Monday 16 October 2017

Umoja wa Afrika

Umoja wa Afrika

Bendera ya Umoja wa Afrika
Ramani ya Umoja wa Afrika. Nchi zote za Afrika ni wanachama (baada ya Moroko kujiunga upya tarehe 30 Januari 2017).
Umoja wa Afrika (UA) (kwa KiingerezaAfrican Union (AU)KifaransaUnion Africaine (UA)KihispaniaUnión Africana (UA) ; KirenoUnião Africana (UA) ) [1] ni muungano wa nchi 55 za Afrika ulioanzishwa mnamo Julai 2002.
Umoja huu unaendeleza kazi za Umoja wa Muungano wa Afrika (kwa Kiingereza: Organisation of African Union - OAU) uliokuwepo 1963 hadi 2002.
Nia ya umoja huu ni kujenga muundo na mfumo wa kisiasa, wa kiuchumi, na wa kijamii ili kufikia wakati ambapo bara la Afrika litakuwa na bunge moja, benki moja, jeshi moja, rais mmoja, sarafu moja, n.k.
Dhumuni kubwa la umoja huu ni kuunganisha nguvu za mataifa ya Afrika ili kuweza kutatua matatizo yanayokabili bara hili kama vile vitanjaaUkimwi, n.k.

Nchi wanachama

Umoja wa Afrika ina nchi wanachama 55, yaani nchi zote za bara la Afrika (baada ya kurudi kwa Moroko, iliyokuwa imejiondoa mwaka 1985kwa sababu UA ilitambua Sahara ya Magharibi kuwa nchi ya kujitegema wakati Moroko inadai ya kwamba ni eneo la majimbo yake ya kusini). [2]Hata hivyo mwaka 2016 Moroko ilionyesha nia ya kujiunga tena na UA.[3]
Mkutano wa kwanza wa Bunge la Umoja wa Afrika ulifanyika mwaka 2004 huko Afrika Kusini.

Mikutano mikuu ya UA

  1. Durban (Afrika Kusini): 9-11 Jul. 2002.
  2. Maputo (Msumbiji): 10-11 Jul. 2003.
  3. Sirte (Libya), mkutano wa dharura: Feb. 2004.
  4. Addis Ababa (Ethiopia): 6-8 Jul. 2004.
  5. Abuja (Nigeria): 24-31 Jan. 2005.
  6. Sirte (Libya): 28 Jun. - 5 Jul. 2005.
  7. Khartoum (Sudan): 16-24 Jan. 2006.

Viongozi

Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya UA ni N. Dlamini-Zuma.

Umoja wa Muungano wa Afrika

Nchi za Umoja wa Maungano ya Afrika
buluu: nchi zilizounda OAU;
kijani: nchi zilizojiunga hadi 1969
kichungwa: nchi zilizojiunga hadi 1979
nyekundu:Zimbabwe ilijiunga 1982
dhambarau:nchi zilizojiunga tangu 1990
Umoja wa Muungano wa Afrika (Kiingereza: Organisation of African Unity, OAU; Kifaransa: Organisation de l'Unité Africaine, OUA) ulikuwa jumuiya ya nchi huru za Afrika iliyoanzishwa 1963 na kudumu hadi 2002. Ulikuwa mtangulizi wa Umoja wa Afrika ambao ni jumuiya ya nchi za Afrika tangu Julai 2002.
OAU iliundwa tarehe 25 Mei 1963 mjini Addis Abeba na nchi 30 za Afrika. Kwenye mkutano wa 11 Julai 2001 Mkutano Mkuu uliamua kuunda Umoja wa Afrika kama haua mpya kwenye harakati ya kuungana Afrika na OAU ilifungwa tar. 9 Julai 2002.
Mwishoni nchi zote za Afrika zilikuwa wanachama isipokuwa Moroko iliyojitenga mwaka 1985 baada ya Sahara ya Magharibikupokelewa katika OAU.


Bunge

Bunge ni chombo cha kutunga sheria na pia ni mmoja wa mihimili mitatu inayounda mfumo wa utawala kulingana na mgawanyo wa madaraka katika dola. Mihimili mingine ni mahakama na serikali.
Bunge ni chombo kinachotokana na mfumo wa utawala wa Westminster, ambao umerithiwa na nchi nyingi duniani kutoka Uingereza. Kutokana na mfumo huo kuenea, mara nyingi Bunge la Uingereza huitwa "Mama wa Bunge" duniani.
Bunge la kwanza nchini Uingereza liliundwa wakati wa utawala wa Mfalme Henri III katika karne ya 13. Bunge hilo lina sehemu mbili, Bunge la Makabwela na Bunge la Mabwanyeye.
Katika nchi nyingi zinazofuata mfumo wa WestminsterWaziri Mkuu huwa ndio kiongozi mkuu wa serikali bungeni.
Shughuli za bunge husimamiwa na mbunge aliyechaguliwa kama mwenyekitirais au spika wa bunge.
Kuna aina mbili za bunge
  • bunge la "chumba kimoja" ambako wawakilishi wote wa wananchi hukaa na kufanya maazimio pamoja
  • bunge la "vyumba viwili" ambako kitengo kikubwa zaidi kina kazi ya kutunga sheria na wabunge wake huchaguliwa moja kwa moja na wananchi katika majimbo ya uchaguziyanayotakiwa kuwa takriban na idadi ya wapiga kura sawa. Kitengo kingine mara nyingi huitwa "senati" au "chumba cha juu" kwa kawaida ni kidogo zaidi, wabunge wake huchaguliwa ama na wawakilishi wa mikoa au majimbo au wanateuliwa pia kufuatana na kanuni za katiba (k.m. kwa shabaha ya kuwakilisha makundi maalumu katika jamii) na madaraka yake kwa kawaida ni madogo lakini inathibitisha au kukataa sheria zilizoamuliwa na bunge la kwanza; lakini hapa kuna tofauti nyingi kati ya nchi na nchi.

Benki

Taiwan Cooperative Benki katika Taipei
Benki ni taasisi inayoshughulika biashara ya fedha. Shughuli zake za msingi ni pamoja na kukopa na kukopesha fedha.
Kwenye ngazi hii benki inatunza pesa ya watu wengi. Kwa utunzaji huu benki haiachi pesa kukaa bure tu lakini inaitumia kwa biashara yake. Inaitumia kukopesha kampuni au watu wanaohitaji fedha.
Wanaokopa pesa wanalipa riba ambayo ni bei ya benki kwa huduma ya kukopesha; kutokana na mapato haya benki inalipa pia riba ndogo zaidi kwa wale waliopeleka pesa zao kwake. Tofauti kati ya viwango vya aina hizi mbili za riba ni faida na pato la benki. Jambo muhimu linaloangaliwa na benki wakati wa kukopesha pesa ni uwezo wa mkopaji kurudisha deni lake.
Asili ya benki ilikuwa biashara ya wakopeshaji fedha. Siku hizi kuna benki za aina mbalimbali pamoja na:
  • Benki za biashara ambazo ni makampuni yanayolenga kupata faida kubwa kwa kutoa huduma za kifedha. Benki hizi zinashughulikia mawasiliano kati ya watu au makampuni yenye pesa za ziada na watu au makampuni wanaohitaji pesa.
  • Benki za ushirika ambazo mara nyingi hazilengi faida kubwa lakini huduma kwa wateja wasio na pesa nyingi; benki hizi zinapokea pia kiasi kidogo cha pesa na kutoa mikopo kwa wajengao nyumba au wafanyabiashara wadogo. Benki hizi hutumia mfumo wa uwekezaji pesa ili kujikuza pamoja na wateja wao. Wamarekani pia hutumia mbinu hii ambayo wanaiita 401k[1].
  • Benki kuu ambayo kwa kawaida ni taasisi ya serikali inayosimamia utoaji wa pesa taslimu na kiasi cha pesa inayopatikana sokoni kwa jumla. Inasimamia pia kazi ya benki za biashara na za ushirika.

Jeshi

  • Jeshi ni jumla ya watu wanaopewa mamlaka ya kutumia nguvu ya silaha kutetea nchi kwa niaba ya dola au kutekeleza maagizo ya serikali dhidi ya maadui wa nje kwa nguvu ya silaha.
    Neno latumika hasa kwa kutaja jeshi la ardhijeshi la wanamaji na jeshi la anga.

Yaliyomo

  1. Kazi ya jeshi

  • Kazi ya jeshi ni
    • kulinda nchi dhidi ya maadui wa nje
    • kutetea nchi dhidi ya mashambulizi kutoka nje au
    • pia kushambulia nchi nyingine kama hatua hii imeamriwa na serikali halali.
    Kusudi hili shidi ya hatari na nje ni tofauti kuu na kazi ya polisi ambayo ni mkono mwingine wa serikali ya taifa mwenye silaha. hata hivyo kuna nchi ambako tofauti kati ya jeshi na polisi si wazi vile hasa kuna nchi nyingi ambako jeshi limepewa wajibu wa ndani ya taifa au ambako wanajeshi walichukua mamlaka mkononi mwao kwa nguvu ya silaha zao.
    Katika nchi mbalimbali kuna vikosi vinavyotekeleza shughuli ndani ya taifa lakini vina silaha sawa na sehemu za jeshi na wakati mwingine vinahesabiwa kama sehemu ya jeshi. Kwa mfano vikosi vinavyolingana na FFU ya Tanzania vinaitwa gendarmerie huko Ufaransa na nchi nyingi za Afrika Magharibi au carabinieri huko Italia na kule vinahesabiwa kama mkono wa jeshi ingawa kazi yao ni ya ndani ya nchi.
    Hali ya jeshi vitani husimamiwa na sheria ya kimataifa ya vita jinsi ilivyoundwa katika mikataba mbalimbali ya kimataifa. Sheria hii inalenga kulinda watu raia wakati wa vita na pia haki za wanajeshi wakikamatwa na adui. Sheria inadai ya kwamba wanajeshi wote wanahitaji
    • kuwa na sare rasmi inayoonekana na kuwatofautisha na watu raia
    • kuwa chini ya mamlaka rasmi inayoeleweka na kuwajibika kwa serikali yao
    • kubeba silaha zao wazi
    • kuitikia masharti ya sheria ya kimataifa
    Wanajeshi wanafuata utaratibu huu wanalindwa na sheria inayokataza pia watu raia kubeba na kutumia silaha na kushiriki katika mapigano. Katika vita nyingi sheria ilipuuzwa lakini kuna mifano kadhaa katika karne ya 20 ambako jinai za vitani zilifuatiliwa kwa mfano kwenye Kesi za Nuremberg kuhusu jinai za vitani upande wa Ujerumani na kesi zilizofikishwa mbele ya Mahakama ya Kimataifa ya Jinai tangu mwaka 2000.

Jeshi la ardhi

Jeshi la ardhi lina kituo ama kambi ambayo kambi hii yaweza kulinda kundi ya Jeshi, divisheni ama umma wajeshi. Kukitokea vita, Jeshi huwa wakipeleka divisheni na kundi za kijeshi kwa vipimo kulingana na vita na mbinu za kusukuma ama kushinda adui kwa vita. Na pia ratili ya vita ikiwapendukia, Jeshi hupeleka wanajeshi pulikiza ili kusukuma adui kabisa ama kumshinda adui.

Jeshi la taifa

Shurutisho la jeshi

    No comments: