Tuesday 17 October 2017

Uingereza or [history of england]

Uingereza 

Kwa maana nyingine, tazama Uingereza (maana).

England
Uingereza
English FlagEnglish Coat of Arms
(Bendera ya Uingereza)(Nembo la Uingereza)
Wito (Kifaransa): Dieu et mon droit
("Mungu na haki yangu")
Uingereza katika Ulaya
Uingereza kwenye visiwa vya Britania
Mahali pa Uingereza (kijani cheusi) kwenye visiwa vya Britania ndani ya Ufalme wa Muungano (kijani nyeupe) pamoja na Jamhuri ya Eire (buluu) upande wa magharibi
LughaKiingereza
Mji MkuuLondon
Mji MkubwaLondon
Eneo
– jumla

130,395 km²
Wakazi
2004
–sensa ya 2001
– Msongamano wa watu
50.1 millioni [1]
49,138,831 [2]
377/km²
Umoja wa nchi yote927 BK na mfalme
Athelstan
Dini rasmiChurch of England(Anglikana)
PesaPound sterling (£) (GBP)
MasaaUTC / (GMT)
Summer: UTC +1 (BST)
Ua la TaifaWaridi ya Tudor (nyekundu, nyeupe)
Mtakatifu wa kitaifaMt George
Uingereza (pia: IngilandiEngland) ni nchi kubwa ndani ya Ufalme wa Muungano yenye wakazi milioni 50 au 83% ya wakazi wa Ufalme wote na eneo lake ni theluthi mbili ya kisiwa cha Britania.
Katika lugha ya kila siku "Uingereza" hutaja mara nyingi Ufalme wote au kisiwa chote cha Britania. Lakini hali halisi "Uingereza" ni ile sehemu kubwa zaidi kwenye kisiwa kile pamoja na Uskoti (Scotland) na Welisi (Wales).
Asili ya jina la Kiswahili ni neno "إنجليزي injilisi (matamshi ya Kimisri: ingilisi)" katika lugha ya Kiarabu na kwa namna ya Kibantu sauti ya "l" ikawa "r"; Waarabu walipokea jina kutoka kwa Kihispania "Ingles" ambalo ni neno lao kwa Mwingereza.

Yaliyomo

Jiografia

Uingereza iko kwenye kisiwa cha Britania ambayo ni kisiwa kikubwa cha Ulaya. Imepakana na Welisi upande wa magharibi na Uskoti upande wa kaskazini. Mji Mkuu ni LondonUfaransa iko upande wa kusini ng'ambo ya Mfereji wa Kiingereza. Tangu mwaka 1994 kuna njia ya reli kwa tobwe chini ya mfereji inayounganisha Uingereza na Ufaransa.
Kati ya miji mikubwa ya Uingereza ni: LondonManchesterBirminghamLeedsSheffieldBradford na Liverpool.
Uingereza ina visiwa vingi vidogo; kikubwa ni Isle of Wight katika kusini.



Mito ya Uingereza



Mto Thames katika London mnamo mwaka 1750







Mikoa ya Uingereza

Historia

Uingereza ilikaliwa na makabila ya Wabritania wenye lugha za Kikelti na kuvamiwa na Dola la Roma katika karne ya pili BK. Ikawa sehemu ya Dola la Roma hadi karne ya tano BK. Wakati ule Waroma walipaswa kuondoa wanajeshi wao kisiwani kwa ajili ya ulinzi wa nchi za bara.

Uvamizi wa Waanglia-Saksoni

Katika karne za 5 na 6 BK makabila ya Kigermanik walivamia kisiwa hasa WasaksoniWaanglia na Wadenmark. Walileta lugha zao za Kigermanik zilizochukua nafasi ya lugha ya Wabritania.
Wabritania na Waroma waliokuwa wamebaki walihamia maeneo ya kando kama Welisi au Cornwall au kuvuka mfereji wa Uingereza kwenda Britania Ndogo (Kiingereza:Brittany; Kifaransa: Bretagne).
Karne zilizofuata kisiwa kiliona madola madogo na hali ya vita. Mwaka 937 Mfalme Athelstan aliweza kuunganisha karibu eneo lote la Uingereza ya leo.

Uvamizi wa Wanormani

Mwaka 1066 wanajeshi Wanormani kutoka kaskazini ya Ufaransa walivamia Uingereza na kuteka yote chini ya mtemi William Mshindi. Wavamizi walitawala wakitumia aina ya Kifaransa. Lugha zote mbili za wananchi na za mabwana ziliendelea pamoja sambamba hadi kuwa lugha moja cha Kiingereza.

Ufalme wa Muungano

Tangu mwaka 1601 mfalme James VI wa Uskoti alichaguliwa kuwa mfalme wa Uingereza pia. Nchi jirani zote mbili ziliendelea na wafalme wa pamoja hadi mwaka 1707. Mwaka ule Uingereza pamoja na Welisi na Uskoti ziliunganishwa kuwa Ufalme wa Muungano wa Britania. Tangu 1801 jina likawa Ufalme wa Muungano wa Britania na Eire (United Kingdom of Great Britain and Ireland) hadi 1927 wakati sehemu kubwa ya Eire ikapata uhuru wake. Tangu 1927 Uingereza ni sehemu ya Ufalme wa Muungano wa Britania na Eire ya Kaskazini(United Kingdom of Great Britain and Northern Ireland).

Mji wa Liverpool


















Ufalme wa Muungano wa Britania na Eire ya Kaskazini(United Kingdom of Great Britain and Northern Ireland).

Ufalme wa Muungano

Ufalme wa Muungano wa Britania
na Eire ya Kaskazini

United Kingdom of Great Britain
and Northern Ireland
Bendera ya Ufalme wa MuunganoNembo ya Ufalme wa Muungano
BenderaNembo
Kaulimbiu ya taifa: "Dieu et mon droit" (Kifaransa)
"Mungu na haki yangu"
Wimbo wa taifa:
MENU
0:00

"God Save the Queen"
Lokeshen ya Ufalme wa Muungano
Mji mkuuLondon
51°30′ N 0°7′ W
Mji mkubwa nchiniLondon
Lugha rasmiKiingereza
Serikali
• Waziri Mkuu wa Ufalme wa Muungano
Unitary, Katiba kifalme
Theresa May MP
'
Eneo
 - Jumla
 - Maji (%)

243,610 km² (80th)
1.34%
Idadi ya watu
 - 2013 kadirio
 - 2011 sensa
 - Msongamano wa watu

64,100,000 (22nd)
63,181,775
255.6/km² (51st)
FedhaPound Sterling (£) (GDP)
Saa za eneo
 - Kiangazi (DST)
Greenwich Mean Time (GMT) (UTC+0)
British Summer Time (BST) (UTC+1)
Intaneti TLD.uk
Kodi ya simu+44
-


Ufalme wa Muungano wa Britania na Eire ya Kaskazini (kwa KiingerezaUnited Kingdom of Great Britain and Northern Ireland); kifupi "Ufalme wa MuunganoKiing.United Kingdom) ni nchi ya visiwani ya Ulaya ya kaskazini-magharibi.
Mara nyingi huitwa kwa Kiswahili "Uingereza" tu ingawa nchi ya Uingereza ni moja tu kati ya sehemu za ufalme huo pamoja na UskotiWelisi na Eire ya Kaskazini.
Nchi iliongoza mapinduzi ya viwanda duniani, ilenea katika mabara yote kwa makoloni yake mengi ikabaki hadi leo kati ya nchi muhimu zaidi ulimwenguni.
Ni mwanachama mwanzilishi wa Umoja wa Mataifa, ambapo ana kiti cha kudumu na kura ya turufu katika Halmashauri ya Usalama, pia ni mwanachama wa Umoja wa Ulaya.

Historia

Milki kubwa kwenye kisiwa cha Britania Kuu ilikuwa Uingereza. Tangu mwaka 1284 Welisi ilitawaliwa na Uingereza na katika Sheria ya Muungano (Act of Union) ya 1536 ilikuwa sehemu ya Milki ya Uingereza. Sheria ya Muungano ya 1707 iliunganisha milki mbili za Uingereza na Uskoti kuwa Milki ya Britania Kuu. Nchi zote mbili ziliwahi kuwa chini ya mfalme mmoja tangu mwaka 1603. Tangu wakati uleule Ufalme wa Eire (Ireland) ilitawaliwa na Uingereza pia. Sheria ya 1800 iliunganisha Ufalme wa Britania Kuu na Ufalme wa Eire na hivyo kuunda Ufalme wa Maungano (United Kingdom of Great Britan and Ireland).
Baada ya Vita ya uhuru ya Eire bunge la London kwa sheria ya 1920 (Government of Ireland Act 1920) liligawa Ireland kwa sehemu mbili za Northern Eireland na Southern Ireland. Wabunge waliochaguliwa katika Ireland ya Kusini walijitangaza kuwa bunge la Eire na kwa mapatano ya 1922 uhuru wa Dola Huru la Eire ilitambuliwa. Nchi mpya ilijiita tangu 1922 1937 "Jamhuri ya Eire na kuendelea kama nchi ya pekee. Mikoa ya Northern Ireland iliendelea kuwa sehemu za Ufalme wa Maungano.
Elderly lady with a yellow hat and grey hair is smiling in outdoor setting.
Elizabeth IIMalkia wa Ufalme wa Muungano na wa nchi mbalimbali za Commonwealth.
Mwaka 1999 Uskoti, Welisi na Northern Ireland zilirudishwa bunge zao za pekee. Uskoti ilikuwa na harakati pana ya kuondoka katika Ufalme wa Maungano lakini katika kura ya watu wa Uskoti ya mwaka 2014 asilimia 55 waliamua kubaki.
Kura ya wananchi ya 2016 iliamua kuondoka katika Umoja wa Ulaya kwa asilimia 51.9.

Wakazi

Upande wa dini, kadiri ya sensa ya mwaka 2011, 59.5% za wakazi ni Wakristo (hasa wa Anglikana, halafu WakatolikiWakalvini na wengineo), 4.4% ni Waislamu, 1.3% ni Mabanyani. 25.7% hawana dini yoyote.

Muungano na utawala

BenderaNchiHaliWakaziVitengoMji mkuu
Flag of England.svg
UingerezaUfalme50,431,700 London
Flag of Scotland.svg
UskotiUfalme5,094,800 Edinburgh
Flag of Wales 2.svg
WelisiUtemi2,958,600 Cardiff
HapanaEire ya KaskaziniJimbo1,724,400 Belfast

Tazama pia

Orodha ya miji ya Ufalme wa Muungano
 Hii ni orodha ya miji ya nchi ya Ufalme wa Muungano yenye angalau idadi ya wakazi 100,000 (2001).[1]

No comments: