Monday 2 October 2017

Kimondo


Vimondo vinavyong'aa angani; picha imechukuliwa kwa muda wadakika kadhaa na kuonyesha vimondo vilivyoonekana katika kipindi hicho.Nyota hazionekani tena kama nukta, bali kama mistari mifupi kutokana namwendo wa dunia na anga katika muda wa kupigwa kwa picha.
Vimondo (pia: meteoroidimeteorimeteoridi) ni violwa vidogo vya angani vinavyozunguka jua katika anga la nje. Vikingia katika angahewa ya dunia vinaonekana kama miale ya moto angani.

Majina na Ukubwa

Kimsingi hakuna tofauti kati ya vimondo na asteroidi ni swali la ukubwa tu. Violwa vidogo kuanzia ukubwa wa punje ya mchanga hadi kufikia kipenyo cha mita kadhaa huitwa vimondo. Vikubwa zaidi huitwa asteroidi. Hivyo kimondo ni kidogo kuliko asteoridi na kikubwa kushinda vumbi la angani.

Kimondo hiki cha chuma kilipatikana China.
Katika lugha nyingi kuna majina tofauti kutaja hali mbalimbali za vimondo.
  • Meteoroidi ni kimondo wakati iko kwenye anga la nje (en:meteroid)
  • Meteori ni kimondo wakati inapita katika angahewa ya dunia na kuwaka kutokana na msuguano na molekuli za hewa ikionekana kama mstari mfupi wa nuru. Waswahili wa Kale waliita hali hii "kinga cha sheitani" (taz. chini). (en:meteor)
  • Meteoriti ni mabaki ya kimondo - meteoroidi zilizofika kama mawe kwenye uso wa ardhi bila kuugua kabisa hewani (en:meteorite)

Kugonga angahewa ya dunia

Obiti ya kimondo unaweza kuingiliana na obiti ya dunia au sayari nyingine. Kimondo kikilikaribia kiolwa cha angani kikubwa zaidi kinavutwa na graviti yake.
Kikikaribia mno dunia yetu kinaingia katika angahewa na kuanguka chini kwa kasi kubwa sana. Njiani kinapashwa moto kutokana na msuguano wa hewa dhidi yake. Kiasi cha joto kinatosha kuchoma kimondo kidogo kabisa hewani. Hii inaonekana kwa macho matupu kama mstari wa moto angani unaowaka kwa sekunde 1-2. Hii ni hali inayoitwa pia "meteori". Waswahili wa Kale waliita "Vinga vya sheitani" walieleza miale hii ya moto angani kuwa malaika angani wanazuia masheitani kupanda juu vipande vya kuni vya kuwaka
Kama kimondo ni kikubwa zaidi ni sehemu zake za nje tu zinazochomwa na kiini kinagonga uso wa dunia.
Kati ya vimondo kumi vikubwa kabisa duniani ambavyo mabaki yake yanaonekana, kimojawapo ni Kimondo cha Mbozi nchini Tanzania.

Hatari za vimondo ?

Vimondo ni hatari kwa vyombo vya angani kwa sababu ya kasi yake kubwa. Hata punje ndogo yaweza kusababisha uharibifu mwingi.
Duniani kuna pia hatari fulani lakini si kubwa hali halisi. Katika miaka yote ya karne ya 20 kuna taarifa 21 pekee za nyumba kugongwa na kimondo.
Katika karne ya 20 kuna taarifa zifuatazo kuhusu watu walioathiriwa na vimondo:
Hata ni kubwa kweli pale ambako magimba makubwa zaidi yaani asteroidi yanagonga dunia. Pigo la asteroidi linaachisha nishati sawa na mabomu ya nyuklia na mgongano na asteroidi kubwa chenye kipenyo cha km 180 unaaminiwa kulisababisha vifo vya viumbehai wengi duniani miaka milioni 65 iliyopita. Soma zaidi hapa Hatari kutokana na violwa vya kukaribia dunia.

No comments: