Monday 9 October 2017

NCHI ZENYE WATU MAARUFU DUNIAN

Ujerumani

Bundesrepublik Deutschland
Shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani
Bendera ya UjerumaniNembo ya Ujerumani
BenderaNembo
Kaulimbiu ya taifa: Einigkeit und Recht und Freiheit
(Kijerumani: "Umoja na Haki na Uhuru”)
Wimbo wa taifaWimbo wa Wajerumani (beti ya tatu)
Umoja na Haki na Uhuru
Lokeshen ya Ujerumani
Mji mkuuBerlin
52°31′ N 13°24′ E
Mji mkubwa nchiniBerlin
Lugha rasmiKijerumani 1
Serikali
Rais
Chansella (Waziri Mkuu)
Shirikisho la Jamhuri
Joachim Gauck
Angela Merkel
Dola Takatifu la Kiroma

Dola la Ujerumani
Shirikisho la Jamhuri
Maungano
843 (Mkataba wa Verdun)

18 Januari 1871
23 Mei 1949
3 Oktoba 1990
Eneo
 - Jumla
 - Maji (%)

357,050 km² (ya 63)
2.416
Idadi ya watu
 - 2014 kadirio
 - 2011 sensa
 - Msongamano wa watu

80,716,000 (ya 16)
80,219,695
226/km² (ya 58)
FedhaEuro (€) 2 (EUR)
Saa za eneo
 - Kiangazi (DST)
CET (UTC+1)
CEST (UTC+2)
Intaneti TLD.de
Kodi ya simu+49
1 KideniKijerumani cha KaskaziniKisorbiaKifrisia ni lugha rasmi katika mikoa kadhaa 2 hadi 1999: Mark (DM)


Ujerumani (pia: Udachi, kwa KijerumaniDeutschland) ni nchi ya Ulaya ya Kati.
Ni nchi yenye watu wengi katika Ulaya, isipokuwa Urusi ina watu zaidi.
Uchumi wa Ujerumani una uwezo mkubwa: ni nchi inayouza bidhaa nyingi nje kushinda mataifa yote ya dunia.
Muundo wake kiutawala ni shirikisho la jamhuri lenye majimbo 16 ndani yake na kila jimbo lina kiwango cha kujitawala.
Lugha asilia ni Kijerumani kinachojadiliwa kwa lahaja mbalimbali, lakini wenyeji wote wanasikilizana. Katika maeneo mawili kuna wasemaji asilia wa Kideni na Kisorbia.
Wahamiaji wa karne ya 20 wameleta lugha zao, hasa Kituruki na lugha za Ulaya ya Kusini.
Upande wa diniWakristo ni 66.8% (Wakatoliki 30.8%, Walutheri 30.3%, Waprotestanti wengine 5.7%), huku Waislamu wakiwa 1.9%. Thuluthi moja ya wakazi haina dini yoyote.

Jina la nchi

Wenyeji wanaiita "Deutschland" (De-Deutschland.ogg Deutschland (info), tamka: doich-land) na jina hilo limeingia katika Kiswahili kama "Udachi". Lilikuwa jina la kawaida katika karne ya 19 na mwanzoni mwa karne ya 20.
Siku hizi neno "Ujerumani" limechukua nafasi yake kutokana na Kiingereza kinachoiita "Germany". Watu wengine hulichukua "Udachi" kuwa na maana "Uholanzi" wakilichanganya na neno la Kiingereza "Dutch" (tamka datsh) linalomaanisha "Kiholanzi".[1]

Jiografia

Ujerumani unaenea kati ya Bahari ya Kaskazini halafu ya Bahari Baltiki upande wa kaskazini na milima ya Alpi upande wa kusini. Mpaka na Denmark inakata sehemu ya kusini ya rasi ya Jutland. Mpaka wa kusini unafuata sehemu za chini za Alpi, Ziwa la Konstanz na mto Rhein dhidi ya Austria na Uswisi.
Mipaka yake upande wa magharibi na mashariki ilibadilika mara nyingi katika historia yake; baada ya vita kuu mbili za karne ya 20 maeneo makubwa yalitengwa na Ujerumani na kuwa sehemu za Poland, Urusi, Chekia na Ufaransa. Wakazi Wajerumani mamilioni walifukuzwa au kuwa raia wa nchi hizi.
Tangu mwaka 1945 mpaka wa mashariki ni mto Oder dhidi ya Poland na vilele vya Milima ya Madini (jer. Erzgebirge) na Msitu wa Bohemia.
Upande wa magharibi mpaka dhidi ya Ufaransa ni mto Rhein pamoja na vilima kati ya Alsasi na Rhine-Palatino na vilima dhidi ya Luxemburg na milima ya Eifel dhidi ya Ubelgiji. Mpaka dhidi ya Uholanzi katika magharibi kaskazini inapita katika tambarare ikifuata mistari ya kihistoria.
Ujerumani ina kanda tatu za kijiografia:
  • uwanja wa kaskazini ambayo ni sehemu ya Tambarare ya Ulaya Kaskazini ni takriban theluji ya eneo lake
  • nyanda ya vilima na milima ya kati
  • milima ya kusini pamoja na Alpi.
Tambarare ya pwani ya kaskazini ni eneo bapa; hakuna milima na nchi haipandi juu ya mita 200, sehemu kubwa ni kati ya uwiano wa bahari na mita 60 juu yake. Uso wa nchi ni tokeo la kupitiwa na barafuto kubwa za enzi ya barafu iliyopita iliyonyosha uso wa nchi ikiacha vilima vya mchanga, kokoto na ardhi ambavyo ni miinuko ya pekee inayofika hadi mita 200 juu ya uwiano wa bahari.
Nyanda ya milima ya kati ni mabaki ya milima ya kale iliyotokea miaka milioni 350 iliyopita na kupungua sana tangu zamani ile kwa njia ya mmomonyoko. Kwa hiyo hakuna vilele vikali bali vyote vina umbo poa.
Alpi katika kusini ni milima mirefu Ujerumani ingawa sehemu kubwa na za juu zaidi ziko nje ya mipaka ya Ujerumani huko Uswisi na Austria. Milima hii ilianza kutokea miaka 135-50 iliyopita tu. Kilele cha juu atika Ujerumani ni mlima wa Zugspitze yenye urefu wa mita 2,962 juu ya UB

Historia

  1. Dola Takatifu la Kiroma (900-1806)

    Dola Takatifu la Kiroma

    Dola Takatifu la Kiroma si sawa na Dola la Roma la Kale.
    Ramani ya Dola Takatifu la Kiroma yaonyesha mikoa yake.
    Maeneo ya Dola Takatifu la Kiroma pamoja na mipaka ya nchi za sasa.
    Dola Takatifu la Kiroma (KijerumaniHeiliges Römisches ReichKilatiniSacrum Romanum Imperium) lilikuwa jina la Ujerumani kati ya takriban mwaka 1000 na 1806. Lakini dola hilo, licha ya Ujerumani, lilikuwa pia na maeneo makubwa, yakiwa ni pamoja na AustriaItalia ya Kaskazini, UbelgijiUholanzi na Ucheki wa leo.
    Mipaka yake yalibadilika mara kadhaa katika karne nyingi za kuwako kwake.

    Tabia za Dola

    Maeneo hayo yote yaliunganishwa chini ya Kaisari aliyekuwa pia mfalme wa Wajerumani.
    Maeneo hayo yalikuwa na kiwango kikubwa cha kujitegemea yakitawaliwa na makabaila wa ngazi mbalimbali na maaskofu wa Kanisa Katoliki au yakiwa miji huru.
    Halikuwa dola la kisasa, kwa kuwa vyombo vya dola vilikuwa vichache. Kaisari alitegemea hasa mali yake binafsi pamoja na haki ya kuthibitisha watu waliopokea vyeo mbalimbali.
    Tangu 1438 hadi 1806 cheo cha Kaisari kilibaki katika familia ya Habsburg waliotawala Austria.

    Chanzo baada ya Karolo Mkuu

    Asili ya dola lilikuwa milki ya Karolo Mkuu aliyefaulu kuunganisha Ujerumani, Ufaransa na Italia chini yake. Mwaka 800alipokea cheo cha Kaisari wa Roma kutoka mikono ya Papa Leo III.
    Hatua hii ilichukuliwa kama kuendelezwa kwa Dola la Roma la Kale katika magharibi ya Ulaya hata kama hali halisi ilikuwa kwamba milki ya Karolo ilikuwa milki ya Wafranki na Wagermanik wengine na taasisi zote za Roma ya Kalezilikuwa zimeshakwisha kabisa katika magharibi ya Ulaya.
    Yaliyobaki ya Roma ya Kale yaliendelea Ulaya mashariki kwa umbo la Milki ya Bizanti.
    Lakini makaisari walijenga hoja la "translatio imperii" (kwa Kilatini: ukabidhi wa mamlaka) la kuwa mamlaka ya Kaisari yaliyokuwa na Waroma wa Kale na sasa yalikabidhiwa kwa Wajerumani.
    Karolo aligawa urithi wake kati ya wanae na hii ilikuwa chanzo cha Ufaransa upande wa magharibi na Ujerumani upande wa mashariki. Cheo cha Kaisari kiliendelea upande wa mashariki. Hivyo Ufaransa iliendelea kuwa ufalme wa nchi moja lakini upande wa mashariki Wajerumani waliunganishwa pamoja na watu jirani chini ya Kaisari aliyekuwa pia mkuu wa Italia ya Kaskazini, Bohemia (Ucheki) na sehemu mbalimbali ambazo leo hii ni ama Ufaransa au Ubelgiji na Uholanzi.
    Mjerumani wa kwanza aliyepokea ukaisari kutoka kwa Papa wa Roma alikuwa Otto I mwaka 962.
    Dola likaendelea hadi 1806 wakati Napoleon alipolifuta.
    Jina la "Dola Takatifu la Kiroma" lilianza kutumiwa tangu 1100 likaitwa baadaye pia "Dola Takatifu la Kiroma la Wajerumani".

    Matatizo ya Dola

    Hadi karne ya 13 dola lilikuwa na nguvu. Baadaye maeneo ndani yake yalijiongezea kiwango cha kujitawala. Kila Kaisari alichaguliwa na kamati ya makabaila na watemi wakuu. Kabla ya uchaguzi Makaisari walipaswa kuahidi ya kwamba wataheshimu haki ya makabaila juu ya maeneo yao. Mwishoni maeneo yalikuwa kama nchi huru kabisa yaliyoendelea kujitawala, kuendesha vita dhidi ya majirani kufuata siasa zao.
    Mwishoni dola lilikuwa za zaidi ya maeneo 300 ya kujitegemea; mengine makubwa kama Austria na Prussia, mengine madogo mno yenye eneo la mji mmoja tu.
    Tangu karne ya 16 dola halikuwa na uwezo tena wa kufuata siasa ya nje kwa pamoja isipokuwa dhidi ya Waturuki Waosmani walioshambulia mara mbili Viennamji mkuu wa makaisari (1529 na 1683).
    Lakini vita vya kuwasukuma Waturuki watoke katika maeneo ya Ulaya ya kusini-mashariki waliyowahi kuvamia viliendeshwa na Kaisari kama mkuu wa Austria bila ya msaada wa dola takatifu.
    Dola lilifaulu kwa kiasi fulani kutunza amani au angalau kuepuka vita kati ya maeneo yake. Isipokuwa Vita ya Miaka 30 kati ya 1618 na 1648 ilionyesha uwezo mdogo wa dola na karibu theluthi moja ya wakazi wa Ujerumani walikufa.
    Tangu karne ya 17 majirani kama Ufaransa na Sweden walijiingiza zaidi na zaidi katika siasa ya Ujerumani na maeneo makubwa kama Prussia hayakujali tena maazimio ya Kaisari. Dola Takatifu likaendelea kudhoofika.
    Vita vya Napoleon vilimaliza mabaki yake.
  2. Shirikisho la Ujerumani (1815-1866)

    Shirikisho la Ujerumani

    Shirikisho la Ujerumani katika Ulaya.
    Sehemu za nchi mbili kubwa ndani yake Austria na Prussia zilikuwa nje ya shirikisho
    Shirikisho la Ujerumani (Kijer.: Deutscher Bund") ilikuwa ushirikiano wa nchi za Ulaya ya Kati hasa za shemu za Ujerumanibaada ya Mkutano wa Vienna 1815 hadi vita ya Prussia na Austria ya 1866.
    Nchi hizi ziliwahi kuwa sehemu za Dola Takatifu la Kiroma hadi 1806 iliyokwisha kutokana na vita za Napoleoni.
    Nchi na maeneo ya kujitawala 38 zilijiunga ndani yake. Hizi zilikuwa nchi 34 zenye utaratibu wa kifalme (ufalme, utemi) na miji huru minne yenye katiba ya kijamhuri. Kila nchi ilijitawala na kujitegemea hata kimataifa.
    Nchi mbili kubwa kati ya wanachama zilikuwa Dola la Austria na Ufalme wa Prussia. Zote mbili zilikuwa na maeneo makubwa ambayo yalihesabiwa kuwa nje ya eneo la shirikisho kwa sababu hazikuwahi kuwa sehemu za Dola Takatifu kabla ya 1806.
    Shirikisho lilikuwa na nguvu wakati ambako Austria na Prussia zilishirikiana vizuri. Tangu 1860 na hasa tangu vita ya Schleswig ya 1864 uhusiano ulikuwa mbaya na kusababisha vita ya Ujerumani ya 1866 iliyomaliza shirikisho.
    Tokeo la vita lilkuwa ya kwamba Austria ilibaki nje ya siasa ya Kijerumani; sehemu kubwa ya Ujerumani iliunganishwa katika Shirikisho la Ujerumani ya Kaskazini chini ya uongozi wa Prussia na madola ya Ujerumani kusini kama Bavaria yalibaki pekee.
    Katika vita ya Ujerumani na Ufaransa nchi za Ujerumani kusini zilishikamana na Prussia. Tokeo lake likuwa kuundwa kwa Dola la Ujerumani tar. 18 Januari 1871 mjini Versailles (Ufaransa).
  3. Dola la Ujerumani (1871-1945)

    Dola la Ujerumani

    Dola la Ujerumani 1871-1918
    Dola la Ujerumani 1919-1937
    Dola la Ujerumani Kubwa 1942
    Dola la Ujerumani (Kijer.: Deutsches Reich) lilikuwa jina la Ujerumani kati ya 18 Januari 1871 hadi 1949 (wengine husema: 1945).
    Dola hili lilikuwa na vipindi vitatu:

    Dola la Kaisari

    1871 nchi mbalimbali katika Ujerumani ziliungana chini ya uongozi wa Prussia baada ya ushindi katika vita dhidi ya Ufaransa wa 1870/71. Mfalme Wilhelm I wa Prussia alitangazwa kuwa Kaisari wa Kijerumani 18 Januari 1871 mjini Versailles katika Ufaransa.
    Dola lilikuwa na katiba, serikali na bunge. Chansella wa kwanza alikuwa Otto von Bismarck.
    Kipindi hiki kilikwisha katika mapinduzi ya Kijerumani ya Novemba 1918 mwishoni wa vita kuu ya kwanza ya duniaKaisari Wilhelm IIakajiuzulu na kuondoka nchini.

    Jamhuri ya Weimar

    Dola la Ujerumani lilitangazwa kuwa jamhuri. Mkutano wa katiba ulikaa mjini Weimar hivyo katiba mpya iliitwa "Katiba ya Weimar" na hivyo kipindi kilichofuata huitwa Jamhuri ya Weimar.. Ujerumani ilikuwa nchi ya kidemokrasia iliyojenga upya uhusiano mwema na nchi jirani.
    Utaratibu wa kisiasa iliporomoka katika matatanisho ya kiuchumi baada ya 1930. Vyama vya kikomunisti na kifashisti vilianza kupata kura nyingi.

    Dola la Hitler

    30 Januari 1933 Adolf Hitler alikuwa chansella wa Dola la Ujerumani akaanza mara moja kujenga udikteta wake wa Dola la Tatu. Sehemu ya siasa yake ilikuwa kujenga uwezo wa kijeshi wa Ujerumani.
    Tangu 1938 Hitler alipanusha eneo la Dola kwa kutwaa Austria na Uceki na kuingiza maeneo haya ndani ya Dola la Ujerumani.
    Utawala wake ulilenga kwa vita kuu ya pili ya dunia iliyoanza 1 Septemba 1939. Katika miaka ya kwanza ya vita hii Ujerumani ilitawala sehemu kubwa ya Ulaya. 1942 jina lilibadilishwa kuwa "Dola la Ujerumani Kubwa" (Kijer.: Grossdeutsches Reich) na maeneo mengi ya Poland na Ulaya ya Mashariki yalitangazwa kuwa shemu za Dola.

    Mwisho wa Dola la Ujerumani

    Ujerumani ilishindwa na tangu 8 Mei 1945 mataifa washindi walichukua mamlaka ya serikali katika Ujerumani. MarekaniUrusiUingereza na Ufaransa ziligawa nchi katika kanda za utawala. Maeneo yote yaliyotwaliwa na Hitler yalitengwa tena. Sehemu kubwa ya Ujerumani katika mashariki -takriban robo ya eneo lake hadi ya 1937- iliondolewa na kuwa sehemu ya Poland ilhali wakazi Wajerumani zaidi ya milioni 10 walifukuzwa.
    1949 Wajerumani walianza tena kujitawala katika nchi mbili. Kanda za MarekaniUingereza na Ufaransa ziliungana kwa jina la Shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani. Kanda la Kirusi lilikuwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kijerumani.
    Hali halisi kipindi cha Dola la Ujerumani kilikwisha hata kama sehemu zote mbili zilidai kuendeleza urithi wake na hakuna tangazo rasmi la kumaliza dola hili.
  4. Shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani (1949 hadi 1990 Ujerumani wa Magharibi)
  5. Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kijerumani (1949 hadi 1990 Ujerumani wa Mashariki)

    Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kijerumani

    Bendera ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kijerumani
    Ramani ya Ujerumani; sehemu ya kijani ni Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kijerumani
    Ujerumani, kanda za utawala wa washindi wa Vita Kuu ya Pili mw. 1946
    Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kijerumani (JKK) ilikuwa jina la dola katika mashariki ya Ujerumanikati ya 1949 - 1990. Iliundwa 7 Oktoba 1949 katika eneo la ukanda wa utawala wa Kirusi kama nchi mshindi wa Vita Kuu ya Pili ya Dunia.
    Dola hili lilijulikana pia kama "Ujerumani wa Mashariki". Sehemu ya wakazi wake hawakupendezwa na jina hili kwa sababu katika historia na utamaduni wa nchi maeneo makubwa yalihesabiwa zaidi kuwa "Ujerumani wa Kati" au "Ujerumani wa Kaskazini".
    Mji mkuu ulikuwa Berlin lakini sehemu ya kiutawala iliyokuwa chini ya Urusi pekee.
    Dola nyingine ya Kijerumani ilianzishwa katika maeneo ya kanda za utawala ya MarekaniUingerezana Ufaransa kwa jina la Shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani (SJU): Ujerumani ya Magharibi.
    Wakazi wengi wa nchi hii hawakupendezwa na utaratibu wa kisiasa na maendeleo ya kiuchumi chini ya muundo wa ukomunisti.
    Mwaka 1989 utawala wa chama cha kikomunisti uliporomoka. Serikali iliyochaguliwa katika uchaguzi huru ilianza majadiliano na serikali ya SJU kwa kusudi la kuunganisha pande zote mbili za Ujerumani. Mwishowe mikoa yote ya JKK iliamua kujiunga na SJU tarehe 3 Oktoba1990.
    Gari mashuhuri la Trabi ilikuwa moja kati ya modeli mbili za motokaa zilizotengenezwa katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kijerumani












Miji

Majiji yenye wakazi zaidi ya milioni moja ni:
  1. Berlin
  2. Hamburg
  3. München
  4. Köln
Miji mikubwa mingine ni:
  1. Bonn
  2. Bremen
  3. Düsseldorf
  4. Essen
  5. Hannover
  6. Frankfurt am Main
  7. Stuttgart

Majimbo

Makala kuu: Majimbo ya Ujerumani
  1. Flag of Baden-Württemberg.svg Baden-Württemberg
  2. Flag of Bavaria (lozengy).svg Bavaria (Freistaat Bayern)
  3. Flag of Berlin.svg Berlin
  4. Flag of Brandenburg.svg Brandenburg
  5. Flag of Bremen.svg Bremen (Freie Hansestadt Bremen)
  6. Flag of Hamburg.svg Hamburg (Freie und Hansestadt Hamburg)
  7. Flag of Hesse.svg Hesse (Hessen)
  8. Flag of Mecklenburg-Western Pomerania.svg Mecklenburg-Pomerini (Mecklenburg-Vorpommern)
  9. Flag of Lower Saxony.svg Saksonia Chini (Niedersachsen)
  10. Flag of North Rhine-Westphalia.svg Rhine Kaskazini-Westfalia (Nordrhein-Westfalen)
  11. Flag of Rhineland-Palatinate.svg Rhine-Palatino (Rheinland-Pfalz)
  12. Flag de-saarland 300px.png Jimbo la Saar (Saarland)
  13. Flag of Saxony.svg Saksonia (Freistaat Sachsen)
  14. Flag of Saxony-Anhalt.svg Saksonia-Anhalt (Sachsen-Anhalt)
  15. Flag of Schleswig-Holstein.svg Schleswig-Holstein
  16. Flag of Thuringia.svg Thuringia (Freistaat Thüringen)

Watu maarufu

Alberto Mkuu

Alberto Mkuu

Alberto Mkuu alivyochorwa na Tommaso da Modena mwaka 1352
Alberto Mkuu (LauingenDonau, leo nchini Ujerumani1205 hivi - Cologne, Ujerumani, 15 Novemba 1280) ni jina alilopewa kwa heshima askofu Alberto wa Bollstädt (au wa Cologne) kutokana na mchango wake mkubwa upande wa elimu ya kawaida na ile ya dinina vilevile upande wa uchungaji na wa upatanishi wa watu na watawala.
Mtawa wa Shirika la Wahubiri, anahesabiwa kuwa mwanafalsafa na mwanateolojia bora ya Ujerumani katika Karne za Kati.
Alijitahidi kulinganisha imani na akili akiingiza falsafa ya Aristotle katika Ukristo, jambo lililoendelezwa na mwanafunzi wake bora, Thoma wa Akwino.
Alitangazwa na Papa Gregori XV kuwa mwenye heri mwaka 1622, halafu na Papa Pius XI kuwa na mtakatifu na mwalimu wa Kanisatarehe 16 Desemba 1931.
Mwaka 1941 Papa Pius XII alimtangaza msimamizi wa wanasayansi.
Sikukuu yake inaadhimishwa kila mwaka tarehe 15 Novemba.

Maisha

De animalibus
Alberto, mtoto mdogo wa mtawala wa Bollstädt, alizaliwa Lauingen (Svevia, Ujerumani) lakini mwaka haujulikani: 12051206 kama si 1193.
Vilevile hakuna hakika kuhusu elimu yake ya msingi, kama aliipata nyumbani au shuleni, lakini ujanani alitumwa kwenye chuo kikuu cha Padova (Italia), maarufu kwa masomo yaliyompendeza zaidi: lughahojahisabatifalaki na muziki.
Akiwa huko, alikuwa anahudhuria ibada katika kanisa la Wadominiko, ambao utakatifu wa maisha yao ulichangia, pamoja na uhusiano wake wa dhati na Mungu, kumfanya atamani kuwa mmojawao hata akaweza kushinda upinzani wa familia yake.
Mwaka 1223, baada ya kusikia hotuba ya Jordano wa Saksoniamwalimu mkuu wa pili katika historia ya Shirika la Wahubiri, alijiunga na utawa huo ulioanzishwa na Dominiko Guzman. Jordano mwenyewe alimvika kanzu ya shirika.
Alipomaliza masomo yake, ama Padova ama kwingine, na kupata upadrisho, alitumwa kufundisha katika vituo vya teolojia vilivyounganika na konventi za shirika huko HildesheimFreiburg in BrisgauRegensburgStrasburg na Cologne mmoja kati ya miji mikuu ya mikoa, ambapo aliishi kwa awamu kadhaa na hatimaye ukawa mji wake.
Akiwa katika konventi ya mji huo, akisoma Liber Sententiarum ya Petro Lombardo mwaka 1245, aliagizwa kwenda Paris (Ufaransa) alipojipatia digrii katika kituo kikuu cha huko, maarufu kuliko vyote upande wa teolojia.
Tangu hapo alianza kazi yake kubwa ya kuandika, mbali ya kutekeleza majukumu makubwa alivyozidi kupewa.
Akiwa safarini alisikilizwa na Thoma wa Akwino, kijana mkimya mwenye kutafakari, ambaye Alberto alitambua ukuu wa akili yake akamtabiri umaarufu wa kimataifa. Kati yao kukawa na heshima na urafiki mkubwa hadi mwisho. Huyo mwanafunzi mpya aliongozana naye hadi Paris halafu (1248) Cologne, ambapo Alberto alikuwa amechaguliwa kuwa gombera wa kwanza, wakati Thoma akawa mwalimu wa pili na Magister Studentium ("mwalimu wa wanafunzi").
Katika mkutano mkuu wa Wadominiko uliofanyika Valenciennes mwaka 1250, pamoja na Thoma na Petro wa Tarentaise, alitunga taratibu za masomo na za stahili shirikani.
Mwaka 1254 alichaguliwa mkuu wa kanda ya Ujerumani, wadhifa mgumu alioshughulikia vizuri sana. Alijitokeza kwa ari yake katika kutembelea jumuia za eneo lake kubwa, lililojumlisha Ulaya Kaskazini na ya Kati, huku akihimiza uaminifu kwa mafundisho na mifano ya Mt. Dominiko.
Mwaka 1256 alikwenda Roma ili kutetea mashirika ya ombaomba dhidi ya mashambulizi ya Wiliamu wa Saint-Amour, ambaye kitabu chake De novissimis temporum periculishatimaye kililaaniwa na Papa Aleksanda IV tarehe 5 Oktoba 1256.
Akiwa Roma, vipawa vyake viligunduliwa na Papa aliyetaka awe naye ili kufaidika na mashauri yake ya kiteolojia. Hivyo Alberto alishika nafasi ya mwalimu wa nyumba ya Papa na kufafanua Injili ya Yohane.
Mwaka 1257 alijiuzulu kama mkuu wa kanda ili ajitose kusoma na kufundisha.
Mwaka 1260 kwa uamuzi wa Papa huyohuyo, alipewa daraja takatifu ya uaskofu kwa ajili ya Jimbo la Regensburg, ambalo lilikuwa kubwa na maarufu, lakini wakati huo lilipitia matatizo mbalimbali. Basi, aliliongoza kwa bidii isiyokoma, akifaulu kurudisha amani mjini, kupanga upya parokia na nyumba za kitawa pamoja na kuchochea upya huduma za huruma.
Mwaka 1262 alijiuzulu, halafu miaka 1263-1264 alihubiri katika Ujerumani na Ucheki wa leo kwa agizo la Papa Urban IV akarudia kazi ya kufundisha na kuandika huko Cologne.
Kama mtu wa salaelimu na upendo, aliingilia kwa mafanikio matukio mbalimbali ya Kanisa na jamii: hasa alipatanisha watu wa Cologne na askofu mkuu wao aliyekuwa ameharibu sana.
Mwaka 1270 alimuandikia Thoma, aliyekuwa Paris, ili kumsaidia dhidi ya hoja za Sigieri wa Brabante na wafuasi wa Averroe. Ilikuwa kitabu cha pili dhidi ya huyo mwanafalsafaMwarabu (cha kwanza kiliandikwa mwaka 1256 kwa jina De Unitate Intellectus Contra Averroem).
Mwaka 1274 aliitwa na Papa Gregori X ashiriki Mtaguso wa pili wa Lyon, ambamo alifanya kazi kubwa ili kurudisha umoja kati ya Kanisa la Kilatini na lile la Kigiriki. Huko alipata taarifa ya kifo cha Thoma akasema, "Mwanga wa Kanisa umezimika".
Alijitokeza tena kwa nguvu mwaka 1277, ilipotangazwa nia ya Etienne Templieraskofu mkuu wa Paris pamoja na wengine ya kulaani maandishi ya Thoma kama yenye uzushi. Ili kumtetea alifunga safari kwenda Paris kuyafafanua.
Mwaka 1278 (alipoandika wasia wake) alianza kusahausahau mambo, na mwili wake uliodhoofishwa na maisha magumu ya kujinyima na ya kazi ulizidi kushindwa na uzee hadi akafa tarehe 15 Novemba 1280 katika chumba chake konventini.
Alizikwa katika kanisa la parokia ya Mt. Andrea ya Cologne.

Maandishi

Vitabu vyake vingi vinahusu fani zote za elimu ya wakati ule: mantikisayansi mbalimbali, elimunafsiafalsafamaadilisiasateolojia, ufafanuzi wa Biblia n.k. Orodha yake inashangaza kwa upana wa mada alizozikabili kitaalamu. Ndiyo sababu Papa Pius XII alimpangia jina la “Doctor universalis” (yaani Mwalimu wa kila jambo).
Akiwa mtaalamu mkuu wa biolojia wakati wake, aliunganisha vizuri sayansi na ufunuo wa Mungu, falsafa na teolojia. Ulinganifu huo unamfanya awe karibu na watu wa leo katika maswali wanayojiuliza kuhusu asili na maendeleo ya ulimwengu.
Upana wa mawazo yake ulijitokeza hasa katika kuelekeza Kanisa lipokee falsafa ya Aristotle katika ufafanuzi wa ulimwengu, kutokana na hakika ya kwamba kila kinachokubaliwa na akili nyofu kinapatana na imani katika ufunuo wa Mungu. Kwa namna hiyo Alberto aliwezesha falsafa kuwa fani inayojitegemea, ikishirikiana na kuunganika na teolojia katika umoja wa ukweli tu, bila kuchanganyikana.
Yeye alifaulu kushirikisha hata mawazo hayo kwa namna sahili na ya kueleweka, kama alivyofanya katika mahubiri aliyowapa watu wa kila kiwango cha elimu, waliovutiwa na maneno yake na mfano bora wa maisha yake.

Watu maarufu

No comments: