuzaliwa: Los AngelesCalifornia,Marekani
    Jina Jingine: Donald Gordon
    Kazi: Mwigizaji
    Mke: Bek Nelson
    (1959 - ?) (alimpa talaka)
    Denise Farr
    (1979 - hadi sasa )

    Wasifu

    Don Gordon (alizaliwa 13 Novemba 1926) ni mwigizaji wa filamu na vipindi vya televisheni wa Marekani. Wakati mwingine, yeye huorodheshwa kama Donald Gordon.
    Gordon alizaliwa jijini Los AngelesCalifornia, akapewa jina la Donald Walter Guadagno. Filamu zake maarufu ni zile alizoigiza akiwa na mwenzake Steve McQueen hasa Bullitt, Papillon na The Towering Inferno. Aliigiza kama mwigizaji mgeni katika kipindi cha McQueen katika stesheni ya CBS kilichoitwa Wanted: Dead or Alive. Katika mwaka wa 1981, Gordon aliigiza kama msaidizi wa Mpinga Kristo Damien Thorn katika filamu. Gordon ,pia, aliigiza sehemu ndogo kama afisa wa polisi katika filamu ya Lethal Weapon, iliyohusisha Mel Gibson na Danny Glover. Katika mwaka wa 1962, alichaguliwa kama mshindani kwa tuzo ya Primetime Emmy kwa uigizaji wake kama Joey Tassil katika kipindi cha CBS cha The Defenders.
    Gordon aliigiza katika toleo la In a Deadly Fashion la 1959 katika kipindi cha televisheni ya Border Patrol, kilichohusisha Richard Webb. Uigizaji mwingine wa Gordon ulikuwa katika toleo la kipindi cha Twilight Zone lililoitwa The Four of Us are Dying. Katika msimu wa 1960 -1961, Gordon alikuwa mwanachama katika kipindi cha The Blue Angels akiwa pamoja na waigizaji maarufu kama Dennis Cross, Warner Jones, Morgan Jones, na Mike Galloway. Kipindi hicho kilikuwa kama makumbusho ya kikundi maarufu cha rubani mashuhuri wa kivita wa Marekani kilichoitwa Blue Angels (Malaika Samawati).
    Mwaka wa 1963, Gordon alihusishwa katika "Without Wheat, There is No Bread katika kipindi cha CBS cha The Lloyd Bridges Show. Mwaka uo huo, yeye alihusishwa katika kipindi cha televisheni ya stesheni ya NBC cha The Eleventh Hour. Katika msimu wa 1963 -1964, yeye aliigiza kama askari kutoka vita ya Vietnam Kusini katika kipindi cha ABC, Channing,kilichohusisha kampasi ya kubuni ya Chuo cha Channing.Channing ilihusisha waigizaji maarufu kama Jason Evers na Henry Jones. Alipewa jukumu jingine katika toleo la The Invisible katika kipindi cha The Outer Limits. Katika mwaka wa 1974, yeye aliigiza mhusika ambaye ni mwasi aliyekuwa ametoka gerezani. Mhusika huyu anauawa na Dick Van Dyke katika toleo la kipindi cha Columbo la Negative Reaction.
  • Donald "Flash" Gordon

    Donald "Flash" Gordon

    Donald Gordon
    Siku ya Kuzaliwa: 17 Julai 1920
    Jina la utani: "Flash"
    Pahali pa Kuzaliwa: GarlandTexas
    Uzalendo: Marekani
    Kikosi cha Jeshi: Wanamaji
    Miaka ya Kazi: 1942 - 1967
    Cheo: Kapteni
    Vita aliyoshiriki: Vita ya Pili ya Dunia
    Tuzo: Distinguished Flying Cross
    Donald "Flash" Gordon (17 Julai 1920) ni rubani shujaa wa vita wa Marekani. Alipiga risasi zaidi ya ndege 7 za Ujapani katika Vita Kuu ya Pili ya Dunia. Alikuwa rubani wa kivita wa Kikosi cha Wanamaji wa Marekani na alipokea tuzo ya Distinguished Flying Cross.

    Wasifu

    Donald alizaliwa Garland, Kansas mnamo tarehe 17 Julai 1920. Alisoma katika Shule ya Upili ya Fort Scott na kumaliza masomo yake ya kiwango hicho katika mwaka wa 1931.Akaendelea na masomo yake katika Chuo cha Fort Scott Junior College akimaliza katika mwaka wa 1941. Gordon alisoma ,pia, mafunzo ya urubani kwa raia na akapata leseni yake. Baada ya kumaliza chuo, Gordon aliingia mpango wa mafunzo ya Naval Aviation Cadet Program mnamo 7 Julai 1941. Alimaliza mafunzo yake na akaajiriwa kazi kama Ensign mnamo 12 Machi,1942, akiwa umri wa miaka 21. Kazi yake ya kwanza ilikuwa kama rubani wa kikundi cha Fighter Squadron 10 (VF-10). Kikundi hiki kiliitwa hapo baadaye Grim Reapers.
    Katika mwezi wa Oktoba 1942, kikundi cha VF-10 kikabebwa na meli ya kivita,Enterprise. Ndege ya kwanza aliyoiendesha Gordon kutoka meli hiyo,Enterprise, ilikuwa ndege ya aina ya F4F Wildcat. Gordon alipata nafasi ya kuumiza adui wake mnamo 26 Oktoba katika Vita ya Santa Cruz. Gordon aliangusha ndege mbili ya aina ya Mitsubishi 97 kwa kutumia risasi na bomu. Katika rekodi zake waliongeza ndege moja ingine chini ya orodha ya "labda" kwa sababu vita ilikuwa kali na haingewezwa kuthibitishwa.
    Alipata nafasi ingine mnamo 30 Januari 1943 katika ziara ya uchunguzi iliyohusisha ndege 12 ya Combat Air Patrol(CAP). Walikuwa wakizuru sehemu kaskazini mashariki ya meli, Gordon akawa wa kwanza kuona ndege 11 ya aina ya Mitsubishi G4M. Akawaarifu wenzake kuhusu adui aliowaona na wakashambulia adui waliokuwa wakiwapiga risasi pia. Gordon alishambulia ndege moja ya Ujapani. Ndege hiyo ikapata moto na kuanguka baharini. Kisha akageuza ndege yake na akaangusha ndege nyingine vivyo hivyo.
    Gordon hakupata sifa aliyostahili kwa kuangusha ndege hizo mbili kwa sababu alikuwa wa mwisho kufika katika chumba maalum cha kupiga ripoti. Alipokuwa akifika chumba hicho na ripoti yake na madai yake ya ushindi, akagundua kuwa kulikuwa na madai 19 kwa ndege 11 za adui ingawa yeye alijua kuwa alipiga risasi mbili zikaanguka na mbili zikahepa.
    Huu ulikuwa mwanzo mzuri sana katika kazi ya rubani huyu wa kivita. Baada ya kushiriki katika mapambano mawili tu na adui, Gordon alipewa jina la utani la "FLASH GORDON". Jina ambalo lilikuwa jina la shujaa wa kivita wa hekaya za kisayansi. Sifa hii ilistahili kwa sababu aliangusha ndege tatu zilizothibitishwa ,ndege mbili zingine akiwa na wenzake na moja iliyoorodheshwa kama "labda ilianguka".
    Ilipofika mwezi wa Juni 1943, kikosi cha ndege cha VF-10 kikarudi Marekani. Walipokuwa huko, kikosi hicho kikaongezewa silaha za vita na ndege ya aina ya F6F Hellcat. Hellcat ilikuwa ndege bora zaidi ya kivita: kubwa, kasi sana na yenye nguvu nyingi. Vilevile,ilikuwa na risasi na bomu nyingi: risasi 1600 za aina ya 0.5 in(12.7 mm) badala ya zile 1300 za ndege ya Wildcat.
    Katika mwezi wa Januari 1944, akiwa Luteni wa daraja la chini, Gordon alirudi vita tena akiwa kwenye meli ya Enterprise. Aliipiga risasi ndege ya aina ya A6M Zero na kuiangusha karibu na Taroa mnamo 29 Januari na 16 Februari akawa mashuhuri kivita alipopiga risasi na kuangusha Zero ingine.
    Mnamo 1 Aprili 1944, Gordon alipandishwa cheo akawa Luteni kamili. Katika vita iliyojulikana kama "Marinas Turkey Shoot", Luteni Gordon alipiga risasi ndege ya aina ya Yokosuka D4Y "Judy" iliyokuwa ikijaribu kushambulia ndege za Marekani. Siku iliyofuata , alihusika katika mpango wa kukabiliana na mashambulizi ya ndege za Kijapani. Alipokuwa akisindikiza ndege ya kikosi cha wanamaji, alipiga risasi Zero ingine katika harakati za ulinzi.
    Baada ya vita, Gordon aliendelea kufanya kazi na kikosi cha Wanamaji huko Marekani na akawa mmoja katika kikosi cha kwanza kutumia ndege mpya za kivita. Gordon aliendelea kimasomo na akafuzu kutoka Chuo cha Jackson, Hawaii. Alipandishwa cheo kuwa Kapteni mnamo 1 Februari 1962 na akastaafu kutoka kikosi chake katika mwezi wa Julai 1967.
    Katika kazi yake, alipewa sifa kwa kuangusha ndege saba za adui zilizothibitishwa, mbili akiwa na wenzake na moja ikaorodheshwa katika orodha ya "labda ilianguka". Alipokea tuzo ya Distinguished Flying Cross yenye nyota mbili za dhahabu, Air Medal yenye nyota tatu za dhahabu, Commendation yenye Combat “V” kwa ndege mbili alizoangusha na wenzake, Navy Unit Citation na tuzo mbili ya Presidential Unit (moja ya kazi yake kwenye Guadalcanal na moja kwa kazi yake kwenye meli ya Enterprise).

N

  • Dugary Ndabashinze

    Dugary Ndabashinze


    Dugary Ndabashinze
    Maelezo binafsi
    Jina kamiliDugary Ndabashinze
    Tarehe ya kuzaliwa8 Oktoba 1989 (umri 28)
    Mahala pa kuzaliwa   Burundi
    Urefumita 1.82
    Nafasi anayochezeaKatikati
    Maelezo ya klabu
    Klabu ya sasaK.R.C. Genk
    Namba21
    Klabu za ukubwani
    MiakaKlabu
    2008K.R.C. Genk
    Timu ya taifa
    2007Burundi
    * Magoli alioshinda
    Dugary Ndabashinze (amezaliwa tar. 8 Oktoba 1989) nimchezaji wa mpira wa miguu wa kulipwa kutoka nchini Burundi. Kwa sasa anaichezea Klabu ya K.R.C. Genk huko Ubelgiji. Klabu hiyo ni katika Klabu kubwa huko Ubelgiji.
    Dugary ni kiungo muhimu katika Timu ya Taifa ya Burundi. Alijiunga na Klabu hiyo ya K.R.C Genk mwaka 2008 na mechi nyingi amecheza dakika nyingi amefaanikisha kufunga goli mbili katika mechi zake zote na timu hiyo msimu uliopita.
    Mechi yake ya kwanza alipoingizwa uwanjani alifunga goli,na hiyo mechi yake ya kwanza magazeti mengi ya Ubelgiji yalizungumzia kua anaonekana ni mchezaji mzuri.

No comments: