Monday 23 October 2017

Vita Kuu ya Pili ya Dunia na uhuru

Jamii:Koloni za Uingereza

Makala katika jamii "Koloni za Uingereza"

G
  • Gold Coast

    Gold Coast


    Koloni ya Gold Coast mnamo 1896

    Vita kati ya Waingereza na Waashanti
    Gold Coast (sw.: Pwani la Dhahabu) ilikuwa jina la koloni ya Uingereza katika Afrika ya Magharibi kwenye mwambao wa Ghuba ya Guinea ambayo imekuwa nchi ya Ghana tangu uhuru wake.

    Vyanzo kwenye pwani

    Vyanzo vya koloni vilikuwa vituo vya wafanyabiashara kutoka Ulaya waliofika sehemu hii ya pwani tangu karne ya 15 kwa biashara ya dhahabu, watumwa, visu, vioo, pombe kali na silaha kama bunduki. Kituo cha kwanza kilikuwa boma la Elmina la Wareno.
    Kuanzia mwaka 1800 milki ya Ashanti ilianza kupanuka hadi pwani. Hapa kulitokea vita kati ya Ashanti na milki za pwani. Ashati ilidai kodi kutoka kwa hao wageni na 1817 shirika la wafanyabiashara Waingereza lilikubali malipo. Wakati ule Waingereza walianza kuchukua hatua za kukandamiza biashara ya watumwa wakiwa na makao makuu katika Sierra Leone na manowari za Kiingereza zilipita kwenye pwani. Mwaka 1821 vituo vya Kiingereza kwenye Pwani la Dhahabu viliwekwa chini ya gavana ya Sierra Leone. Wafanyabiashara na waloezi Waingereza waliomba pwani hili liwe koloni kabisa. Hapo walikuwa na matumaini ya ulinzi dhidi ya Ashanti wakidokeza ya kwamba Ashanti iliendelea katika biashara ya watumwa iliyowahi kupigwa marufuku na nchi za Ulaya katika Mkutano wa Vienna wa 1815. Lakini serikali ya London ilikataa kuanzisha koloni kamili kwa sababu waliona gharama za koloni zisingelingana na mapato. Vituo vya pwani viliwekwa chini ya usimamizi wa gavana wa Sierar Leone. Waingereza walipigania vita kuhusu vituo vyao na usalama wa falme za pwani dhidi ya Ashanti kati ya 1823-1831 wakifaulu hatimaye kupanusha eneo lao hadi 120 km kutoka pwani.

    Maeneo lindwa na koloni tangu 1873

    Wakati wa vita na baadaye Waingereza waliimarisha ushirikiano wao na falme za pwani. Tangu mkataba wa 1844 hali ya pwani ilikuwa kama mkusanyiko wa maeneo ya kulindwa chini ya Uingereza. Baada ya vita ya 1872/73 dhidi ya Ashanti Uingereza ilifuta mapatano ya 1844 na kutangaza maeneo yote kati ya pwani na Asante kuwa koloni kamili. Gavana Mwingereza alichukua boma la Christiansborg (Accra) kuwa makao makuu yake.
    1895/96 ilitokea tena vita kati ya Waingereza na Ashanti. Waingereza waliona upanuzi wa koloni za Ufaransa na Ujerumani katika Afrika ya Magharibi wakadai Ashanti ikubali kuwa nchi lindwa ya Uingereza. Asantehene alipokataa Waingereza walishambulia wakachoma Kumasi. Ashanti ililazimishwa kusalimia amri na kuwa eneo lindwa.
    Mnamo 1902 maeneo upande wa kaskazini ya Ashanti yaliongezwa kufuatana na mapatano na Ujerumani na Ufaransa. Kwa hiyo sehemu tatu za Gold Coast yenyewe, Ashanti na maeneo ya kaskazini yalikuwa koloni ya pamoja chini ya gavana wa Accra.

    Gold Coast


    Stempu ya posta 1953
    Tangu 1919 gavana aliwajibika pia kwa sehemu ya Togo ya Kiingereza (maeneo ya Togo ya Kijerumani ya awali zilizokabidhiwa kwa Uingereza) iliyotawaliwa kama "Togo ng'ambo ya mto Volta". Wakati wa mwisho wa ukoloni wakazi wengi wa sehemu hii walipiga kura ya kujiunga na Gold Coast na sasa ni sehemu kamili ya Ghana.
    Utawala ulikuwa mkononi wa gavana. Lakini mapema sana gavana aliunda halmashauri mbili kuwa kamati za kushauriana. Mwanzoni aliita wazungu pekee kuwa wanachama wa halashauri lakini kuanzia mwaka 1900 Waafrika kadhaa waliungwa pia. Katika sehemu kubwa ya eneo Waingereza walitegemea mfumo wa utawala usio wa moja kwa moja yaani kupitia machifu wazalendo. Idadi ya waafrika wenye elimu ya kisasa ilikua na tangu 1920 walianza kudai halmashauri ya kuchaguliwa si ya kuteuliwa na gavana.

    Kuelekea kwa uhuru


    Shule ya Ufundi katika maeneo ya kaskazini kabla ya uhuru 1957
    Mwaka 1946 gavana mpya aliunda katiba ya koloni iliwapa wajumbe wachaguliwa kura nyingi katika halmashauri kuu (legislative council). Harakati za kudai haki zaidi kwa wazalendo iliendelea kupata nguvu. Chama cha United Gold Coast Convention (UGCC) kilidai haki ya kujitawala tangu 1947. Miaka miwili baadaye kwenye Juni 1949 chama kipya cha Convention People's Party (CPP) kiliudwa na Kwame Nkrumah. Madai yake yalikuwa makali zaidi kwa kudai serikali ya kuchaguliwa mara moja. Nkrumah alitumia mikutano ya hadhara, maandamano na migomo kwa kutangaza madai yake. Katika uchaguzi wa 1951 chama cha CPP kilishinda. Nrumah alikuwa waziri mkuu wa koloni.
    Ndani ya koloni wawakilishi kutoka kaskazini na Ashanti walitaka kuwa mfumo wa shirikisho wakiogopa Nkrumah alilenga kukusanya mamlaka yote mkononi mwake. Hata hivyo, serikali ya Uingereza ilisimama upande wa CPP na hivyo koloni iliingia katika uhuru tarehe 6 Machi 1957 kwa jina la Ghana.

K

  • Koloni ya Rasi

    Koloni ya Rasi

    Cape Colony - Kaapkolonie
    Koloni ya Rasi
    Bendera ya Koloni ya Rasi
    Lugha rasmiKiingereza na Kiholanzi 1
    Mji mkuuCape Town
    Eneo569,020 km² (1910)
    Koloni ya Rasi katika Muungano wa Afrika Kusini
    1 Hadi 1806 Kiholanzi ilikuwea lugha rasmi pekee; kati ya 1806 na 1882 Kiingereza. Tangu 1882 lugha zote mbili zilikuwa lugha rasmi.
    Koloni ya Rasi ilikuwa koloni ya Uholanzi hadi 1806 na baadaye ya Uingereza katika Afrika Kusini ya leo. Jina limetokana na Rasi ya Tumaini Jema iliyoko karibu na mji wa Cape Town.

    Koloni ya Uholanzi

    Historia ya koloni ilianza 1652 wakati Mholanzi Jan van Riebeeck aliunda Cape Town kwa niaba ya Kampuni ya Kiholanzi kwa India ya Mashariki. Kampuni ilihitaji kituo kwa ajili ya jahazi zake zilizosafiri kati ya Ulaya na visiwa vya Indonesia. Eneo la rasi lilifaa kuwa mahali pa kupumzika na kuongeza vyakula njiani tena kwa sababu hali ya hewa iliwafaa watu wa Ulaya.
    Waholanzi walipeleka wakulima kwenda rasi waliotakiwa kulima vyakula kwa ajili ya mahitaji ya jahazi.

    Koloni ya Uingereza

    Wakati wa vita za Napoleoni eneo la Uholanzi lilitawaliwa na Ufaransa na Uingereza ilivamia koloni za Uholanzi pamoja na rasi. Waingereza waliogopa ya kwamba Wafaransa wangehatarisha mawasiliano na koloni yao huko Uhindini kama wangetwaa Afrika Kusini. Baada ya miake kadhaa Waingereza walinyang'anya eneo hili rasmi mwaka 1806. Hali hii ilitambuliwa na Uholanzi 1815kwenye Mkutano wa Vienna.
    Koloni ya Rasi iliendelea chini ya Uingereza hadi 1910. Mwaka ule Muungano wa Afrika Kusini yaliundwa na rasi iliingia kama "Jimbo la Rasi".

M

S

Somalia ya Kiingereza

Somalia ya Kiingereza


Mahali pa Somalia ya Kiingereza
Somalia ya Kiingereza' au British Somaliland ilikuwa eneo lindwa la Uingereza katika Somalia ya Kaskazini. Eneo lake lilikuwa tangu 1961sehemu ya Jamhuri ya Somalia na tangu 1991 limekuwa Jamhuri ya Somaliland yaani nchi isiyotambuliwa na umma wa kimataifa lakini yenye tabia zote za nchi huru.

Koloni mwaka 1884/1885

Uingereza uliingia katika eneo hili baada ya Misri kuondoka mwaka 1885 baada ya kushindwa na jeshi la Mahdi huko Sudan. Uingereza uliingia kwa sababu iliona umuhimu wa kutawala pande zote mbili za Bab el Mandeb ikihofia uenezaji wa nchi nyingine za Ulaya hasa Ufaransa iliyokuwa na koloni ya kwanza ya Ubuk (Obok) katika Djibouti ya leo tangu 1862. Pamoja na hayo Waingereza walitegemea kununua nyama kwa ajili ya mji wa Aden na meli zilizopita hapo kati ya Uhindi na Ulaya.
Somaliland ilitawaliwa awali kama mkoa wa Uhindi wa Kiingereza ikawa baadaye chini ya wizara ya koloni huko London.

Upinzani wa Mohammed Abdullah Hassan

Hata kama Uingereza haukuwa na nia ya kuingilia mno katika maisha ya wenyeji ulikutana na upinzani mkali kuanzia mwaka 1899. Kiongozi wa kidini Mohammed Abdullah Hassan aliyeitwa na Waingereza "Mullah majununi". Waingereza walijibu kwa ukali katika vita ya miaka 20 iliyoua takriban theluthi moja wa wakazi wote wa eneo.
Mwishowe Uingereza iliweza kumaliza upinzani kwa teknolojia mpya ya eropleni za kijeshi zilizotumia mabomu na bunduki za mtombo kutoka angani mara ya kwanza katika Afrika.

Vita Kuu ya Pili ya Dunia na uhuru

Wakati wa Vita Kuu ya Pili ya Dunia eneo likatwaliwa na Italia katika Agosti 1940 lakini kuchukuliwa tena na Uingereza katika Machi 1941.
Uhuru ulifika 26 Juni 1960. Tar. 1 Julai kulitokea muungano na Somalia ya Kiitalia iliyopokea uhuru wake pia.

Nchi ya pekee

Baada ya kuporomoka kwa serikali ya Somalia eneo la Somalia ya Kiingereza la awali likatangaza uhuru wake Mei 1991 kama Jamhuri ya Somaliland.

  • matokeo ya utafutaji wa matokeo
  • Historia ya Austria (Kusanyiko Mbegu za historia)
  • sehemu kubwa za Ulaya ya Mashariki. Watawala wa Austria walishika pia vyeo vya kifalme vya nchi za Bohemia na Hungaria. Wakati wa vita za Napoleoni Kaisari
    2 KB (maneno 264) - 13:09, 12 Oktoba 2016
  • 1866. Nchi hizi ziliwahi kuwa sehemu za Dola Takatifu la Kiroma hadi 1806 iliyokwisha kutokana na vita za Napoleoni. Nchi na maeneo ya kujitawala 38 zilijiunga
    2 KB (maneno 223) - 14:28, 22 Aprili 2015
  • Austria (Kusanyiko Mbegu za jiografia ya Ulaya)
    sehemu kubwa za Ulaya ya Mashariki. Watawala wa Austria walishika pia vyeo vya kifalme vya nchi za Bohemia na Hungaria. Wakati wa vita za Napoleoni Kaisari
    9 KB (maneno 577) - 14:10, 15 Aprili 2016
  • Georgetown (Kusanyiko Mbegu za jiografia ya Amerika Kusini)
    "Stabroek". Wakati wa vita za Napoleoni Uholanzi ilivamiwa na Ufaransa na Uingereza kama adui wa Napoleon ilikamata koloni za Uholanzi. Hivyi mji ulikuwa
    2 KB (maneno 155) - 09:46, 19 Mei 2016
  • Stuttgart (Kusanyiko Mbegu za jiografia ya Ujerumani)
    wa Württemberg walioendelea kujipatia cheo cha kifalme wakati wa vita zaNapoleoni. Hivyo Stuttgart ikawa mji mkuu wa Ufalme wa Württemberg kuanzia 1805
    2 KB (maneno 171) - 08:38, 9 Machi 2013
  • Habsburg (Kusanyiko Mbegu za jiografia ya Ulaya)
    na koloni zake katika Amerika ya Kati na Amerika Kusini. Wakati wa vita zaNapoleoni Kaisari Franz II wa Ujerumani alilazimishwa kuacha taji la kaisari
    2 KB (maneno 283) - 21:31, 22 Aprili 2015
  • mpya katika Ulaya baada ya vita za Napoleoni. Katika miaka iliyotangulia mtawala huyu wa Ufaransa aliwahi kuvuruga nchi zote za Ulaya bara; alifuta madola
    4 KB (maneno 575) - 17:51, 8 Machi 2013
  • Koloni ya Rasi (Kusanyiko Koloni za Uingereza)
    mahitaji ya jahazi. Wakati wa vita za Napoleoni eneo la Uholanzi lilitawaliwa na Ufaransa na Uingereza ilivamia koloni za Uholanzi pamoja na rasi. Waingereza
    2 KB (maneno 187) - 18:39, 20 Septemba 2017
  • Kiroma baada ya Austria. Baada ya vita za Napoleoni mwanzo wa karne ya 19 umuhimu wa Prussia uliendelea kukua. Katika ya vita ya wenyewe kwa wenyewe katika
    4 KB (maneno 508) - 14:26, 22 Aprili 2015
  • Madrid (Kusanyiko Mbegu za jiografia ya Hispania)
    fedha za koloni zake huko Amerika ya Kusini na utajiri huu uliwezesha wafalme kupamba mji kwa majengo mengi makubwa na mazuri. Wakati wa Napoleoni Madrid
    2 KB (maneno 236) - 21:16, 22 Aprili 2015
  • Denmark (Kusanyiko Mbegu za jiografia ya Ulaya)
    76.9% za wakazi. Denmark ilikuwa kati ya nchi muhimu sana ya Ulutheri, lakini leo 3% tu wanashiriki ibada ya Jumapili. Baada ya vita za Napoleoni Denmark
    9 KB (maneno 782) - 13:04, 17 Oktoba 2016
  • Luxemburg (Kusanyiko Mbegu za jiografia ya Ulaya)
    watemi wa Luxemburg walichaguliwa kuwa wafalme wa Ujerumani. Baada ya vita zaNapoleoni, Ufaransa na Prussia zilivutana juu ya Luxemburg. Walipatana kwenye
    6 KB (maneno 341) - 13:15, 10 Novemba 2014
  • Napoleon Bonaparte (elekezo toka kwa Napoleoni)
    gani kurudisha utaratibu wa kale katika Ulaya uliowahi kuharibiwa na Napoleoni. Wakati huohuo Napoleon aliamua kurudi Ufaransa. Tar. 1 Machi 1815 alifika
    19 KB (maneno 1,957) - 11:08, 25 Mei 2015
  • Machi 1793. Wakati wa vita vya Napoleoni, Waingereza walivamia kisiwa mwaka 1810 lakini wakakirudisha kwa Wafaransa baada ya vita (1815). Walowezi
    5 KB (maneno 607) - 13:41, 22 Aprili 2015
  • 1814 alipokuwa na miaka 17 aliamrisha kikosi cha wanajeshi katika vita dhidi ya Napoleoni. Mwaka 1829 alimwoa Augusta binti wa mtemi wa Sachsen-Weimar-Eisenach
    3 KB (maneno 356) - 16:44, 11 Machi 2013
  • Ufaransa (Kusanyiko Mbegu za jiografia ya Ulaya)
    serikali kwa vita vingi dhidi ya Uingereza na ujenzi wa majumba makubwa. Matatizo makali ya kiuchumi pamoja na mawazo mapya ya Zama za Mwangaza yalisababisha
    13 KB (maneno 1,348) - 12:55, 14 Mei 2017
  • Mjerumani. Katika vita ya maneno ya kidiplomasia chansella aliweza kumwaibisha mtawala wa Ufaransa. Napoleoni III alitangaza hali ya vita dhidi ya Prussia
    7 KB (maneno 815) - 13:32, 7 Desemba 2016
  • Mfereji wa Kiingereza (Kusanyiko Mbegu za jiografia ya Ulaya)
    mwaka 1066. Mipango yote ya baadaye ilishindikana: Wahispania mwaka 1588, Napoleoni mwanzo wa karne ya 19 na Hitler wakati wa vita kuu ya pili ya dunia.
    2 KB (maneno 185) - 11:16, 11 Machi 2013
  • kuhifadhi uhuru wao kati ya madola makubwa Austria na Prussia. Wakati wa vita zaNapoleoni Saksonia ilipambana dhidi ya Mfaransa pamoja na Prussia lakini baada
    10 KB (maneno 672) - 14:22, 11 Machi 2013
  • Surinam (Kusanyiko Mbegu za jiografia ya Amerika Kusini)
    Uholanzi ilivamiwa na Ufaransa na kutawaliwa kama sehemu ya himaya ya Napoleoni. Wakati ule Uingereza ilitwaa makoloni ya Uholanzi na kuyatawala. Baada
    11 KB (maneno 1,041) - 12:14, 8 Aprili 2017
  • Dikteta


    Benito Mussolini (kushoto) na Adolf Hitler(kullia) walikuwa madikteta wa Italia na Ujerumani katika karne ya 20.

    Idi Amin wa Uganda pamoja na askofu Luwum aliyemwua baadaye
    Dikteta (kutoka Lat. dictator yaani mwenye kutoa amri kama imla) ni neno la kumtaja mtawala asiyebanwa na sheria na kutumia nguvu ya dola kuendeleza utawala wake na kutokubali upinzani dhidi yake. Pale ambako mtu au kundi la watu hutawala kwa mbinu huu hali ya kisiasa huitwa udiktetaMfalme anayeweza kuwa na madaraka yaleyale haitwi dikteta.

    Asili ya cheo

    Kiasili "dikteta" ilikuwa cheo cha muda kwa ajili ya afisa wa jamhuri ya Roma ya kale. Kwa kawaida Waroma wa Kale waligawa madaraka makuu kati ya maafisa watendaji wawili walioitwa konsuli.
    Lakini katika hali ya hatari kuu kama vita au ghasia kubwa senati ya Roma -yaani bunge- iliweza kuamua kuwa na dikteta kwa muda. Uteuzi wa dikteta ulikuwa mkononi mwa makonsuli au kama konsuli mmoja alikuwa mbali na Roma pia mkononi mwakonsuli aliyekuwepo.
    Muda wa ofisi ya dikteta ilikuwa hadi miezi 6 lakini mara nyingi dikteta alirudisha madaraka yake kwa senati mara baada ya kumaliza shughuli kama kushinda vita au kugandamiza ghasia.
    Dikteta alikuwa mtendaji mkuu wa serikali na amiri mkuu wa jeshi. Alishika pia madaraka ya kihakimu. Aliweza kuwaondoa maafisa wote wengine madarakani, aliweza kutoa hukumu ya mauti na kuagiza kifo cha mtu yeyote. Baada ya kumaliza kipindi chake hakuweza kuwajibika au kushtakiwa kwa maazimio na matendo yake. Kwa kawaida madiketa wa Roma walishirikiana na senati lakini hawakupaswa kufanya hivyo.

    Dikteta wa kisasa

    Leo hii "dikteta" si cheo rasmi tena lakini namna ya kumtaja mtawala mkali anayeshika mamlaka yote mkononi mwake na kutawala kwa mabavu. Mara nyingi dikteta hakubali uchaguzi wa kisiasa au anahakikisha uchaguzi si huru. Haheshimu haki za kibinadamu kama zinamsumbua. Anatoa amri kama sheria; kama anaruhusu kuwepo kwa bunge na mawaziri ni sharti wafuate maagizo yake. Hakubali upinzani dhidi yake na matamko ya mawazo yasiyopendezwa naye.
    Katika karne ya 20 madikteta mara nyingi walitumia mfumo wa chama kimoja cha kisiasa, usimamizi wa magazeti, redio na televisheni.
    Kuna madikteta waliofika madarakani kwa njia ya uchaguzi lakini baadaye waliondoa upinzani na kuzuia uchaguzi huru. Mfano wake alikuwa Adolf Hitler wa Ujerumani; chama chake cha NSDAP kilipata kura nyingi kidogo katika uchaguzi wa Januari 1933 akaanzisha serikali kwa msaada wa chama kidogo akatumia mamlaka yake juu ya polisi kwa kuwakamata wapinzani wengi na kutisha mahakama pamoja na wabunge wa upinzani kwa hiyo alipewa madaraka ya kidikteta na bunge; baada ya kuwa na madaraka haya alipiga vyama vingine marufuku akatawala peke yake.
    Kuna madikteta waliofika madarakani kwa njia ya mapinduzi ya kijeshi; mifano yake ni Francisco Franco wa Hispania au Idi Amin wa Uganda. Wote walikuwa maafisa wa jeshi walitumia mamlaka yao juu ya wanajeshi kupindua serikali halali kwa njia ya mabavu na kujifanyia wenyewe watawala. Mara nyingi hao madikteta wa kijeshi huanza kwa vyeo kama mwenyekiti wa kamati ya kijeshi au mwakilishi mkuu wa wanajeshi lakini baada ya muda mfupi hakuna tena anayeweza kuwapinga.
    Kuna madikteta wengine wanaopanda ngazi ndani ya udikteta wa kikundi au chama ambako awali kamati ilitawala kwa pamoja. Mfano ni Josef Stalin wa Urusi (Umoja wa Kisovyeti) alikuwa mwanzoni Katibu Mkuu wa chama cha kikomunisti tu na wala mkuu wa dola wala mkuu wa serikali. Alitumia nafasi yake kuondoa kwanza upinzani dhidi yake ndani ya chama na baada ya mabadiliko katika vyeo vya dola pia kuimarisha usimamizi wake wa maazimio wa vyama kuhusu maafisa wa dola. Mwishowe alishtaki wapinzani wake kuwa wasaliti na kushawishi mahakama ya kuwahukumu. Tangu miaka 1935-36 hakuwa tena na mpinzani na matakwa yake yalikuwa kama sheria.

    Togo ya Kijerumani


    Ramani ya Togo ya Kijerumani
    Togo ya Kijerumani ilikuwa koloni ya Ujerumani kati ya 1884 na Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia.

    Yaliyomo

    Chanzo cha koloni

    Wafanyabiashara Wajerumani kutoka Hamburg na Bremen waliwahi kuwa na ofisi zao hasa huko Aneho kuanzia miaka ya 1870 BK. 1882 kampuni ya Woermann ilianzisha usafiri kwa meli kati ya Hamburg na Afrika na kufanya Togo kituo kimoja.
    Wakati ule pwani la Togo ya leo ilikuwa bado eneo huru kati ya Pwani la Dhahabu (Ghana) chini ya Uingereza na eneo la Porto Novo (Benin) chini ya Ufaransa. Lakini Waingereza walisikitika ya kuwa biashara ya watu wa Aneho na Lome ilipanuka na nchi za Ulaya bila kuwaletea mapato ya ushuru kwa sababu bidhaa zilifika nje ya eneo lao.
    1884 Mwingereza aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Kitta (Gold Coast - Ghana) alijaribu kutuma wanajeshi Aneho lakini alishindwa. Baada ya tukio hili chifu Mlapa alikuwa tayari kufanya mapatano ya ulinzi na konsuli wa Ujerumani Gustav Nachtigal. Mkataba wa ulinzi ulitiwa sahihi tarehe 6 Julai 1884. Hii ilikuwa mwanzo wa ukoloni wa Ujerumani katika Togo. Katika Septemba mtawala wa Porto Seguro alifanya mkataba wa ulinzi wa pili na mfanyabiashara Mjerumani Randad.
    Katika mapatano ya 1885 na 1887 Ufaransa ulikubali utawala wa Kijerumani na mpaka kati ya Togo na Dahomey (Benin). Mkataba wa Helgoland-Zanzibar iliondoa wasiwasi juu ya mipaka na eneo la Kiingereza upande wa magharibi. Mwaka 1914 koloni ilikuwa na eneo la 87,200 km².

    Mjerumani safarini Togo.PNG

    Utawala

    Koloni iliongozwa na maafisa waliokuwa mwanzoni na cheo cha kamishna wa Kaisari, halafu nkuu wa nchi, halafu gavana.
    • 1884/1885 Freiherr von Soden, Kamishna Mkuu wa Kaisari kwa Togoland
    • 1885-1889 Ernst Falkenthal, kamishna, yeye alianzisha kikosi cha polisi ya Togo Novemba 1885.
    • 1889-1895 Jesko von Puttkamer, kamishna, tangu 1893 Mkuu wa Nchi (Landeshauptmann)
    • 1895-1902 August Köhler, Mkuu wa nchi, tangu 1898 gavana
    • 1902-1903 Waldemar Horn , gavana
    • 1904-1910 Graf Zech, gavana
    • 1910-1912 Edmund Brückner, gavana
    • 1912-1914 Herzog Adolf Friedrich zu Mecklenburg, gavana aliyekabidhi koloni mkonono mwa Waingereza na Wafaransa
    Upanuzi wa Wajerumani ulianza kwa njia ya mikataba na machifu mbalimbali. Lakini kadiri utawala wao jinsi ilivyoingia zaidi ndani walikuta pia upinzani hasa kwa Wakabya na Wakonkomba hadi mwaka 1898. Kwa ujumla Wajerumani waliweza kupanuka bila jeshi kamili lakini kwa kutumia kikosi chao cha askari 700 wa polisi.

    Uchumi

    Wajerumani waliona ya kwamba wenyeji walikuwa na michikichi na kakao. Wajerumani walijenga bandari ya Lome na kuanzisha mashamba makubwa hasa ya michikichi na viwanda vya mawese. Wakajenga reli. Sehemu kubwa ya kazi hizi zilitekelezwa na wenyeji kwa njia ya kazi za kulazimishwa.
    Togo ilikuwa kielelezo cha koloni za Ujerumani hasa kwa sababu iliendelea vizuri kiuchumi. Kinyume cha koloni zote nyingine Togo haikupokea misaada kutoka Berlin lakini iliweza kugharamia utawala wake kutokana na mapato yake yenyewe.

    Togo iligawiwa 1918; magharibi liliwekwa chini ya Ghana (=Goald Coast), mashariki ikawa chini ya Ufaransa

    Elimu

    Elimu ya shule ilibaki zaidi mkononi mwa misioni ya kikatoliki na kiprotestant. Mnamo mwaka 1910 nchi ilikuwa na shule 196 za kikatoliki na shule 163 za kiprotestant. Wakatoliki walikuwa pia na shule ya ufundi. Kwa ujumla Wamisionari Wajerumani walipendelea lugha za kienyeji kama lugha za mafundisho. Wamisionari wa Shirika la Misioni ya Bremen waliendesha shule zote kwa Kiewe. Serikali ya kikoloni ilikuwa na shule 4 pekee zilizofundisha kwa Kijerumani.

    Vita Kuu na mwisho wa koloni ya Kijerumani

    Mwanzoni wa Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia Waingereza na Wafaransa waliingia Togo kutoka pande zote. Wajerumani walikabidhi Lome kwa Waingereza tar. 8 Agosti 1914 wakarudi nyuma hadi Atakpame. Hapa walijisalimisha tarehe 27 Agosti 1914.
    Nchi iligawiwa kati ya Wafaransa na Waingereza chini ya mamlaka ya Shirikisho la MataifaTogo ya Kiingereza ilitawaliwa pamoja na Pwani la Dhahabu(Ghana) ikabaki kwa Ghana hata baada ya uhuru.

    Otto von Bismarck


    Otto von Bismarck
    Otto von Bismarck (1 Aprili 1815 – 30 Julai 1898) alikuwa mwanasiasa mashuhuri wa Ujerumani katika karne ya 19.
    Akiwa waziri mkuu wa Prussia alijenga umoja wa Ujerumani katika vita tatu dhidi ya Denmark (1864), Austria (1866) na Ufaransa (1870/71).
    Kama Chansella wa Dola la Ujerumani aliongoza siasa ya nchi hadi 1890 alipoachishwa na Kaisari kijana Wilhelm II.

    Yaliyomo


    Maisha yake ya awali


    Bismarck mwaka 1836
    Jina lake kamili lilikuwa Otto Eduard Leopold von Bismarck-Schönhausen. Alizaliwa katika familia ya kitemi wa cheo cha chini katika ufalme wa Prussiamama yake alikuwa wa asili ya kiraia.
    Alisoma sheria na kilimo kwenye chuo kikuu baada ya kumaliza elimu ya sekondari, halafu akajiunga na jeshi kwa utumishi wake wa lazima.
    Baada ya kifo cha baba mwaka 1845 akachukua utawala wa mashamba ya familia yake.
    Mwaka 1847 akafunga ndoa na Marie von Thadden akazaa naye watoto watatu: Marie (1847–1926), Herbert (1849–1904) na Wilhelm (1852–1901).

    Mwanasiasa, mbunge na balozi wa Prussia


    Bismarck-Monument, Hamburg
    Wakati wa mapinduzi ya kwanza ya kidemokrasia katika Ujerumani (1848/49) alijiunga na siasa akawa mtetezi wa haki za mfalme na mpinzani wa wanademokrasia. Akachaguliwa katika Bunge la Prussia.
    Mwaka 1851 mfalme wa Prussia alimteua kuwa mwakilishi wa Prussia katika halmashauri ya Shirikisho la Kijerumani huko Frankfurt - wakati ule Ujerumani ilikuwa shirikisholisilo na nguvu ya madola 38 yaliyojitegemea. Madola makubwa katika shirikisho hili yalikuwa Austria na Prussia. Bismarck alikuwa pia na vipindi vifupi vya utumishi kama balozi wa Prussia huko St. Petersburg na Paris.

    Waziri mkuu wa Prussia

    Mwaka 1862 aliteuliwa na mfalme Friedrich Wilhelm IV kuwa waziri mkuu wa Prussia. Shabaha yake kuu ilikuwa kuongeza uwezo wa nchi. Aliimarisha jeshi la Prussia dhidi ya upinzani wa wabunge wengi. Jeshi hilo lilipewa nafasi ya kuonyesha uwezo wake katika vita dhidi ya Denmark ya mwaka 1864. Matokeo ya vita yaliongeza mashindano kati ya Prussia na Austria juu ya kipaumbele ndani ya Shirikisho la Kijerumani.
    Matokeo yake yalikuwa vita ya mwaka 1866. Prussia, pamoja na madola kadhaa madogo, ilishinda Austria na jeshi la Shirikisho la Kijerumani. Shirikisho lilivunjika, Prussia ilimeza madola kama Hannover na Hesse yaliyokuwa yameshikamana na Austria ikawa dola kabisa ndani ya Ujerumani. Austria ilijiondoa katika siasa ya Kijerumani na idadi kubwa ya madola ya Kijerumani ilijiunga na Prussia katika shirikisho la Ujerumani ya Kaskazini.
    Bismarck alilenga sasa kukamilisha kipaumbele cha Prussia katika Ujerumani. Alitumia nafasi ya magongano na Ufaransa juu ya uchaguzi wa mfalme mpya wa HispaniaKaisari Napoleon III wa Ufaransa alitaka Mfaransa achaguliwe lakini Bismarck alimsukuma mgombea Mjerumani. Katika vita ya maneno ya kidiplomasia chansella aliweza kumwaibisha mtawala wa Ufaransa. Napoleoni III alitangaza hali ya vita dhidi ya Prussia lakini madola ya Ujerumani ya Kusini, kama falme za Bavaria na Wuerttemberg, yalijiunga na Prussia.

    Bismarck (sare nyeupe) akimtangaza mfalme wa Prussia kuwa Kaisari wa Ujerumani Wilhelms I tarehe 18 Januari 1871 katika jumba la kifalme la Versailles, Ufaransa.
    Vita hii ilikuwa mara ya kwanza ya kwamba Wajerumani wote -isipokuwa Austria- walishikamana pamoja tangu muda mrefu sana. Bismarck alitumia nafasi ya ushindi wa jeshi la Wajerumani kuwakusanya viongozi wa madola yote ya Ujerumani katika jumba la Kifalme la Ufaransa huko Versailles. Mfalme wa Prussia Friedrich Wilhelm IV alitangazwa kuwa Kaisari Wilhelm I wa Ujerumani - cheo hiki hakikutumika katika Ujerumani tangu mwaka 1806. Dola la Ujerumani liliunganisha madola yote ya Ujerumani ya kale, isipokuwa Austria, chini ya mfalme wa Prussia aliyekuwa sasa pia na cheo cha Kaisari wa Ujerumani.
    Bismarck alikuwa mkuu wa serikali kama Chansella wa Ujerumani.

    Bismarck akivaa sare ya kijeshi

    Bismarck na ukoloni

    Bismarck alikuwa kiongozi wa Ujerumani wakati nchi za Ulaya ziliendelea kujipatia pande kubwa za dunia kama koloni. Mwanzoni alipinga makoloni kwa Ujerumani. Aliona gharama kubwa za kupata, kujenga na kutetea koloni akaona ya kwamba faida yoyote ya kuwa nazo hailingani na gharama hizo.
    Tangu miaka ya 1870 iliongezeka idadi ya watu katika Ujerumani waliodai koloni kwa sababu mbalimbali. Wengine walidai koloni kama ishara ya nchi kubwa na muhimu, wengine walikuwa wafanyabiashara waliotafuta ulinzi wa manowari za Kijerumani kwa ajili ya biasharayao dhidi ya wenzao wa mataifa mengine. Bismarck aliona ya kwamba hali ya Ujerumani haitegemei kuwepo kwa bendera yake katika pembe za dunia, bali uhusiano na majirani makubwa katika Ulaya hasa Uingereza, Ufaransa na Urusi. Tamko maarufu alipotembelewa na mgeni aliyetaka kumhamasisha kuunda koloni katika Afrika likawa "Ramani yako ya Afrika ni ya kuvutia sana. Lakini ramani yangu ya Afrika iko Ulaya. Ufaransa iko upande wa kushoto, Urusi upande wa kulia, katikati tuko sisi".[1]
    Alipenda kuwahamisha Wafaransa kujipatia koloni kwa matumaini ya kwamba watatumia nguvu zao Afrika na kusahau fikra za kulipiza kisasi baada ya kushindwa na Ujerumani katika vita ya 1870/71.
    Tangu mwaka 1880 Bismarck alitegemea bungeni vyama vya kisiasa vilivyotaka kuunda makoloni, hivyo alilegea na polepole kukubali kuanzishwa kwa makoloni kadhaa. Mwanzoni alitoa tu nyaraka za ulinzi kwa makampuni yaliyopatana kukodi maeneo na watawala wa Afrika na wa Pasifiki.
    Baada ya makampuni hayo kushindwa kuendesha maeneo hayo alikubali pia kuingilia moja kwa moja, kwa mfano baada ya Kampuni ya Kijerumani kwa Afrika ya Masharikikushindwa katika vita ya Abushiri mwaka 1889. Kwa hiyo Ujerumani ikajiunga na mataifa mengine ya Ulaya katika ugawaji wa Afrika kwa sababu za siasa ya ndani.

No comments: