Tuesday 17 October 2017

lugha ya Kiingereza

Kiingereza


EN (ISO 639-1)
Kiingereza ni lugha ya jamii ya Kigermanik cha Magharibi iliyokua nchini Uingereza kwa muda wa miaka 1,400.
Leo, zaidi ya wasemaji milioni mia nne duniani wanazumgumza Kiingereza kama lugha ya kwanza. Watu wengi zaidi wanazumgumza Kiingereza kama lugha ya pili, kwa sababu ni muhimu sana kwenye nyanja za mawasilianosayansi na uchumi wa kimataifa.

Historia ya Kiingereza


Buluu nyeusi: Nchi ambako Kiingereza ni lugha ya kwanza ya wananchi wengi;
buluu nyeupe: nchi ambako Kiingereza ni lugha rasmi lakini si lugha ya kwanza ya watu wengi.

Mwanzo wa lugha[hariri | hariri chanzo]

Lugha ya Kiingereza ilianzia huko Uingereza kutokana na kuingiliana kwa lugha mbalimbali, hasa lugha za kale za UjerumaniDenmark na Ufaransa.
Sehemu ya kusini ya kisiwa cha Britania ilikuwa ndani ya Dola la Roma hadi mwanzo wa karne ya 5Wenyeji walitumia lugha ya Kikelti pamoja na Kilatini cha Waroma, hasa mjini.

Uvamizi wa Waanglia-Saksoni: kuja kwa Kigermanik

Baada ya Waroma makabila kutoka Ujerumani wa kaskazini na Denmark walianza kuvamia kisiwa hicho. Katika mwendo wa karne mbili waliteka sehemu kubwa ya Britania isipokuwa sehemu za magharibi kama vile Cornwall na Wales na sehemu za kaskazini walipoishi Waskoti.
Wavamizi walileta lugha zao za Kisaksoni na Kianglia (Ujerumani wa Kaskazini) zilizounganika kuwa lugha ya Kiingereza cha Kale. Inaonekana ya kwamba wenyeji walio wengi walianza kutumia lugha ya watawala wapya, wengine waliuawa au walihamia sehemu zisizo chini ya Waanglia-Saksoni.
Lugha hii iliathiriwa mara mbili. Kwanza Wadenmark ndio waliojaribu kujenga ufalme wao kisiwani. Waliteka sehemu za Uingereza ya Magharibi. Kiasi cha maneno kutoka lugha yao kimeingia Kiingereza cha kale kama Wales.

Uvamizi wa Wanormandy: kuja kwa Kifaransa, lugha mbili kando

Mwaka 1066 jeshi la Wanormani kutoka Ufaransa wa Kaskazini walivamia na kuteka Uingereza. Wanormani walikuwa wa asili ya Skandinavia lakini walikuwa wameshaanza kutumia lugha ya Kifaransa cha kale. Wanajeshi hao walikuwa mabwana wapya wa Uingereza wakitumia Kifaransa chao cha Normandy.
Kwa karne kadhaa lugha mbili zilitumika kandokando: Kiingereza cha Kianglia-Saksoni cha watu wa kawaida na kile Kifaransa cha Kinormandy cha tabaka la watawala. Kwa jumla watawala walianza kutumia lugha ya raia lakini lugha hii ilibadilika pia kwa kupokea maneno mengi kutoka Kifaransa. Kuna makadirio ya kwamba zaidi ya theluthi moja ya maneno yote ya Kiingereza yana asili ya Kifaransa.

Kuingiliana kwa lugha zote mbili: Kiingereza cha Kati

Kipindi hiki cha kuingiliana kati ya Kifaransa cha mabwana na lugha ya kawaida kilileta Kiingereza cha Kati. Hadi leo asili ya maneno kutoka Kijerumani na Kifaransa ni wazi kabisa.
Mfano mzuri ni maneno tofauti ya wanyama kadhaa na nyama yao: ng'ombe huitwa "cow" (sawa na Kijerumani wa Kaskazini "Kau") lakini nyama yake ni "beef" (kutokana na neno la Kifaransa kwa ng'ombe "boeuf"); vilevile "sheep" kwa mnyama kondoo na "mutton" kwa nyama yake (Kijerumani ya Kaskazini: "Schaap" - Kifaransa: "mutton"), vilevile swine – pork (nguruwe) na calf – veal (ndama).
Wakulima wafugaji walitumia lugha yao kwa mnyama - mabwana wasiogusa mnyama lakini hula nyama yake waliendelea kutumia neno la Kifaransa kwa ajili ya mnyama yuleyule. Maneno yote mawili yaliingia katika Kiingereza cha Kisasa lakini kwa mambo mawili tofauti.

Kiingereza cha Kisasa

Kiingereza cha Kisasa kimeanza na tafsiri ya Biblia ya William Tyndale; baadaye na washairi wakuu kama William Shakespeare.
Teknolojia ya uchapaji vitabu ilisambaza lugha hii nchini kote na kupunguza athira ya lahaja mbalimbali.
Wakati ule Kiingereza kilipokea pia maneno mengi kutoka lugha za Kilatini na Kigiriki zilizokuwa lugha za taaluma na sayansi hadi karne ya 18 kote Ulaya.
Kiingereza cha Kisasa kimeendelea kurahisisha lugha. Lakini urekebisho wa tahajia umeshindikana hadi leo hata kama kulikuwa na majaribio mbalimbali. Kutokana na historia yake Kiingereza kimebaki na tahajia isiyolingana na matamshi ya maneno.
Mwandishi George Bernhard Shaw alionyesha tatizo hilo kwa pendekezo la dhihaka kwamba neno "fish" (samaki) liandikwe "ghoti": gh kama sauti ya "f" katika "cough", o kama sauti ya "i" katika "women", na ti kama sauti ya "sh" katika "nation".
Pamoja na hayo, lahaja za Kiingereza zinazidi kutofautiana, zile muhimu zaidi zikiwa zile za Britania na Marekani.

Uenezi wa Kiingereza duniani

Pamoja na Dola la Uingereza, lugha iliyo ilienea duniani kati ya karne ya 17 na 19.
Tangu karne ya 19 idadi kubwa ya wasemaji wa Kiingereza hawaishi tena Uingerezea bali Marekani. Katika karne ileile Kiingereza kilikuwa lugha ya utawala katika maeneo makubwa ya makoloni ya Dola la Uingereza.
Baada ya makoloni kuwa nchi huru mara nyingi Kiingereza kimeendelea kuwa lugha rasmi za nchi hizo.
Kutokana na matukio hayo yote, na Marekani kujitokeza katikati ya karne ya 20 kama nchi tawala kisiasa, kiuchumi na kiteknolojia, Kiingereza kimekuwa leo lugha ya kwanza ya mawasiliano duniani hata kama si lugha yenye wasemaji wengi wa lugha ya kwanza.
Pia aina nyingi za Krioli na Pijini zimetokana na Kiingereza na kudumu hadi leo.
Kiingereza ni lugha rasmi pekee katika nchi za Uingereza, MarekaniAustraliaNyuzilandiJamaica, na nchi nyingine.
Kiingereza ni lugha rasmi pamoja na lugha nyingine katika nchi nyingi, kwa mfano Kanada (pamoja na Kifaransa), India (pamoja na Kihindi na lugha za majimbo), Ireland (pamoja na Kigaelik), Philippines (pamoja na Kitagalog).
Kwa jumla ni lugha rasmi katika nchi karibu 60, mbali ya Umoja wa Mataifa na Umoja wa Ulaya.

Kiingereza barani Afrika

Nchi nyingi za Afrika zinatumia Kiingereza kama lugha rasmi, lakini ni Waafrika wachache (isipokuwa Waafrika Kusini) wanaoitaja kuwa lugha ya kwanza kwao. Nchi hizo ni Afrika KusiniGhanaLesothoLiberiaKamerunKenyaNamibiaNigeriaSierra LeoneSwazilandZambia na Zimbabwe.
Kiingereza kinazumgumzwa pia katika nchi nyingine za Afrika ambapo si lugha rasmi. Lugha nyingi za Afrika zimekopa maneno ya Kiingereza. Maneno hayo yamerekebishwa kulingana na sauti ya lugha nyingine, kwa mfano: Kiingerezatrain --> Kiswahilitreni.

Lugha

Lugha (kutoka neno la Kiarabu: لغة) ni utaratibu wa kuwasiliana kati ya binadamu (wengine wanadai hata kati ya viumbe wenye akili).
Somo la lugha linaitwa maarifa ya lugha au isimu.
Mwaka wa 2008 ulikuwa Mwaka wa Lugha wa Kimataifa.

Maana ya neno "lugha"

Lugha ni mfumo wa sauti za nasibu zenye maana na zilizokubaliwa na jamii ya watu fulani ili zitumike katika kuleta mawasiliano.
Lugha ni mfumo wa sauti za nasibu kwa sababu zilitokea kama bahati tu kwa binadamu. Wanyama hawatumii lugha kama chombo cha mawasiliano, kwa kuwa lugha ni sauti zenye maana na kukubaliwa na jamii.
Hakuna lugha bora zaidi duniani, kwa kuwa lugha zote zina ubora, mradi zikidhi matakwa ya jamii husika.

Umuhimu wa lugha

  • Lugha ni kitambulisho cha jamii
  • Lugha hutolea elimu
  • Lugha huleta mawasiliano katika jamii
  • Lugha hukuza utamaduni
  • lugha huburudisha

Tabia za lugha

Lugha huwa na tabia zifuatazo:
  • Lugha huzaliwa: ni kutokana na lugha nyingine moja au zaidi zilizotangulia kuwepo.
  • Lugha hukua: lugha hukua (kuongezeka kwa maneno, kuongezeka kwa idadi ya wazungumzaji, kuwa na mawanda mapana, kusanifiwa) kadiri inavyoendelea kutumiwa na jamii.
  • Lugha hutohoa: lugha ina tabia ya kuchukua au kukopa maneno kutoka lugha nyingine.
  • Lugha hufundishika: mtu yeyote anaweza kujifunza walau kiasi lugha yoyote hata kwa njia ya ufundishaji.
  • Lugha huathiriana: lugha yoyote inaweza kuathiriwa na lugha nyingine.
  • Lugha lazima ijitosheleze: kila lugha inajitosheleza kulingana na mahitaji ya jamii inayotumia lugha yenyewe.
  • Lugha zina ubora: lugha zote ni bora hakuna lugha bora kuliko nyingine zote.
  • Lugha hurithiwa: jamii hurithi lugha kutoka kizazi hadi kizazi.
  • Lugha hufa: inapozidi mno kubadilika mwisho si yenyewe tena, lakini pia inapoachwa isitumike tena kwa kuwa wahusika wanapendelea lugha nyingine.

Sifa za lugha

  • Lugha lazima iwe inahusu binadamu
  • Sauti-sauti hufanywa na mwanadamu
  • Lugha hufuata misingi ya fonimu, yaani, a, b, ch, d, f, h, z n.k.
  • Lugha huwa na mpangilio maalumu wenye kubeba maana. Mpangilio huo huanza na fonimu ---> Silabi ---> Neno
  • Lugha hujitambulisha ili kuzalisha maneno mengi.

Dhima za lugha

  1. Lugha hutumika kama chombo cha mawasiliano kwa kupashiana habari.
  2. Lugha hutumika kujenga umojamshikamano na ushirikiano miongoni mwa wanajamii.
  3. Lugha hutumika kutunza, kukuza, na kuendeleza utamaduni wa jamii.
  4. Lugha hutumika katika kutetea maarifa mbalimbali (ni nyenzo ya kufundishia).
  5. Lugha hutumika kama alama ya utambulisho wa kabila/jamii au taifa fulani.
  6. lugha hutumika kutoa burudani.

Aina za lugha kwa kigezo cha uwasilishaji

Kimsingi lugha ni moja. Uwasilishwaji wake ndio huigawa katika tanzu/aina kuu mbili:
  1. Lugha ya mazungumzo
  2. Lugha ya maandishi

Lugha ya mazungumzo

Hii ni lugha ambayo huwasilishwa na watu kwa njia ya mazungumzo ya mdomo - na hurithishwa kutoka kizazi kimoja hadi kingine kwa njia ya mazungumzo. Lugha ya mazungumzo ni kongwe, hai na halisi zaidi ya mzungumzaji na ina maana nyingi, kwani mzungumzaji na msikilizaji huwa ana kwa ana katika mazingira mamoja.
Stadi za lugha ya mazungumzo ni kuzungumza na kusikiliza.
Na.ChanzoKikomo
1KuzungumzaKusikiliza
2MzungumzajiMsikilizaji

Lugha ya maandishi

Hii ni lugha ambayo huwasilishwa kwa njia ya maandishi. Hii ni kiwakilishi cha lugha ya mazungumzo katika mfumo wa maandishi. Lugha ya maandishi ni changa kwani imeanza milenia za hivi karibuni baada ya kuvumbuliwa kwa maandishi.
Stadi za lugha ya maandishi ni kuandika na kusoma:
Na.ChanzoKikomo
1Kuandika/MaandishiKusoma
2MwandishiMsomaji
Kwa kawaida, lugha ni sehemu ya utamaduni wa umma fulani. Lugha ya aina hii inaitwa lugha asilia. Lakini pia kuna lugha za kuundwa.

Nyanja za lugha

Lugha ina nyanja kuu mbili, nazo ni:
  • Sarufi - hushughulikia kanuni za lugha
  • Fasihi - hushughulikia sanaa zitokanazo na lugha husika ili kuumba kazi mbalimbali za kifasihi.

Kukua na kufa kwa lugha

Tangu siku za kwanza za binadamu, lugha zimekuwa zikichipuka, kukua, kutangaa na kufa kama kiumbe yeyote mwingine. Kwa hivyo, lugha zilizopo leo ulimwenguni, huenda baada ya karne nyingi kupita zikatoweka na kuzuka nyinginezo.
Leo ulimwenguni mathalan, kuna lugha karibu 6,700, zikiwa 1,000 katika bara la kaskazini na la kusini la Amerika, 2,000 zikiwa kwenye bara la Afrika, 230 katika bara la Ulaya, 2,200 katika bara la Asia, na 1,300 katika bara la Oshania (Australia na nchi jirani nayo).

Kigermanik

Lugha za Kigermanik ni kikundi cha lugha zenye asili ya Ulaya ya Kaskazini.
Lugha za Kigermanik zenye wasemaji wengi ni Kiingereza (milioni 380) na Kijerumani (milioni 120). Lugha nyingine za Kigermanik ni lugha za Skandinavia, halafu Kiholanzi na Kiafrikaans wa Afrika Kusini.

Historia

Mwanzo wa lugha hizi uko gizani. Wataalamu wamejaribu kutambua sifa za lugha asilia kwa kulinganisha lugha mbalimbalimbali zilizo karibukaribu ikiwa habari zao zimejulikana.
Kutokana na makisio hayo Kigermanik kilianza Ulaya ya Kaskazini, labda Sweden ya Kusini katika miaka elfu ya kwanza K.K..
Wasemaji wa Kigermanik walianza kuhamahama wakati wa Dola la Roma na ndipo habari za kwanza za kihistoria zimepatikana.
Matembezi ya Wagermanik yalifika hadi Urusi wa Kusini na Afrika ya Kaskazini.

Lugha za Kigermanik katika Ulaya; buluu: Kigermanik cha kaskazini; njano: Kigermanik cha magharibi tawi la Kifrisia-Kiingereza; kibichi: Kigermanik cha magaharibi tawi la Kusini
Lugha za Kigermanik hugawanywa katika aina tatu:
a) Kigermanik ya KaskaziniKiswidiKidenmarkKinorweiKiiceland na Kifaroe
b) Kigermanik ya MagharibiKiingerezaKijerumani (Kidachi), KiholanziKiafrikaansKijerumani ya KaskaziniKifrisiaKiyiddish (Kiyahudi cha Ulaya)
c) Kigermanik ya Mashariki: lugha hizi kama Kivandali au Kigoti zimekufa zote zinajulikana kama lugha za kihistoria tu

No comments: