Monday 9 October 2017

Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia

Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia


Shirikiano za kijeshi katika Ulaya mwaka 1915. Nyekundu: Mataifa ya Kati; kijani: Mataifa ya Ushirikiano; njano: mataifa yasiyoshiriki vita

Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia:
1.Mifereji huko Verdun (Ufaransa) baada ya kulimwa kwa mizinga mikubwa;
2. Ndege za kijeshi na faru za kwanza;
3. bunduki ya mtombo na manowari

Ramani ya dunia ikionyesha nchi na maeneo yaliyoshiriki katika Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia. Kijani: Mataifa ya Ushirikiano; njano: Mataifa ya Kati ; nchi zisizoshiriki kwa rangi ya kijivu
Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia ilikuwa vita iliyopigwa kuanzia mwaka 1914 hadi 1918. Mataifa wapiganaji yalikuwa UjerumaniAustria-HungariaBulgaria na Uturuki (ziliitwa "Mataifa ya Kati", ing. central powers) kwa upande mmoja dhidi ya UfaransaUrusiUingerezaItaliaMarekani na nchi mbalimbali zilizoshirikiana nazo (zilitwa "Mataifa ya Ushirikiano", ing. allied powers).
Vita hii ilianza katika Ulaya ikapanuka haraka hadi Mashariki ya KatiAfrika na Asia ya Mashariki ikasababisha kifo cha takriban watu milioni tisa.

Sababu na matokeo

Sababu yake ilikuwa mashindano makali kati ya mataifa ya Ulaya kuhusu kushika nafasi ya kipaumbele barani Ulaya na duniani kote.
Matokeo yake yalikuwa mwisho wa kipaumbele cha Ulaya duniani na kupanda ngazi kwa Marekani, mapinduzi katika nchi mbalimbali, mwisho wa falme za Ujerumani, Austria na Urusi pamoja na mwanzo wa utawala wa kikomunisti katika Urusi, mwisho wa Dola la Austria-Hungaria na wa Dola la Uturuki la Kiosmani pamoja na mwisho wa ukoloni wa Kijerumani duniani.
Katika Ulaya nchi mpya zilijitokeza kama vile ChekoslovakiaUfiniLatviaEstonia na Yugoslavia pamoja na nchi za zamani zilizotokea tena katika uwanja wa kimataifa ndizo AustriaHungariaLithuania na Poland.

Hali kabla ya vita

Sehemu kubwa ya Ulaya iliwahi kuwa na kipindi kirefu cha amani tangu vita kati ya Ufaransa na Ujerumani mnamo 1870-1871. Mataifa ya Ulaya yalikuwa na mfumo wa mikataba na mapatano kati yao yaliyolenga kuhakikisha uwiano wa mataifa. Mataifa makubwa ya Ulaya yalikuwa Uingereza, Ufaransa, Ujerumani, Urusi na Italia pamoja na milki ya Austria-Hungaria.
Hali ilikuwa tofauti katika Kusini-Mashariki mwa bara hilo. Hadi nusu ya pili ya karne ya 19 sehemu kubwa ya Balkani ilitawaliwa na Milki ya Osmani iliyokuwa milki ya Kiislamu ya kutawala Wakristo wengi. Milki hii iliendelea kudhoofika wakati wa karne ya 19. Nchi mbalimbali zilijitenga na kupata uhuru, kama vile UgirikiSerbiaBulgaria na Romania. Nchi hizi mpya zilipigana kivita kati yao na Milki ya Osmani hadi mwaka 1912.

Mwanzo wa vita

Vita Kuu ilianza kutokana na ugomvi kati ya Austria-Hungaria na Serbia. Kutokana na muundo wa mikataba ya kusaidiana kati ya nchi za Ulaya mwanzo huo ulisababisha mfululizo wa hali ya vita kati ya mataifa, na mengine ya Balkani yalitafuta uhuru wao.
Tarehe 28 Juni 1914 katika mji wa SarayevoBosniamwana wa Kaisari wa Austria aliyekuwa mfalme mteule aliuawa pamoja na mke wake na mgaidi Mserbia mwanachama wa kundi la "Mkono Mweusi" lililopinga utawala wa Austria-Hungaria katika Bosnia. Austria iliamuru Serbia ifuate masharti makali katika uchunguzi wa tendo lile. Serbia ilipokataa sehemu ya mwisho ya masharti, Austria ilitangaza hali ya vita dhidi ya Serbia tarehe 28 Julai 1914.
Agosti ya 1914 iliona kupanuka kwa vita hii: Warusi walikuwa na mkataba wa usaidizi na Serbia wakatangaza hali ya vita dhidi ya Austria-Hungaria. Hapo wakaingia Wajerumani waliokuwa na mapatano ya usaidizi na Austria-Hungaria wakitangaza hali ya vita dhidi ya Urusi. Urusi kwa upande wake ulikuwa na mkataba wa kusaidiana na Ufaransa, kwa hivyo hali ya vita ikajitokeza pia kati ya Ufaransa na Ujerumani. Uingereza ilijiunga na vita baada ya Wajerumani kuvamia eneo la Ubelgiji kwa shabaha ya kupita eneo lake haraka kwa uvamizi wa Ufaransa Kaskazini.
Japan iliyokuwa na mkataba wa kusaidana na Uingreza tangu mwaka 1902 iliona nafasi ya kukamata koloni za Ujerumani katika Pasifiki ikaingia upande wa maadui wa Ujerumani.
Kuanzia Oktoba 1914 Milki ya Osmani (Uturuki) ilijiunga na vita kufuatana na mkataba wake wa siri na Ujerumani.
Mwaka 1915 Italia ilijiunga na Wafaransa na Waingereza kwa kushambulia Austria-Hungaria iliyotawala bado maeneo katika kaskazini ya rasi ya Italia, ingawa awali ilikuwa na mkataba na dola hilo.

Vita katika nchi mbalimbali

Vita ilipigwa kwa ukali miaka ya 1914-1918. Wajerumani waliingia ndani ya Ufaransa lakini walikwama kabla ya kufikia jiji kuu la Paris. Kwa muda mrefu mstari wa mapambano ulibaki palepale.
Katika Mashariki Wajerumani walifaulu kurudisha mashambulio ya Kirusi na kuteka sehemu za Urusi.
Katika Kusini mwa Ulaya Waustria walifaulu kwa shida kubwa kuteka Serbia na Montenegro pamoja na Albania.
Waturuki walishindwa kwa ujumla katika mashambulio yao dhidi ya Warusi katika eneo la Kaukazi na dhidi ya Waingereza katika Misri. Lakini walifaulu kuzuia Waingereza wasifike Uturuki penyewe. Waingereza walipeleka jeshi katika Irak ya kusini wakafaulu kuwarudisha Waturuki hadi kaskazini ya nchi hii.

Vita katika makoloni

Vita ilienea haraka baharini na katika makoloni ya Ujerumani yaliyovamiwa na Waingereza, Wafaransa, Afrika Kusini na Japani. Makoloni yalikuwepo Afrika na kwenye visiwa vya Pasifiki pamoja na China. Ujerumani ilikuwa na vikosi vya kijeshi katika makoloni ya Afrika na pia huko Qingdao nchini China.
Kwa ujumla makoloni yote yasiyokuwa na jeshi yalitekwa na mataifa ya ushirikiano bila mapigano.

Mwisho wa vita

Wakati 1917 mataifa ya Ulaya yalionyesha dalili za uchovu. Katika hali hiyo mabadiliko mawili makubwa yalitokea: Marekani ilijiunga na vita dhidi ya Wajerumani na Urusi iliona mapinduzi yaliyolazimisha serikali mpya kutia sahihi mapatano ya kumaliza mapigano dhidi ya Wajerumani walioteka maeneo makubwa ya Urusi.
Nguvu ya Marekani ilionekana haraka na bahati ya Ujerumani ilipungua sana. Austria-Hungaria ilidhoofishwa vilevile.
Mwaka 1918 iliona mwisho wa vita. Jeshi la Uturuki lilishindwa hadi serikali ya milki kuomba kusimamishwa kwa vita. Mataifa ya ushirikiano yalikaribia mipaka ya Ujerumani na hapo mgomo wa wanamaji ilifuatwa na migomo ya wafanyakazi katika viwanda vikubwa iliyosababisha mapinduzi yaliyoangusha serikali ya Kaisari Wilhelm II. Migomo ya wanajeshi ililazimisha Austria-Hungaria kuomba kusimamisha vita.
Milki za Austria na Uturuki zilikwisha zikagawiwa na sehemu zao zilikuwa nchi mpya au nchi zilizoundwa upya.

Mkutano wa Paris

Mwaka 1919 mataifa washindi walikutana Paris (Ufaransa) wakikubaliana masharti ya kumaliza hali ya vita dhidi ya Mataifa ya Kati. Mikataba mbalimbali iliandaliwa kati ya washindi na kuwekwa mbele ya nchi zilizoshindwa.
Mikataba hii ilikuwa:
Mkutano wa Paris ulitoa masharti makali dhidi ya Ujerumani katika Mkataba wa Versailles. Ujerumani uliondolowa makoloni yote yaliyokabidhiwa kwa niaba ya Shirikisho la Mataifakama maeneo ya kukabidhiwa kwa Uingereza, Ufaransa, Ubelgiji, Japani, Afrika Kusini na Australia.
Mkutano wa Paris ulikuwa jaribio la kuunda utaratibu mpya duniani uliotakiwa kulindwa na Shirikisho la Mataifa. Lakini ukosefu wa nguvu kwa upande wa Shirikisho la Mataifa pamoja na kuanza na kupanuka kwa mwendo mpya wa Kifashisti iliyochukua utawala katika Italia na Ujerumani vilishinda nia hiyo.
Wataalamu wasio wachache wanasema mwisho wa vita kuu ya kwanza ulipanda tayari mbegu za Vita Kuu ya Pili ya Dunia.
Ni kwamba Wajerumani na wakazi wa nchi nyingine zilizoshindwa walijiona wamekosewa haki, lakini pia Waitalia walioshinda kwa gharama kubwa ya damu walijiona wamedanganywa kwa kutotimiziwa ahadi walizopewa ili wasaliti Ujerumani na Austria-Hungaria na kuingia vitani upande wa pili. Hivyo vyama vya mrengo wa kulia viliweza kupata nguvu na hatimaye kupanga kisasi.

Vita ya kwanza ya dunia?[hariri | hariri chanzo]

Vita hii ilitwa "Vita ya Dunia" kwa sababu mapigano yalisambaa kote duniani. Sehemu kubwa ya mapigano yalitokea Ulaya na Asia ya Magharibi lakini pia katika makoloni ya Afrika, Asia na Pasifiki. Nchi za Amerika hazikuona mapigano kwenye nchi kavu lakini manowari za Ujerumani zilipigana na mataifa ya ushirikiano mbele ya pwani za Marekani na Amerika Kusini.
Ilikuwa pia vita ya kwanza iliyopigwa kote duniani ilhali habari zake ziliweza kufika katika muda wa masaa au siku chache kwa mataifa yote kutokana na upatikanaji wa vyombo vya mawasiliano hasa simu za kimataifa na redio.
Lakini kwa kweli haikuwa vita ya kwanza ya "dunia" maana vita ya miaka saba (1756-1762) ilipigwa pia kwenye mabara yote ya dunia baina ya nchi zenye makoloni hasa Uingereza, Ufaransa na Hispania.

Tazama pia

  • Kampeni za Kivita katika Afrika ya Mashariki (Vita ya Kwanza ya Dunia)

    Kampeni za Kivita katika Afrika ya Mashariki (Vita ya Kwanza ya Dunia)


    Ramani ya vita ya Afrika ya Mashariki mwaka 1915 (kutoka New York Times)
    Historia ya Tanzania
    Coat of Arms of Tanzania
    This article is part of a series

    Uendo
    Historia ya Zanzibar
    Ukoloni
    Mgawanyo wa Afrika
    Afrika ya Mashariki ya Kijerumani
    Mkataba wa Zanzibar-Helgoland
    Mkwawa
    Vita ya Maji Maji
    Vita vikuu vya kwanza Afrika Mashariki
    Tanganyika
    Uhuru
    Mapinduzi ya Zanzibar
    Julius Nyerere
    Ujamaa
    Tamko la Arusha
    Ali Hassan Mwinyi
    Benjamin Mkapa
    Jakaya Kikwete
    John Magufuli
    {Kigezo:Data99

    Tanzania Portal
    Kampeni za Afrika ya Mashariki ulikuwa mfululizo wa mapigano ya kivita yaliyotokea Afrika ya Mashariki ya Kijerumani(Tanganyika, Rwanda na Burundi ya leo) na koloni jirani za MsumbijiRhodesia ya Kaskazini (Zambia), Afrika ya Mashariki ya Kiingereza (Kenya), Uganda, na Kongo ya Kibelgiji. Kampeni hizi zilianza mwezi wa Agosti 1914 zikaisha rasmi mnamo mwezi wa Novemba katika mwaka wa 1918.[1]

    Wajerumani na mataifa ya ushirikiano

    Wapiganaji katika vita hii walikuwa Schutztruppe (jeshi la kikoloni cha Kijerumani) lililofanywa hasa na askari Waafrika waliosimamiwa na maafisa Wajerumani pamoja na walowezi Wajerumani na wanamaji wa manowari waliokaa Afrika ya Mashariki wakati wa mwanzo wa vita 1914. Dhidi yao walisimama jeshi dogo la kikoloni la Kiingereza katika Kenya na Rhodesia, halafu vikosi vya jeshi la kikoloni la Uhindi ya Kiingereza na vikosi kutoka Afrika Kusini. Kutoka magharibi walishiriki vikosi za Force Publique ya Kibelgiji kutoka Kongo. Tangu mwaka 1916 jeshi la kikoloni la Kireno liliingia upande wa Uingereza.
    Mikakati ya jeshi la kikoloni la Kijerumani lililoongozwa na Luteni Koloneli (baadaye Meja-jeneraliPaul Emil von Lettow-Vorbeck ililenga kuwalazimisha wapinzani hasa Waingereza kutumia wanajeshi wengi iwezekanavyo katika Afrika kwa shabaha ya kuwazuia wasipatikane kwenye vita ya Ulaya.
    Mkakati yake ilifaulu kiasi cha kwamba Waingereza walipaswa kuleta vikosi vikubwa kutoka Uhindi ya Kiingereza na Afrika Kusini kupigania kempeni ya Afrika ya Mashariki. [2][3]

    Awamu ya kwanza: 1914-1915

    Katika awamu la kwanza la vita vikosi vya Schutztruppe vilishambulia reli ya Uganda na vituo vya mpakani na Kenya. Waingereza walijibu kwa kukusanya walowezi wao katika Kenya bila kufaulu kuwazuia Wajerumani walioteka mji wa Taveta. Hiyvo Waingereza walichukua askari 12,000 Wahindi na 2 Novemba 1914 walishambulia Tanga. Lakini askari Waafrika wa jeshi la Kijerumani waliwashinda Tanga na baadaye pia Longidokaribu na mlima Kilimanjaro, wengine huko Yasini.

    Mapigano ya Tanga
    Hapo Waingereza waliamua kuchukua wanajeshi Wazungu kutoka Afrika Kusini chini ya amri wa jenerali Jan Smuts waliofika Kenya hadi mwisho wa 1915. Wakati huohuo Wabelgiji walipanga pamoja na Uingereza kupeleka vikosi vya jeshi lake Force Publique katika Kongo mpakani wa magharibi.

    Awamu ya pili: shambulio dhidi ya Tanganyika

    Januari 1916 jeshi hili lilishambulia. Jeshi la Kijerumani lilikuwa ndogo likafuata mikakati ya kuwachelewesha maadui na kuwashambulia walipokuwa wadhaifu au walipofanya makosa.
    • Vikosi kutoka Uhindi, Afrika Kusini na Uingereza vilivamia Tanganyika kutoka upande wa Kenya
    • Wanajeshi 5,000 Waingereza na Waafrika Kusini walivamia kusini magharibi ya Tanganyika kutoka Nyassaland na Rhodesia
    • Wabelgiji waliingia Rwanda na Burundi kutoka Kongo wakafuata njia ya reli kuelekea Tabora
    • Wareno walivamia pembetatu ya Kionga (nchi ng'ambo ya mto Rufiji) na nyanda za juu za Umakonde. Lakini walishindwa hapa wakaswa kurudi Msumbiji
    Hadi Agosti 1916 mataifa ya ushirikiano yalishika miji muhimu ya Tanganyika isipokuwa Daressalaam. Moshi iltekwa mwezi wa Machi. Reli ya Kati ya Tanganyika kuanzia Tabora, Dodoma hadi Morogoro ilikuwa mkono mwao. Walisita kuvamia Daressalaam kwa sababu waliogopa mapigano makali lakini Lettow-Vorbeck aliwahi kuondoa askari wake tayari kwa sababu hakutafuta mapigano makubwa dhidi ya maadui mwenye nguvu zaidi. Alipeleka jeshi lake katika eneo kusini ya mstari Daressalaam-Morogoro-Iringa pasipo na njia nzuri akitegemea Waingereza wasingeweza kutumia usafiri kwa malori na reli.
    Hadi hapa maendeleo ya vikosi vya maungano yalikuwa na matatizo mengi. Walitegemea hasa askari Wazungu na Wahindi waliozoea kusafiri na mizigo mikubwa ya vyakula, nguo na hema na kwa hiyo walihitaji wapagazi wengi. Hivyo maendeleo yao yalikuwa polepole wakahitaji chakula kingi kulisha askari pamoja na wapagazi. Askari pamoja na sehemu ya wapagazi walikuwa wageni ambao hawakuzoea vema hali ya hewa na magonjwa hivyo walisumbuliwa na ugonjwa. Kwa mfano kikosi cha 9th South African Infantry ilifika kwa askari Wazungu 1,135 mwezi wa Februari 1916 na hadi Oktoba ni 116 pekee waliobaki tayari kwa vita, ingawa kikosi hiki hakikuona mapigano na wote wengine walikufa au bila uwezo kutokana na magonjwa.[4]
    Kinyume chake Lettow Vorbeck aliwategemea hasa askari Waafrika waliokuwa na mahitaji madogo waliojua nchi na kuzoea magonjwa ya mazingira. Waingereza walitumia askari Waafrika hasa kwa kulinda reli ya Uganda kwa sababu mwanzoni walikosa imani katika uwezo wao.

    Awamu ya tatu: vita ya msituni

    Tangu mwaka 1917 Waingereza walipunguza idadi ya Wazungu na Wahindi badala yake waliunda vikosi vipya vya Waafrika vya King's African Rifles waliokuwa na uwezo wa kushindana na Waafrika wa Lettow Vorbeck.
    Walifaulu kusukuma jeshi la Schutztruppe kusini zaidi. Katika Oktoba 1917 waliwalazimisha Wajerumani kusimama kwenye mapigano ya Mahiwa ambako Lettow Vorbeck aliwashinda lakini alipoteza askari mamia. Pia akiba yake ya risasi ilielekea kwisha. Kikosi kikubwa cha askari 1000 chini ya kapteni Tafel walilazimishwa kusalimisha amri baada ya kuishiwa chakula na risasi kabisa. Hata kama hakushindwa Lettow Vorbeck hakuweza kuendelea vile akaamua kuondoka katika Tanganyika na kwenda Msumbiji alipotegemea Wareno kuwa adui mdhaifu.

    Awamu ya nne: Msumbiji na mwisho

    Mwisho wa Novemba 1917 Lettow aliwaacha wajeruhiwa na sehemu kubwa ya Wajerumani walioongozana naye nyuma akavuka mto Rovuma na askari 280 Wajerumani na Waafrika 1600.
    Katika Msumbiji aliweza kuteka kambi ya kijeshi ya Wareno alipokamata bunduki na risasa pamoja na chakula. Waingereza walijaribu kumfuata laini walishindwa kumkuta katika Msumbiji. Katika miezi ya 1918 iliyofuata Lettow Vorbeck alizunguka katika Msumbiji ya kaskazini, mara nyingi kwa umbali wa siku 2 au tatu na Waingereza na Wareno waliomtafuta bila kumpata. Alivamia vituo mbalimbali vya Wareno na kupata risasi na vyakula mara kwa mara.

    Jeshi la Kijerumani ilivyosalimisha amri 1918 (uchoraji wa siku zile)
    Katika Septemba 1918 alipata habari ya kwamba Waingereza walikuwa nyuma yake kwa jeshi kubwa. Hapa aliamua kurudi Tanganyika na kuelekea Rhodesia kwa sababu habari zilimfikia ya kwamba Waingerea hawakuwa tena na jeshi huko. Tarehe 28 Septemba alivuka tena mto Rovuma akaendelea katika sehemu za kusini kupitia Songea na Mbozi. Mwezi wa Novemba aliingia Rhodesia ya Kaskazini. Tarehe 13 Novemba kikosi chake kiliteka mji wa Kasama ambako Waingereza wachache walikimbia walpomwona. Siku iliyofuata afisa Mwingereza alikaribia kambi yake na kumletea habari ya kwamba vita ilikwisha tayari na Ujerumani iliwahi kusimamisha mapigano yote tangu 11 Novemba 1918. Lettow alipatana na Waingereza kuongoza askari hadi mji wa Abercorn (leo Mbala, Zambia) aliposalimisha amri tarehe 23 Novemba 1918.

    Tanbihi

    1. Jump up Holmes 2001, p. 361.
    2. Jump up Holmes 2001, p. 359.
    3. Jump up Strachan 2003, p. 642.
    4. Jump up Falls, Cyril. The Great War. New York: Capricorn Books. 1961, p. 253

    Tazama pia

  1. Schutztruppe























































  1. Afrika ya Mashariki ya Kijerumani

Afrika ya Mashariki ya Kijerumani

Afrika ya Mashariki ya Kijerumani
Bendera ya Afrika ya Mashariki ya Kijerumani
Nembo ya Afrika ya Mashariki ya Kijerumani
Mwanzo wa utawala wa kikoloni1885
Makao ya serikali ya kikoloniBagamoyo hadi 1891 halafu Daressalam
Eneo995.000 km²
Wakazi7.665.234 (1-1-1913)
Wakazi Wajerumani4100 (1913)
PesaRupie= 64 Pesa,
kuanzia 1904
1 Rupie = 100 Heller
Nchi huru za leo1961 Tanganyika, tangu 1964 Tanzania

Ramani ya Kijerumani ionyeshayo Zanzibar na pwani (mnamo 1888)
Afrika ya Mashariki ya Kijerumani (au: ya Kidachi; kwa Kijerumani Deutsch-Ostafrika -DOA-; kwa Kiingereza German East Africa) ilikuwa jina la koloni la Ujerumani huko Afrika ya Mashariki kati ya miaka 1885 na 1918/1919.
Eneo lake lilijumlisha nchi za kisasa za Tanzania bara (yaani bila Zanzibar), Burundi na Rwanda. Ilikuwa koloni kubwa kabisa la Dola la Ujerumani.

Eneo, mipaka na wakazi

Eneo na mipaka

Eneo la koloni lilikuwa na kilomita za mraba 997,000 pamoja na sehemu za maziwa makubwa kama Ziwa Tanganyika na Ziwa Viktoria. Eneo hili lilikuwa karibu mara mbili kuliko eneo la Ujerumani wenyewe kabla ya mwaka 1914.
Mipaka iliamuliwa katika mapatano na UingerezaUbelgiji na Ureno zilizotawala makoloni ya jirani ya Afrika ya Mashariki ya Kiingereza (leo Kenya na Uganda), Kongo ya Kibelgiji (leo Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo), Rhodesia (leo Zambia na Zimbabwe), Nyasaland (leo Malawi) na Msumbiji. Mipaka hii ni pia mipaka ya Tanzania, Rwanda na Burundi hadi leo hii.
Upande wa Kenya mstari ulichorwa kuanzia Bahari Hindi kwa mdomo wa mto Umba hadi Ziwa Jipe, halafu kufuata mitelemko ya kaskazini ya mlima Kilimanjaro na kutoka hapa hadi Ziwa Viktoria. Mipaka na Uganda ilifuata latitudo ya kwanza ya kusini ya ikweta hadi mpaka na Kongo. Upande wa Kongo mpaka ulifuata sehemu za chini za bonde la Ufa na katikati ya maziwa kama Kivu na Tanganyika.
Upande wa kusini ulifuata mstari kati ya ncha ya kusini ya ziwa Tanganyika hadi mdomo wa Mto Songwe katika Ziwa Nyasa. Eneo lote la ziwa lenyewe lilibaki upande wa Nyasaland ya Kiingereza, halafu mstari kutoka Ziwa Nyasa kwa kufuata mto Ruvuma hadi Rasi ya Delgado kwenye Bahari Hindi.
Jinsi ilivyo na mipaka ya kikoloni mistari hii ilikata mara nyingi maeneo ya makabila ya wenyeji.

Wakazi

Mwaka 1913 takwimu ya Wajerumani ilihesabu wakazi Waafrika 7,645,000, Waasia (Wahindi na Waarabu) 14,898 na Wazungu5,336, kati yao Wajerumani 4,107. Nusu ya wakazi wote waliishi katika eneo la maziwa makubwa ambako serikali ya kikoloni iliacha maeneo ya Rwanda (wakazi 2,000,000), Burundi (1,500,000) na Bukoba (275,000) kama maeneo lindwa chini ya watawala wa kienyeji waliosimamiwa na afisa mkazi Mjerumani.[1]

Historia ya koloni

Historia ya Tanzania
Coat of Arms of Tanzania
This article is part of a series

Uendo
Historia ya Zanzibar
Ukoloni
Mgawanyo wa Afrika
Afrika ya Mashariki ya Kijerumani
Mkataba wa Zanzibar-Helgoland
Mkwawa
Vita ya Maji Maji
Vita vikuu vya kwanza Afrika Mashariki
Tanganyika
Uhuru
Mapinduzi ya Zanzibar
Julius Nyerere
Ujamaa
Tamko la Arusha
Ali Hassan Mwinyi
Benjamin Mkapa
Jakaya Kikwete
John Magufuli
{Kigezo:Data99

Tanzania Portal
Historia ya koloni ilikuwa na awamu tatu:
  1. mwanzo kama koloni la kampuni binafsi (Kampuni ya Kijerumani kwa Afrika ya Mashariki) kuanzia 1885 hadi kuporomoka kwa utawala wake mnamo 1890
  2. koloni la Dola la Ujerumani (kwa Kijerumani Deutsches Reich) kuanzia 1891
  3. mwisho wa utawala wa Kijerumani wakati wa Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia kuanzia mwaka 1916 wakati jeshi kubwa la Uingereza na Afrika Kusini pamoja na Ubelgiji lilivamia, hadi kusalimu amri kwa jeshi la Schutztruppe kwenye Novemba 1918
Katika mapatano baada ya vita koloni liligawiwa kati ya Uingereza (iliyopata Tanganyika) na Ubelgiji (iliyopata Rwanda na Burundi). Kwa historia ya baadaye ilikuwa na maana ya kwamba walikabidhiwa maeneo ya koloni la Kijerumani la awali si kama mali kamili lakini kama maeneo ya kudhaminiwa kwa niaba ya shirikisho la Mataifa (mtangulizi wa Umoja wa Mataifa (UN).

Utangulizi

Hadi mnamo mwaka 1880 serikali ya Ujerumani chini ya chansella Otto von Bismarck ilikataa kuanzisha makoloni. Sehemu ya wafanyabiasharaWajerumani walidai koloni. Walisikitika kuona faida za wenzao Waingereza waliopata mara nyingi msaada kutoka kwa wanajeshi na serikali za koloni za Uingereza hasa Asia. Waliona pia faida ya viwanda vya Uingereza vilivyokuwa na soko la kulindwa katika nchi kama Uhindi kwa sababu serikali ya kikoloni ilidai kodi kali kwa bidhaa zisizotoka Uingereza.
Bismarck hakuamini ya kwamba koloni lingeleta faida kwa taifa kulingana na gharama kubwa kwa serikali. Lakini wapigania koloni walikuwa na wabunge muhimu kwa serikali na polepole Bismarck alianza kukubali hatua za kwanza.
Mwenyewe aliamini mwanzoni ya kwamba itatosha kuwapa wafanyabiashara ulinzi kwa shughuli zao kwa kuwaruhusu matumizi ya bendera ya Ujerumani na kuwa na askari wao wa ulinzi kama wamepatana na viongozi wazalendo katika eneo fulani kuanzisha shughuli huko. Kwa njia hii alifungua mlango kwa harakati iliyoendelea kuwa mchango wa Ujerumani katika mbio wa kugawa dunia, hasa Afrika.

Juhudi za Karl Peters


Maeneo ya kwanza yaliyotwaliwa na Karl Peters.
Koloni hili lilianzishwa na mfanyabiashara Mjerumani Karl Peters mwaka 1885 kwa niaba ya "Kampuni ya Kijerumani kwa Afrika ya Mashariki".
Peters, aliyewahi kusoma chuo Uingereza, aliona wivu juu ya ukoloni wa Uingereza, akiamini ya kwamba Ujerumani ungestahili nafasi hiyo pia. Hivyo alianza kudai koloni katika mikutano, akaanzisha "Shirika kwa Ukoloni wa Kijerumani " mwaka 1884 iliyokuwa kitangulizi cha kampuni.
Shirika hii ilimtuma pamoja na wenzake wawili kwenda Afrika na kutafuta nafasi ya kuanzisha koloni. Peters alifika Zanzibar alipoambiwa na konsuliya Ujerumani ya kwamba hawezi: serikali ya nyumbani haikubali mipango yake. Hivyo alivuka barani akapita kanda la eneo la Kizanzibari kwenye pwani na kutembelea machifu na masultani barani.
Hapa alifaulu kushawishi watawala wa UsagaraNguruUseguha na Ukami kutia sahihi kwenye mikataba ya Kijerumani ambayo hawakuielewa. Mikataba hii ilisema ya kwamba mtawala alikabidhi kwa kampuni nchi yake pamoja na haki juu ya ardhi na mali yote.
Mwaka 1885 Peters alirudi Berlin na kuonyesha mikataba yake kwa magazeti na serikali. Chansela Bismarck alikataa, akacheka mikataba kama karatasi bila maana.
Peters alitumia mbinu: akatisha kupeleka mikataba yake kwa mfalme Leopold II wa Ubelgiji aliyekuwa kununua haki zake. Hapa Bismarck aliogopa kilio cha wapenda koloni akakubali kumpa Peters barua ya ulinzi kwa maeneo yaliyokuwa ya kampuni kufuatana na mikataba.

Upanuzi wa eneo la kampuni

Upanuzi na ugomvi na Zanzibar

Peters na wawakilishi wake walirudi wakaendelea kutafuta machifu waliokuwa tayari kutia saini mikataba yake. Sultani wa Zanzibaralipinga juhudi hizi. Zanzibar ilisimamia pwani ya Afrika ya Mashariki na tangu karne watu wa miji ya pwani walikuwa na mawali wa Sultani.
Zanzibar ilidai pia utawala ya bara hadi Ziwa Tanganyika na Kongo, ingawa hali halisi athira yake haikwenda mbali na njia za misafara ambako ndovu na watumwa walipelekwa pwani.
Tarehe 27 Aprili 1885 serikali ya Zanzibar ilituma barua Berlin kupinga kazi na madai ya kampuni na kutangaza maeneo ya Tanzania ya leo kama milki yake. Iliongeza pia wanajeshi wake barani zilizokuwa chini ya amri ya mwanajeshi mstaafu Mwingereza Matthews. Hapo serikali ya Berlin ilituma kikosi cha manowari kwenda Bahari Hindi.
Mwezi Agosti manowari za Kijerumani chini ya amri ya admirali Eduard von Knorr zilifika mbele ya Unguja zikalenga mizinga yao kwa ikulu ya sultani. Akishauriwa na balozi wa Uingereza, Sultan Bargadh alipaswa kutoa tamko kuwa, "Kutokana na madai tunayopelekewa kwa matishio na Kaisari wa Ujerumani, tunatambua ulinzi wa Ujerumani juu ya nchi za Usagara, Nguru, Useguha, Ukami na juu ya wilaya ya Witu. Mipaka yake itaelezwa baadaye na sisi tunatambua ulinzi wa Kaisari juu ya mahali palipotajwa." [2].
Sultani alipaswa pia kutia sahihi mkataba wa biashara na Ujerumani alipokubali haki nyingi kwa Wajerumani katika milki yake.[3].
Mwaka 1886 Uingereza na Ujerumani walipatana juu ya ugawaji wa Afrika ya Mashariki na Sultani alipaswa kukubali tena. Katika mapatano hayo Sultani alibaki na visiwa vya UngujaPembaMafia na funguvisiwa ya Lamu pamoja na kanda la pwani barani lenye upana wa maili 10 kati ya mto Ruvuma upande wa Kusini na mto Tana upande wa Kaskazini, halafu miji ya KismayuBarawaMerka na Mogadishu upande wa kaskazini zaidi. [4].

Mkataba kati ya Zanzibar na Kampuni juu ya kofo na pwani


Sarafu ya rupia 1 iliyotolewa kwa jina la "Deutsch-Ostafrikanische Gesellschaft" (Kampuni ya Kijerumani ya Afrika ya Mashariki); tangu 1904 zilitolewa kwa jina la koloni yenyewe bila kutaja kampuni tena
Mapatano ya 1886 yaliwapa Wajerumani nafasi ya kuendeleza upanuzi barani nyuma ya kanda la pwani la Kizanzibari na mstariwa mpaka ulichorwa kuanzia mdomo wa mto Umba kupitia mlima Kilimanjaro hadi Ziwa Viktoria. Lakini kwa ajili ya matumizi ya kibiashara suala la mabandari bado lilibaki wazi. Hapo Peters na kampuni yake walianza kujadiliana na Sultani Seyyed Bargash(alitawala 1870 hadi 1888) kuhusu utawala wa pwani katika sehemu ya Tanganyika.
Mnamo mwaka 1887 Bargash alikuwa amechoka: alitafuta pesa tu kwa ajili yake binafsi; alikuwa tayari kukodisha utawala wa kanda la pwani ya Tanganyika kwa Wajerumani. Wajerumani walidai kuongezeka haki na Bargash alikufa bila kumaliza mapatano.
Lakini mwandamizi wake Sultani Seyyed Khalifa aliwapa Wajerumani walichotaka. Tarehe 15 Agosti 1888 wawakilishi wa kampuni ya Kijerumani walifika kwenye mabandari yote wakatangaza utawala wao kwa niaba ya sultani.

Vita ya Abushiri na mwisho wa utawala wa Kampuni

Badiliko hili lilisababisha upinzani na hatimaye ghasia ya wenyeji. Vipengele vya mkataba vilisema mali isiyokuwa na hati za kimaandishi haiwezi kutambuliwa. Wenye mali kama mashamba walitakiwa kununua hati kutoka kwa watawala wapya. Hapo Waswahili wa pwani walijisikia wamesalitiwa na sultani asiyekuwa na haki ya kuchukua mali zao na kuzipa kwa wageni.
Mara baada ya kufika kwa Wajerumani kwenye miji ya pwani ghasia ilianza mjini Pangani na kuenea haraka kote pwani kati ya Tanga na Lindi.
Kampuni ilikuwa na Wajerumani wachache tu walioshindwa kujitetea. Walipaswa kukimbia au wakauawa. Bagamoyo pekee palikuwa na kikosi cha askari kutoka manowari ikatetewa.
Serikali ya Ujerumani iliona lazima kuingia kati na kutuma manowari pamoja na askari waliokandamiza ghasia.
Baada ya upinzani wa wenyeji wa pwani mwaka 1889/1890 wakiongozwa na Abushiri na Bwana Heri serikali ya Ujerumani iliamua kutwaa mamlaka kutoka kwa kampuni na kufanya eneo lote kuwa koloni la Dola la Ujerumani badala ya shirika.

Koloni la Dola la Ujerumani

Utawala wa Kijerumani ulikwisha katika Vita Kuu ya Dunia ya Kwanza (1914 - 1918) kutokana na uvamizi wa Uingereza na Ubelgiji.
Katika Mkataba wa Versailles mwaka 1919 eneo la koloni la Kijerumani liligawiwa. Sehemu ya Tanganyika ilikabidhiwa kwa Uingereza na maeneo ya Rwanda na Burundi yaliwekwa chini ya Ubelgiji.

Utawala

Eneo lote la koloni liligawiwa katika mikoa 21 na maeneo matatu yaliyokuwa bado chini ya watawala wenyeji kwa mfumo wa maeneo lindwa. Hadi 1913 mikoa 19 ilikuwa chini ya utawala wa kiraia, yaani chini ya maafisa wa serikali ya kikoloni. Mikoa miwili ya Iringa na Mahenge ilikuwa bado chini ya utawala wa kijeshi yaani hapo walikuwa maafisa wa Schutztruppe waliotekeleza majukumu yote ya serikali.
Mikoa chini ya usamimizi wa maafisa Wajerumani wa kiraia ilikuwa:
1. Tanga (DOA)
2. Pangani pamoja na ofisi ndogo Handeni
3. Bagamoyo pamoja na ofisi ndogo Saadani
4. Daressalam pamoja na ofisi ndogo ya polisi Kisangire
5. Rufiji, makao makuu Utete
6. Kilwa (DOA) pamoja na ofisi ndogo za Kilindoni, Kibata na Liwale
7. Lindi pamoja na ofisi ndogo za MikindaniNewala und Tunduru
8. Langenburg (Tukuyu) pamoja na ofisi ndogo Itaka na Mwakete na kituo cha polisi Muaja
9. Wilhelmstal (Lushoto)
10. Morogoro pamoja na ofisi ndogo za Kilossa na Kissaki
11. Songea pamoja na ofisi ndogo Wiedhafen
12. Moshi
13. Arusha pamoja na ofisi ndogo Umbulu
14. Kondoa-Irangi pamoja na ofisi ndogo Mkalama
15. Dodoma pamoja na kituo cha polisi Mpapwa na kituo cha kijeshi Singida
16. Mwanza pamoja na ofisi ndogo Shirati na kituo cha kijeshi Ikoma
17. Tabora pamoja na ofisi ndogo za Shinyanga na Ushirombo
18. Ujiji pamoja na kituo cha kijeshi Kasulo
19. Bismarckburg (Kasanga (Ufipa)
Mikoa ya kijeshi (jer. Militärbezirke) chini ya usimamizi wa maafisa wa Kijerumani wa kijeshi:
21. Iringa pamoja na kituo cha kijeshi Ubena
22. Mahenge
Maeneo lindwa (jer. Residentur) chini ya watawala wenyeji waliopaswa kufuata ushauri wa afisa mkazi Mjerumani (jer. Resident):
Bukoba pamoja na vituo vya kijeshi Usuwi na Kifumbiro, kwa ajili ya watawala wa Wahaya
Rwanda, mji mkuu Kigali, kituo cha kijeshi Mruhengeri
Burundi, mji mkuu Gitega, pamoja na ofisi ndogo Usumbura (Bujumbura).

No comments: