Tuesday 24 October 2017

Katika Sayansi

Sayansi

Sayansi ni maarifa yanayopatikana kwa kufanya vitendo, kutazama na kujaribu kweli ambazo zimebainishwa hazijathibitishwa.
Mara nyingi Galileo Galilei anahesabiwa kuwa baba wa sayansi ya kisasa.
Aina za sayansi

Galileo Galilei, baba wa sayansi ya kisasa.[1]: Vol. 24, No. 1, p.Sayansi ni maarifa yanayopatikana kwa kufanya vitendo, kutazama na kujaribu kweli ambazo zimebainishwa hazijathibitishwa.Aina za sayansi

Mtu aliyerushwa hadi angani. Kufikia katikati ya karne ya 20 binadamu ameweza kukua kisayansi na hivyo kuvumbua teknolojia zilizomwezesha kuruka na kuelea anga za juu kabisa za Dunia kwa mara ya kwanza na kuchunguza Anga la nje.
Kuna sayansi mbalimbali ambazo huainishwa katika makundi yafuatayo:
Sayansi Asili k.m.
Sayansi Umbile k.m.
Kemia
  • Akiolojia

    Akiolojia


    Wanaakiolojia wakichimba kwenye misingi ya maghofu ya monasteri huko Sweden.

    Barabara hii ya Pompei (Italia) ilifunikwa mwaka 79 na majivu ya volkeno kwa muda wa miaka 1800 hadi kufunuliwa tena na wanaakiolojia kuanzia mwaka 1863.
    Akiolojia (kutoka Kiyunani αρχαίος = zamani na λόγος = neno, usemi) ni somo linalohusu mabaki ya tamaduni za watu wa nyakati zilizopita. Wanaakiolojia wanatafuta vitu vilivyobaki, kwa mfano kwa kuchimba ardhi na kutafuta mabaki ya majengomakaburisilaha, vifaa, vyombo na mifupa ya watu.

    Akiolojia na historia

    Tofauti na somo la Historia, akiolojia haichunguzi sana maandishi hasa ili kupata ufafanuzi wa mambo ya kale. Historia inatazama zaidi habari zilizoandikwa lakini akiolojia inatazama vitu vilivyobaki kutoka zamani. Wanaakiolojia wanaweza kutumia maandishi na habari za historia wakiamua jinsi gani waendelee na utafiti wao, kwa mfano wachimbe wapi. Lakini hutumia mitindo ya sayansi mbalimbali kuchunguza vitu vinavyopatikana kwa njia ya akiolojia.
    Kinyume chake, matokeo ya akiolojia ni chanzo muhimu kwa wachunguzi wa historia. Mara nyingi matokeo ya akiolojia yanaweza kupinga au kuthibitisha habari zilizoandikwa au kufungua macho kwa kuzielewa tofauti.
Elimu
Elimu

Darasa la chekechea nchini Afghanistan.

Darasa la shule ya msingi katika Meksiko.

Darasa la chuoni katika New York City.
Elimu kwa maana pana ni tendo au uzoefu wenye athari ya kujenga akilitabia ama uwezo wa kimaumbile wa mtu binafsi. Katika dhana ya kiufundi, elimu ni njia ambayo hutumiwa makusudi na jamii kupitisha maarifaujuzi na maadili kutoka kwa kizazi kimoja hadi kingine.
Walimu katika taasisi za elimu huratibisha elimu ya wanafunzi wao kupitia masomo kama vile ya kuandika, kusoma, kuhesabu (hisabati), sayansi na historiaMbinu hii wakati mwingine huitwa masomo haswa tunaporejelea somo la aina fulani, kwa kawaida mbinu hii hutumiwa na maprofesa katika taasisi za masomo ya juu.
Kuna elimu maalumu kwa wale wanaohitaji ujuzi wa kitaaluma, kama vile wanaohitaji kuwa marubani. Juu ya hayo, kuna nafasi nyingi za elimu katika viwango vingine visivyo rasmi kama vile majumba ya ukumbushomaktaba pamoja na mtandao na tajribaza maisha.
Haki ya kusoma imeweza kuelezwa kuwa haki ya msingi ya binadamu katika kifungu cha pili cha itifaki ya kwanza ya maagano ya haki za binadamu barani Ulaya kuanzia mwaka wa 1952 ambapo wanachama wote wanashurutishwa kuhakikisha elimu kwa wote. Katika kiwango cha kimataifa, Mapatano ya Umoja wa Mataifa ya haki za kiuchumi, za kijamii na za kiutamaduni katika mwaka wa 1966 yanahakikisha haki hii katika kifungu cha 13.
Saikolojia

Elimunafsi

Elimunafsia (pia: saikolojia kutoka Kigiriki ψυχολογία psikhologia) ni fani ya elimu jamii inayolenga kujua nafsi ya binadamu ili kurahisisha ukomavu wake na uhusiano wake na wenzake.

Kujifahamu

Hakuna mtu wa jana, leo au kesho aliye sawasawa na mwingine: kila mmoja ni wa pekee. Mungu ametufanya tofauti ili tutimilizane. Kila mmoja anahitaji wengine, na kila mmoja ni muhimu kwa wenzake. Katika maisha ya jamii kuna sehemu ambayo yeye tu anaweza kuijaza. Wazo hilo linaweza kumsaidia kijana ambaye ni mwepesi kukata tamaa na kujitupa. Daima uhai ni zawadi nzuri kwa mhusika na kwa wenzake wote. Kijana ni zawadi yenye nguvu na wema hata kwa taifa, kiasi kwamba kujali ustawi wa kijana ni kujenga taifa.
Tunataka kujifahamu tulivyoumbwa (mwilinafsi na roho, ambavyo vyote vinafungamana ndani mwetu):
  • 1. ili tuweze kujithamini hasa kwa kuona sisi ni nani mbele ya Mungu;
  • 2. ili tufahamu mipaka yetu na kuikabili inavyofaa;
  • 3. ili tufahamu vipawa tulivyojaliwa tuwashirikishe wenzetu;
  • 4. ili tubadilike kuwa bora zaidi na kuchangia ustawi wa jamii;
  • 5. ili tuhusiane vizuri zaidi na wenzetu;
  • 6. ili tuweze kujieleza kwa watu fulanifulani na kupata mashauri ya kutufaa






Siasa

Siasa

Siasa ni njia ya kufanya maamuzi katika taifamji au hata dunia nzima (siasa ya kimatatifa).
Sehemu muhimu ya siasa ni majadiliano kati ya watu mbalimbali wenye nguvu au mamlaka.
Katika demokrasia kila mtu ana kiasi fulani cha nguvu, kwa hiyo siasa ya demokrasia ina maana ya watu wote kuchangia maamuzi.
Hapa chini, mifumo mingine ya kisiasa huelezwa kifupi:
Sayansi Tumizi k.m.
  • Teknolojia

    Teknolojia


    Katika nusu ya pili ya karne ya 20wanadamu walifaulu kutumia teknolojia mbalimbali kuwafikisha watu kwenye anga la nje.
    Teknolojia ni elimu inayohusu uhandisiufundiujenzi, vifaa na mbinu za uzalishaji wa vifaa na huduma katika jamii.
    Asili ya neno ni Kigiriki "τέχνη" (tamka: tékhne): „uwezo, usanii, ufundi".
    Teknolojia inaweza kumaanisha:
    • vifaa na mashine zinazotumika katika matengenezo au uzalishaji wa vitu
    • elimu ya matumizi yake pamoja na mbinu na maarifa jinsi ya kutumia sayansi
    • uwezo wa kubadili malighafi asilia na kuwa bidhaa yenye thamani inayoweza kukidhi mahitaji ya binadamu. Hapa bidhaa haimaanishi tu vitu kama magodoromagari ya kutembelea, unga wa ngano n.k., la hasha: ni huduma yoyote inayotolewa kwa jamii, mfano huduma ya usafiri, huduma ya utalii, huduma ya chakula, na pamoja na vitu vyote vinavyozalishwa viwandani.
  • Uhandisi

Uhandisi

Uhandisi ni elimu ya sayansi kutatua matatizo ya kiutendaji.
Mhandisi ni mtu anayetumia elimu hiyo, kwa mfano katika fani ya ujenzi

Pia, kuna sayansi zinazohusu mada mbalimbali:
  • Maarifa
  • Unajimu

    Unajimu


    Mvindaji Orion: watu waliwaza ya kwamba nyota kadhaa zinazoonekana kwa pamoja angani ni picha ya mungu fulani au nguvu muhimu katika ulimwengu, hata kama nyota hizi hali halisi hazina uhusiano kati yao.
    Unajimu (wakati mwingine pia: astrolojia) ni mafundisho juu ya uhusiano kati ya nyota na maisha hapa duniani. Wafuasi wa unajimu hufundisha ya kwamba nyota zinaathiri maisha ya watu na matukio duniani kama amani, vita au maafa.
    Kuna aina nyingi za unajimu:
    • wengine wanataka kugundua mwendo wa dunia na utabiri wa mambo yajayo kutokana na nyota
    • wengine wanaamini ya kwamba tabia za mwanadamu zinatokana na hali ya nyota wakati wa kuzaliwa kwake
    • wengine wanaona nyota kama alama za miungu au nguvu za mbinguni.

    Tofauti ya unajimu na astronomia

    Unajimu na astronomia zilianza pamoja kama kazi ileile zikaendelea hivyo kwa karne nyingi. Tangu mwanzo wa sayansi ya kisasa takriban miaka 500 iliyopita wataalamu walitambua tabia za nyota kuwa magimba ya angani yenye sifa za kifizikia sio pepo, roho au miungu zinazoweza kutawala dunia au wanadamu. Kwa hiyo njia za unajimu (astrolojia) na astronomia zimeachana tangu karne kadhaa. Lakini miaka 400 iliyopita wanasayansi muhimu kama Tycho BraheJohannes KeplerGiordano Bruno au Galileo Galilei walitengeneza horoskopi, ingawa waliweka misingi ya astonomia ya kisasa.

    Uchoraji wa Meksiko ya Kale unaonyesha zodiaki ya kundinyota za unajimu wa Waazteki

    Asili ya unajimu

    Tangu mwanzo wa historia wanadamu katika sehemu mbalimbali za dunia walitazama nyota.
    Nyota zinaonekana wakati wa usiku kwa kufuatana na mwendo wa dunia yetu kuzunguka jua. Kwa namna hiyo kuonekana kwa nyota kunalingana na majira ya mwaka. Kwa hiyo katika dunia kabla ya kupatikana kwa kalenda watazamaji wa nyota waliweza kutabiri mabadiliko ya hali ya hewa, kuja kwa majira ya mvua, baridi, joto na kadhalika. Kati ya nyota zilizotazamiwa hivyo ni kwa mfano Kilimia na Zuhura.
    Kwa mfano kuonekana kwa nyota fulani (hii inategemea mahali duniani) inaweza kuwa alama ya kwamba mvua ni karibu, au majira ya baridi inaanza. Sababu yake ni ya kwamba nyota huonekana kwa vipindi fulani wa mwaka tu; wakati wa miezi mingine zingeonekana wakati wa mchana ambako nuru ya jua inaficha nyota zote hazionekani tena. Masaa za usiku kuna vipindi ambako nyota fulani zinaonekana vizuri angani juu kabisa na kwa njia hiyo zinaweza kutambuliwa kama ishara za majira.
    Leo hii watalaamu wengi huamini ya kwamba hapo ndipo msingi muhimu wa imani ya kwamba nyota zinaathiri maisha duniani.
    Watu wa kale walikuwa hodari sana kutazama nyota na kutambua mabadiliko yao katika mwendo wa wakati. Hali hii haieleweki kirahisi na watu wa leo waliozoea nuru ya taa za umeme wakitumia wakati wa usiku kutazama TV au kompyuta. Lakini kwa watu wa kale -jinsi ilivyo hadi leo kwa watu wengi vijijini au porini- nyota na mwezi zilikuwa taa hasa wakati wa usiku.
    Uhusiano ulioonekana kati ya mabadiliko ya nyota na mabadiliko ya majira yalianzisha elimu ya kalenda pamoja na elimu ya unajimu na astronomia.
    Kwa wazee hawa ilionekana kama nyota fulani inatawala majira, hali ya hewa na hivyo maisha ya kibinadamu kwa sababu maisha ya jamii yalitegemea majira na mwendo wa mvua, ukame, baridi au joto. Hapo ni asili ya kuziangalia nyota kama miungu au pepo zenye uwezo fulani. Hasa tabia ya hali ya hewa ya kuchelewa au kuwahi kidogo ilijenga imani ya kwamba kuchelewa kwa mvua ni dalili ya hasira ya mungu yule anayeonekana katika nyota fulani.

    Alama kwa kundinyota 12 za Zodiaki katika mapokeo ya Ulaya; zinadaiwa kuwa muhimu na kutawala tabia za watu kwenye horoskopi.

    Horoskopi

    Kati ya mbinu za unajimu zinazojulikana sana duniani ni horoskopi. Tangu zamani watu walitazama nyota zilizoonekana pamoja kama kundinyota kama nukta angani na kuwaza kuwa na mistari kati yao hivyo kuona picha ya watu, wanyama au miungu. Ni hasa kundinyota 12 za aina hii zilizorudia kila mwaka kukaa juu kwenye anga wakati wa mwezi fulani. Kundinyota hizi zilichukuliwa kama "watawala" wa kipindi ambako zilionekana juu angani wakati wa usiku na kwa pamoja zinafanya "zodiaki" yaani ufuatano wa kundinyota zilizoaminiwa kuwa muhimu. Unajimu unafundisha ya kwamba kila kundinyota kuw na tabia fulani na mtu aliyezaliwa "chini" ya nyota hizi kuwa tabia zilezile na kuwa. Hizi kundivyota za zodiaki ziliunganishwa na athira iliyoaminiwa kutokea kwa sayari ambazo zilipewa pia tabia zao. Hayo yote ni mfumo usioeleweka kirahisi na kuwa msingi wa horoskopi.
    Hadi leo chini ya vichwa kama "Nyota zinasema" magazeti mengi huchapisha namna za utabiri wa kila wiki kwa watu kufuatana na tarehe zao za kuzaliwa.
    • Astrology Zodiac
    • William Shao: Kuna uhusiano wowote kati ya unajimu na sayansi? (2007)
  • Tiba

    Tiba

    Tiba (au: Uganga) ni elimu kuhusu magonjwa ya watu mwilini na rohoni, jinsi ya kuzuia magonjwa na kuhusu njia ya kurudisha uzima. Elimu hii inafuata mbinu za kisayansi, tofauti na uganga wa kienyeji au wa kimila.
    Watu wanaoshughulikia magonjwa ya watu huitwa matabibu au waganga. Mara nyingi watu huwaita "daktari", lakini neno hili lamaanisha zaidi cheo cha kufaulu chuo kikuu kwenye ngazi ya juu; mara nyingi waganga husoma hadi cheo cha daktari wa tiba.
    Watu wanaofanya kazi pamoja na tabibu ni muuguzi (nesi) na wasaidizi wengine.
    Tiba imeendelea kiasi cha kuwa na masomo yake madogo yanayoangalia hasa magonjwa ya sehemu fulani ya mwili tu. Kila somo dogo lina wataalamu wake. kwa mfano tiba ya moyo, ya ngozi, ya viungo vya ndani, ya upasuaji, ya magonjwa ya watoto na kadhalika.

Mbinu za kisayansi


Charles Darwin mwaka 1854, alipokuwa anatunga kitabu chake "On the Origin of Species".
Msingi wa sayansi ni vitendo. Vitendo vya kisayansi vina njia zake zinazotumika kuthibitisha kweli za kisayansi.
Namna ya kueleza jambo kisayansi huchimbuka toka nadharia ama udhanifu. Halafu, ili kweli ikubalike, hutoka kwenye udhanifu na kwa kupitia majaribio rasmi, hutengeneza dhana kamili ama nadharia kama ni shauri la kueleza mwenendo na tabia.
Kwa hivyo, asili ya njia ya kisayansi ni mtazamo unaokwenda sambamba na vitendo vinavyochunguzwa. Kutoka mitazamo wanasayansi wanaunda nadharia. Baadaye wanaangalia kama bashiri za nadharia ni kweli. Isipokuwa kweli watakanusha nadharia hiyo. Ikionekana kwamba mara nyingi sana nadharia ilibashiri ukweli, na haijakosea, itakuwa nadharia inayokubalika.

Sura ya kisayansi

Mara chache, maarifa yatokanayo na sayansi yanaweza kupinga hali ya kawaida. Kwa mfano nadharia ya atomu inasema kwamba katika jiwe (maada yabisi) kuna uvungu (dutu tupu), na kwamba atomi zinacheza katika nafasi ndogo katika jiwe ukifananisha na maada kimiminika. Lakini kwa nadharia hii tunaweza kueleza mambo mengi, hata kwa nini tunaweza kusema kwamba jiwe halina uvungu.

Historia


Aristotle (384 KK – 322 KK) alichangia katika ukuaji wa sayansi.

Sura ya kiutamaduni

Sayansi iliaanza kama udadisi wa mtu mmojammoja; lakini kadiri maarifa yanavyopanuka, inakuwa vigumu kwa mtu mmoja kufanya mchango wa kujitenga. Hivyo jumuiya zimebeba kusudi ambalo hapo mwanzo lilionekana kama ni shauku la mtu mmojammoja kama awali.
Hii hufanya mkururo wa ugunduzi ama uvumbuzi kuwa sehemu ya historia ya sayansiMajina na sifa kutajwa sambamba na shauri la aliyepelekea.
Sayansi na jamii huenda pamoja katika kuleta mabadiliko, kwa kuwa mabadiliko huletwa na watu wenyewe.

Sayansi na siasa za dunia


Picha ya dunia ikionyesha kutokea kwa mabara kutoka kugawanyika kwa Pangea mpaka hivi leo.
Katika dunia hii ya leo, maendeleo ya watu hujidhihirisha sana kutokana na jinsi jamii husika ilivyopiga teke katika uwanja huu.
Ingawaje haibainishwi wazi miongoni mwa sura ya mambo ya kidunia, sayansi kwa kweli ni nguvu inayoweza kubadili maishaya watu kwa wema; lakini katika kilele chake cha mafanikio, vyombo vyenye nguvu za mamlaka na fedha hushikilia baadhi ya matunda yake katika hali ya kibiashara na kiutawala zaidi.

Sayansi na maendeleo


Mambo mbalimbali ya kikemikali yaliyosomwa na Michael Faraday na kuripotiwa katika historia yake kabla ya mamlaka ya kisheriaHistoria ya kikemikali ya mshumaa, mwaka 1861.
Wapo watu pia ambao hutumia sayansi kujaribu kuboresha maisha ya watu wote kwa ujumla. Hivyo sayansi haibakii tu mikononi mwa wenye kushika dau kimifumo, bali changamoto ya wote wenye kutaka kuleta maendeleo ya ujumla.
Hivyo roho ya uchunguzi ndiyo iliyoleta kuzaliwa, kukua na kutapakaa kwa sayansi.


katika ufuatiliaji

Galileo Galilei


Uchoraji wa Galileo Galilei
Galileo Galilei (5 Februari 1564 – 8 Januari 1642) alikuwa mtaalamu wa fizikiahisabati na astronomia kutoka nchini Italia.
Anakumbukwa kwa sababu aliweka misingi kwa mbinu mpya za sayansi zinazoendelea kutumiwa hadi leo. Akiwa mtaalamu wa kwanza aliyetumia darubini kwa kutazama nyota na sayari alipanusha ujuzi wa binadamu juu ya ulimwengu.

Ujana wake

Baba yake alikuwa mfanyabiashara aliyejishughulisha pia na maswali ya hisabati.
Galileo alisomeshwa kwenye shule ya monasteri akaendelea kusoma tiba mjini Firenze lakini akaacha masomo hayo akachukua hisabati badala yake.

Kanuni za anguko

Miaka 1589 - 1592 alipata nafasi ya profesa ya hisabati kwenye chuo kikuu cha Pisa. Hapa alifanya utafiti juu ya kanuni za anguko la magimba. Aliweza kuonyesha kwamba magimba yote huanguka kwa mkasi uleule yakianguka pasipo hewa kama ni makubwa au madogo. Kwa tamko hili alionekana kumpinga Aristotelesaliyepokewa na wataalamu na kanisa kama msingi wa utaalamu wote.

Astronomia na darubini

Akahamia chuo kikuu cha Padua alipofanya kazi kati ya 1592 na 1610. Alisikia kuhusu chombo kipya cha darubini (kionambali) kilichobuniwa na Mholanzi Hans Lipperhey akaiiga na kujenga yake. Alikuwa mtu wa kwanza aliyetumia chombo hicho kwa kutazama mwezisayari na nyota. Aliona milima kwenye mwezi akawa mtu wa kwanza aliyeona miezi ya sayari Mshtarii. Vilevile aliweza kuangalia sayari Ng'andu (Zuhura/Venus) jinsi ilivyoonyesha awamu sawa na mwezi zilizoonekana kama mwezi mwandamu, nusu mwezi au mwezi mpevu. Aliona pia madoa ya jua.
Mwaka 1610 mtawala wa ToskanaCosimo II kutoka nasaba ya Medici, aliyewahi kuwa mwanafunzi wake, alimkaribisha kuwa mwanahisabati mkuu na pia profesa huko Pisa.
Alipendwa na watu wengi, pia na kardinali Maffeo Barberini aliyeendelea baada ya kuwa Papa Urban VIII.

Kesi ya Kanisa dhidi yake


Sanamu ya Galileo Galilei kwenye kaburi lake ndani ya Kanisa la Msalaba Mtakatifu mjini FirenzeItalia
Matokeo ya utafiti wa Galilei yalipinga hoja la awali lililofundishwa na wataalamu wa Ugiriki ya Kale na kukubaliwa katika Kanisa Katoliki. Kwa Galilei ilikuwa wazi ya kwamba dunia yetu si kitovu cha ulimwengu tena aliamini lilikuwa jua badala yake na kwamba Nikolaus Kopernikus pamoja na Johannes Kepler‎ waliwahi kusema ukweli. Hivyo Galilei alishtakiwa kuwa mafundisho yake yalipinga Biblia na imani.
Katika kesi alionywa asiseme maoni yake mapya ni ukweli badala yake alitakiwa kusema ni uwezekano tu. Sehemu ya vitabu vyake vilipigwa marufuku na mwenyewe aliambiwa kukaa ndani ya nyumba yake.
Mwaka 1992 Papa Yohane Paulo II alisema kuhusu kesi dhidi ya Galilei: « Kama wapinzani wake walio wengi, Galileo hakutofautisha mtazamo wa sayansi kuhusu mambo ya kimaumbile na fikra za kifalsafa juu ya maumbile ambazo kwa kawaida zinadaiwa nao. Ndiyo sababu alikataa pendekezo alilopewa la kuita 'dhana' mafundisho ya Kopernicus, hadi yathibitishwe moja kwa moja, ingawa hilo lilikuwa sharti la mbinu ya majaribio aliyoibuni mwenyewe kwa akili kubwa. [...] Kumbe, suala walilojiuliza wanateolojia wa wakati huo lilikuwa lile la ulinganifu wa mafundisho ya jua kuwa kiini cha ulimwengu na Maandiko Matakatifu. Hivyo sayansi mpya, kwa mbinu zake na uhuru wa ukufanya utafiti unaodaiwa nazo, ililazimisha wanateolojia kujiuliza juu ya vigezo vyao vya kufafanulia Maandiko. Wengi wao wakashindwa kufanya hivyo. Ajabu, Galileo, mwamini mnyofu, alijitokeza anaelewa kuliko wanateolojia waliompinga kuhusu jambo hilo. » (Yohane Paulo II kwa wanasayansi wa Akademia ya Kipapa ya Sayansi, 31 Oktoba 1992)

No comments: