Tuesday 24 October 2017

Maajabu ya dunia

Maajabu ya dunia

Maajabu saba ya dunia ya kale
Orodha ya makala yafuatana na picha hizi saba
Maajabu ya dunia ni orodha ya majengo saba ya pekee iliyojulikana na Wagiriki wa KaleWagiriki waliita majengo hayo ΤÀ ΕΠΤÀ ΘΕÁΜΑΤΑ ΤΗΣ ΟΙΚΟΥΜÉΝΗΣ (ΓΗΣ) ta hepta theamata tes oikumenes (ges) - Maajabu saba ya dunia inayokaliwa).
Mara ya kwanza majengo ya ajabu yaliorodheshwa na mwandishi Herodoti mnamo 450 KK. Ilhali maandiko yake hayakuhifadhiwa, habari hii inatokana na waandishi wengine waliomrejea. Kulikuwa na orodha tofauti[1][2] lakini ile inayojulikana na kutajwa zaidi ni ile ya Antipater wa Sidon[3]
Ilhali orodha hii ilikusanywa na waandishi wa Ugiriki ya Kale kuna majengo tu yaliyojulikana katika ustaarabu huo. Kwa hiyo hakuna mifano kutoka UhindiChinaAsia ya MasharikiAmerikaAfrika kusini ya Sahara wala Ulaya ya Kaskazini.
Majengo ya orodha ya Antipater hayakudumu hadi leo, isipokuwa Piramidi za Giza. Mengine yaliharibika kutokana na matetemeko ya ardhi au kubomolewa, tena hadi leo hapajulikani mahali pa "Mabustani ya Semiramis". Sanamuna picha za kuchongwa kutoka Kaburi la Mausolo na Hekalu la Artemis zilikusanwa na kuhifadhiwa katika Makumbusho ya Britania mjini LondonUingereza.

Maajabu saba ya Kale

  1. Piramidi za Giza (Misri ya Kale)

    Piramidi za Giza

    Piramidi kubwa za Giza: upande wa kushuto piramidi ya Mykerinos, katikati ya Khefren na kulia ya Kheops
    Piramidi za Giza ni kati ya majengo yanayojulikana zaidi duniani. Pamoja na mava mengine ni sehemu ya makaburi ya Giza yaliyokuwa mahali pa kuzika wafalme wa Misri na wakubwa wa milki yao kwa muda wa miaka 2500.
    Ziko kando ya bonde la mto Nile, karibu na mji wa Giza takriban kilometa 15 kutoka Kairomji mkuu wa Misri.

    Historia ya maeneo ya makaburi ya Giza kwa jumla

    Makaburi ya kwanza yalijengwa huko tangu chanzo cha milki ya Misri ya Kale takriban miaka 3,000 KK.
    Wakati wa nasaba ya 4 ya Misri eneo la makaburi hayo liliongezeka sifa kwa sababu wafalme KheopsKhefren na Mykerinos waliamua kujenga huko piramidi kwa ajili ya makaburi yao wenyewe.
    Kutokana na ujenzi wa makaburi ya kifalme ndugu wa familia zao na maafisa wa juu walizikwa huko pia hadi mwisho wa nasaba ya 7 ya Misri.
    Baada ya hapo na kwa sababu ya kuhamishwa kwa mji mkuu wa milki kwenye kusini ya nchi umuhimu wa eneo la makaburi ya Giza ulipungua. Mazishi ya maana yalitokea tena wakati wa nasaba za mwisho za Misri, katika vipindi vya kuvamiwa na Uajemi.

    Piramidi kubwa na Sfinksi

    Eneo la makaburi ya Giza hujulikana hasa kutokana na piramidi kubwa pamoja na sfinksi kubwa zilizokuwa maarufu tayari katika nyakati za kale. Mwanahistoria wa Ugiriki wa Kale aliyeitwa Herodoti alizihesabu kati ya Maajabu Saba ya Dunia na tangu siku zile miaka 2,500 iliyopita zilitembelewa na watalii.
    Piramidi tatu kubwa zinajulikana kufuatana na majina ya Kigiriki ya mafarao au wafalme wa Misri waliozikwa ndani yao: piramidi za Kheops, Khefren na Mykerinos. Piramidi za Kheops na Khefren ziko karibu kimo moja, ile ya Kheops ni kubwa kidogo lakini ile ya Khefren inaonekana kubwa kwa macho kwa sababu imejengwa juu ya ardhi ya juu kiasi kwa hiyo kwa macho ya mtazamaji inafika juu zaidi.
    Jina la KigirikiJina la KimisriAlitawala mnamoKimo asiliaKimo cha leoKipimo cha
    upande wa msingi
    Piramidi ya KheopsKhufru~ 2620
    - 2580 KK
    146.1 m138.75 m230 m
    Piramidi ya KhefrenKhafre~ 2558
    -2532 KK
    143.6 m136.4 m215.25
    Piramidi ya MykerinosMenkaure2558
    -2532 KK
    65.55 m62 m102.2 m
    x 104.4 m
    Piramidi hizo zote hazikukaa peke yake bali zilijengwa pamoja na majengo ya kando.
    • Kila piramidi ilikuwa na mahekalu mawili ambako makuhani walitoa sadaka kwa ajili ya roho za mafarao marehemu peponi. Hekalu 1a kwanza lilijengwa mbali kidogo, kwenye chanzo cha barabara ya maandamano yaliyoendelea hadi hekalu la pili karibu na piramidi. Njia hizo za maandamano zilitumiwa hasa wakati wa sherehe za kumkumbuka farao.
    • Kwa kawaida malkia (wake wa farao) walizikwa katika piramidi ndogo au makaburi mengine kando ya piramidi kubwa. Piramidi za Kheops na Mykerinus huwa na piramidi 3 za malkia wa kila mfalme. Kwenye piramidi za Khefren hakuna makaburi ya malkia yaliyotambuliwa.

    Historia ya baadaye

    Tangu siku za kale watu walichukua mawe kutoka majengo ya Misri kwa kuyatumia katika majengo ya nyakati zao. Hii ndiyo sababu ya kwamba kimo cha piramidi kimepunga na hasa mawe mazuri yaliyofunika nyuso za piramidi yamepotea.
    Katika karne ya 12 BK mtawala wa Misri al-Malek al-Aziz Othman ben Yusuf alijaribu kubomoa piramidi akizitazama kama ushahidi wa upagani wa kale. Wafanyakaziwalianza kukata mawe kutoka piramidi ndogo ya Mykerinos lakini ikaonekana ya kwamba kazi ya kubomoa labda ingekuwa ghali sawa na kujenga. Baada ya miezi kadhaa shughuli hizo zilisimamishwa na hadi leo kuna pengo katika ukuta wa kaskazini.
  2. Mabustani ya Semiramis (Babeli, leo Irak)
  3. Hekalu ya Artemis mjini Efeso ((Ugiriki ya Kale, leo Uturuki, Asia Ndogo)

    Hekalu la Artemis mjini Efeso

    (Elekezwa kutoka Hekalu ya Artemis mjini Efeso)
    Maghofu ya hekalu huko Efeso
    Hekalu la Artemis mjini Efeso (kwa Kigiriki ὁ ναὸς τῆς Ἀρτέμιδος Ἐφεσίης, τὸ Ἀρτεμίσιον (ho naòs tês Artémidos Ephesíês, tò Artemísion), kwa Kilatini: Templum Dianae Ephesi(n)ae au Artemisium Ephesi(n)um) lilikuwa jengo kubwa la kidini lililojulikana kote katika mazingira ya Mediteraneo wakati wa Ugiriki wa Kale na Roma ya Kale.
    Hekalu hilo lilihesabiwa kati ya maajabu saba ya dunia.

    Historia[hariri | hariri chanzo]

    Lilijengwa mjini Efeso kwa muda wa miaka 120 kuanzia mwaka 560 KKMfalme Kroisos wa Lidia ndiye aliyeanzisha ujenzihuu.
    Hekalu lilikuwa na urefu wa mita 115 na upana wa mita 55. Nguzo zake zilisimama mita 18.
    Liliharibika na kujengwa upya mara kadhaa. Mwaka 262 BK liliharibiwa kabisa wakati wa uvamizi wa Wagodoni.
    Leo hii kuna nguzo moja tu inayoonekana.
  4. Sanamu ya Zeus mjini Olympia (Ugiriki ya Kale)

    Sanamu ya Zeus mjini Olympia

    Mchoraji mholanzi alichora picha hii ya Zeus wa Olympia katika karne ya 16 kufuatana na vitabu vya kale.
    Sanamu hii ya Kiroma ilitengenezwa kutokana na mfano wa Zeus wa Olympia.
    Sanamu ya Zeus mjini Olympia ilimwonyesha mungu mkuu wa dini ya Ugiriki ya KaleZeus aliaminiwa kuwa baba wa miungu wa Ugiriki.
    Sanamu yenye kimo cha mita 12 ilimwonyesha mungu huyu akikalia kitini kama mzee mwenye hekima. Ilikaa kwenye hekalu kubwa ya Zeus ya Olympia kando la uwanja wa michezo ya Olimpiki. Ilitengenezwa na mchongaji mashuhuru Phidias aliyejenga kiini cha ubao na chuma pamoja na jasi na kuifunika kwa ubao, dhahabu na pembe. Phidias aliifanyia kazi kwa miaka 8 kuanzia mwaka 438 KK. Baada ya kuimaliza Phidias alishtakiwa kuwa ameiba kiasi cha dhahabu iliyokusudiwa kwa sanamu akauawa.
    Watu wa Kale walihesabu sanamu hii kati ya maajabu saba za dunia.
    Mwaka 40 BK Kaisari wa Roma Caligula alishindwa kupeleka sanamu kwenda mjini Roma. Lakini wakati wa karne ya 4 ilipelekwa Konstantinopoli ikasimamishwa pale hadi mwaka 475 ilipoharibiwa katika moto kubwa.
  5. Kaburi la Mausolo mjini Halikarnassos (Ugiriki ya Kale, leo Uturuki)
  6. Sanamu ya Kolossos kisiwani Rhodos (Ugiriki ya Kale)

    Sanamu ya Kolossos kisiwani Rhodos

    Picha ioneshayo jinsi gani watu wa baadaye waliwaza Kolossos; hali halisi hakusimama juu ya mlango wa bandari lakini kando lake
    Sanamu ya Kolossos kwenye kisiwa cha Rhodos ilikuwa kati ya maajabu saba ya dunia ya kale.
    Kolossos ilikuwa mnara wa taa mwenye umbo la sanamu ya mtu aliyesimama kwenye mlango wa bandari na kushika moto kama mwenge. Kazi ya sanamu ilikuwa kuelekeza meli bandarini wakati wa usiku. Sanamu ilimwonyesha mungu wa jua Helios.
    Ilijengwa kwa muda wa miaka 12 ikakamilishwa mnamo 300 KK na kuwa na kimo cha zaidi ya mita 30. Ilikuwa sanamu kubwa kabisa ya dunia ya kale. Kumbukumbu zimehifadhiwa kuwa matumizi ya vifaa yalikuwa pamoja na tani 13 za bronzina tani 8 za chuma zilizofunika nguzo za matofari na mawe zilizokuwa majenzi ya ndani.
    Sanamu ilisimama miaka 60-70 tu ikaanguka wakati wa tetemeko la ardhi mnamo 226 KK. Ikakatika kwenye magoti. Mabaki yalikaa palepale kwa sababu watu wa Rhodos waliogopa hasira ya mungu Helios wakisimamisha kitu kilichoangushwa na miungu.
    Kwa miaka karibu 900 watalii wa dunia ya kale walishangaa mabaki makubwa.
    Mwaka 654 Rhodos ilivamiwa na Waarabu Waislamu na Muawiya (wakati ule bado gavana wa Shamu bado khalifa) aliuza metali kwa mfanyabiashara. Inasemekana ya kwamba ngamia 900 walihitajika kubeba mzigo.
  7. Mnara wa Pharos ya Aleksandria (Misri)

    Pharos ya Aleksandria

    Pica ya Pharos kwenye sarafu za Aleskandria zilizotolewa wakati wa Dola la Roma.

    Pharos ya Aleksandria ilikuwa mnara wa taa mjini Aleksandria ya Misri ikahesabiwa kati ya maajabu saba ya dunia. Kimo chake hakikujulikana kikamilifu lakini kilikuwa kati ya mita 110 na 150.
    Mnara huu ulijengwa kwenye kisiwa kidogo kilichoitwa "Pharos" kiliochokuwa mita chache mbele ya mwambao wa Aleksandria. Baadaye mnara uliitwa kwa jina la kisiwa.
    Ujenzi ulitokea mnamo mwaka 282 KK. Kwa karne nyingi Pharos ilikuwa kati ya majengo marefu ya dunia. Iliporomoka baada ya matetemeko ya ardhi yaliyotokea Aleksandria 1303 na 1323.
Kati yake piramidi pekee zimebaki hadi leo.

Maajabu ya dunia ya sasa

Katika ulimwengu kila siku maajabu yanaongezeka na kufanya maajabu mapya ya dunia kukubalika mara kwa mara. Kwa mfano, mwaka 2016 kuna maajabu yake. Orodha ya maajabu hayo hutolewa na watu mbalimbali kwa mitazamo tofautitofauti: wengine wanaishia upande wa majengo, wengine wanahesabu hata mazuri ya uasilia n.k.
Vitu hivi hadi kufikia kuitwa maajabu ya dunia ina maana ni vya pekee duniani kote, na hakuna kitu kingine kama hicho au cha kufanana nacho.
Tanzania kuna kitu kimoja ambacho kinasemekana ni kati ya maajabu ya dunia ambacho ni kasoko ya Ngorongoro, iliyoko mkoa wa Manyara.

Picha za "Maajabu ya Kisasa"

No comments: